Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Lively Michuzi, ukiwa na muda kufotoa kila siku Mungu atakuongezea maisha. Sina cha kukupa, waafrika tunatoa sala inatosha.

    ReplyDelete
  2. Kusema la ukweli Kabwe ni Machachari sana, na anawasumbua vichwa watu viongozi bungeni, kwa kuwa ana akili, halafu anajua anachokiongea. Mbali na umri wake nadhani yeye kama mbunge yupo sawa kuhoji jambo kama hilo ambalo sisi tulikuwa hatulifahamu. Watu kama hawa ndio tunaotaka watuongoze ili watupe nyepesi za mambo WANAYOYAFANYA HAO WALA JASHO LA WATU TENA WALALA HOI. HIVI HAO WABUNGE BUNGENI WANAOMSUPPORT SPIKA AKILI ZAO NZIMA? HIVI WAO WANATETEA NINI HASA? HILO LIKO WAZI KUWA WAKO BUNGENI KWA MASLAHI YAO WENYEWE, NDIO MAANA WANAUNGA MKONO UPUMBAVU, NONSES KABISA HILO BUNGE LA BONGO OVYOOOOOO!!!

    Ila pia wasi wasi wangu ni kwamba, jamani wasije mmm ''Chifupalize'' manake kwa kweli tunamhitaji sana. Kwanza ni msomi bwana.

    Kabwe We are proud of you lakini naomba na wewe KAWANGE KWANI HAO WANAENDAGA WAPI KUROGA WANA CCM, NA WEWE NENDA ILI WASIKUWEZE.
    aLL THE BEST KABWE! WE REALY LOVE YOU!

    ReplyDelete
  3. Hii issue nzito hasira inanifanya nitoe maoni kila mara,
    lazima mtu atoke damu-Zitto hawezi kuondoka mwenyewe:
    Napendekeza wafuato wachunguzwe na kuadhibiwa ipasavyo:
    1) Karamagi-kwa kutia saini mikataba bila kufuata utaratibu uliowekwa
    2)Sitta-kwa kupindisha sheria za bunge kwa manufaa ya CCM

    Kikwete kama unasoma haya maoni, tafdhali ongea na wananchi la sivyo umaarufu wako utakwisha!!

    ReplyDelete
  4. Aibu sana kwa 'Sirikali' ya huyu Mkwere, yaani kaaaaazi kweli kweli! Asitarajie kupata tena asilimia 80 mwaka 2010. Yaani mbunge kukosoa maamuzi ya ubinafsi imekuwa nogwa?

    ReplyDelete
  5. michu hebu tuweke picha ya nazir karamagi tumuone tafadhali, maana hata kwa sura simjui.
    kutoka ughaibuni

    ReplyDelete
  6. toa pumba hizi na rushwa zenu za siasa huko bongo, lets talk about social events and not corrupted politics

    ReplyDelete
  7. yaoneni majambo hayo!
    http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4503

    Posted Date::8/16/2007
    Slaa aondoa hoja ya BoT, adai hakuna jema bungeni
    *Aenda kushtaki kwa wananchi
    *Ikishindikana, kuchongea kwa wafadhili

    *Adai ameanza kutishiwa maisha yake

    Na Waandishi Wetu, Dodoma

    MBUNGE wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa (Chadema), amefuta kusudio lake la kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kutaka iundwe kamati teule kuchunguza ubadhirifu katika taasisi nyeti za umma, ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kile alichoeleza kuwa Spika wa Bunge, Samwel Sitta, hajaiweka hoja hiyo katika shughuli za Bunge tangu alipoiwasilisha.

    Dk Slaa alitangaza kufutwa kwa kusudio hilo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa jana, huku akieleza kuwa suala hilo limezua mzozo ambao utakuwa na madhara kwa mustakabali wa Tanzania.

    Pia, mbunge huyo alitangaza mchakato mbadala wa kutaka suala hilo sasa lianze kushughulikiwa kwa njia mbalimbali ili hatimaye ukweli uweze kudhihiri na kuwekwa wazi.

    Akiongozana na wabunge karibu wote wa kambi ya upinzani, akiwamo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Wawi-CUF), Dk Slaa alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini kutokuwapo kwa dhamira thabiti na dhati ya Bunge, chini ya Spika Samwel Sitta kuweza kukaa, kusikiliza, kujadili suala hilo nyeti wakati wa kikao cha Bunge kinachomalizika leo.

    Licha ya kuvipongeza vyombo vya habari nchini kwa kuwezesha kufichuliwa kwa maovu mengi, Dk Slaa alieleza kuwa vikwazo alivyowekewa tangu mwanzo na Spika Sitta alipoamua kueleza dhamira ya kuanza rasmi mchakato huo, vimemkatisha tamaa.

    Jumanne asubuhi, kabla ya Bunge kuanza kusikiliza hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (aliyesimamishwa), Zitto Kabwe, Spika Sitta alieleza kwa ufupi kuhusu hoja ya Slaa.

    Alieleza kuwa suala hilo ni zito, lakini linalohitaji ushahidi, lenye kumtaka pia yeye (Spika) ajiridhishe kwanza na ushahidi wowote ambao unawasilishwa kwake na mtoa hoja (Slaa).

