celtel wameniletea picha hiyo na ujumbe huu leo. kama mjuavyo mie inglishi yangu ni ya kudip hivyo someni halafu mnibonyeze wameongea nini...


Forest Whitaker (left) and Tanzania 's former president Benjamin Mkapa (right) at the Celtel sponsored Africa premiere of the Last King of Scotland. The premiere was held in Kampala on 17 February, one week before Forest Whitaker won the best actor Oscar at the 79th Academy Awards, held in Los Angeles 25 February 2007.
At the premiere the Ugandan president Yoweri Museveni paid tribute to the role of Tanzania in ousting former dictator Idi Amin in 1979. Forest Whitaker won the Oscar for his role portraying the late Ugandan dictator.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Mr. Ben Mkapa. Huyu ndo Raisi bwana. katika marais wa bongo, nadhani huyu alikuwa bomba sana. Hakuna kuchekacheka wala utani. Watu wanaangalia upande mmoja tu. Hawaangalii upande wa maendeleo ya barabara, shule, miundo mbinu pamoja na ukuaji wa miji na vijiji nchini.

    Mkapa, tunaku-mis sana. Umetufanye tuonekane watu Duniani. Challenge ni kwa mtalii uliyemwachia nchi. Sijui, lakini tunaendelea kumwangalia kwa makini.

    UBARIKIWE SANA

    ReplyDelete
  2. mlisho-nyuma:
    habari inasema eti celtel watatoa huduma bure za simu ndo maana mkapa amefurahi... (lost in translation?)

    ReplyDelete
  3. Anon wa hapo juu kabisa, mie enatofautiana nawe. Kweli aliibadilisha Tanzania, lakini wakati huo huo alituletea deal za ajabu ajabu ambazo mpaka leo ni kitenedawili. Unakumbuka deal ya TANESCO, Radar na zinginezo. Unajua jinsi panya anavyokula vidole na kupuliza? Haya!

    ReplyDelete
  4. Wewe anon unayeponda deal alizoleta bwm ni mfano wa wale watu wasioridhika hata siku moja. Hizi deal unazoponda zilimwezesha bwm kuzalisha maelfu ya ajira na kutuwezesha kuwa na foreign foreign reserves tunazotumia mpaka leo.

    ReplyDelete
  5. Anon number tatu hapo juu kukujibu shwala lako ni kwamba, usiangalie shillingi upande mmoja. Hayo matatizo hayakwepeki. Hata kama ni nyumbani kwako, ni vitu vya kawaida kutokea. Kinachotakiwa kwa wewe ni kujumlisha faida zote na kutoa hizo hasara (matatizo). Then ukiona faida kubwa ujue ndivyo ilivyotakiwa. Ukiona hasara (matatizo) mengi basi ujue amefanya vibaya. Lakini kwa hakika, huyu Mr. Benny si mchezo. Nimetaja vitu vichache tu hapo juu, lakini pia na msamaha wa madeni ambao sasa hivi ndo tunaringia kwa kuanzisha shue nyingi za secondary, aliweza pia ku-stabilise shillingi (muda wake wote TSHS haijawahi kuyumba hata mara moja), heshima ya wafanyakazi imepanda sana, foreign reserve iko ya kutumia 9 months.

    Tanesco alikuwa wameoza toka zamani. Kwa mfano, Badala ya kutangaza kuwa kuweka umeme ni bure ili wateja waongezeke kutoka 10% ya watanzania wenye umeme na kufikia angalau 50% ili mapato yaongezeke, wenyewe wanaongeza bei ya umeme. Makampuni ya simu kama VODA, Celtel na Tigo wamefanikiwa kuwa na wateja wengi namna hii. Kuhusu Radar ni politics tu. Mbona Ndege ya Rais anayotumia JK huisemi? Kwanini JK asiiuze basi?Blair, PM wa UK hana ndege ya serikali. Anapanda BA.

    Tuwe waangalifu wakati wa kujadili hivi vitu. Tulia na kuwa makini sana. Mr. Ben was the PRESIDENT.

