Na John Walter-Babati

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuboresha mazingira kwa kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange wakati wa zoezi la upandaji miti katika kituo cha afya Maisaka mjini Babati ambapo amesema katika wilaya ya Babati atahakikisha zoezi hilo linafanyika kikamlifu.

Amesema agizo hilo la serikali kupitia ofisi ya makamu wa Rais kupandwa miti milioni 1.5 kila Halmashauri, katika wilaya ya Babati atatumia mbinu mbalimbali za uhamasishaji ili lengo litimie.

Aidha amewataka wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti ya matunda na vivuli ili kulinda na kutunza mazingira.

Twange amesema mbali na miti kupandwa katika maeneo ya taasisi kama Shule, Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya, lakini pia kampeni ya upandaji miti itawafikia wanachi wote kwa kugawa miti kwa kila mwananchi kupitia watendaji kwenye mitaa na vijiji.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahmani Kololi (Diwani wa Maisaka) amesema watahakikisha katika halmashauri hiyo kila mwananchi anapanda mti.

Kiongozi wa Walimbwende mkoa wa Manyara Aminatha amewaasa warembo kujiutokeza kushiriki kupanda miti katika maeneo yao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...