kama mtakumbuka desemba 16, mwaka jana nilialikwa kula pilau nyumbani kwa familia hii waliyoandaa kumshukuru muumba kwa yote. hivi leo kuna kila uvumi juu ya ndoa hii na mimi kwa vile sipendi umbea nitaanika ukweli wa mambo baada ya kupata stori toka kinywani mwa farasi. kaeni mkao wa kula

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 64 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2007

    tanzania daima wameshaanika!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2007

    PREDICTABLE

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2007

    hehehe kimetokea nini tena kwani i loveeeee story za udaku hebu nipasheni!!!!!! hahahahahahhaaaaaa samahani kama wadau mtakereka

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2007

    Ungetumia picha hii CHIFUPA NA MEDI

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2007

    Michuzi, umbea gani tena wakati Baba Mzazi wa Mheshimiwa Amina leo kaanika hadharani kuwa mwanawe katwangwa Talaka. Sema tofauti ni idadi ya Talaka, wakati inasemekana Mpakanjia anasema katoa talaka 3 (yaani ndio bai bai), Baba Amina anadai mwanawe kalimwa talaka 1 tu (kwa hiyo baada ya Eda anaweza kurudi kwa mumewe).
    Ni stori tamu lakini (yaani ni kama Bekham na Victoria hapa UK)

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2007

    Mimi naisubiri kwa hamu sana nafikiri tutajifunza mengi sana kutoka hapa. Nijuavyo ngombe wa masikini hazai, akizaa huwa ni dume.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2007

    AMINA chifupa anaonyesha mfano mbaya sana wa wabunge kwa kupenda kuanika mambo yake hadharani. anaweka mkutano na waandishi wa habari ili aeleze sababu za kuachwa na mumewe wakati ni umalaya wake? nani anahitaji kujua sasa?alafu aache ushambenga asha kuwa mheshimiwa ila ndo tatizo la waswahili! HEEE!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2007

    Mbona story imetoka toka Jana kwenye Magazeti , na wewe ulishindwa kututaarifu? Mimi nilikuwa naingia kwenye site yako kila baada ya Dakika , lakini wapi, au ulikuwa unajaribu kusuluhisha , sasa umeshindwa?
    Lakini mimi naomba uendelea kuwa suluhisha mambo ya kuachana sio mazuri, na huyu naibu waziri kizabina zabina aliyo sababisha haya naomba umuonye , awe kama Mwanaume, sio kushindwa kumpata bibie, ndio achonge huo mdomo wake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2007

    Michuzi mbea na wewe

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2007

    Lete issue michu maana hata mimi nina hamu yakujua hasa baada ya kusoma gazeti moja kwenye mtandao lilikuwa linasema ndoa imevunjika na mvunjaji ni kigogo wa chama ambaye kamwambia uongo mpakanjia nao bila kusika kaiandika kisa mkewe anakula sahani moja na mbunge mwenzake kijana. Yaani hapa ndio panasubiriwa hasa. Au watayamaliza chamber court?. Maana bibie alitarajia kuanika mambo hadharani pale maelezo leo je hakufanya hivyo?.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2007

    Amina Chifupa kulipua bomu leo

    na Mwandishi Wetu (http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/7/habari2.php)

    MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), amesema leo analipua bomu mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuvunjika ndoa yake na Mohamed Mpakanjia, tukio analosema limesababishwa na kiongozi mmoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Naibu Waziri.

    Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Amina, alisema anamuomba Mwenyezi Mungu amuamshe salama, ili aweze kuzungumzia suala hilo ambalo anafahamu kuwa linaweza kumuweka katika wakati mgumu kabisa.

    “Nafahamu ninapambana na watu hatari, lakini kesho (leo) namuomba Mwenyezi Mungu aniamshe salama, ili niweze kuliweka bayana suala hili mbele ya waandishi wa habari MAELEZO. Nimekusudia kusema ukweli wote kuhusu suala langu,” alisema Amina.

    “Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu… hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa ‘ndiyo mzee’,” alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.

    Amina ambaye ameihakikishia Tanzania Daima kuwa alipewa talaka na mumewe, Mei 3 mwaka huu, anasema tukio hilo lilikuja baada ya kiongozi huyo wa CCM ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho kumuita mumewe ofisini kwake.

    “Nilipewa talaka siku ile ile baada ya Mpakanjia kutoka ofisini kwa kiongozi huyo. Kwa kweli (anamtaja) ndiye aliyevunja ndoa yangu kwa kumuambia mume wangu mambo ya uongo,” alisema.

    Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kwamba, Amina anaamini kwamba kikubwa kilichosababisha akutwe na masahibu hayo, ni kile kinachoelezwa kuwa uamuzi wake wa kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), hatua ambayo inaonekana kuwashtua na kuwakera baadhi ya viongozi wa sasa wa umoja huo.

    Hivi sasa Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana anayetarajiwa kumaliza kipindi chake mwakani.

    Hata hivyo, Amina alipotakiwa kueleza iwapo alikuwa akikusudia kugombea nafasi hiyo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kumtaka mwandishi kusubiri hadi wakati utakapofika kwani kuna muda mrefu bado, kabla ya yeye kufikia uamuzi huo.

    Mbali ya hilo, Amina alielezwa kushangazwa kwake kuona masuala yake ya ndoa, yakipelekwa bungeni, wakati mahusiano yake ya nyumbani hayana uhusiano wowote na ubunge wake au uanasiasa wake.

    Habari ambazo zilithibitishwa zinaonyesha kuwa, Amina amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbunge kijana wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambaye alipopigiwa simu na gazeti hili jana, aliyapuuza madai hayo ambayo alisema; “hayana ukweli.”


    Zitto mmoja wa wabunge machachari wa upinzani, alisema anafahamu kwamba suala hilo limeandaliwa na kundi la watu wenye sababu za kisiasa, ambao wamekuwa wakimtafuta yeye na Chifupa kwa muda mrefu.

