wafanyakazi wakiandamana jana kushinikiza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyongeza za mishahara. habari kamili fungua www.dailynews-tsn.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wanablogu wenzangu, kuna madau ameomba Bro. Michu aweke picha za maandamano ya wafanyakazi. Wakati na mimi nikitaka kusapoti hoja hii nikakumbuka Michu ni mfanyakazi wa serikali na serikali kwa hili la maandamano ni KAMBI YA UPINZANI sasa itakuwaje???

    Hongera bro naona angalao umetunyamazisha waosha vivywa kwa kutuelekza tukasome kwa mwajiri wako Dailynews, ila sio mbaya

    adagio

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli inasikitisha sana kwa ndugu zetu hao wanaotumikia Taifa kwa mshahara mdogo sana na kwa kazi ngumu wanayo ifanya,kitu cha kusikitisha viongozi au wabunge wanakaa chini kwa muda mfupi wanachukua pesa nyingi sana.Serikali fanyeni kila njia kuinua maisha ya wananchi amasivyo tunaweza kuleta matatizo ndani ya nchi.

    ReplyDelete
  3. Unajua nimesoma comment kwenye farasi weupe kuwa tuwekee picha za maandamano,sikuelewa ila sasa ndio naelewa. Ila nina swali kwako michuzi, ulitoa picha za Farasi weupe ili kutishia wafanyakazi wa serikali wasiandamane?
    Actually hao TUCTA watanifurahisha wakiitisha na mgomo in less than two weeks.
    Sasa tunaanza kuamka,ila michuzi you need to know to role you are playing and you should play it. Since I have known your blog I hardly visit IPP;only now come to learn that you against even your self!

    ReplyDelete
  4. Bwana Michuzi, mimi si mtoaji wa maoni ila kwa hili naomba nilizungumzo maana linantia nchecheto.
    Wabongo tunapozungumzia uzalendo ni pamoja na mambo kama haya ya haki za wafanyakazi. Siwezi kumlaumu Bwana michuzi kwa kuto post picha za maandamano kwa kuwa najua yeye ni mtu makini na inawezekana anasababu za msingi za kufanya hivyo. Ingawa bado hainiingii akilini kama hali ya maisha ya watumishi wa umma wa kada za chini in any way inamfurahisha mtu yeyote. Ndugu zetu TUCTA wameshindwa kuvumilia wakaamua kuandamana, Bw. Michu kavumilia, kaamua kutotoa support kwa kutokupost picha zao. Suala hili siyo la kisiasa kama wengine wanavyoweza kufikiri. Ni bomu ambalo linaweza kulipuka any time kama hakuna hatua zitakazochukuliwa maana leo ni TUCTA, kesho itakuwa TUCTA, wanafunzi, wakulima, wafanyabiashara n.k sijui hali itakuwaje.
    Kwa hali hii,ikihusishwa na mambo mengine ya kashfa za rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma,maamuzi na usimamizi wa utekelezaji wa maamuzi hayo ya serikali yaliyotufikisha katika hali hii nashindwa kumjua mzalendo ni yupi....Wadau nisaidieni.

    ReplyDelete
  5. what i see here dear tanzanians.....TUCTA should give the gvt a dealine for a resonable answer or else TUCTA should call a national buoycott....some thing im sure its like a day dreaming coz till now im sure some top leaders of TUCTA MIGHT HAVE STARTED RECEIVING INTIMIDATIONS FROM ANNONIMUS and others, the dubious ones have received MIRAHABA and they will never open their mouth any more...this is how TZ operates....NAWAPENI MIEZI MIWILI TUPINGE KM MTAWASIKIA TENA tucta...wakipigwa tu bit wote watasepa....hata ivo nina shaka hawa TUCTA wamewika ili kuwawahi Wadanganyika wasije kuwakaba makoo kuwa TUCTA hawakutoa tamko juu ya nyongeza hii finyu.....byebye...watizedi bora yetu sie...

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na anony wa August 13, 2007 10:24:00 AM EAT: TUCTA nao wanaweza kuwa ni danganya toto kabla halijalia. Kwa mtizamo wangu kuleta mabadiliko ya kweli inashindikana kutokana na factor nyingi zinazomkabili mtanzania wa leo, chache zinazoonekana wazi ni: Uoga-unaotokana na intimidations zinazotolewa na wenye system; Kutoaminiana-mtu akisimama kidete kutetea wanyonge anaonekana kama katumwa au ana dili;Umaskini-Mtu hawezi kutetea haki yake kwa sababu anaogopa hata kidogo alichonacho atakipoteza.
    Kuna watu wazuri tu wanaoweza na wana platform ya kutetea wanyonge kama Michuzi na wengine, lakini hawawezi kwakuwa wako linked na system, pamoja nakuwa tunajua hawapendi mambo mengi yanavyoenda. Kwa hali hii kweli anony bora yenu nyie.....

    ReplyDelete
  7. michuzi uko kwenye ninja moja nini mbona comment yangu hujaweka...au na wewe kazi yako iko hapo inakusubiri....vinaumiza sana lakini Mungu atawaona tu siku moja...Machozi ya walalahoi hayaendi bure kama hizo kazi mnagawiana wenyewe..
    uweke usiweke lakini umeelewa

    ReplyDelete
  8. Serikari kuweni makini haya mambo ya maandamo ndiyo chanzo cha matatizo na machafuko ya nchi,kitu muhimu jaribu kuwafikiria hao wanaojiita walala hoi, na kweli ukiona maisha wanayoishi ni mabaya sana.

    ReplyDelete
  9. MAANDAMANO NINI BWANA!!! UPUUZI MTUPU....WATANZANIA WANAFIKI TUUU SI HAO HAO JUZI TU NDO WALIMPIGIA KIKWETE KURA?????Wangefanya mabadiliko,SI HAO HAO KILA UCHAGUZI WANAWAPA CCM????Lazima mkomae na wabunge mishahara iongezwe sana mpaka wafanyakazi na wakulima watakapojua cabbage ni mboga na pia ni kachumbari......na uchaguzi ujao mtapatia kura tena yaone eti yanaandamana WANAFIKI TUU.

    ReplyDelete
  10. KUANDAMANA SAA HIZI WAKATI MMEWACHAGUA WENYEWE

    HALAFU WABUNGE WENYEWE BUNGENI NIMICHEMSHO TU. JAMANI MNAANGALIAGA START TV...HILI BUNGE LINALOENDELEA IT IS SO FUNNY?

    ONE DAY NILICHEKA SANA ETI RAIA TUNAOISHI NJE TUNAUZA UNGA AT, THE SAME TIME AKASEMA INGEFAA SERIKALI IWE KARIBU NA RAIA TUNAOISHI NJE ILI TUWEKEZE NCHINI ZAIDI....WHAT .....TUWEKEZE BIASHARA YA UNGA....? ETI UBALOZI HAIJUI IDADI YA WATU WALIO NJE...HIVYO WAKIJUA NANI YUKO WAPI ITASAIDIA HIYO BIASHARA YA UNGA....I WAS LIKE...HE MUST NOT BE SERIOUS...?????

    ReplyDelete
  11. mi kusema ukweli naona hata Tanzania yenyewe inge binafsishwa maanake wenye nchi wenyewe wana struggle(wanahangaika)kuiendesha vizuri labda matatizo yatapungua najua hayawezi kuisha.msiwanyime watu haki zao.haya mambo hayakuwepo siku za mwinyi!

    ReplyDelete
  12. hivi kila mtu ni anonymous jamani? hata kwenye zama hizi za uhuru wa vyombo vya habari? acheni hizo, msiwe waoga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...