njenje plaza a.k.a ambassador plaza a.k.a gogo hotel ndiyo hiyo inapigwa nyundo kupisha kikwangua anga cha kampuni moja ya simu (jina kapuni hadi kieleweka). lakini wapenzi wa kilimanjaro band wana njenje waliokuwa wakiduarika hapo kila jumamosi wasikonde kwani tayari waziri na wenzie wameshahamia bwalo la polisi ostabei ambako watakuwa wakitumbuiza kila siku ya ijumaa kuanzia ijumaa hii ya tarehe 27 julai. nyote mnakaribishwa huko ijumaa hii na nyingine zote kuanzia ijumaa hii. nani kasema mduara wa njenje utakufa baada ya hili?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2007

    Watakao kuja kuchezea mduara hapo ni waboreshaji maisha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2007

    Bwana Michu bwalo la polisi mbali kishenzi huko wataenda hao wenye nazo. Japokuwa wapo wapenzi wa njenje wengi kwenda huko itakuwa tabu kwanini wasihamia Laprima maeneo ya Victoria? Pale pamekaa safi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2007

    Kweli wewe ni kiboko! Kikwangua anga!. Hili ni neno brand new. Du! Kaka, tafsiri zako ni mwanana kweli kweli

    ReplyDelete
  4. Kwa kifupi ni kwamba CELTEL wamechukua eneo lote hilo wanajenga ofisi zao mpya ambazo zitakuwa hapo i think wameamua kuachana na TTCL kila mtu awe kivyake.

    ReplyDelete
  5. Michuzi, kweli una camera nzuri. Nakumbuka ulivyopiga hiyo snap ya ubomaji wa UWT hostel kipapparazzi hasa, huko unendesha gari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...