    “Ukaribu wangu na Amina ni wa kikazi tu… na ukaribu huo ulianza siku Spika wa Bunge alipotuteua tuhesabu kura za wabunge zilizomuidhinisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

    “Siku hiyo tulipokuwa tukihesabu kura, afisa mmoja wa bunge alitufuata katika chumba cha kuhesabu kura na akatutaka kutozitaja kura mbili zilizokuwa zimeharibika, jambo ambalo mimi na Amina tulilikataa. Tangu hapo nilianza kumheshimu Chifupa baada ya kubaini kuwa alikuwa mtu makini na mwenye msimamo. Tangu wakati huo tumekuwa na uhusiano wa karibu kikazi,” alisema Zitto, alipohojiwa kwa njia ya simu.

    Alisema, siku zote amekuwa na uhusiano mzuri na wabunge wote vijana kwa wazee, lakini anashangazwa na uvumi juu ya uhusiano wake na Amina kuonekana vinginevyo.

    Gazeti moja la kila siku, (si Tanzania Daima), jana lilimkariri Mpakanjia, akithibitisha kumtaliki mkewe baada ya kubaini ndoa yake ikiingiliwa na mbunge wa CHADEMA ambaye hata hivyo hakumtaja.

    Habari zaidi ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kwamba, ushahidi mkubwa unaoonekana kuwaunganisha kimapenzi wabunge hao vijana, ni tukio la siku moja jioni, ambalo Amina alionekana akiwa amevaa koti la Zitto, wakiwa wameketi pamoja katika Hoteli ya Dodoma.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2007

    kichekesho na inashangaza sana kwani hata wiki 2 hazijapita nilimsikia kwa masikio yangu huyo mpakanjia akiongea radioni ambapo gadna alimpigia simu (wakati amina akiwa studio na gadna kwenye kipindi cha jahazi)kwa kusema kwamba mke wake ni msikivu, mwenye tabia nzuri, n.k.alimsifu sana tena sana. sasa nashangaa leo eti mtu katoa talaka. swali,huo uthibitisho ameupata kwa uhakika au?
    pia huyu mpakaroad kanishangaza sana kutoa habari zao kwenye vyombo vya habari mpaka kufika kwa spika bungeni! jamani huu si ushamba jamani. hata kama kweli amina anatembea na zito kabwe(not sure) sasa ndiyo apeleke kwenye vyombo vya habari! ama kweli wengi hatujui matumizi ya vyombo vya habari.
    hayo ni matatizo yenu malizaneni wenyewe bwana. la sivyo mataoa na kuolewa kila siku.
    kingine cha kushangaza! hivi huyu baba yake amina atakuwa anamsea mwanawe mpaka lini? amina kaweka watu pale maelezo matokeo yake anakuja mdingi. ila nasukia mdingi ali-ishia kuchekesha tu watu pale. mdingi nae msanii sana ingawa alivyokuwa anaviongelea aliongelea zaidi matatizo yanayoikabili nchi, akazima kabisa issue ya amina na kudai kwamba nchi ina matatizo kibao hakuna maji, barabara mbovu, nk.
    bwana Michu,tunasubiri habari hiyo hebu tuletee tufaidike sisi, ila waambie wawe wakubwa matatizo kama hayo wamalizane wenyewe si kupeleka kwenye vyombo vya habari kwani wao nani. mbona wakati ule mama Anna Mkapa na Mkapa walipopigana hawakutoa kwenye vyombo vya habari. tulishtukia tu Mkapa anachechemea miguu inauma na mama Anna Mkapa ana piopii mkononi. very funy.
    nawakilisha, NOPE

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2007

    NENDENI TANZANIA DAIMA, UHURU NA KWA MAGGID MJENGWA-WAMETOA COVERAGE KIDOGO YA HII HABARI.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2007

    kwa wote mnaotaka kujua nini kinaendelea

    checkini hii link

    http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2787

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2007

    Sawa kaka ila bwana Bungeni bwana wabunge wakipita kwenye himaya yako wanabeba, wamezoea kudanganya wananchi na wanakubalika sembuse kumdanganya Amina!! Haya mazee bwana michuzi mi mwenyewe mpenzi wangu kaenda!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2007

    kaka michuzi nakuomba niko chini ya miguu yako mimi nataka kumoa huyu dada najua yule jamaa mnene hawezi mambo na hajasoma kizungu zero hana communication skills, ukijumlisha na inferiority complex ndio bas hamuwezi huyu dada yupo juu japo ana zero lakini mimi nataka kumuoa michuzi najua unayo email yangu mimi nipo chupo kikuu kikubwa ughaibuni mpe email mh mbunge niseme naye nipo serious michuzi mkuu!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2007

    Mimi bado sijaelewa akili zetu zikoje.Ikiwa wameachana kutakuwa na nini na ikiwa hawajaachna kutatokea nini!

    Hao ni maarufu kiasi gani! Mpaka njia au Chifupa what makes them different na wananchi wengine!Wabongo kwa umbeya!

    "If anything goes wrong it will"
    Tushughulikie mambo ya msingi na sio kuingia mpaka uvunguni mwa mpakanjia na Chifupa!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2007

    Mr Michuzi hao wote hapo wameoana watu wa misifaz kwa hiyo yanayowatokea wameyataka wenyewe wasikuumize kichwa tupe mambo mengine kwenye blog yetu makini

    ReplyDelete
  19. Umechelewa kutuletea stori. Nimekusbiri hapa tangu asubuhi hadi sasa hivi usiku wa manane sijakusikia. Je na wewe unaficha jambo kama Baba yake Amina?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2007

    MICHUZI MBONA COMMENTS HUPOST AMA UNASIKILIZIA ISSUE NINI?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2007

    mwaga issue hizo michuzi wacha kuibana au kwa vile una juana nao siis tunasubiri toka juzi naona unaanza kuzungusha issue yenyewe

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2007

    Amina amezidi kudhihirisha U-ZERO BRAIN wake!
    issue ya yeye kukandamizwa Talaka na mumewe ni swala la kifamilia zaidi na sio kisiasa. hata kama chanzo ni mwanasiasa. Yeye analipeleka Maelezo na kulifanya kama swala la kitaifa

    Nashangaa sana kusikia anaitisha pressi konferensi ya kujadili hili. short minds...

