Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA)Nebart Mwapwele ameipongeza Serikali kwa kuandaa mafunzo ya Kilimo kwa vijana kwani vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wanategemewa katika kuinua uchumi wa nchi yetu.

Ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati miongoni mwa vijana nchini tayari  wamejitokeza kwa wingi kuomba nafasi ya mafunzo ya kujenga Kesho Mpya kupitia kilimo biashara (Building Better Tomorrow-BBT).

Dirisha hilo lilifunguliwa Januari 10, 2023 na Wizara ya kilimo ikiwa ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuzalisha ajira milioni tatu kwa wanawake na vijana katika sekta ya kilimo nchini.

Akifafanua zaidi amesema  mpango huo wa Serikali utasaidia vijana kushiriki kazi za kilimo na  wao kama TCCIA watahusika kuwatafutia masoko  katika soko la kimataifa.

"Kwa kuwa bajeti ya kilimo nchi imeongezwa mara nne zaidi ya miaka ya nyuma yapo  matumaini makubwa ya vijana hao kufanya kilimo kitakachoonesha mapinduzi mazuri katika uzalishaji mkubwa wa kibiashara,"amesema.

Mwapwele amesema hadi sasa nchi yetu imekuwa na maeneo mazuri kwa kilimo na yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji nayo yakitajwa kuwa ni mengi.

Mkurugenzi huyo ameusifia uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mpango wake wa kuongeza wawekezaji wengi kuingia nchini.

Amesema kutokana na kilimo  nchini kutegemea mvua hivyo mwaka 2022 kulikuwa na ukame kwa maeneo mengi na hali hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Wakati wa kuzinduliwa kwa mpango huo pamoja na mambo mengine Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza miongoni mwa vijana waliochaguliwa wanawake ni 282 sawa na asilimia 34.73 na wanaume ni 530 sawa na asilimia 65.27.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...