    ReplyDelete
  6. We anon wa kwanza unamsifu mkapa kwa lipi???ivi haujiulizi kwanini saivi Kikwete amekua ombaomba???hana chakufanya bongo,sanasana apige kelele na rushwa pale bongo,majambazi,hakuna kingine zaidi,maana nchi Mkapa alishauza yote,sehemu ambazo tulitakiwa ndio tuziendeleze sasa kama vyanzo vya mapato,vimeuzwa. Angalia mfano Botswana, madini ilikuwa ni 40% inaenda kwa mwekezaji, na 60% kwa nchi,Hatupingi ubinafsishaji,ila ulifanywa bila kuzingatia masilahi ya nchi,nchi inapta asilimia tatu ya mapato ya madini,unamsifia Mkapa???watu wanasign dili moja ya kuuza kiwanda wanatoka na ten percent billions of Tshs???ndio unamsifu Mkapa,nyie hamuoni marais wanaohangaika na matatizo ya nchi yao hawanenepi kwanza???ebu ona Nyerere alivostaafu alikuwaje???angalia mkapa alivoingia madarakani na wakati anatoka madarakani amekuwaje???pale kichwa ilikuwa imelala ile,ndio maana saivi amekuwa kijeba cha mtu,napia ni tycoon fulani,anamiliki hotel south africa,yeye anaenda kuwekeza nje,wakati upande mwingine anasema watu wa nje waje kuwekeza Tz., haingii akilini hapo???. Wewe kama ndugu yake na mkapa au una undugu na mawaziri walioshiriki kusaini dili za ajabu bongo wakaneemeka,nakuwaacha watanzania wengi maskini usiseme amefanya la maana hapa,tulia hukohuko. Nchi ilizidi kuwa maskini wakati wa utawala wake,katika viwango vya umaskini vya dunia,nenda kijijini kule,zamani tulikuwa tukienda kijijini nakumbuka tulikuwa tunapewa mahindi,karanga,na maharage,ila kuanzia miaka ya 96,wazee walikuwa wanapeleka pesa kwaajili ya mbolea,kwaajili yakunua chakula kimewaishia walicholima,peleka pesa ya palizi,peleka pesa ya chumvi,sukari na mafuata ya taa,kila kitu kinatoka Jijini,we unasema mkapa ameleta maendeleo gani????,Leta hoja hapa,acha kuwa limbukeni wakuona viinimacho nakusema mkapa ameleta maendeleo.Wakati anaondoka madarakani nchi ilikithiri kwa ujambazi,matatizo ya umeme,njaa,rushwa,nawao kuuza nyumba za serikali,unasema ameleta maendeleo???tulia mtu wangu hujui ile nchi inavoendeshwa we kula pesa wanazopewa ndugu zako kwa rushwa,na subiri hukumu yako,siku ya kifo chako.

    ReplyDelete
  7. Forest Whitaker = charles hillary, mzee wa macharanga, jamani, don't they look alike, mie kabla sijasoma maelezo ya pic, kuona hiyo pic nikajua ni charles na mstaafu rais, wachangiaji mnasemaje, au macho yangu trakoma inaninyemelea nini... haha haa,

    nafikiri mkapa alifanya yaliyomema na yaliyokubalika kwa jamii, tumetoka mbali jamani kama hakuna mtu anaeona mabadiliko ya tz kwa kipindi chote cha mkapa basi hatuna shukrani,tz ya sasa sio tz ya miaka 10 au 15 iliyopita, nchi imebadilika kiteknolojia na hata kimaendeleo, nakubali yapo ambayo hayakukubalika kwa jamii vilevile but mtu hawezi kuwa perfect 100% sie si ni binadamu jamani, hata wakubwa wa nchi za nje wanavurunda pia, kwani hatujasikia kwenye vyombo vya habari waziri wa uk, tony blair alihojiwa na mapolisi tena mara mbili kwa kile walichosema chama cha labour kilipata fungu fulani la pesa sijui ni kwa mkono wa nyuma au vipi,

    hawa marais na mawaziri na viongozi wote kwa ujumla wenyewe sio 'mungu' jamani makosa yanakuwepo na jamiii inayaona, ndo mana kuna uhuru wa vyombo vya habari so tunavitumia vyombo hivyo kukosoa viongozi kwa lengo la wao kujirekebisha na kuona walivyoboronga.

    pongezi kwa pacha wa charles,

    ReplyDelete
  8. Naungana na Anon wa kwanza,Mkapa kajitahidi sana,tena sana.Sema tatizo alikuwa na huruma na watendaji wake,na hawa ndugu za mke wake.Maana tunajua hata ya NetGroup ilipita hivyohivyo.Ila Mkapa kama Rais kajitahidi sana kututoa alipotukuta.Kweli Hayati baba wa Taifa aliona mbali kumleta huyu jamaa.Mapungufu yake ni ya kibinadamu tu

    ReplyDelete
  9. Hivi, ukienda hotelini kuagiza chakula halafu mhudumu akakuletea chakula, utaenda kuwaambia watu jinsi ambavyo mhudumu amekuhudumia vizuri kwa kukuletea chakula ulichostahili?