    Angalau Baba yake ametumia busara katika ku-hndle issue ya mwanae. ni Aibu kwa huyu amina kutaka nyadhifa za juu zaidi kichama na kitaifa. Hajakomaa ki-uongozi na ki-utawala.

    Wasiwasi wangu ni kwamba kwa vile hii issue inawahusu WAHESHIMIWA (Aminia, Zitto na Nchimbi) hukawii kusikia wameundiwa 'ka-tume'!. itapewa bajeti ya Mamilioni (ile ya Sakata la Mengi na Malima ilikamua Millioni 100!).

    hizi ndio effects za kupeleka Ma-ZERO brains ktk uongozi na utawala.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2007

    Pole Spika Sita na kamati yako ya Maadili. Naona siku hizi huko busy....hata mambo yanayotokea ndani ya shuka unaletewa urekebishe.

    ReplyDelete
  24. Ama kweli lisemwalo lipo na kama halipo ujue lipo njiani........sasa hapo sijui hapo nani ni nani maan hii ishu balaa tupu.....all in all ukweli utajulikana tu

    ReplyDelete
  25. For heaven'sake watanzania tuache hizo. Private issues za watu zina tuhusu nini hata kama ingekuwa ni Rais wa nchi?!

    Kuna mengi tu yakuongelea hapa watu watoe points hasa matatizo yanayo kabiri vijana wa kitanzania.

    Matukio kama ndege ya Kenya Airways iliyo potea...... anything constructive/informative

    Winny Mandela alimngoja miaka yote hiyo Nesoln akiwa jela lkn waliachana mi sikusikia Winny/Nelson wajieleze hadharani. Mwanamke wa kiafrika anatunza siri za unyumba wake whatever happens!!

    Tabia gani hiyo Amina!? I bet you have kids with this man and just for your children's respect...
    Waridi

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 08, 2007

    TAFADHALINI WADAU!
    ukisha kuwa na umbo kama la huyu mume wa anna chifupa hata kupiga bao inakuwa issue mafuta mengi mwilini matokeo yake bao linakuwa la WIKI MBILI mara moja kama vidonge sasa binti mtamu kama huyu hawezi kuvumilia jibaba nene mpini mdogo umezibwa na kitambi wapi na wapi. watoto wa karne hii wajanja wanapenda mtu mwenye mpini anaye piga mashine kutwa mara nne siyo wiki mara moja tena mpaka uimbiwe kasimama dede! ANGALIA HILO UMBO KAMA VOLKSWAGEN BITTLE jasho kila mahali anasweat kama mtoto mdogo tena kabla hata bao halijaitika nani atavumilia wakati kuna wabunge vijana kama kina PETER SERUKAMBA! MZEE BALOON ANZA IMETOKA HIYO POLE ILA UMBO LIMEKUPONZA KAKA YANGU NENDA GYM LABDA ATARUDI UKIPUNGUA NA TAFUTA DAWA ZA KUONGEZA MPINI!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 08, 2007

    wabongo bwana your are think cheaply,u too AC marriage saga is a new but too a s......!!
    find something which has public interest for our Nation benefit

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 08, 2007

    Tatizo la Chifupa anapenda kula mbele na nyuma yaani mbele kule kunakoitwa bungeni anakupenda na nyuma kule kunakoitwa kwa Mpakanjia anakupenda sana.

    Na hakubali kuacha kokote.Huku anapenda na huku anataka.Mshika mawili moja lazima limpokonyoke. Hawezi kula kote kuwili kwa mara moja shurti uchague upande mmoja ati!!!.Ndiyo maana apata shida.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 08, 2007

    hivi Chifupa ana elimu gani? mbona vitu vyake anavyoongea doesnt make sense at all,tangu ajidai ana majina ya vigogo wa rushwa nilijua ile head ni ZERO..naomba waandishi akiitisha mkutano wamwambie mama tunashukuru lakini leo hatuhitaji kujua juu ya talaka yako lakini yale majina ya vigogo ya rushwa yamefikia wapi na hapo arushiwe rocket moja baada ya nyingine nafikiri atajifunza kutokurupuka na kujiona bwege tuu

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 08, 2007

    Wewe Mwita Chacha unaonekana wewe mtoto si ridhki mana jinsi unavyoongelea mpini na shughuli ya Mpakanjia inaonekana alikushughulikia na unaonekana unatafuta wateja humu ndio maana umetoa jina lako full....anyway sio vibaya maana na nyie mna mahitaji yenu labda vijana watakuona humu na kukusaidia

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 08, 2007

    Michuzi,
    ulifuatilia sana Story ya yule Miss TZ wa the 60's na kutupasha habari za kifo na mazishi.

    Sasa ni Hivi....
    Fuatilia habari za huyu MBUNGE mbumbu, ZERO BRAIN wa karne hii anaitwa Amina Chifupa aliyekuwa wa MPAKANJIA.

    Naona leo umepata kigugumizi, huweki picha mpya. Una-approve Maoni Tu. umenyamazishwa nini Michuzi??????....

    Mimi sitakuelewa ukiiweka hii issue kapuni hivi hivi.

    tunataka habari za Hili sakata. kabla spika hajaunda tume.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 08, 2007

    Naomba nami nimwage yangu machache kuhusiana na sakata hili.Nadhani ya kwamba suala hili si la kulaumu upande mmoja bali inategemea mtu unalitazama kwa nyanja zipi.Upembuzi yakinifu ukifuatwa utatumbua ya kwamba suala hili lipo namana hii kwa uchache:
    Suala la talaka sio jipya kwa jamii,na zipo dini zimelipa baraka,hivyo punde wanandoa watofautianapo wanaweza kupeana talaka nadhani hili linaeleweka bayana.
    Pili hili ni suala la ndanini sana kati ya Amina na Mpakanjia na baadaye pande zote mbili za wazazi ingawaje jamii inhaki ya kulijadili kiundani

    Tatu Mpakanjia alicha mke wake wa awali na kuungana na Amina hivyo inaweza ikawa ndio taabia yake,tabia haina dawa.

