Na Mwandishi Wetu,Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewahimiza wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji kwa kutunza mazingira na kupanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji
Mgeni ametoa ushauri huo wakati wa kilele cha Wiki ya Maji kitaifa yaliyofanyika katika Kata ya Hedaru mbapo pia amepanda mti huku akihimiza kila kaya kupanda mti kwenye maeneo ya nyumba zao,
Pia amesisitiza wananchi kuepuka kulima ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji. Aidha amewaelekeza wataalamu wa maji kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala zima la mita 60.
Aidha amewaomba wananchi wote kumuunga mkono Rais Dk.Samiha Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo katika jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...