    This is the point: Mkapa fulfilled his obligations, and we aren't obligated to sing praises. That's what he signed up to do. Full stop.

    Why are Tanzanians' expectations so low? Why aren't we even thinking of the baggage he left behind?

    ReplyDelete
  10. ISSUE YA RADA MKAPA ALIIKUTA, NDIO MAANA HATAGUSWA HUYO.

    ReplyDelete
  11. Na pia naungana na anonymous wa kwanza, mpaka sasa mimi namwona mkapa amefanya vitu vya nguvu. Alikuwa na maono ya mtu kutoka Kagera hadi Mtwara kwa TAXI, ila naona kwamba hayo yanafifia tu kila siku toka serikali ya awamu nne ilipoingia madarakani.

    Kinachonishangaza ni style ya hawa jamaa wapya jinsi ambavyo wanawaendesha wenzao kwa style ya kidikta huku wakiibatiza kasi mpya. Mimi sipendi jinsi Boyz 2 men wanavyochanachana ripoti za viongozi wenzao wa chini. Wanachotakiwa kufanya ni kupokea taarifa na kutolea maamuzi, lakini swala la kuwadhalilisha viongozi mbele ya wananchi ni kutafuta "cheap popularity"

    Ni lazima tushukuru kwamba pamoja na mambo, mengine lakini Mkapa alifanya vingi vizuri. Yeye ni mtu na ana mapungufu, ila kafanya mengi. Tatizo lenu ni kwamba mmejikalia huko ughaibuni na mmebaki mnafanya comparisons kwa kutumia huko mlipo.

    God bless Mkapa and Tanzania. I pray for the current leadership, so they may see you grace and wisdom. God we need results, and come out of this viscious cycle of poverty. AMEN

    ReplyDelete
  12. nawewe usituchanganye wote wa ugaibuni,tuko class tofauti brother Ben mungu amzidishie maisha marefu kurudisha hadi ya tanzania kimataifa na mengi mazuri aliofanyia nchi yetu,mikataba aliikuta mbona amjadidili alie muachia kiti acheni ukiritimba nyie.

    ReplyDelete
  13. Mpaka keshokutwa nacheka jinsi watanzania wanayopenda ushabiki wa ajabu ajabu tu. Mimi nampongeza Mkapa kwa kuwa kazi ya Urais ni ngumu sana. Wale mnaojidai kuimba 'Kikwete Kikwete' blah blah, tuone baada ya miaka kumi kama hamtakuwa na mambo ya kulaumu mengi tu pia. Point blank ni kwamba hii ni dunia hatuko mbinguni, kila rais na kila binadamu atakuwa na mazuri na mabaya, hata huyo JK atakosea mengi tu, na yeye mwenyewe pia ameshawaambia wananchi kuwa hawezi kupatia kila kitu, kwahiyo Mkapa was no different. If anything, Kikwete ana hazina kubwa sana kutokana na kujifunza kutoka kwa Mkapa, both good and bad.

    ReplyDelete
  14. Jaduong,
    Heko mtu wangu umefunga kazi. Tanzanians' expectations are so low. Uharibufi aliofanya huyu kifutu naamini iko siku moja atakuja kulipa. Unayesema ndege ya Rais unafahamu ni mara ngapi rais kaitumia kwenda kwenye ziara zake za kuvumbua dunia? Msinitie hasira miye.

    ReplyDelete
  15. Nyie wachangiaji wengi hapa mnaosema Mkapa kafanya la maana hakuna point,ni vibaraka tu wote nyie,mnaongea bila statistics???
    Acheni kusifia bure hapa,deni amesamehewa yap,na akakopa zaidi???Alipoingia madarakani,deni la TZ lilikuwa Dola billion 6,ameondoka deni ameacha limefikia dolla billion 8 ???mnasema nini hapo???. Nchi imerudi nyuma kwa viwango vya dunia kiutajiri,yaani imekuwa maskini zaidi,matatizo lukuki kwenye ile nchi aliacha,wanaondoka wamevimba na utajiri,kuanzia mahita,mboma,na sumaye pamoja na mkapa mwenyewe.Nyie mnasema amefanya cha maana kuwatajirisha hao wachache,ndio cha maana,kutuachia rushwa kubwa na ujambazi ndio cha maana???vijijini kuwa maskini zaidi ndio mnampa big up,kuporomoka kwa thamani ya shilingi,alipoingia madarakani 1995,ilikuwa dolla moja sawa na sh 480 alipoondoka ilikuwa sh 1120 ndio cha maana hicho???kuuuza nyumba za uma ndio cha maana???mnatoa credits za nini,leteni hoja hapa,sio mnajiongelea tu,kama vipi kaeni kimya.