    Nne,Amina alipoingilia nyumba ya Mwenzie alitegemea nini,mtenda hutendewa.
    Kama mwanaharakati wa kuchambua nadhani watu wazame kiundani na kubaini nini chanzo cha mgogoro,kwani hata Medi alipomwoa Amina alikuwa anafahamu fika tabia yake hivyo aliridhia ,sioni kwamba ndio sababu ya kuachwa,inawezekana tu wamehitilafiana kwenye biashara na kazi ya ubunge.
    Mwisho,ukiona kwa mwenzio kunaungua safari nyingine ni kwako,kaa chonjo mwanajamii mambo haya yalikuwepo yapo na yaytaendelea kuwepo,tufanye nini ili kuyapunguza

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 08, 2007

    Michuzi mtoto umemficha kwako nini? manake hata baba hajui alipo

    Siasa zaharibu ndoa ya Chifupa

    *Kisa ni kuutaka uenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM
    *Baba yake Amina amzuia kutoa siri kwa waandishi

    Na Waandishi Wetu

    TALAKA kwa Mbunge wa Viti Maalum-Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amina Chifupa imeingia katika sura mpya baada ya kubainika kuwa kiongozi mmoja wa UVCCM, alikataa ombi la mbunge huyo kutaka ampigie debe katika nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

    Chifupa alikaririwa na vyombo vya habari jana akilalamika kuwa, kiongozi mmoja wa UVCCM ambaye pia ni Naibu Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri ya CCM, alitumia ushawishi wake kwa mumewe hali iliyosababisha yeye kupewa talaka.

    Taarifa zingine zilieleza kuwa, tukio hili la kupewa talaka linahusishwa na kitendo cha Mbunge huyo kuonyesha tamaa ya madaraka ya juu katika UVCCM. Hata hiyo, mbunge huyo alipoulizwa kufafanua ukweli wa dai hilo, hakupenda kubainisha wazi kuhusu dai hili.

    Kilichobainika baadaye kufuatia uchunguzi wa gazeti hili ni kuwa, Chifupa amekuwa katika kampeni za chinichini zenye lengo la kutaka kuiongoza UVCCM.

    Katika harakati za Mbunge huyo kusaka sapoti, alifika kwa kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika UVCCM na kutaka baraka zake. Kiongozi mmoja wa UVCCM aliiambia gazeti hili kuwa, Chifupa alikataliwa bila kuelezwa sababu za kukataliwa kwake.

    Habari zaidi zinasema kwamba kiongozi huyo alisema Chifupa hawezi kuwa kiongozi wa umoja huo, kwa madai kwamba hana uwezo wa kushika nafasi nyeti kama hiyo.

    Kuna hali ya kuanza harakati za kutaka madaraka katika UVCCM. Kwa sasa makundi yameashaanza kujiandaa huku yakifanya kampeni za chini chini.

    Hali hii, inaonyesha kuwepo uchaguzi mgumu kabisa mwakani katika UVCCM na kama utaratibu wa CCM utatumika, kuna uwezekano zoezi la kufungia makada kadhaa kutogombea likafanyika. Ni jambo la wazi kuwa kuna ushahidi wa makundi na baadhi ya makada kuanza kupiga kampeni.

    Tukio hili la Chifupa kumhusisha kiongozi mmoja wa UVCCM linabainisha hali iliyopo ndani ya chama hicho. Kinachoelezwa sasa ni kuwa, uongozi wa UVCCM umekuwa ukitumika kama nguzo ya kusaidia kampeni za urais kupitia CCM. Zoezi hili mara kadhaa linawahusisha viongozi wa juu katika serikali na chama, kama inavyoanza kujionyesha sasa.

    Mwananchi ilipowasiliana na Mwenyekiti wa UVCCM, Emanuel Nchimbi, ili kupata upande wa uongozi wa umoja huo, simu yake ilikuwa imezimwa. Lakini habari zaidi zinadai kuwa Nchimbi kwa sasa yupo Songea kikazi.

    Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti juzi na jana kuwa Amina alitalikiwa na mumewe baada ya kubainika kuwa na uhusiano na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kwamba mwanaume huyo alichukua uamuzi huo baada ya 'kuumwa sikio' na kiongozi huyo wa UVCCM.

    Hata hivyo, Kabwe alikaririwa na gazeti moja jana akikanusha kuwapo kwa uhusiano huo, akisema amemzoea Amina kama Mbunge mwenzake, kuanzia siku walipoteuliwa kuhesabu pamoja kura za wabunge wakati walipokuwa wakithibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu.

    Wakati huo huo, Mbunge huyo jana alishindwa kutimiza ahadi yake ya kuzungumza na waandishi wa habari kumtaja Naibu Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne anayedaiwa kuvuruga ndoa yake.

    Badala yake, Baba mzazi wa Mbunge huyo, Luteni Mstaafu Hamis Chifupa, alifika katika Ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam na kutangaza kuwa amemzuia mwanawe kutangaza jambo hilo kwenye vyombo vya habari kwa kuwa ni suala la ndani ya familia.

    “Kila jambo linapotokea lina taratibu zake, namna ya kulitatua hivyo hata mgogoro huu wa Amina na mumewe lazima ufuate taratibu zinazotakiwa katika kuusuluhisha, hata kama angekuja kuongea na ninyi angeongelea masuala mengine lakini siyo hili la kuachwa kwa talaka moja,” alisema Chifupa.

