Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV- Tanga

WATU 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya magari mawili likiwemo gari iliyokuwa ikisafirisha msiba kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 4, 2023 katika eneo la Magira Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Imeelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi.

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesemaa wananchi wa Mkoa Wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko makubwa tukio la ajali hiyo iliyotokea usiku wa leo ikihusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12 pamoja na uharibufu mkubwa wa nagari hayo.

"Ajali imetokea Februari 3,2023 , saa 4.30 usiku eneo la Magila Gereza katika Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera - Buiko. Magari yaliyohusika na ajali hiyo ni gari namba T 673 CUC aina Mitsubish Fuso Ikiendeshwa na Dereva ambaye jina lake halijafamika iligonga na gari T 863 DXN aina ya Coaster Coaster Iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na Abiria 26 Ikiyokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

"Ajali hii imesababisha vifo 17 na najeruhi 12 ambao majina yao wote Hayajafahamika. Miili ya narehemu imehifafhiwa katika Hospital yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospital ya Mkoa wa Tanga Bombo na majeruhi 2 wamebaki Hospital ya Korogwe kwa Matibabu,"amesema Mgumba

Aidha ameeleza kwamba chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa gari namba T 673 CUC M/Fuso Kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso gari namba T863 DXN T/Coaster.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa bada ya magari yote yaliyopata ajali yamekaguliwa na yameshaondolewa barabarani na sasa barabara inapitika.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...