    ReplyDelete
  16. Mungu akupe maisha Marefu BWM,wafanyakazi wa serikalini watu walikuwa wanatudharau sana,lakini tangu umeingia madarakani maisha yetu ni mazuri kupita kiasi hata hao wafanyakazi kwenye makampuni wanatutamani sana na wengine wanataka kurudi serikalini.Mshahara mzuri,Mkukuta tunapata,yaani we acha tuuu

    ReplyDelete
  17. Kaifanyia nini Tanzania kama siyo kiuza kwa wachukuaji.

    Kawaleta wachukuaji ambao hawataki kuwaajiri Watanzania kwa visingizio visivyo na misingi au kuwalalia pale wanapowaajiri.

    Kawaleta Makaburu Net Group Problems na kuwalipa mabilioni ya pesa na Tanesco wameiacha vibaya kuliko walivyoikuta.

    Kawaleta wachukuaji ili waendeshe TTCL, wakafanya wizi wa mali ya TTCL na kisha wakaanzisha kampuni yao ya simu, na kuiacha TTCL solemba.

    Kawaleta wachukuaji wa madini na kuwaacha wachukuaji hao kuchukua 97% na Wabongo tunaambulia 3% tu. Wakati nchi nyingine za Africa zinagawana 50% na wachimbaji.

    Katika mazingira ya kutatanisha mdogo wa mkewe Fred Maro ndiye aliyehusika na kuwaleta makaburu wa Tanesco, ndiye huyo huyo ka hali kutatanisha akapewa usimamiaji wa mali za TTCL.

    Akawabeza Watanzania walipopinga ununuzi wa rada kwa kuwa tulikuwa hatuihitaji na ilikuwa ya bei mbaya, leo ununuzi huo unanuka rushwa baada ya kubainika kwamba bilioni 12 zililipwa kwa mdosi.

    Haya yote hayakutokea wakati wa Baba wa Taifa au Mzee Rukhsa. Hata Baba wa Taifa kabla hajafariki alishaanza kumsemea hovyo kwa kuwa alikuwa anaweka mbele mawazo ya WB na IMF bila kujali mawazo hayo yangewaathiri vipi Watanzania.

    Fumbueni macho muone huyu Mkapa haikufanyia Tanzania chochote bali kazidi kuididimiza. Hizo ajira mnazosema kaongeza aliongeza wapi katika shirika la umma, wachukuaji ama la kusadikika?

    ReplyDelete
  18. nani wewe unasema Tony Blair hana ndege eti anatumia BA, acheni ujinga.

    Tony Blair visited a school in Bolton, before returning to London
    Prime Minister Tony Blair's election campaign plane has been struck by lightning during a flight.

    ReplyDelete
  19. Duuuh! Leo ndio nimeshuhudia watu vichwa maji humu kwenye hii blog. Watu wana chuki binafsi na wanashindwa ku-analyse mambo kwa undani. Mbona statistics zipo wazi kuwa Ben Mkapa amefanya mengi mazuri. Kukosea kiubinadamu ni mambo ya kawaida. Huyu bwana kama kiongozi alikuwa na washauri wake wa fani tofauti, kuanzia uchumi mpaka ufundi na sheria. Kuna wakati kama kiongozi unaweza kushauriwa vibaya na washauri wako kwa labda kutojua, makusudi au bahati mbaya.
    Sasa basi mnapokuja kuweka hoja zenu mnatakiwa kuwa na vigezo na takwimu halisi na sio kusema tuu. Huyu bwana was a highly respected person na bado ataendelea kuwa hivyo. Subirini muone awamu ya nne baada ya miaka mitano ndio mtajua tunaelekea wapi. Cha moto tutakiona. I smell rat. Ngoja tumwangalie huyu Christopher Columbus atamaliza lini ziara zake za kuvumbua dunia.

    Amkeni watanzania muone ukweli acheni kuwa vichwa maji. Panya nyie

    ReplyDelete
  20. anonymous wa feb 28;3:56pm umemaliza kila kitu,na maana umeongea point zote kasoro umesahau moja bmw alikuwa mvivu and he did'nt give a shi....t,angalia swala la ujambazi ilikuwa kama hamna serikali,lakini jibaba umeongea point zote!ambaye hataki ameze nyembe!