    Luteni Chifupa alikiri kuwa mtoto wake huyo ameachwa na mumewe, Mohamed Mpakanjia kwa talaka moja kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.

    Hata hivyo, alikataa kueleza kwa undani sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo.

    Alisema kwa kuwa suala la kuachwa kwa mtoto wake ni jambo la ndani ya familia, wamemzuia Amina kulizungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.

    Mbunge huyo jana alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa alitaka azungumze na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa kuachika kwake, lakini kinyume na matarajio ya waandishi waliokuwa wamefurika kumsuburi, alijitokeza baba yake na kutangaza kutokuwepo kwa mkutano huo.

    Alisema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa kigogo huyo wa serikali ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, alikwenda kwa ofisi kwa mumewe na siku hiyo hiyo akapewa talaka, jambo analohisi kuwa lilichangia kuachwa kwake.

    Alipoulizwa na waandishi wa habari mahali alipo mtoto wake, Kapteni Chifupa, alisema hajamuona tangu alipoachwa ili wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu.

    “Kwa kuwa tuna ndugu wengi siwezi kujua anakaa wapi, licha ya kuwa kwa taratibu za dini ya Kiislamu anatakiwa kukaa eda huku akiendelea kuhudumiwa na mume wake,” alisema Chifupa.

    Alisema watoto ni sawa na pensheni kwa wazazi, hivyo wameamua kumlinda mtoto wao kwa kulizungumzia suala hilo wakati taratibu nyingine zinafanywa ili kuweka mambo sawa.

    Alipoulizwa juu ya sababu iliyomfanya mtoto wake apewe talaka moja, alisema haelewi akisisitiza kuwa hayo ni mambo ya ndani ya familia.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 08, 2007

    Mambo ya 'Unyumba' kuanikwa hadharani si vizuri. Pole sana Amina.

    Wanaume wako wengi, utampata mwingine mzuri zaidi ya huyo!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 08, 2007

    Mimi niliamua kutoroka uislamu mchana kweupe baada ya kuona mume wangu dude lake la katikati ya mapaja limemsimama alipoona mwanamke mwingine msikitini akasema anataka kumuoa tuwe wawili. Nikakataa.Nikamwambia siwezi ku-share jembe na mtu mwingine akaja juu akanilima talaka tatu akasema dini inamruhusu nikamwacha na kuacha dini ya kiislamu palepale kwa hasira.

    Chifupa Kazi kwako!Talaka ndiyo hiyo na dini inamruhusu kukupa talaka! Mwenzio akikupa talaka anaenda ahera anapokelewa na Allah na kupongezwa kwa kitendo cha kukupa talaka na wewe unaenda kuzimu utajijua na mashetani.Na hapo inakuwa rahisi kupata shwaitani Si unajua mtoto wa kike ukikosa kidume lazima upore kidume hata kama ni cha mtu kinachozubaa karibu! Kinachojifanya kina nyege na kina hela za kubangaiza, Maana huwezi kubali kukumbatia mto wakati kulikuwa na Mpakanjia Karibu 24/7.

    Wanawake kwenye Uislamu mbona kazi ipo! Talaka zinagawiwa ovyo kama kondomu.Mtu akilala akiamka anampa mwanamke talaka.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 08, 2007

    wadau acheni ulongo. hadi sasa hakuna anayemfikia cynthia masasi kwa kuvuta maoni mengi. muulizeni mithupu ama cheki hapa http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=cynthia+masasi&x=56&y=14

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 08, 2007

    Anony.. Tuesday May 08 5.34 unataka kutuambia baaday kutoroka uislamu na kumpata huyo uliyenaye sasa (kama yupo) anakuruhusu ufanye ujinga kama wa AC. Basi huyo bwana atakuwa 'Bushoke'. Hakuna dini inayoruhusu uchafu bwana usitudanganye hapa.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 08, 2007

    aah huyu ndio prezidaa bwana. cheki alivyo sosho

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 08, 2007

    Mtaliki wa Chifupa azungumza

    *Asema hakushawishiwa kumwacha mkewe
    *Asema anamwachia Mungu kila kitu

    Na Waandishi Wetu (http://mwananchi.co.tz/habari/habari3.asp)

    MTALIKI wa Mbunge wa Viti Maalum, Amina Chifupa, Mohamed Mpakanjia, amejitokeza hadharani na kusema hakushawishiwa na mtu yoyote kumtaliki mkewe wa zamani.

    Mpakanjia aliliambia gazeti hili jana kuwa uamuzi wa kumtaliki mkewe aliuchukua baada ya tafakuri binafsi na kwamba hakuna mtu yeyote aliyemshawishi kuchukua hatua hiyo.

    "Ni kweli nilimuona Nchimbi (Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa UVCCM) na nilitaka tu kumueleza kuhusu uamuzi wangu na si vinginevyo. Alinishauri tu na maamuzi ya kumuacha mke wangu yalibakia mikononi kwangu," alisema na kuongeza;

    "... Alionyesha kiburi na ndio maana niliamua kuandika barua ile kwa Spika wa Bunge. Naamini kuwa siku si nyingi yote yataonekana na kwa sasa namuachia Mwenyezi Mungu."

    Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, aamekataa kuzungumzia jambo hilo akisema halihusiani na chama chake.

    Makamba aliliambia gazeti hili kuwa, "usiniulize masuala ya watu, hilo ni suala la watu na kama unataka kuniuliza uliza kuhusu uchaguzi."

    Katibu huyo alifafanua pia kuwa, yeye hawezi sasa kulijadili suala hilo, badala yake yuko radhi kujadili masuala ya uchaguzi.

    Alipotakiwa kuelezea kuhusu utata wa azma ya Amina Chifupa kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM mwakani na kisha kupewa kauli ya kukataliwa, kauli iliyotoka kwa kiongozi mmoja wa juu wa UVCCM, Makamba pia hakutaka kuzungumza na akalitaka gazeti hili kumuuliza siku nyingine.

