Njombe

Watuhumiwa 17 wa matukio ya utekaji wa magari na uporaji wa fedha na mali kwa kutumia silaha mkoani Njombe wamekamatwa baada ya kufanyika msako mkali uliohusisha Makamanda kutoka mikoa ya Njombe,Ruvuma Songwe,Iringa na Mbeya.

Sambamba na kuwanasa watuhumiwa wa ujambazi wanaohusika na utekaji wa magari katika msako huo,vikosi vya polisi vimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine 70 wanaodaiwa kuhusika na matukio ya wizi na uvunjaji majumbani ambapo katika uchunguzi wa awali imeonekana wengi wao wanatoka mikoa mingine kuja kufanya kazi kwenye makampuni ya wachina ya ujenzi wa barabara.

Akitoa taarifa ya matokeo ya operesheni iliyofanyika katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja na vikosi vya polisi wa mikoa hiyo,Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah anasema katika kundi hilo la majambazi 17 kuna wanawake watatu waliokuwa wakishirikiana nao kuweka mipango huku Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga akisema katika uchunguzi wa awali wamebaini ongezeko la matukio ya kihalifu mkoani Njombe umetokana na uwepo wa fursa nyingi za uchumi.

"Tulibaini kuwa wageni ndio waliokuja kufanya uhalifu na walikuja kufanya kazi katika kambi ya wachina na kuna mwenyeji alikuwa amewahifadhi sasa kulikuwa na hali ya kutoelewana baada ya vitu vilivyoibiwa kuviweka sehemu tofauti,Hawa wahalifu 17 waliokamatwa wengi wao ni waliokuja kuomba kazi za udereva lakini kazi zinapochelewa wanaamua kufanya kazi nyingine"amesema Hamis Issah RPC Njombe

Aidha Makamanda wamesema imekuwa jambo rahisi kuwanasa watuhumiwa kwasababu baada ya kutekeleza matukio ya uhalifu walizurumiana fedha na kuanza kugombana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...