    ReplyDelete
  21. MKAPA AND KIKWETE LEADERSHIP STYLE/ABILITIES COMPARED


    BWMIntelligent na uwezo wa kushawishi pia mchambuzi na ana upeo JKAkili ya kawaida na hana uwezo wa kushawishi. Si mchambuzi. Hana upeo. Anaweza kutumika kirahisi
    BWMAlikuwa na sababu dhahiri hata nje ya CCM kwa nini alitaka kuongoza nchi JKHakuwa na hoja binafsi. Alikumbatia ilani ya CCM. Hakuwa na sababu za kwa nini urais
    Hana mvuto wa sura na maumbile JKAna mvuto wa sura na maumbile
    BWMJasiri JKSi jasiri. Alilia wakati wa msiba wa baba wa taifa
    BWMUwezo wa kuchukua maamuzi magumu JKHapendi maamuzi ya kuudhi watu.
    BWMAlipunguza inflation hata kama nchi haiukuwa na exports JKInflation yakua kwa kasi ya enzi za RUKSA
    BWMAliiheshimisha nchi katika anga za kimataifa JKNchi itadoda sana ktk utawala wake
    BWMAlijenga miundo mbinu hasa barabara JKHakuna kifanyikacho. Nchi haipitiki
    BWMAlijali na kutambua fani za watu/watendaji JKAnapenda kulipa fadhila bila kuthamini fani
    BWMUkubwa wa serikali yake walau JKSerikali ni kubwa mno na ina matumizi ya ajabu. Alipashwa kupunguza matumizi ya serikali kama hatua ya awali ya kukuza uchumi
    BWMRushwa kubwa ilimshinda na alikubali JKRushwa zote zitamshinda. Richmond ni mfano mbaya wa kwanza
    BWMAliogopa kuwaadhibu mawaziri wake JKNi mwoga pia. Lakini hili laweza kuwa tatizo la kichama zaidi
    BWMAlithamini elimu na alifanya kazi nzuri ktk kuikuza JKAna mwelekeo mzuri ktk hilo
    BWMHakupenda mabadiliko makubwa ya nchi kama katiba, muundo na mifumo duni ya nchi, muungano n.k. JKNia ya mabadiliko hasa ya muungano ipo kidogo
    BWMAna ukatili fulani JKSikatili
    BWMSi bwana MISIFA JKBWANA MISIFA
    BWMAlikuwa intellectual alikuwa na falsafa ya uongozi kichwani mwake JKHaelekei kuwa intellectual
    BWMAlikata tamaa mwisho wa utawala wake JKAtakata tamaa haraka zaidi
    BWMHakutoa ahadi ngumu kutekelezeka kwa raia JKAlitoa ahadi nyingi ktk mazingira magumu ya nchi
    BWMAlikumbatia ukoloni mamboleo kwa kasi JKHawezi kuukwepa ukoloni mamboleo

    ReplyDelete
  22. Kwana nianze na Mwegelembegele, kwa jina hili sijui kama ni mbongo au mkongo,,, Blair au PM yoyote wa UK hajawahi kuwa na official plane. Hiyo iliyokuwa ya campaign ilikuwa chartered na si ya kazi kama ya hii Gulf Stream yetu ya JK.

    Kwa wengine, hasa wewe Jaduong na mwenzako Mkurabita, nadhani nyie ndo mna "impossible expectations" ambazo mnataka nchi hii iwafanyie. Si ajabu nyie ndo mnakimbia nchi na kuzamia Ulaya au Ughaibuni kwa kudhani kule maisha yako nje nje tu na mtu yoyote anaweza kuishi bila kutumia akili. Hapana. Kila sehemu ni akili yako tu, na si akili ya mwingine.

    Kwa hakika Mkapa ameipeleka hii nchi mbali sana. Hii kasi ya ukuaji wa kiuchumi tukiweza kui-maintain na hawa 2 boys wetu tutakuwa tumeipita Kenya in four years time. Tutakuwa sawa na Botswana in 8 years time. Wakati huo huo, mafanikio ya mtu binafsi kwenye kasi hii yanatoka na yeye mwenyewe na si serikali. Kuna watu miaka ya nyuma walikuwa wanalalamika eti Serikali kwanini imeruhusu SA national kuanzisha mgahawa wa Debonaires pale opposite na British Council (DSM) wakati wazawa wanaweza!! Sasa hao wazawa walikuwa wapi siku zote kuanzisha? Kwani maeneo yameisha?

