Na Anthony Ishengoma


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ameimbia kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kuwa Wizara yake inakuja na mageuzi makubwa ya tehama kwa lengo la kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi ili serikali iweze kuongeza mapato yake kupitia kodi hiyo.   

" Tunaenda kuwa na mageuzi makubwa kwa upande wa tehama kwa kuwa Wizara sasa inapitia mifumo upya ili wananchi waweze kupata ujumbe kwa njia Simu kama njia rafiki ya ukusanyaji mapato."Alisema Dkt.Angeline Mabula Waziri Wizara ya Ardhi.

Waziri Mabula amesema hayo leo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii inayokutana leo kujadiliana  kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa hata kabla ya bunge la bajeti kuanza baadhi ya wananchi wataanza kupokea ujumbe mfupi kupitia mitandao ya simu kuhusu makadirio ya kodi ya pango la Ardhi.

Waziri Mabula aliongeza kuwa zoezi hili liko mbioni kukamilika kwani timu ya wataalamu wa tehama iko kazini na wananchi wataanza kulipia kama zilivyo bili za maji zinazotolewa na mamulaka za maji hapa Nchini.

Akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge hao Waziri Mabula amesema azima ya serikali ni kuimarisha usalama wa milki kwa kuhakikisha kila kipande cha Ardhi nchini kinatambuliwa,kupimwa na kumilikishwa na hivyo kudhibiti Migogoro ya matumizi ya Ardhi.

Waziri Mabula aliongeza kuwa hatua hiyo itawezesha kukua kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.

Aidha Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa Wizara yake imeendelea kufanyia kazi mapendekezo na ushauri vilivyotolewa wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi jijini Arusha na kuwapongeza kamati kwa jinsi ushauri wao unavyo unavyowezesha kufikia malengo ya Serikali.

Waziri Mabula amewasilisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi fungu 48 na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi fungu 3 kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambayo yanajumuhisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2022/23 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akiwasilisha Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.Baadhi ya Wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakimfuatilia kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula wakati akiwasilisha kwao Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...