Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema kwa sasa hakuna chama chochote cha Siasa au Mtu yeyote aliye na uhitaji mkubwa wa Katiba iliyo bora na yenye manufaa kwa Watanzania kuliko CCM.

Ndugu Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipowasili wilayani Mufindi mkoani Iringa akizungumza na Wanachama,wafuasi wa chama hicho pamoja na Wananchi  ikiwa ni Siku ya kwanza ya Ziara yake ya Siku 7 inayolenga kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi za Shina, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi

"Nimesikia sikia huko watu wanasema sema kuhusu katiba mpya, labda niwaambie tu kwamba CCM tunahitaji katika iliyobora kuliko mtu yoyote yule, ndio Maana Chama cha Mapinduzi kimempa ridhaa na dhamana mwenyekiti wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuanzisha mchakato wa mapitio kuhusiana na suala la Katiba mpya" amesema Chongolo.

Katibu Mkuu Ndugu Chongolo amewasili Mafinga, wilaya ya Mufindi mkoani Iringa tayari kuanza ziara ya siku 7 akiwa ameongozana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akizungumza mbele ya Wanachama,wafuasi wa chama hicho pamoja na Wananchi (hawapo pichani) alipowasili wilayani Mufindi mkoani Iringa kuanza ziara yake ya Siku 7 inayolenga kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi za Shina, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi
Katibu Mkuu NDudu Daniel Chongolo akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kimila waliofika kumpokea jioni ya leo Wilayni Mufindi
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akizungumza jambo kulia kwake ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Gavu.
 Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi Gavu akiwasalimia baadhi ya Wanachama wa CCM na Wananchi waliofika kuwapokea.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Chongolo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Isimani Mhe,William Lukuvi pamoja na wageni wengine
katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo  akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi ,Daud Yasin mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama hicho Wilayani Mufindi mkoani Iringa jioni ya leo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...