September 2005

Ni ajabu na kweli. kuna kuku hapa tz wanaolea bata. ukiwa dar tembelea bamboo bar, kinondoni kwa John Fedha, utajionea. kwa mujibu wa uchunguzi wangu, jirani ya bar hiyo kuna jamaa anafuga kuku na bata. huwa anachukua mayai ya kuku na kuyaweka kwenye kiota cha bata ambaye anayaatamia hadi kutotoa. ujanja utumikao ni kwamba kwa vile uatamiaji wa kuku huchukua siku takriban 14, wakati bata ni siku kati ya 29 na 40, jamaa hukadiria muda wa mayai ya bata na kuyaweka chini ya kuku ambaye, baada ya kutotoa, hujua ni vifaranga vyake. na huvilea kama vitoto vyake, na ni mkali kama kawaida ukivisogelea. ni sayansi nyepesi lakini yenye kuhitaji ubongo na uvumilivu.

Nani kasema bongo tumechacha? na simaanishi kuwa na gari ni utajiri, ila utitiri wa ma-long stretch (kama hili White Lincoln la Iddi Jangua) yapo kibao na yanatia kiwewe hata donors wanaoituta wa nne toka chini kwa umaskini. haya, mjadala naufungua, leta maneno...
no image
Hi everybody!

Mi ndo nimeishaingia bongo na kukuta mambo yote poa. poa kwa maana ya kwamba kampeni zimepamba moto na kila mtu anaongoelea uchaguzi ujao. nilipokuwa helsinki washkaji waliomba picha za miss tanzania mpya na aliyepita. kwa hiyo nawapatia washindi wa tatu wa kwanza na pia miss tz 1999 hoyce temu ( anayesoma marekani na alikuja mwanzoni mwa mwezi, na keshaondoka), miss tz 2004 faraja kotta pamoja na taji.
no image
Mamboz?

Naandika nikiwa nina masaa machache kabla ya kupaa kurudi bongo 11/09/05 ambapo naambiwa niamke saa 11 alfajiri (urgh!) kuwahi pipa. Hata hivyo nafurahi kusema kwamba nimepata faraja kukutana na wabongo kibao waishio helsinki, ambao wote si wabangaizaji kama nilivyodhani, wote wanafanya kazi za maana na heshima. Bravo 2 u guys! Shukrani za pekee ziende kwa fide tungaraza, dennis londo, stephen lyabandi, kisa kisa (?) kiwala, eric kilala, beni kakengi, magonela malima, ray mtafungwa na tiko mwalukasa waliotupa taff pale chelsea club, helsinki. mie niliingia mitini wakati fulani kutokana na mwaliko mwingine sehemu ingine (unajua tena ukiwa supastaa - hahahaaaa!) na kushindwa kurudi mahali pale ambapo nilifurahi ila tu sema ningefurahi hiyo klabu ingekuwa liverpool kwani mie ni "neva wok aloni" damu.

Vinginevyo, alamsiki ya kuonana. nasema tena mtu akitaka kuona snepu yoyote ya bongo anibonyeze tu!

Chaaaaooo!

Rais wa Finland akisalimiana na mtanzania Ismail Abdulnuru Suleiman wa NGO inayoshughulikia elimu ya ukimwi kwa watoto iitwayo Watoto Salama ya Dar, pamoja na Bi. Hope Gabone wa NGO ya Mwanza iitwayo Kuleana, wakati wa uzinduzi wa juhudi za kuchangisha fedha kuzisaidia NGO hizo leo katika viwanja vya Esperance hapa Helsinki. Kiasi cha Euro 500,000 zinatarajiwa kupatikana kutoka katika michango hiyo inayoratibiwa na Operation a Day's Work ya Finland.


sura tanashati za watanzania waliohudhulia mkutano wa utandawazi wa helsinki mara tu baada ya mkutano huo kufungwa rasmi leo. mtafute mwana mfalme wa blogu alipo. mbele wa pili kushoto ni katibu mkuu wizara ya kazi, vijana na michezo, abubakar raja, balozi wetu misri kassim mwawado (nyuma yake) akifuatiwa na balozi wetu ethiopia Mzee mangachi, nyuma yake ni balozi wetu india mama eva nzaro, wa kulia mbele ni mwanaharakati na kiongozi wa tango (mwavuli wa ngo bongo) maria shaba. mimi simo kwa kuwa nilikuwa nasnepu
no image
hatimaye kikao cha utandawazi cha heksinki kimemalizika na tanzania na finland zimeahidi kuendeleza libeneke la utandawazi kwa miaka miwili ijayo. pichani ni ujumbe wa tanzania. mie simo kwa vile ndo niliepiga picha. au vipi. lakini rasta unaziona upande wa kushoto? hudhani ni za ndesanjo...

Not everyday you get snugged by gorgeous gals but that's exactly what ndesanjo and i have just bumped into during tea break at the helsinki process conference. miss tanzania 2000 angela damas (right) and miss university 2005 felista rugambwa were the beauties. oh, no! no! there is nothing between the lines here. like us, the two they have been invited to attend the conference in their capacities as youth leaders back home.

Jamani nimejiunga kwenye gari hili la blogu. Tusionane noma. Leteni vituz. Anayetaka masnepu ya bongo aseme tu atapata. Muulizeni Ndesanjo ambaye ananifungulia hii blogu tukiwa pamoja Helsinki kwenye mkutano huu hapa. Picha hii kapiga dada mmoja hivi...sijui anaitwa nani. Picha hii ni kwenye tafrija fupi ya kunipokea ndani ya jengo la Finlandia Hall.