mwaikumbuka siku hii?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hivi huo udongo uko wapi? Nasikia siku watu wanauliza kama kweli udongo ulitoka Zanzibar au wote ulitoka Tanganyika.

    Kuna documentary iliytongenezwa juu ya Muungano?

    ReplyDelete
  2. Muungano ni ridhaa, twataka hati hadharani. Picha hiyo haitoshi ili kutoa utata.

    ReplyDelete
  3. Kwa anayewafahamu hao kina mama wawili naomba anisaidie majina yao.

    ReplyDelete
  4. Sitaki kuwa mchokozi, lakini nadhani ingekuwa bora kama Mzee Karume angeshika kibuyu chenye undongo wa Zanzibar halafu Mwalimu aangeshika kibuyu chenye udongo wa Tanganyika halafu wote wangemwaga huo udongo/mchanga ndani ya bakuli kwa wakati moja.

    ReplyDelete
  5. kwani mzee Karume hapo si aliishakufa? sio kwamba aliyehusika na hilo zoezi alikuwa ni Jumbe - raisi wa pili wa visiwa?

    hapo wazee walizua utata unaosumbua hadi leo. wameenda shule bado wakatuzeveza kumalizia mambo kwenye udongo?

    huyo mama mmoja anaweza kuwa maria nyerere?

    ReplyDelete
  6. mark msaki,

    Hiyo picha si ilipigwa kwenye Muungano 1964? Mzee Karume aliuwawa 1971. Au nimekosea?

    ReplyDelete
  7. hakuuwawa 72? ok nimeelewa, ina mana basi muungano ulikuwepo kabla ya kuzaliwa CCM...ya sawa.. karume hakuwepo 77 wakati CCM inazaliwa!

    ReplyDelete
  8. Muungano ni swala la nchi mbili kukubali kuunganisha mamboyao yote na kuwa kitu kimoja.Leo hii serikali ya zanzibar ina Rais wake na bendera yake Tanzania inabendea yake na rais wake,watu walioingia darasani wataelewa dhika kuwa hakuna muungano kati ya Zanzibar na Tanzania labda wangeliita shirikisho(federal)ambapo kila nchi ina sheria zake na srikali yake isipokuwa wanaungana kwenye maswala kadhaa ambayo wanayashughulikia kama serikali moja,lakini kwa mtindo uliopo huu ni utapeli wa viongozi wetu,na kama viongozi wetu ndo matapeli namba one tusishangae kuwa hayamkini hata raia nao wataiga kutoka kwa wakubwa wao.
    Hilo ndo linalokufanya ujiulize udongo ulitokea wapi,hilo ndo watu wanahoji makubaliano yalikuwa je na wapi mkataba wa kushirikisha nchi hizo.Wazo kubwa ninalopata hata ni kwamba wakati huo mwalimu Nyerere alikuwa ame graduate makerere na edinburgh.wakati huo huo mzee Karume alikuwa ndo ametoka tu kwenye ubaharia (sea man)sasa mwalimu alimzidi kete mwenzie lakini sikuzote ukidanganya leo jiandaee kudanganya na kesho ili kuufanya uongo wako uonekane si sahihi,hilo ndilo tunaloliona sasa mwalimu hayupo aliye chora laini hii ya uongo sasa hawa wengine wanashindwa waanzie wapi na hawana mbinu ya uongo matokeo yake wanajitafuna watu wanapo hoji swala hili.Lakini yote haya ni matunda ya Siasa,maana hata neno lenyewe walilibadilisha neno halisi lilikuwa (sihasa wao wakatoa h na kubakia siasa)kwenye kiswahilisanifu sihasa linaeleweka je siasa maana yake nini(kwa kuwasaidia wale ambao hawajasoma political science,siasa ni uongo uliokoma na kugeuka kuwa ukweli).

