Na Haika Mamuya, WFM , Dodoma.

BUNGENI



Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Serikali haijajificha kwenye vita ya Ukraine na Urusi, uviko na mabadiliko ya tabianchi katikasuala la mfumuko wa bei nchini kwa kuwa mambo hayo ni halisia na Serikali imeendelea kuchukua hatua.

Dkt. Nchemba amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo, aliyesema kuwa Serikali inajificha katika vita ya Ukraine na Urusi katika suala la mfumuko wa bei.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imechukua hatua ambazo nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika hazijazifikia

“Kwa ujumla hamna nchi imechukua hatua ya kutoa bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kupunguza gharama, ndio maana hata nchi jirani zinakimbilia Tanzania kuchukua vitu”, alisema Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa Serikali imeondoa tozo na kodi zote katika mafuta ya kula na ikachukua nusu ya gharama ya bei ya kila mfuko wa mbolea na bado Serikali ina jitihada nyingineinazoendelea kuchukua na inaendelea kuwa makini katika jambo hilo.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu hoja ya Mbunge wa Arusha (Mjini), Mh. Mrisho Gambo Bungeni jijini Dodoma leo Januari 31, 2023


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...