Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Shedrack Masanika akipanda mti ishala ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji

Joseph Lyata mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa akipanda mti ishala ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.
Na Fredy Mgunda, Iringa.


JUMUIYA ya wazazi wilaya ya Iringa imejipanga kupanda zaidi ya miti milioni 2 kwa lengo la kutunza mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kama ambavyo ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025 inavyosema kunywe ibara ya 100 ya ilani.

Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji Kata ya Kitwiru, mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Shedrack Masanika alisema kuwa wamejipanga kwa kuanza jumuiya hiyo itakuwa inapanda zaidi ya 1000 kwa mwezi ili kuendelea kuhifadhi mazingira na kutunza vya maji.

Masanika alisema kuwa toka uongozi mpya wa jumuiya hiyo wamekuwa wakitekeleza agizo la chama cha mapinduzi kwenye Ilani ya chama hicho ya mwaka 2020/2025 katika ibara ya 100.

Alisema kuwa miti hiyo rafiki na mazingira itapandwa kwenye vyanzo vya maji, Shuleni, kwenye taasisi za chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa, taasisi mbalimbali za kiserikali na zile zisizo za kiserikali.

Masanika alisema kuwa jumuiya ya wazazi kuendelea kutoa elimu ya utanzaji wa mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa hadi kizazi kijacho.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya wilaya ya Iringa,Baraka Kimata alisema kuwa moja ya jukumu la jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa ni kuhakikisha wanatoa elimu ya umuhimu wa upandaji wa miti na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Kimata alisema kuwa upandaji wa miti na utunzaji wa vyanzo vya maji ni jukumu la kila wananchi kwa uhai wa binadamu na viumbe hai vingine.

Alisema kuwa wameanzimisha Miaka 46 ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Iringa kwa kupanda miti na jukumu hilo la upandaji miti linatakiwa kuwa la Taifa zima.

Naye Joseph Lyata mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa alisema kuwa ibara ya 100 inazungumzia maswala ya maji na mazingira jambo ambalo ni jukumu la wanachama wote wa CCM.

Lyata alisema kuwa jambo la kutunza mazingira na vyanzo vya maji ni jukumu la kila wananchi na vyama vyote vya kisiasa hivyo wananchi hawatakiwi kuichia serikali na chama cha mapinduzi pekee yangu.

Alisema kuwa ukataji wa hivyo unachangia ukame ambao umekuwa na madhara mengi kwa jamii na viombe hai ambao mara nyingi wanategemea maji na mazingira mazuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...