THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


There was an error in this gadget

SHUKURANI NA MISA YA KUMALIZA MSIBA

MAREHEMU RICHARD AZZA MGAYA 
04. 04 , 1939 - 22. 05,  2015. 

Familia ya Marehemu Mzee Richard Azza Mgaya inawaarifu ndugu, jamaa, marafiki na jirani kwamba shughuli ya kumaliza msiba itafanyika Jumapili hii ya tarehe 02 agosti, 2015 nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha.
Misa ya shukurani na sadaka itaanza saa tatu za asubuhi na baadaye chakula cha mchana.
Familia inatoa shukurani kwa wote walioshiriki kikamilifu katika shughuli za mazishi toka mwanzo hadi mwisho wa kumuweka kwenye nyumba yake ya milele. Familia inasema haina cha kuwalipa zaidi ya kusema AHSANTE SANA kwa yote na Mola awajaalie afya na uzima zaidi.

SISI TULIMPENDA, LAKINI BWANA ALIMPENDA ZAIDI.
HIVYO JINA LAKE BWANA NA LIHIMIDIWE - AMINA

Marehemu Mgaya atakumbukwa daima kama  Mfanyabiashara maarufu aliyekuwa akimiliki duka pekee lilikokuwa linauza bidhaa zitokanazo na maliasili za wanyama pori  kama vile pembe na ngozi pamoja na vinyago. Duka lake lilikua mtaa wa Samora wakati huo ukiitwa  Independence Avenue na duka lake likiitwa National Trophy and Carvings Co Ltd. 


BBC DIRA YA DUNIA KUTOKA LONDON - IJUMAA


WAZIRI WA UJENZI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA TENGERU-SAKINA (KM 14.1) ITAKAYOJENGWA KWA NJIA NNE MKOANI ARUSHA

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Patandi wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya kukagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akizungumza na wakaazi wa Patandi, Sangis na Tengeru kuhusu ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS  Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Barabara ya Arusha bypass km 42.2
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akizungumza na wakazi wa Patandi mkoani Arusha kuhusu ujenzi wa barabara ya Tengeru-Sakina utakaojengwa kwa njia nne.
 Wakaazi wa Patandi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla hiyo. 

Sehemu ya barabara ya Tengeru-Sakina katika eneo la Patandi ikiwa imeanza kufanyiwa ukarabati utakaohusisha ujengwaji wa njia nne kwa kiwango cha lami.Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi


MKURUGENZI MTENDAJI WA 8020 FASHIONS SHAMIM MWASHA ATOA MADA NAMNA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA MANUFAA KWENYE SEMINA YATAASISI YA MANJANO

Mkurugenzi Mtendaji   8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekhar Nasser
Washiriki wakimsikiliza Kwa Makini Mentor Shamim Mwasha aliyetoa Mada kwenye semina hiyo Namna ya Kutumia Mitandao ya Kijamii kwa Manufaa ya Maisha yetu ya Kila siku na Kucha Kupoteza Muda Kwenye Mitandao ya Kijamii Bila Manufaa yoyote. 
 Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi  ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser AkitoaMafunzo  kwa njia Vitendo kwa Washiriki wa Semina hiyo yenye lengo la Kumsaidia Mwanamke wa Kitanzania Kudhubutu Kujikita Kwenye Biasha ra hususani Kwa Kutumia Vipodozi Pekee  vinavyozalishwa na Shear Illusion vya Luv Touch Manjano.
Washiri Wakiwa Pamoja Mra baada ya Kumaliza Mafunzo kwa Njia ya Vitendo. Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania
CHAGUA AMANI RAI KATIKA KURA ZA MAONI SINGIDA MJINI

Chagua Amani Rai Jimbo la Singida Mjini.


USIKU WA HERIETH PALLANGYO ULIVYOFANA

 Biharusi mtarajiwa Herieth Charles Pallangyo akiwa kwenye pozi muda mfupi kabla ya kuanza tafrija yake maalum ya kugana na familia yake kbla ya kufunga ndoa. Tafrija ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika ukumbi wa Giraffe Sunset, Mbezi Beach Dar es Salaam. Production by: MD Digital Company +255 717002303, +255 755 373999.
 Herieth akiwa katika pozi la picha na mama yake
 Wazaa chema Bwana na Bibi Charles Pallangyo wakiwa katika pozi.
 Wageni waalikwa wakiwa ukumbini hapo. PICHA ZAIDI HAPA


Simba Imeshinda katika mchezo wake wa Pili wa Mazoezi dhidi ya Timu ya Black Sailor kwa mabao 4--0

Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Black Sailor, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 4--0
Mchezaji wa timu ya Black Sailor akiwapita wachezaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki.
                    Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Rished Bade:Sheria mpya ya kodi kuwanufaisha wafanyabiashara


TANZIA- MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA AFARIKI DUNIA


                                                Marehemu SACP Aneth Laurent  enzi za uhai wake

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza - SACP Aneth Laurent kilichotokea jana Julai 30, 2015 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba ambapo mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwa ndege kutoka Mwanza kuja Jijini Dar es Salaam na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
                    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya 
Marehemu mahali pema peponi Amina.


