Na. Khadija Seif, Michuzi TV
Bondia wa Ngumi za Kulipwa nchini, Mudy Pesa maarufu ‘Misumari ya Zege’ amechimba mkwara kuelekea pambano lake la ndondi dhidi ya mpinzani wake, Amani Bariki ambaye anatoka kwenye Kambi ya mazoezi ya Uwanja wa Kivita.
Pambano hilo la ‘Kill Boxing Tour’ linatarajiwa kufanyika Februari 25, 2023 katika ukumbi wa YMCA jijini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Michuzi Blog, Mudy Pesa amesema mpinzani wake amekutana na Chuma kizito kisichoogopa ngumi huku akitamba kumtwanga na kutoa dozi nene katika ardhi yake ya Moshi kwenye pambano hilo.
"Namuweza vizuri tu! ‘Manchuga' simuogopi wala simuhofii, nimemuona na ngumi zake hazina madhara, nilishawahi kushuhudia pambano lake uwanja wa Kinesi, Dar es salaam hazijanitisha sijajua atanipiga ngumi gani mpaka niisikie,” amesema Mudy Pesa.
Hata hivyo, Mudy Pesa amewaomba mashabiki wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hiyo na kuahidi kutoa kipigo kwa Bondia huyo akiwa mbele ya Familia yake kutokana na maandalizi aliyofanya.
"Familia yake itashuhudia Mtoto wao anavyopata tabu katika utafutaji wa pesa, nimejipanga kwa ajili ya ‘Manchuga’ nitampiga ninavyotaka mimi,” ameeleza Mudy.
Kwa upande wa Kocha wake, Fadhil Kambi amesema kuwa Bondia Mudy Pesa yupo vizuri siku zote, lakini kutokana na kuwepo kwa pambano hilo wamekuwa wakimpa mazoezi mengi zaidi ili kumkabili mpinzani wake.
"Tutafanya mazoezi mara mbili yake kwa ajili ya pambano hilo na tunaahidi kuvunja rekodi ya ‘derby’ zote zilizofanyika tutakuwa fiti zaidi yake mbele ya mkoani kwake."

Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Tanzania Mudy Pesa maarufu kama "Misumari ya zege" akiwa pamoja na Mashabiki zake wakimpa hamasa ya Mazoezi kuelekea pambano la "Kill Boxing Tour " linalotarajiwa kufanyika Febuari 25,2023 Moshi Mkoani Kilimanjaro litakalomkutanisha na bondia mwenyeji wa Mkoa huo Amani Bariki maarufu kama ''Manchuga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...