Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UBALOZI WA India nchini Tanzania umesema unatarajia biashara kati ya nchi hizo mbili utafikia Dola bilioni Sita kutokana na uwekezaji mpya unaotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu.

Uwekezaji huo mpya ni pamoja na uanzishwaji wa maeneo mapya ya kibiashara , uwekezaji kwenye taasisi z fedha pamoja ba kuongeza ununuzi wa bidhaa za mazao hasa parachichi.

Akizungumza leo Januari 27,2023 Balozi wa India nchini Tanzania Bibaya Pradhan amesema kwamba SERIKALI ya India imesema mwaka jana ulikuwa mwaka mzuri sana wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili, mikataba kadhaa ya uwekezaji ilisainiwa na hivi karibuni utekelezaji utaanza

"Kwa hiyo mwaka huu tunaona utakuwa ni mzuri zaidi kibiashara kwani kuna idadi kubwa ya wawekezaji kutoka India wameonesha nia ya kuwekeza. Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa kuendelea kuweka nazingira mazuri ya biashara ambayo yanafanya uwepo wa uhakika katika kufanya biashara,"amesema Balozi Pradhan.

Aidha amesema katika kukuza biashara hivi karibuni wanatarajia kuanzisha mazungumzo na wadau wa sekta ya fedha hasa benki za Tanzania kushirikiana na zile za India ili kurahisisha ufanyaji bishara.

"Katika kujenga wigo mpana wa kibiashara tunaona haja ya Benki za Tanzania kwenda kufungua matawi nchini India na benki za India nazo zikaongeza matawi yake hapa nchini Tanzania.Tukiwa na ushirikiano kwenye benki zetu itakuwa rahisi kufanya biashara kwa kutumia fedha zetu lakini iwapo mfanyabiashara atataka kutumia fedha nyingine yoyote itakuwa ni uamuzi wake lakini kwa kutumia benki zetu tunaamini itakuwa fursa ya kurahisisha biashara zetu."

Kwa upande wa uhusiano wa katika nyanja mbalimbali za kisisa, diplomasia,elimu,afya , miundombinu , kilimo, utamaduni na maeneo mengine ushirikiano ni mkubwa na nchini ya India inajivunia ushirikiano mkubwa uliopo baina ya nchi hizo.

"Kwenye upande wa afya hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa ujenzi wa Hospitali ya Apolo ambao utasaidia sekta ya afya lakini kwwnye eneo elimu kwenye elimu wanatarajia Chuo cha masuaa ya Sayansi na Teknolojia kitaanza kutoa mafunzo mafunzo yake nchini Tanzania."

Akifafanua upande wa Diplomasia amesema kumekuwepo na ushirikiano mkubwa akitoa mfano kwamba siku za karibuni viongozi wa India wamefanya ziara kuitembelea Tanzania lakini na viongozi wa Tanzania nao wamekuwa wakifanya ziara nchini India.





Balozi wa India nchini Tanzania Binaya Pradhan(katikati)akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 27,2023 jijini Dar es Salaam kuhusu masuala yakiwemo ya uwekezaji huku akieleza kuwa matarajia yao biashara baina ya nchi
hizo mbili utakuwa mkubwa zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...