Dar es Salaam Jumatano 8 Februari 2023:  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kutoa faida ya Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha Julai mpaka Septemba 2022. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikitoa faida hii kwa wateja na mawakala baada ya kuidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Faida ya Gawio la Airtel Money hutolewa kwa wateja, wadau na mawakala wa Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti zao za Airtel Money. Kiasi cha faida ambacho mteja au Wakala unachopata hutegemea na jinsi ambavyo unatumia huduma za Airtel Money na faida hii huwekewa moja kwa moja kwenye akaunti  yako ya Airtel Money ambapo mteja au Wakala unaweza kuitumia kwenye matumizi ya kawaida  kama vile kutoa au kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma kama DAWASCO, LUKU au huduma zingine kulingana na vile unavyotaka.

 kizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anatangaza kuanza kutoa Gawio la faida la Airtel Money, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Airtel Money Daudi Ndovu alisema, “Gawio la Faida la Airtel Money hili litatolewa kwa wateja na Mawakala wote ambao walikuwa wakitumia huduma za Airtel Money kwa kipindi cha Julai hadi  Septemba 2022 kote nchini kuanzia leo”.

 “Dhamira yetu ni kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya kupanua huduma za kifedha kwa ujumuhishi. Leo tunatangaza kuanza kugawa faida ya gawio la Airtel Money la Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala wa huduma za Airtel Money kote nchini. Tunayo furaha kuona ni jinsi gani huduma ya Airtel Money inavyozidi kukua hapa nchini.” alisema Ndovu

 Ndovu aliongeza ‘Airtel imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta huduma za Airtel Money karibu na wateja na kufikia Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki hasa  maeneo ya vijijini. Na ili kuendelea kukuza huduma kifedha jumuishi, Airtel Money imeweza kuzindua promosheni ya Bila Tozo ambapo kwa sasa wateja wanaweza kutuma au kutoa fedha BILA TOZO na hivyo kuendelea kukuza biashara kwa kufanya malipo kwa unafuu zaidi.  Airtel itaendelea kuleta bidhaa na huduma zenye kutoa masuluhisho kwa watanzania kila wakati  ikiwemo kutuma au kutoa fedha pamoja na kufanya malipo kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuwekeza kwenye kupanua wigo wa mtandao wa Airtel Money ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora zaidi. “Tunayo furaha kwamba kwa sasa tumejipanaga vyema kwa kuweka miundombinu bora ya usambazaji wa huduma zetu za Airtel Money yakiwemo maduka ya Airtel Money Branch zaidi ya 3,500 kote nchini pamoja na Mawakala wa Airtel Money waliosambaa nchi nzima zaidi ya 170,000.”

 Tutae ndela kutoa huduma iliyo bora ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma zetu kila kona  saa 24 / siku 7 za wiki aidha wakiwa nyumbani au ofisini. 

Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kutoa faida ya Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha Julai mpaka Septemba 2022. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikitoa faida hii kwa wateja na mawakala baada ya kuidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money Daudi Ndovu.Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money Daudi Ndovu (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kutoa faida ya Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha Julai mpaka Septemba 2022. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikitoa faida hii kwa wateja na mawakala baada ya kuidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...