    Katika hatua nyingine, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Amos Makalla, amewashangaa na kuwabeza wanachama wa umoja huo wanaofikiria kuwania uenyekiti wa umoja huo kwa sasa.

    Akizungumza na Mwananchi jana, alisema yeyote anayefikiria kuwania nafasi hiyo kwa sasa si makini katika siasa.

    Alisema umoja huo hauna taarifa za Chifupa kutaka kuwania uongozi katika umoja huo, lakini akasema hadhani kama mtu makini anaweza kujitokeza hivi sasa kuwania uongozi huo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.

    "Mimi sijui kama Amina Chifupa anataka kugombea UVCCM. Lakini sidhani kama mtu makini anaweza kujitokeza hivi sasa," alisema Makala.

    Chifupa alikaririwa na gazeti moja juzi akisema kwamba kuvunjika kwa ndoa yake kulitokana na nia yake ya kutaka kuwania uenyekiti wa umoja huo.

    Mbunge huyo juzi alishindwa kutimiza ahadi yake ya kuzungumza na waandishi wa habari kumtaja Naibu Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne anayedaiwa kuvuruga ndoa yake.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 08, 2007

    michuzi ebu washawishi nature na inspecta wafanye project album pamoja. tumemis bongoflava project za maana kama ile ya wachuja nafaka! watupe vile vitu vyenyewe sio flava za siku hizi. kuhusu hao juu nachoweza kusema tujadili watu wanaoweza kuadd kwenye uchumi, sio wanaoibia uchumi wa nchi.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 08, 2007

    Umalaya umewazidi wote 2 hakuna aliyetulia kwani mumewe naye ni kipanga wamekutana ngoja waendelee kula uroda kila mtu na nafasi yake. mwisho wa siku UKIMWI

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 08, 2007

    Nani kasema Mh. Amina hajasoma,,, Mh. Amina ana Diploma na vyeo kedekede vya CCM. Angalia URL ifuatayo, si vyema kumchafulia mtu jina kama huna data.

    Mambo yote yapo hadharani!

    http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=314&vusername=GUEST%22)

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 08, 2007

    Jamani eeh, tuongelee generally..Mwanaume akicheat aaah inaonekana kawaida..Hapo sasa mwanamke akicheat (whether Amina cheated or not) inakuwa big deal...Huyu Amina kama kacheat, hayamhusu mtu na ana sababu zake za kucheat, na kama kaachwa ni ya kwao hapo ndani kwake na mumewe..Na kuna udaku ya kwamba huyu bwana ashaoa some Mwarabu chick..Kaaaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 09, 2007

    Hivi mwanamke hawezi kutoa talaka? kwavile ukimwangalia huyu babu na huyo mwanamke hata haviendani sijui alikuaanasubiri nini kupewa talaka. Mimi ningeitoa siku nyingi tu.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 09, 2007

    Kuna a pre-nup hapo? Na nani atapokea alimony....he heh he heeee
    yangu macho

    Ndoa yao ni ya muda gani?

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 09, 2007

    Kumbe bongo kumekua kama sijui wapi vile siku hizi. Watu walikua wanajua kutofautisha sana mambo ya nyumbani na kazini.

    Hivi hizo kazi manazifanya kweli mkishapeleka mambo ya nyumbani kazini. Au mnawaiga kina anjelina jolie na brad pit, britney spear and so forth. Hao ni maentertainer na hata maisha yao wanavyoishi ni yakuentartain. Sasa hata tukisikia habari zao hamna jipya sasa siye tuliwaamini mtu wakilishe bungeni mara


    oh kaingia kwenye office katoka kanipa talaka. Kesho mwingine ataolewa akiiingia kwa office akitoka naye atakuwa mbunge au ataajiriwa kazi nzuri tu

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 09, 2007

    anony wa 5:34:00 PM hujui ulisemalo ni inaonekana uliingia uislam kwa kufata PESA or something else lakini kama unaujua uislam huwezi kusema kuwa TALAKA ni jambo la kawaida,basi kwa taarifa yako UISLAM haupendi TALAKA na nikitu cha mwisho ambacho ALLAH,MTUME na HATA MALAIKA hawakipendi.
    Na kama nawe ulipewa TALAKA jitizame una kasoro gani{waweza kuwa huyawezi mambo,mjeuri,kiburi,hujui kuwajibika,hujui majukumu yako,huna unachokijua kazi kiguu na njia}mbona wako wanaume kwenye ukristo na wana wanawake kibao,ana mke ndani na vihawara nje kibao
    Shogaeee mtoa TALAKA ni tabia ya wanaume kuchukua na kutema.......

    kazi kwako utaolewa na kuachika,jikaze mama kwani ukibebwa JIKAZEEEEE

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 09, 2007

    Sir Issa vipi ..USTAADHI..PICHA HII METOKA VIZURI..NAONA WEWE UKO KULIA MWENZIO YUKO KUSHOTO..SIO MBAYA..." MAMSAP ANATALAKA REJEA HUYO.."..INDEPENDENTI_____"

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 09, 2007

    Hii aikuwa ndoa bali usanii. Ndoa inatokana na penzi la dhati lakini hapa hapakuwepo na penzi la aina yoyote. Amina alitamani pesa za Mpakanjia na Mpakanjia alitamani umaarufu wa Amina kwa ufupi pesa zilioa umaarufu. Hawa watu walikuwa hawakuoana. Kwahiyo nashangazwa na hiyo talaka, labda kama pesa ndiyo imetoa talaka kwa umaarufu. Sababu Amina alikuwa akijirusha kivyake na Mpakanjia kivyake. Mambo ya kupiga picha wamelaliana ni mambo ya kuwaonyesha watu walio wageni katika kijiji cha mahaba.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 09, 2007

    Mimi nawashauri wadau wa blog hii kutembelea tovuti ya bunge kupata Profile ya huyu Amini Chifupa aliyekuwa wa Mpakanjia.
    http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=314&vusername=GUEST%22
    tena huko kaweka hadi na simu yake ya Mkononi. nadhani ni kutekeleza maagizo ya przidaa ya kutaka viongozi waweke simu hazo wazi ili wananchi wawapate kirahisi.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 09, 2007

    jamani mimi nawashangaa sana watu nyie hivi kwani wao ni nani hasa kwa Tanzania hiyo mpaka wazungumziwe usiku kucha? Kama kapewa talaka si basi kwani cha ajabu nini kupewa talaka?