    Tusilalamike. Tusisinzie. Tusiimbeimbe tu. Tufanye kazi na kuwa wabunifu. Watanzania wachache amabo ni wabunifu ndo wanakwenda kwa kasi. Walalamishi kama niliowataja hapo juu watakufa maskini. Mfano mwingine, ukienda Segera njia panda, utakuta malori yamepanga foleni yakinunua machungwa kwa viwanda vya Kenya ambavyo baadaye vinauza Juice TZ! Hii nayo mnataka serikali iwasadie? nini? Wakulima wanapata bei nzuri kwa machungwa yao kwa malori haya. Wa-TZ sisi akili yetu ni kununua malori, mabus, vidaladala, kujenga unnecessarily expensive mansions badala ya ku-invest kwenye vitu vyenye fast turn over kama hivi. Baadaye, mnalialia eti ohh, Mkapa kauza nchi! Wapi?! Nchi mnayo wenyewe.

    Bado tuna time ya kwenda. Msimlaumu Ben. Ben was a president. Nyie wenye high expectations, keep on expecting. Sisi tunaofanyia kazi expectations zetu mtatuona tu. Badilikeni. Achana na Ukomunisti. Wewe mqwenyewe ndo uchumi na si Mkapa kukusaidia. Mkapa opened rooms for everybody to play.

    Mimi ni Mtoa maoni wa kwanza hapo juu.

    ReplyDelete
  23. We Mkwapa umezidi unene!!!
    Jamani forest whitaker umependeza zaidi afrika: baby welcome back!

    ReplyDelete
  24. We anon March 1 4:47 AM hapo juu huna data hata kidogo. Nyie ndo mnaleta kelele na kusababisha watu wengine wasioenda shule wachanganyikiwe zaidi kuhusu Madini ya bongo.

    Hakuna nchi ya Africa ambayo inapata 50% ya madini yake kutoka kwa investors wa nje. Ghana kwa mfano, inapata 15%, Nigeria na Mafuta yake ikiwa nchi ya sita Duniani inaambulia 39% tu, SA pamoja na kuwa na largest economy in Africa inapata 37%. Sina data kuhusu visima vya mafuta ya Ufaranza na UK vilivyoko Libya.

    Tuwe waangalifu katika kutoa maoni. Maana kama huna data, unachanganya wenzako wasioelewa! Ni bora kuuliza kwanza, kuliko kulipuka lipuka. Na hii lipuka lipuka ndo ndo inawazuzua wabongo wakati wa kampeni. Maana wengi wetu hatutaki kutumia akili nyingi kutafuta facts. Mtu akiropoka, watu wanashangilia! Mnakumbuka Mrema kwenye presidential run-oof ya 1995. Watu hata wasomi, walikuwa wanashindwa kutofautisha ukweli na uwongo! Kwangu mimi nilijisikia vibaya sana sana. Wengi wao, marafiki zangu ndo akili zinawajia sasa. Ahh, kumbe?!! Why?

    Anon mhusika toa data. Hii blog ya kujifunzia. Siyo propaganda

    ReplyDelete
  25. We anon wa 3:47:00 pm ,tunashukuru kwa data zako nusu nusu. Naona unaacha nchi kama zimbabwe, pamoja na kuwa unampiga madongo mwenzako, bado hauonekani kujutia kwanini Tanzania inapata only 3% wakati nchi zingine sio chini ya 15% kama ulivyoonyesha. Ukweli unabaki pale pale kuwa kuna blander kwenye contract za madini na hilo sio la kuficha, aliyeingia kwenye mikataba yote hiyo ni Mkapa. JK amekuja ameamua kuangaliwa upya, kwa kuanzia wamekubaliana kuwa kampuni za madini zitumie at least 200 millioni kwenye miradi ya jamii. Na wamekubali, kama wangekuwa wanaonae sio fair si wangekataa. Pia wamaipitia mikataba kuona inafaidisha vipi nchi. Wewe ndo unaongea pumba zisizokuwa na msingi hapa. Nchi imeuzwa, hilo ni wazi.Tuangalie ktk miaka 10 ya JK tuone nini amefanya ingawa kila binadamu ana mapungufu yake.

    Naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  26. we anony Thursday, March 01, 2007 3:47:00 PM, sio unakuja tu hapa nakujichagulia namba eti 15%,39%,37% tutakuamini vipi hata hatukujui? backup your point toa links tuone hizo data umepata wapi
    pumbafu kabisa
    wazungu wamerudisha hela yao ya kuinvest within 3 month of productivity. thats Geita where i worked and one of the executive was cool with me and gave me this infor. serikali iliwapa tax holiday do you know for how long? mkapa jinga kabisa toka lini madini yakapewa tax holiday? ndege zilikuwa zinatua usiku na mchana kusafirisha madini

    ReplyDelete
  27. Michuzi hutaki nichangie humu? mbona umenibania?

    ReplyDelete
  28. Michuzi umenibania, Hutaki nichangie hoja?

    ReplyDelete
  29. Namjibu Mzalendo halisi na anon hapo juu. Si kweli kuwa wazungu walirudisha hela yao in three months. Huyo aliyekwambia ni kibaka kama wewe. Wote hamjui. La msingi ni kufanya utafiti kuhusu madini yaliyopo na yauzwavyo. Na si kuseima kuwa eti wazungu walirudisha hela ya in three months. Haiwezekani. Je unasemaje kuhusu mafuta ya Nigeria ambayo mapka leo wanapaya asiliamia ndogo. Je nao hawajarusha gharama zao? Wale jamaa wametumia hela nyingi sana ku-invest. Haikuwa shida serikali kuwa tax holiday. Iko kila sehemu Duniani hiyo. La maana ni kwamna namna gani hiyo tax holiday ilikuwa implemented. Itarekebishwa soon.

    Wewe anon unayedai kuwa ninajichagulia number tu na sina data. Nenda kwenye www.iht.com/business utapata information zote. Data hizi ziko kila mahala pia. Watanzania ni wavivu tu wa kutafuta information. Wanadandia information za wanasiasa na kuchanganyikiwa. Tuwe waabngakifu wabongo. Vingenevyo, tutashangaa na kubaki wabishi wabishi tu!

    Ni kwa uvivu wetu ndo maana tunabisha bila sababu. Ndo maana watu wana-stowaway bila sababu. Pesa iko humu humu bongo. Tatizo ni wabongo wenyewe.

    ReplyDelete
  30. we anon Thursday, March 01, 2007 11:38:00 PM,
    kama unakubaliana na tax holiday kwenye contract za madini siwezi ku-debate na wewe tena.
    narudia tena 3 months wakarudisha hela walotumia kuinvest. nili kuwa pale bwm kapewa Gold ka mche wa sabuni. nikiandika kila kitu itakuwa gazeti
    i spent a lil time in mwadui same story mpaka unaona huruma ukikiangalia kijiji cha mwadui, pamebaki mashimo and poverty diamond imeondoka. wananchi wakagundua diamond maganzo serikali ikawakataka kuchimba ili wakubwa wajitafutie dili la 10% may be 30% kama rada

    ReplyDelete
  31. Anon wa March 01,2007 11:38:00 Acha kubishana na huyo bwege,anayesema Mkapa kafanya jambo la maana,nadhani anabisha hata hilo deni kuwa limeongezeka,hata JK akikopeshwa dolla billion 2,nadhani atafanya jambo la maana. Hawa watu bwana ni ndugu zao na wale watu waliokula rushwa enzi za mkapa,kwahio hapa watatetea hadi kufa,kwasababu washatajirika na hizo pesa za baba zao corrupt pipo. Ivo nashauri tuwaache tu,ujumbe washaupata,nasasa wasubiri laana ya mungu tu.Pia namshangaa sana unavosema wabongo wavivu,wewe mwenyewe umekimbia haupo bongo,kwasababu yale mazingira yalikuwa magumu kufanya kazi,kila sehemu ilikuwa ni rushwa tu,mi narudi kule mwaka huu,ila napata matumaini na speed ya JK ya kupambana na rushwa ndio maana narejea.

    ReplyDelete
  32. Tarehe Thursday, March 01, 2007 3:33:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous - Kwa ufupi una akili sana na ninakubaliana na post yako 100%. Wa-TZ wengi shida yao wamezoea mno ujamaa, kila kitu wanasubiri serikali iwafanyie.

    Kama serikali imeona ni gharama mno kumiliki makampuni yanayoishi kwa ruzuku na kuamua kuyauza kuna shida gani. Kwani kama NMB (mfano) likiwa shirika la umma, wewe mkomunisti usiyefikiri, unafaidika nini? Unafikiri utaweza kuenda NMB na kujichotea pesa?