    ReplyDelete
  9. huyu mzee wa upande wa kushoto katika picha hii ni nani

    ReplyDelete
  10. Imekuwa ni kawaida ya SPOILERATL ku-alert jamii kila anapoona jamii inapotoka.Kama mnakumbuka SPOILERATL aliweka bayana kwa kichwa cha habari "BASTOLA YAWA FASHION ATL" hii yote ikiwa kuionya jamii na kumpa kila mtu attention na ya nini kinachoendelea kutokea baina yetu.
    SpoilerAtl kutokana na umri wangu kuwa miaka ya kati kati inakuwa rahisi zaidi kujichanganya na watu wa age zote katika kupata habari.Nilileta Topic hiyo kutokana na vijana kadhaa kununua BASTOLA ,kana kwamba hiyo haitoshi wamekuwa wakija nazo hata sehemu za vilevi.
    SPOILERATL kwa kujitoa kafala niliweza kusimama na kukemea fashion hiyo ya kuwa na BASTOLA ambayo inaonekana kuvutia vijana wengi.Hakuna aliyeungana na mimi kukemea hilo na badala yake watu uwa wanastushwa na vifo ambavyo vyanzo vyake viko wazi.
    Ni vipi tutaepukana na kifo kama cha mazula na Nkya hiyo hatujui !!Sasa hata hivi ambavyo tunaona dalili zake mbona hatufanyii kazi?Hawa vijana wamenunua hizi BASTOLA kwa kuleta utemi baina yetu au "self defence"???Na jibu ikiwa moja kati ya hayo ni vipi BASTOLA hizo zinakuja sehemu za vilevi(Pombe)?SPOILERATL anapofanikiwa kuziona BASTOLA hizo ni kutaka afikishe ujumbe kwa jamii au vilevi vinakuwa vimeanza kazi yake?
    Naomba jamii iangalie suala hili na kila mmoja atoe maoni yake kuhusu hilo, majina ya vijana hao wanaotembea na maisha ya watu viunoni tunayo!!cha muhimu ni kujadili ni vipi tu dili nao na sio kutaka kujua majina yao wenye mawazo endelea

    ReplyDelete
  11. Spoiler-Atlanta, hii topic yako ni nzuri ila inapotosha mtiririko wa maoni ya watu kuhusu hiyo picha hapo juu.
    Kaka Michuzi iweke hii topik ya spoiler kwenye fresh page ili idiscussiwe huko. Samahani kama ntakuwa nimemkwaza muhusika. Ahsanteni.

    ReplyDelete
  12. brother michuzi nipe kinafasi kuwafikishia ujumbe ,si unajua blog ya yako ni WORLD WIDE sema jina lako tu michuzi ndio linakuangusha maana wachina wengi wanashindwa kuiangalia kwa sababu wanashindwa kulitamka!!!
    Asalaam Alyekhum!!!!
    Baada ya vuta nikuvute ya nini kifanyike ili party ya IDD MOSI isiwe inaenda kinyume cha dini sasa RUKHSA.SpoilerAtl nikiwa katika angle ya kuobserve nilifanikiwa kupata muaafaka huo ambao uliwajumuisha wakali wa dini na wakali wa party.
    Mjadala ulikuwa mkali pale wakali wa dini walipokuwa wanapinga kufanyika kwa party hiyo kwa tetesi kwamba ni HARAMU.Wakali wa party nao walisimama kidedea kwa kuwa na pointi nyingi tu za kutetea hoja yao hiyo.
    Hitimisho ya yote SpoilerAtl alifanikiwa kuona viongozi wa mjadala huo wakipeana mikono kwa maafikiano.Spoileratl nilifarijiwa na kwa hitimisho moja lenye maelewano ya pande zote mbili.Kwa kauli moja pande zote zilitangaza party ya IDD MOSI is official announced.
    Deep South Alabama ,N/S carolina ,Tenesee na Georgia tushiriki katika hili.Michango inaombwa iwakilishwe before next Sunday.Swali lolote uliza hawa wafuatao kwa simu 24/7
    MR.HASSAN TELL:404 663 5050
    MR.SAID CHAMBUSO TELL:678-687-0259.
    SISTER ASHURA TELL 404 455 7673.
    SISTER AMALU: 678 612 1681.
    SISTER AMINA: 404 547 7800.
    SISTER sens***:678 768 5530.
    SISTER ZAHARA(LINDA):678 689 7860
    Ni desturi ya watanzania kusheherekea sikukuu pamoja ,wenye dini nyingine na wale wasio na dini nao mnakaribishwa.Mawazo ya jinsi gani tufanikishe sherehe hii au nini maoni yako katika hili Rukhsa!!