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 09, 2007

    Naona wamempiga kipapai Mpakanjia yupo hoi sasa hivi kitandani.. ama sijui ni nini..?

    Mumewe Amina hoi!

    2007-05-09 16:44:36
    Na Badru Kimwaga, Jijini


    Siku chache tu baada ya `kumlima` talaka mkewe kwa tuhuma za kutokuwa muaminifu, katika ndoa, mfanyabiashara maarufu nchini, Bwana Mohammed Mpakanjia almaarufu kama `Meddy` imedaiwa kuwa hivi sasa yuko hoi bin taaban kitandani.

    Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu mapema leo asubuhi, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mkandarasi wa kutengeneza barabara, amesema hivi sasa yu hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hakuweza kuyafichua.

    Meddy ametoa taarifa hizo alipoulizwa juu ya tetesi zilizozagaa mitaani kwamba kumpa kwake talaka mkewe ni kutaka kutikisa kiberiti na kwamba wakati wowote huenda akamrejea mama watoto wake na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

    Mpakanjia ametengana na mkewe, mbunge wa Viti Maalum-UVCCM, Bi.Amina Chifupa kwa kile kinachodaiwa kuwa bibie huyo alikuwa na mahusiano yasiyo rasmi na mbunge mwenzie toka chama cha upinzani cha CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe.

    `Iwe natikisa kiberiti...kibatari...ama vyovyote, siwezi kusema kwa sasa, kwa kuwa nimechoshwa kuzungumza na magazeti, pia hapa nazungumza na wewe nikiwa mgonjwa, hivyo niache nipumzike,` Mpakanjia akasema kwa upole.

    Hata hivyo pamoja na kutoweza kusema anaugua kitu gani, mfanyabiashara huyo hivi karibuni kabla ya kumpa talaka mkewe alipata ajali ya kuunguliwa na gari na kujeruhiwa sehemu kadhaa za mwili wake.

    Ajali hiyo ilimtokea mjini Morogoro wakati wa akielekea Dodoma kwenye shughuli zake za kikandarasi na kupelekea kulazwa hospitali kabla ya kuruhusiwa baadaye.

    `Sisi tumeshawazoea wanapeana talaka na kurudiana, na hata hivi sasa pamoja na Meddy kuonekana yupo `siriasi`, lakini ukweli ni kwamba anatikisa kiberiti na wakati wowote atamrejea mkewe kama siku za nyuma,` chanzo chetu cha habari kilisema.

    Chanzo hicho kimesema kuwa, wawili hao wanapendana mno na kuachana kwao si rahisi ukizingatia kuwa wana mtoto wanayempenda na kumuona kama `lulu` AbdulRahman `Rahmanino`.

    Mtoa habari huyo amesema si mara ya kwanza kwa Meddy na Amina 'kumwagana' na kisha kurejeana mara panapotokea tatizo baina yao.

    `Kwani unadhani ni mara ya kwanza kwa Meddy kumuacha Amina na kuapa kutorudiana naye ni kama mara mbili ameshafanya hivyo na hata hii ya safari hii ni geresha tu na ukweli muda si mrefu watarejeana na kuishi kama zamani,` kikasisitiza.

    Ndipo Alasiri lilipoamua kumsaka mfanyabiashara huyo kwa njia ya simu na yeye kusema hawezi kusema kama atamrejea mkewe au la kwa vile anaumwa.

    Mpaka sasa hakuna uthibitisho rasmi juu ya tuhuma hizo za mauhusiano yasiyo rasmi na haramu baina ya wabunge hao vijana, ingawa juu ya talaka imethibitishwa hata na baba mzazi wa Amina.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 09, 2007

    Huyo anayesema tusome CV yake basi tumesoma na inaonyesha kuwa kweli tuna viongozi bongo.

    Yaani mbunge mpaka leo bado ana kazi nyingine? Manake kazi zote zinaonyesha bado yupo to date.

    Inasikitisha sana TZ. Mbunge ni muwakilishi wa watu na sio mfanyakazi mahali pengine na kuwakilisha wananchi at the same time.

    Hata umri haukubali kabisa utawakilishaje watu wakati huna experience yeyote? Ndio maana hata maongezi yake ni ya kijinga jinga tu.

    Yaani bongo we have a long way to go.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 09, 2007

    Labda kwa vile life expectancy yetu ni ndogo bongo lakini kama kila siku ukisikiliza hotuba za raisi wetu anayema mambo mengi ni lazima tuige kwa wakubwa zety{ nchi zilizoendelea}. Basi tungeiga na minimum age ya kuwakilisha wananchi. Umri wa mbunge ambaye atakua na japo uzoefu mzuri ni 35 yrs of age kwa nchi zilizoendelea. Huyu mwnadada hana hata life experience yake mwenyewe sasa anatuwakilasha vipi?

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 09, 2007

    Nyie mnaonanga Amina na CV yake mujue kuna wabunge wengine wa special seat ni zero kabisa.

    Mafno huyu Halima - http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=317

    Hata CV haina kitu, na hajawahi kuongea chochote hadi leo bungeni. Hata swali la nyongeza hajwahi kuuliza. Sasa mtu kama huyu anawakilisha nini?

    Amina is courageous despite his limited experience and education. Ndio sababu inayomfanya awe controversial kwa sababu hayuko tayari kujidharau kama jamii inavyotaka. Yaani jamii inataka awe kimya wakati yeye ni mtu anayejiamini bwana.

