Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imetenga jumla ya Tsh. Million 36 kwa washindi 22 wa kampeni yake ya “Kapu la Wana”, ambayo washindi watajishindia zawadi mbalimbali, ikiwemo zawadi nono ya gari pamoja na  boda boda, luninga na simu za mkononi.

Kampeni hiyo inayodumisha kauli mbiu ya chapa yake, “SIMAMA IMARA, SONGA MBELE” (kutia moyo na kusaidia juhudi za watu) inarudi kwa mara ya pili na kampeni ya  “Kapu la Wana” ikiwa na dhamira ya kuwapa vijana nafasi ya kujipatia fursa mbalimbali zitakazo wasaidia jikwamua kwenye maisha.


Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja wa Bia ya Pilsner Lager wa SBL, Wankyo Marando, alisema “ Tukirudi nyuma kuangalia lengo la bidhaa hii, Pilsner Lager ipo kwaajili ya kusherehekea mafanikio ya walaji wetu na kuwatunza kwa umaridadi wao kutimiza ndoto zao na kuchapa kazi”.


Kampeni ya “Kapu la Wana” ni mwendelezo wa bia ya Pilsner Lager kuwazawadia watu wote walionyesha udhubutu, kukabiliana na changamoto katika kujikwamua kimaisha na kufanikisha mafanikio waliojiwekea.


Hivyo, kampeni hii inaipa Pilsner Lager jukwaa la kuhodhi nafasi muhimu katika maisha ya vijana wachapakazi, wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.


“Pilsner Lager ni bia ya vijana ambao hawakati tamaa na wenye kiu ya kutimiza mafanikio makubwa. Tunawawezesha vijana kwa kuwapatia vitendea kazi ili wasonge mbele. Hivyo, tunawahamasisha  walaji wote wa Pilsner Lager kuitumia kampeni hii ili kusogeza juhudi zao mbele.”Wankyo Marando aliongezea.


Kampeni ya “Kapu la Wana” ni ya Watanzania wote walioko ndani ya kanda tatu (Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa). Walaji wanatakiwa kununua bia ya Pilsner Lager, kwangua kadi maalum ili kujiweka katika nafasi ya kushinda.


Kampeni hii itakwenda kwa muda wa miezi 8 mfululizo na itahusisha watu wote waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kushindania zawadi, baada ya kutuma nambari maalum na kupokea ujumbe mfupi wa udhibitisho. 


Kwa upande wake, Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi alitoa wito kwa wanywaji wa bia hiyo kushiriki kwenye promosheni hii na kuongeza kuwa, “kwa vile bidhaa yenu ya Pilsner Lager inahamasisha wanywaji wake kunywa kistarabu na kuchapa kazi kwa bidii na kujipongeza baadae, jambo la mfano wa kuigwa na makampunimengine, kwa vile yanaleta tija katika shughuli za kujenga nchi.”


Vilevile mshindi wa mwaka jana wa promosheni hii alisema, “tokea mwaka jana, ambapo nilipo ingia katika shindano la Kampeni ya Kapu La Wana, mambo mengi sana yamebadilika katika shughuli zangu za kiuchumi. Mabadilko haya, yamefanya biashara yangu kupanuka na kunipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii michezo ya kubahatisha, kama Kapu La Wana, ni fursa ya wajasiriamali wadogo kupata nafasi ya kukua na kubadili Maisha yao kwa vile, kampeni kwa ujumla inakuja na lengo la kuinua vijana na kuwapa nguvu ya kusimama imara kusonga

mbele.”


Jinsi ya Kukwangua na Kushinda


  • Nunua bia ya Pilsner Lager

  • Pata kadi ya kukwangua & ikwangue ili kujipata zawadi kila ununuapo bia

  • Kama zawadi ni  bidhaa kama fulana, kofia au shajara, n.k utazawadiwa papo hapo

  • Kama zawadi uliyoikwangua ni nambari maalum, itume kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 mfano: Andika Kapu 4321 Iringa (Acha nafasi)

  • Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utatumwa kudhibitisha ushiriki wako

  • Ujumbe mfupi wa maneno utasomeka hivi:

  • Hongera! Umesajiliwa KAPU LA WANA, 12/03/2022 bahati nasibu itachezwa kuwapata washindi. Sambaza kwa watu wengi zaidi kuongeza nafasi yako kushinda. Simama Imara na Songa Mbele. Mshiriki lazima awe na miaka 18+.

  • Samahani nambari maalum uliyotuma sio sahihi, tafadhali fuata vigezo na masharti kushiriki. Pilsner Lager, Simama Imara na Songa Mbele. Mshiriki lazima awe na miaka 18+

  • Samahani nambari maalum uliyotuma imeshasajiliwa, tafadhali fuata vigezo na masharti kushiriki. Pilsner Lager, Simama Imara na Songa Mbele. Mshiriki lazima awe na miaka 18+

  • Kila baada ya wiki 2, droo mubashara itafanyika na washindi 7 watapatikana katika bahati nasibu tatu za mwanzo, kisha droo nne za mwisho na mshindi wa mwisho atakabidhiwa zawadi ya gari.


Meneja wa bia ya Pilsner Lager ya Serengeti Breweries Limited (SBL), Wankyo Marando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya wiki nane ya bia hiyo, ijulikanayo kama “Kapu la Wana” itakayowapa wanywaji wa bia hiyo nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo gari, pikipiki na luninga. Promosheni hiyo imelenga kanda ya ziwa, kusini nakaskazini. Kushoto kwake ni muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi na mshindi wa mwaka jana wa promosheni hii, Vicent Barnabas Kimario.

Meneja Mawasiliano wa Serengeti Breweries Limited, Rispa Hatibu (kulia), na Meneja wa bia ya Pilser Lager, Wankyo Marando (kushoto) wakionesha waandishi wa habari gari itakayoshindaniwa na wanywaji wa bia hiyo kupitia promosheni ya “Kapu la Wana” iliyozinduliwa jana mahsusi kwa wateja wao wa kanda ya ziwa, kusini na kaskazini.

MenEja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando (kushoto) na muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi w akiwaonyesha waandishi wa habari zawaid zitakazoshindaniwa na wanyawaji wa bia hiyo kupitia promosheni ya “Kapu la Wana” iliyozinduliwa jana. Promosheni hiyo ni mahsusi kwa wateja wa bia hiyo wa kanda ya ziwa, kaskazini na kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...