AZAM YAINGIA FAINALI YA KAGAME 2015, KUCHEZA NA GOR MAHIA

 Beki wa Azam FC, Abbas  Mudathir Yahya akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa timu ya KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akichuana na beki wa KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Beki wa Azam FC, Agrey Morris akichuana na beki wa KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia) akimtoka beki wa KCCA, Ochaya Joseph katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Azam FC, Agrey Morris akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa KCCA, Habib Kavuma katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


GOR MAHIA YATINGA FAINALI YA KAGAME CUP

 Kikosi cha timu ya Khartoum ya Sudan kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo. Gor Mahia inaongoza kwa magoli 3-1. (Picha na Francis Dande)
 Wachezaji wa timu ya Khartoum wakishangilia bao.
 Mashabiki wa Gor Mahia wakishangilia timu yao.
 Golikipa wa timu ya Gor Mahia, Boniface Oluochakiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mashabiki wa Gor Mahia wakishangilia timu yao.


USIKOSE KUANGALIA GEMU LA NGAO YA HISANI JUMAPILI HII KATI YA CHELSEA NA ARSENAL KUPITIA DSTVFOMU ZA WAGOMBEA URAIS ,UBUNGE PAMOJA NA UDIWANI KESHO-LUBUVA

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu juu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi,Clothilde Komba.
 Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu juu  jeshi la polisi lilivyojipanga katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii) 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti 21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva  amesema wakati wa uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.
Lubuva a amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watu wengine.
Amesema kwa fomu za ubunge ni sh.50,000  na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa  wanasiasa wanatakiwa  na lugha za kistaarabu katika mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo.
Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana  na usalama hivyo jeshi limejipanga katika ulinzi katika kipindi hiki.
Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha uchaguzi.


LIFT........BALOZI DR. MAHIGA DAWA SI KUHAMA CCM ASEMA YEYE NI MKOMBOZI WA CCM IRINGA MJINI.


Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini.

Na matukiodaimaBlog
ALIYEKUWA balozi wa kudumu  wa umoja  wa mataifa (UN) na mgombea urais katika mchakato  wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM amewashangaa makada  maarufu wa chama  hicho  walioshindwa katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia  watanzania na kuwa watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .

Balozi Dr Mahiga  alisema kuwa wana CCM hao  walioanza kuhama chama  kwa kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali  walikuwa wawametanguliza  maslahi yao mbele na  kuacha kuangalia maslahi ya Taifa na chama hivyo ni vema watanzania  kuwatazama kwa jicho la tatu na ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa  viongozi  wao.


ASKARI WA TANAPA ASHINDA TUZO YA ULINZI WA FARU BARANI AFRIKA

Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Daraja la Pili,Malale Patrick Mwita akiwa ameshika Tuzo na Cheti alivyokabidhiwa na Mwana wa Mfalme Albert wa Pili wa Monaco nchini Afrika Kusini wiki iliyopita katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tanapa jijini Arusha.
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akitangaza ushindi wa Tuzo hiyo akiwa na maafisa wa Shirika hilo  ambao wana jukumu la kuhifadhi maliasili kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akitangaza ushindi wa Tuzo hiyo ambayo imeipa heshima Tanzania katika mapambano yake dhidi Ujangili nchini.


FILIKUNJOMBE; MAFISADI WAMETUMA WATU WANING'OE UBUNGE NAOMBA WANANCHI WANYIMENI KURA

mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe kulia akiwa na mlemavu wa ngozi (ALBINO) mara  baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za ubunge 

Na Matukiodaima Blog Ludewa
WAKATI wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM)  kesho   wanashiriki  zoezi la kupiga kura  za maoni kuwapata  madiwani na  wagombea  watakao gombea kwa CCM ,mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru wanachama wa CCM  katika jimbo hilo kwa kuonyeha  imani kubwa kwake  ukilinganisha na wagombea  wenzake  wawili na kuwa hadi  sasa anauhakika mkubwa wa kushinda tena ila ushindi utakaompa heshima ni ule wa kupata kura zote na wenzake kuambulia patupu

Filikunjombe  aliyasema hayo   wakati wa mkutano  wa kujinadi kwa  wagombea wa nafasi ya  ubunge katioka kata ya Ludewa mjini ,kuwa hadi  sasa kutokana na mapokeo  ya wananchi na  wana CCM kote walikopata kupita kwenye kata 26 za  jimbo hilo la Ludewa wamekuwa wakitamka  bayana kuwa kura  zote kwake  hivyo  kuwaomba wana CCM kwa umoja  wao kumpa moyo zaidi wa kuwatumikia tena kwa kuhakikisha  wanampatia kura  zote za ndio.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.