    Guys, take note and some insipiration from her. She's a born leader !!

    ReplyDelete
  56. Unajua Shigongo na vigazeti vyake vya UDAKU alisema kwa sauti kubwa kwamba Amina hafai kwa `uheshimiwa` watu wakasema ana wivu.Sasa tumemwelewa Shigongo kuwa alikuwa mzalendo msema kweli,asiye na fitina wala wivu katika suala la huyu dada kiongozi wa kundi la `alkaida` ya kupambana na wezi wa waume za watu.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 10, 2007

    Hey asante kwa huyo aliyeweka link ya bunge. Nilikua siijui kuwa ipo lakini mbona kama ni elimu na certificates nadhani mtu anaweka tu. Na hawako makini sanana hayo.

    Nimemwona mbunge mmoja alimaliza chuo kimoja akapata Associate degree{AA} halafu akaenda kufanya Bachelor degree chuo kingine lakini naona wameeka kama BA kote sijui walikosea au?

    Huyo ni mmoja tu ambaye nimefanya five minutes quick search nikaona hilo kwenye elimu!!!!

    sasa haya macertificates wanayoyaonyesha sijui ni ya kweli?????

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 10, 2007

    MICHUZI NAONA UMESHINDWA KULETA HIYO HABARI.NA MWAMBIE AMINA AACHE KULIPUKA HOVYO,SASA ALICHODAI KUWA ATASEMA KWELI DAIMA MBONA HAJATOKEA HUKO MAELEZO KUSEMA HUO UKWELI.HANA LOLOTE MJINGA WA MWISHO HUYO.HAFIKIRII HATA KIDOGO.ALIKURUPUKA,SIJUI TALAKA MLIMCHANGANYA.MBUNGE GANI HUYO JAMANI???ANACHANYIKIWA VITU VIDOGO...

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 10, 2007

    Kwa nini tufiche ukweli ngoja niwaeleze sababu ya Chifupa kuachika.

    Ilipotokea ajali gari ya Mpakanjia ilipinduka na ikaungua na ikamwunguza mpaka njia vibaya sana sehemu za siri na kufanya ashindwe kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa mheshimiwa Chifupa kwa kisingizio cha kuuguza majeraha.

    Sasa kama mjuavyo Chifupa moto juu.Hivi kama una mume hawezi na daktari katthibitisha kuwa hawezi na wewe uko moto juu unafanyaje?

    Kama chakula nyumbani hamna unaenda kula genge la karibu halafu unarudi nyumbani.Chifupa katoka kidogo kala gengeni karudi.Sasa Mpakanjia anampa talaka ya nini wakati sababu anaijua?

    Eti anaumwa maradhi yasiyojulikana baada ya ajali huo ni uwongo aseme wazi nini anaumwa.

    Chifupa dai chako yaishe maana hata akipona atayaweza? Si unajua makovu ya moto.

    Sura ya Mpini itakuwa imeharibika na mpini unaweza kukuumiza sababu una makovu na mafundo fundo kibao yakwaruzayo vibaya anaweza kujeruhi kama alivyojeruhiwa.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 10, 2007

    jamani naona mmefika mbali, haya maoni nadhani imetosha.punguzeni munari.

    kimsingi amina amechemsha haswa!! hana busara. talaka sio sifa... ni balaaa. lakini mwanamke mwenzetu huyu ameshangaza kulinadi swala hili nchi nzima. kusingiziwa kupo, kuchemsha kupo vyovyote ilivyokuwa ila baada ya kukung'utwa talaka ANGENYAMAZA KIMYA. NA KUFANYA JITIHADA ZA KUZUNGUMZA NA MUMEWE KWA UNYENYEKEVU tena angempa mumewe muda atulie kwanza taratibu pengine mume angebaini heshima na upendo wa mkewe na kujirudi. sasa duu' ndo kwanza anatumia umaarufu wake kujiharibia zaidi. itikadi ya ndoa si kuonyeshana nani ni nani. mi sidhani kama amina alifundwa, maana hajuai kama ndoa ni utakatifu na kifungo cha 'upendo' ambao hauhusudu, hauhesabu mabaya hvumilia wala hauoni kosa. suluhu ya kweli katika ndoa ni kati ya wawili wapendanao. umejiaibisha dada ila mi sidhani kama umechelewa. mtafute mumeo faraga uvae sura ya kike yenye unyenyekevu na upendo uzungumze na baba nino. hope yataisha.

    pamoja na kuchemka huku chonde wadua msiongee matusi, wala tusichochee ndoa kuvunjika. Mungu hapendi.

    mama Gs

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 11, 2007

    GOODNESS WITH ALL SUCH PUBLICITY THESE TWO ARE GOING TO BECOME THE POSH AND BECKS OF TZ!!!

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 11, 2007

    Kaka Michuzi shikamoo!!!!!!!!
    Samahani naomba kuuliza tu kwa wadau wachangia mada,MPINI ndio nini?Maana nimeona sehemu nyingi limetumika,nimejitahidi kuangalia ktk kamusi yetu naona haileti maana hapa.Tafadhali usinibanie,nataka kujibiwa.Ahsante

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 11, 2007

    Wewe "Tarehe Friday, May 11, 2007 8:00:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Kaka Michuzi shikamoo!!!!!!!!
    Samahani naomba kuuliza tu kwa wadau wachangia mada,MPINI ndio nini?Maana nimeona sehemu nyingi limetumika,nimejitahidi kuangalia ktk kamusi yetu naona haileti maana hapa.Tafadhali usinibanie,nataka kujibiwa.Ahsante"

    Unataka kujua MPINI, je unakipago? Wape watu wachane kipago kwa mpini.

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 11, 2007

    We anon 8:00 acha utani bwana yaani wewe kila siku unaushika na kuutumia unauliza MPINI ni nini?,

    MPINI ni MKULUNGU au MJEBELE au
    MWICHI au MTWANGIO au PIPE au
    MKITIKISIO au ....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...