    ReplyDelete
  33. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  34. Anon wote hapo juu, namalizia kwa kusema kuwa tax Ho0liday iko kila shemu Duniani ma inakuwa implemented tofauti tofauti. Hii huhitaji kuwa mchumi kujua. Mfano mzuri, wakati mji wa Dodoma ulipotangazwa rasmi kuwa makao makuu, serikali iliondoa kodi kwa vifaa vingi vya ujenzi ili waru wavutike kwenda kujenga pale. Sasa sikuwahi kuasikia watu wa Ujiji au Mtwara wakilalamikia hii kitu licha ya kwamba viwanda vya cement kwa hii miji ndo viko mbali zaidi. Ilikuwa ni mkakati wa serikali kuibadilisha Dom.

    Pia ukienda miji au nchi nyingi tu, kwa mfano Duabi, Macao, Eilat, Bahamas, etc, huku kote ni either duty free au tax free cities. Lengo ni kuvutia wawekezaji. We unadhani Beckham angenunua kiwanja pale Dubai kama asinge-foresee ukuaji wa mji/nchi ile kwa sababu ya duty-free.

    We unayedai kuwa wale jamaa waliweza kupata faida in three months, ni sawa na wale wanao-stowaway kudani kuwa watatajirika in few months huko waendako. Si kweli na si kweli. Sijui wewe ni nani, lakini ningependa nikupe data kwenye email yako ufunguke macho. Kuna wenzako wengi graduates wa UDSM B.Sc. Engineer and Geology wako kama wewe. Mnarahisisha kila kitu na kukiona chepesi. SIyo hivyo!

    Ndo maana nasisitiza sana sana kuwa, sisi Watanzania ni wavivu sisi kufikiria. Tunapenda kudandia tu kila kitu katikati. Ukiweza kukaa na ku-analyse vitu viko wazi sana sana dunia nzima. Ni kutokana na uvivu wetu wa kufikiria, ndo maana wanasiasa uchwara wanatuchanganya Tanzania. Watu wanashangilia kila kitu, bila kufikiria. Inaniuma sana lakini naamini young generation itabadili upuuzi huu.

    ReplyDelete
  35. Wewe anon March 1; 11.38 mdo kapuku kabisa. Deni siyo issue ya kuifanya nchi iwe maskini. Hii pia huhitaji kusoma uchumu kujua haya.

    Nchi changa zote Duniani zinazokua kiuchumi, hata zile za kati zina madeni makubwa sana sana. Na kuwa na deni kubwa hakumaanishia kuwa wewe ni maskini sana. Hapo bongo, bila kuwataja, kuna watu ambao tunafahamu kuwa ni matajiri wakubwa kabisa, lakini wana madeni makubwa ajabu. Nchi ya Brazil, ni second ina deni linazidi dola billion 100, sijataja Nigeria, Korea na Indonesia. Huwezi fananisha nchi hizi na bongo, lakini zina deni kubwa zaidi ya bongo. Sijui kama huwa unafahamu haya wakati unaandika kuhusu issues zako za madeni. Au wewe unadhani madeni ni dhambi?!!

    La maana unachotakiwa ni kukopa, then kufanyia kazi hilo deni lako. Wether utalipa au hapana, inaregemeana na mdai wako.

    Na nachukua fursa hii kukushauri na wewe kama unampango wowote wa kimaisha, ujaribu kuomba mkopo kwenye benki za bongo hapo. Kuna NMB, Azania, Eurafrica wanatoa mikopo sana kwa SMEs. Sasa wewe kwa akili yako na uwelewa wako unadhani madeni ni dhambi! Ndo mwanzo wa kufa maskini huku ukisema sisi tunakushauri tuna laana ya Mungu! Kachukue mkopo ufanye shughuli. Badilika uwe mjasiriamali na si kulialia eti deni limeongezeka wakati data zako shallow kama akili yako!

    Kalaga bao, tunabanana huko huko mbinguni, lakini hapa Duniani tutaishi tofauti kutokana na kufikiria tofauti!

    ReplyDelete
  36. we anon Friday, March 02, 2007 11:34:00 AM,
    mi sijasoma mlimani wala sina degree ya geology. nilikuwa dereva tu for few month after high school. anyways Let me ask you a question, why do you give tax holiday to a mineral sector especially gold? unataka kumvutia nini mwekezaji? read book and do your assignments there is no tax holiday on mine sector just happened in Tanzania under BWP. do you know how much extraction it takes to kurudisha gharama ya kuwekeza? thats mining they extracted day and night.
    if have infor that make sense am at j4watson@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...