    ReplyDelete
  13. Katika Hali Inayoonyesha Kusikitisha Wengi,Minong`ono ya Hawa Na Sisi Imezidi Kuwa Mingi .SpoilerAtl Akiwa Safarini Katika State Mojawapo Hapa USA Aliona Tofauti Hiyo Kubwa Ya UBARA Na UZANZIBAR.Huku Wabara Wakiwarushia Mawe WANZIBAR Kwa Kujiona Waarab(Next To Mzungu).Na Wanzanzibar Wakiwaona WABARA Ni Mijitu Ya Fujo Fujo Isiyo Na Dini Na Ustaarabu.
    SPOILER Nilipokuwa Dadisi Kujua Nini Kina Cha Tofauti Hiyo Ktk State Hiyo Mabishano Yalikuwa Makubwa Na Tofauti Zikazidi Kuongezeka.
    Wale Wanaosema Wazanzibar Wanajiona Wao Kama Waarabu Hivyo Kuwa Next To Mzungu,Changia Hoja Kwa Kutoa Udhibitisho.Na Wale Wanaosema Wazanzibar Wanaona Wabara Mijitu Isiyo na Dini Ambayo Haijastaarabika Weka Nondo Chini.
    Kwanza Sema Huko Wapi Na Eleza Wewe Uonavyo.........

    ReplyDelete
  14. Spoiler unachanganya mambo kama baadhi ya wengine kwenye hii blog. Ongelea point moja kwa moja na si kupindapinda. Tunaongelea Picha hapo juu na falsafa yake na si bastola wala mshale!

    Kwa ujumla sisi watu wa kizazi kipya tunaamini kabisa kuwa muungano huu ulikuwa na agenda yake iliyofichwa mpaka leo. Inawezekana kabisa hata JK hajui hasa ni nini kiini na siri ya huo Muungano. Ila kwa sababu amekunywa maji ya bendera ya CCM, basi lazima aimbe: "NITAULINDA MUUNGANO KWA NGUVU ZANGU ZOTE.... hata kama sijui maana yake". NI suala la time tu, huo MUUNGANO utabomolewa ili tuache na manung'uniko yasio na utaratibu ya upande mmoja. Zaidi ya kuelimika kwa kiwango cha juu sana, sisi "new generation" hatujawahi kuona hata sehemu moja ambapo panaonyesha kuwa MUUNGANO ni kitu cha muhimu na kujivunia kwa Watanzania. Tunachoona ni migogoro na malalamiko yasiyoisha miongoni mwa mwananchi wa upande mmoja wa MUUNGANO. Tunamsubiri kwa hamu sana "Gorberchev" wetu, labda anaweza kututoa hapa. Kwa hakika tunahitaji wao waende zao, na sisi tubaki zetu. USSR, YUGOSLAVIA, CHECKSLOVAKIA mpaka hapo juu ETHIOPIA yametokea na yakawashinda. Ndiyo IWE BONGO!

    ReplyDelete
  15. Tatizo la wa zenji kujiona waarabu kuliko waarabu wenyewe tunaliona hapa UK pia.
    Histori inatukumbusha Zanzibar lilikuwa ni soko la watumwa na wengi wa watu watokao huko ni mzao wa watu waliokuwa transit kupelekwa uarabuni kama watumwa ama watumwa waliobakwa na "ma master" wao
    Watumwa hawa walitolewa Tabora ,Mwanza ,Komoro nk
    Wakati bara tunawaona waarabu kama binadamu wenzetu kama walivyokuwa wahindi,wachina , wazungu nk
    Hii inasababisha tofauti kubwa ya mila na desturi baina yetu

    ReplyDelete
  16. mimi nafikiri msemo wa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu una maana kubwa sana,kwa mfano angalia jinsi USA ilivyokuwa hivi sasa hawa jamaa wanatawala dunia kwa sababu ya umoja wao [yaani united states of america] huu ni muungano wa vinchi kama hamsini na uchee, okay angalia germany hakuna tena mashariki na magharibi sasa hivi ni nchi moja, sasa mi nashanga sana wenzetu wanaimarisha miungano yao,sisi tunazungumzia kutengana huu ni upumbavu tu.waafrika tuungane tuwe united states of africa.

    ReplyDelete
  17. MICHUZI HAUPO MJINI??
    NAONA HAKUNA KINACHOENDELEA KWENYE BLOG, WIKI NZIMA NI HII PICHA TU, YA MWALIMU NA MUUNGANO.
    WATU WAMEKUKANDIA NINI?
    UKAAMUA KUCHUKUWA BREAK?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...