Na Janeth Raphael.

Hospitali  ya Benjamin Mkapa leo February 6, 2023 imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za Upasuaji wa Moyo kwa watoto na Shirika lisilo la kiserikali la Children Heart Charity Association la nchini Kuwait.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt Alphonce Chandika ameyabainisha hayo wakati wakutia saini makubaliano hayo ambapo  alisema makubaliano hayo yameangazia maeneo makuu matatu.

Dkt Chandika ameyataja maeneo hayo kuwa ni kugharamia watoto wenye matatizo yanayohutaji Upasuaji wa moyo,kuwezesha vifaa tiba vinavyohitajika kwenye matibabu ya moyo.

Alisema eneo la tatu ni kuwajengea uwezo madaktari,wauguzi na wataalam wa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya Moyo wa Hospital ya Benjamin Mkapa.

"Tunaishkuru sana Kuwait kwa kujitolea kutusaidia matibabu ya Moyo kwa watoto wadogo,"amesema Dkt Chandika.

Hospitali hiyo ya Benjamin Benjamin Mkapa ilikuwa inatibu watoto 400 kwa mwezi na kwa sasa watakuwa na uwezo wa kutibu watoto 3400.

Dkt Chandika amesemal zaidi ya kuwa pamoja na utiaji saini tayari jopo la Madaktar, wauguzi na wataalam wa huduma za matibabu ya Moyo kutoka Kuwait wamewasili katika hospital hiyo kutoa huduma za uchunguzi tokea February 3 ambapo watakuwepo hadi February 9 na wanatarajia kuwafanyia uchunguzi watoto 100 na kupatiwa matibabu na hapo jama watoto wawili wameshafanyiwa matibabu.

Kwa upande wake  Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Said Musa alisema ujio wa madaktari bingwa hao hapa nchini  hapa nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za moyo kwa watoto ikiwemo Upasuaji.

Balozi Musa  ameishukuru Hospital Mkapa kutokana na ushirikiano waliotoa kwa madaktari hao na kuwataka waendelee kuwa na Moyo wa utoaji  wa matibabu  hayo ya Moyo.

Naye  Dr Faisal Al-Saied amesema wanaimani malengo wanayotarajia kuyafikia yatafanikiwa kwa sababu wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa  hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa.

"Jamii inapaswa ijitokeze kwa ajili ya kupata matibabu ya Moyo kwa watoto wadogo hususani wale wanaohitaji Upasuaji"

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...