SHEIN AANDAA MIPANGO NA SERA ZA KUSAIDIA VIJANA ZANZIBAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ( Pichani)amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mipango na sera nzuri za kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri wenyewe hasa waliojiunga katika vikundi vya ushirika na SACCOS.

Dk. Shein alisema kuwa Serikali imeanzisha Mfuko wa kuwawezesha Wananchi Kiuchumi na tayari watu kadhaa wameanza kufaidika na Mfuko huo sambamba na kuwapatia mafunzo ya kitaalamu pamoja na kuvipatia vikundi vya ushirika mbinu za kupata masoko na kuwawezesha kuwa wajasiriamali wazuri.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Dk. Shein Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum, Mhe. Haji Omar Kheir, aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Jumuiya ya Watazania Wasio na Ajira (TUEPO) huko katika ukumbi wa afisi za Jumuiya hiyo Rahaleo, mjini Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa katika kuwasaidia vijana walioshindwa kuendelea na masomo yao, Serikali imeyaimarisha mafunzo ya elimu ya amali katika vituo vya amali vya Mwanakwerekwe na Mkokotoni Unguja na Vitongozi huko Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.


TRA YAWAPIGA MSASA CTI JUU YA SHERIA MPYA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI YA MWAKA 2014

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiongea na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel Nyantahe akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa uamuzi wa kuwakutanisha wadau wa sekta ya viwanda na kuwaelimisha kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ili kuweza kuondoa utata kwenye baadhi ya maeneo yaliyo katika sheria hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga akimueleza Jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akiwaeleza jambo baadhi ya wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA HASSAN SILAYO -MAELEZO


BREAKING NEWSSSS !!!!!!! KESI YA IPTL DHIDI YA KAFULILA YATUPWA NJE.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi namba 301 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila kwa madai kuwa Kafulila alichafua jina kampuni hizo na muhusika huyo kwamba walichota zaidi ya 300bn kwenye akaunt ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na taratibu.

Katika shauri hilo, Kampuni ya IPTL,PAP na Herbinder Singh Sethi walitaka Mahakama imuamulu Mhe Kafulila alipe fidia ya 310bn kwa kuchafua jina la kampuni na mkurugenzi huyo.

Katika kesi hiyo Mhe Kafulila alikuwa akitetewa na taasisi za kisheria za Legal& Human Righ Centre pamoja na kituo cha Human Righ Deffenders.

Akitoa uamuzi huo mbele ya mawakili wa Human Right Defenders na Legal & Human Right Center wakiongozwa na wakili Mtobesya huku mawakili wa IPTL, PAP na Sethi wakiwa hawakufika mahakamani, Jaji Rosemary Teemba alisema Mahakama Kuu imejiridhisha kwamba kampuni ya IPTL, PAP na Mkurugenzi wao Harbinder Sethi hawakuwa na hoja za msingi kuthibitisha madai yao kama msingi wa kufungua kesi mahakama kuu na hivyo kwa kuzingatia hali hiyo Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam inatupilia mbali shauri hilo kuanzia.


UGANDA:MBABAZI KUWANIA URAIS NJE YA CHAMA CHA NRM

Waziri mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani.


Mbabazi ametangaza hilo muda mchache uliopita akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala.

''kamwe sitatoka NRM''.
''Lakini sitaweza kugombea urais katika tikiti ya chama hicho cha NRM ilihali vipengee vingi tu vya vya chama vinakiuka katiba ya nchi''.
'' sitawania urais kwa tikiti ya NRM lakini wakati wa uchaguzi nitawania urais'.

''kama mwanzilishi wa chama ,wakili na mwananchi Mzalendo,sitajiingiza katika maswala yanayokiuka sheria''NRM sharti ijipige msasa''Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo.

Mwenyekiti wa jopo la kuchagua viongozi wa chama hicho bwana Tanga Odoi alikuwa ametanga ijumaa tarehe 31 (leo) kuwa siku ya mwisho ye kurejesha fomu za uwaniaji nyadhfa za chama hicho.

Mbabazi anasemekana kuwa alitembelea makao makuu ya chama tarehe 16 akikusudia kuwasilisha ombi lake lakini akakurupuka akidai kuwa gharama ya juu iliyowekwa kwa wagombea itawanyima maskini uwezo wa kuwania nyadhfa katika chama hicho.

Mbabazi alikuwa ameahidi kumpinga rais Museveni kama mwenyekiti wa chama na hivyo mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Mpinzani wake rais Museveni anatarajiwa kurejesha fomu zake mwendo wa saa sita adhuhuri.

katika makao makuu ya chama, wafuasi wake wamemiminika wakiwa wamevalia rangi za chama wakiimba nyimbo za kumsifu.