Na. Damian Kunambi, Njombe.

Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumuiya ya Wazazi Wilayani Ludewa mkoani Njombe imeadhimisha siku hii kwa kupanda miti ya mbao zaidi ya 300 katika shule ya sekondari ya jumuiya hiyo Ludewa mjini sambamba na kutoa elimu kwa viongozi wa ngazi ya kata, matawi na serikali.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilayani Ludewa Nathaniel Mgaya amesema bado wanahitaji kupanda miti zaidi kwakuwa kuna hekari zaidi ya 10 hivyo kwa sasa wamepanda miti hiyo 300 ila wataendelea kupanda zaidi.

Sanjali na hilo pia amewataka viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi zote kuhakikisha wanaanzisha miradi mbalimbali itakayowaletea mapato na kuifanya jumuiya hiyo inakuwa na uwezo wa kujisimamia yenyewe.

"Leo tumepanda miti hii kama mradi wa shule yetu hii hapo baadae ambao utawawezesha kuvuna mbao na kupata kipato lakini pia nasisi viongozi wa matawi, kata na sisi wa wilaya tunapaswa kutengeneza miradi itakayokuza uchumi wetu ili jumuiya yetu iweze kukua zaidi", Amesema Mgaya.

Aidha kwa upande wake kaimu Katibu wa jumuiya ya wazazi wa wilaya hiyo amewaasa viongozi wa shule hiyo kutunza miti hiyo kwakuwa itawasaidia hapo baadae katika kukuza uchumi wa shule na kuwainua zaidi.

Amesema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anajitoa na kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo na uchumi wao unakua hivyo nasi tunapaswa kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...