Na Karama Kenyunko - Michuzi TV
Washtakiwa watatu kati ya 12 wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na meno a Tembo thamani ya zaidi ya bilioni nne, wamemuandikia barua Mkurugenzi wa mashtaka nchini akiomba kuingia makubaliano ili wakiri makosa yao.
Washtakiwa walioandika barua ni Ally Anguzuu, Abbas Hassan na Kasim Saidi ambapo wamefikia hatua hiyo wakati kesi hiyo imeishafika hatua ya usikilizwaji ambapo mpaka sasa shahidi mmoja ameishamaliza kutoa ushahidi wake.
Mapema wakili wa Serikali Felix Kwetukia alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo leo January 30,2023 imeitwa kwa ajili ya kutajwa lakini wamepokea barua tatu kutoka kwa washtakiwa akiomba kuingia makubaliano (Plea bargaining).
Hakimu Rhoda Ngimilanga amekubaliana na maombi hayo ya upande wa mashtaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi Mosi 2023 kwa ajali ya kuwasilisha taarifa ya makubaliano na kesi itaendelea kusikilizwa Machi 13, mwaka huu.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, mfanyabiashara Victor Mawala, Haruni Abdallah, Solomoni Mtenya, Khalfani Kahengele, Ismail Kassa, Juma Buguma, Peter Nyachiwa, John Buhanza na Mussa Abdallah wote wakazi wa Dar es Salaam.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na nyara za serikali bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori, ambazo ni meno hayo yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 4.6.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa na mtandao mkubwa wa uhalifu wa ujangili ambao unajihisisha na kuuza na kununua, kupokea na kuhamisha, kusafirisha nyara za serikaki ambazo ni meno ya tembo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...