Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetangaza kuzinduliwa kwa mashindano ya The Vioce Afrika yenye lengo la kuinua vipaji vya wanamuziki mbalimbali ambapo washiriki 78,804 kutoka nchini 14 watashiriki Shindano hilo.

Akizungumza leo Machi 24,2023 jijini Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jakson Mmbando kupitia kipindi cha XXXL kinachorushwa na kituo cha Radio cha Clouds FM amesema mashindano hayo yatashirikisha wanamuziki kutoka nchi 14.

"Airtel ambaye ni Mdhamini Mkuu kwa kushirikiana na Fame Studio Afrika tutaonesha Shoo ya Mashindano hayo katika kituo cha televisheni cha Clouds TV kuanzia saa mbili usiku na kupitia Airtel TV.

"Washiriki 78,804 kutoka nchi za Nigeria, Kenya, Seychelles, Tchad, Uganda, Congo, Zambia, Tanzania, Rwanda, Gabon, Madagascar, Malawi, na Jamhuri ya watu wa Congo watashiriki,"amesema Mbando

Aidha amefafanua kuwa baada ya mchujo jumla ya washiriki 12,308 wenye vipaji walichaguliwa na baadaye wakachaguliwa tena wakabaki 100 ambao kila nchi imeweza kutoa washiriki 7 ambao wataanza kuonekena kwenye shoo moja kwa moja kutoka jiji la Lagos nchini Nigeria.

"Mashindano ya The Voice Africa yatafuata taratibu za kimataifa za kutafuta vipaji ambapo shoo hii itadumu kwa muda wa wiki 25 chini ya jopo la makocha ambao watakuwa na kazi ya kuwanoa washiriki."

Kwa mujibu wa Mbando kwamba mshindi mmoja kati ya 100 wanaoshiriki Shindano hilo ataibuka kuwa mshindi wa The Voice of Afrika na Airtel Tanzania inaamini katika kukuza vipaji vya vijana kuanzia hapa nchini na kuwapeleka katika viwango vya kimataifa.

Mbando ametoa mwito kwa watanzania wote kukaa tayari kutazama shoo hiyo itakayoanza kwenda hewani kuanzia saa mbili kamili usiku kupitia Clouds TV na wale wanaoutumia simu za mkononi ni vema wakafuatilia kupitia Airtel Tv.

Meneja  Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jakson Mmbando (kushoto) akizungumza  na Watanzania  kupitia kipindi cha XXXL  kinachorushwa na  Radio ya Clouds Fm. kulia Meneja  wa Chapa ya Airtel  Anord Madale.
Meneja  wa Chapa ya Airtel  Anord Madale akifafanua Jambo kupitia kipindi cha XXXL kinachorushwa na Radio ya Clouds Fm.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...