    Akizungumza kwa umakini mkubwa, lakini wenye kuonyesha dhahiri hasira, Dk Slaa alieleza kuwa licha ya kutotakiwa na kanuni za Bunge kumridhisha kwanza Spika Sitta kabla ya kuamua kuwasilisha hoja binafsi, lakini Agosti 13 aliwasilisha ushahidi na vielelezo vyote.

    Jambo hilo alisema alilifanya ili kuthibitisha unyeti wa suala lenyewe na

    kuonyesha kitabu ambacho alisema ushahidi umekusanywa kwa umakini mkubwa kutoka hata ndani ya taasisi za serikali kwa mujibu wa sheria.

    Aliyataja maeneo mahsusi ambayo hoja yake ilikuwa imejielekeza zaidi kuwa ni makampuni ya Mwananchi Gold, Meremeta, Tan Gold na Land Gold na kuongeza kuwa ushahidi wote ulikuwa katika vipengele A-F.

    Alieleza mshangao kuwa licha ya Spika kukabidhiwa tangu Agosti 13, lakini hadi jana hakuwa ameonyesha dhamira ya kuiweka hoja hiyo katika taratibu za mikutano ya Bunge.

    "Ni dhahiri kwamba tumebaini licha ya uzito wake, lakini hoja hii nzito yenye maslahi kwa wananchi inaendelea kupigwa danadana na kutokana na uamuzi huo tumeamua kutafuta njia nyingine kulishughulikia ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwa wananchi," alisema Dk Slaa na kuongeza;

    "Tuna wasiwasi kwamba hizo ni mbinu za makusudi za kuificha ili isiweze kufahamika kwa wananchi wetu ambao ndio wametutuma na kutuingiza hapa bungeni. Viongozi wetu, watueleze wanachokiogopa ni nini hasa," alihoji Slaa na kuongeza;

    "Lakini, viongozi wetu watambue kuwa hata kama Tanzania inaendelea kusifiwa kimataifa, lakini uovu kama huu unaofanyika sasa, unafichwa na matokeo yake walalahoi ambao ni maskini wanaendelea kuteseka ungefichuliwa ungesaidia kulijengea heshima Bunge ambalo ni taasisi inayotakiwa kusimamia serikali," alieleza mbunge huyo.

    Aliongeza kuwa inashangaza kuona viongozi wengi walioko madarakani wanapenda kuwasiliana hata na mashirika na wahisani walioko nje, ikiwamo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa lengo la kujikosha ili waonekane wasafi, kumbe kuna mambo wanaficha ukweli wake.

    Bila kuwataja viongozi wahusika, Dk Slaa alidai kuwa viongozi hao wameikosesha nchi kiasi cha Sh2 bilioni kutoka kwa wahisani hao hao tangu mwaka jana kutokana na kutorejeshwa kwa fedha walizokopeshwa na zilizotokana na mfumo wa

    ununuzi wa madeni.

    "Tuna wasiwasi. Tuhuma hizi za wizi na ubadhirifu ni nzito, zinahitaji uchunguzi na kuchukuliwa hatua zikiwamo za kuwasimamisha wahusika, lakini tunashangaa kuona wanakingiwa kifua," alieleza.

    Aliongeza kuwa wasiwasi wao ni kuwa hicho kinachojaribiwa kufanywa kwa sasa si kizuri, huenda ni kutaka kuuchezea hata huo ushahidi, vielelezo vyote ambavyo vimewasilishwa kwa Spika na huenda ndiyo maana kumekuwapo na ucheleweshaji usio wa msingi.

    Mbunge huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, alisema baada ya kuondolewa kwa hoja hiyo, upinzani umedhamiria kuchukua hatua kadhaa zikiwamo za kisheria, kuwasiliana na wananchi kwa njia mbalimbali, ukiwamo mkutano wa hadhara ambao utafanyika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam kesho.

    Hatua nyingine, aliitaja ya kuwaeleza pia wafadhili na wahisani mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiwamo Benki ya Dunia na IMF kuhusiana na suala hilo.

    Hata hivyo, alisema kuwa rufaa pekee na kubwa itakuwa ile ambayo kwa kutumia umoja wa wapinzani, itakatwa kwa wananchi wote wa Tanzania ambao ndio wamepewa dhamana ya kuwaweka wao madarakani.

    Kuhusu madhara yanayoweza kutokea kutokana na kuondolewa kwa hoja hiyo bungeni, Dk Slaa alisema wamejiandaa kukabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kukumbana na vitisho kama vile ambavyo wamekuwa wakipata vikiwamo vya kutishiwa maisha.

    "Tunajua athari zake, mbona tumekuwa tukipokea SMS kwa kutumia simu na namba binafsi, baadhi zinatishia maisha yetu, nasi tuko tayari kwani hii ni vita ni sawa na askari shupavu anayefia vitani akipigania nchi yake," alisema.

    "Hatuna tone la hofu, tunapigania haki ya maskini wa Kitanzania walio wanyonge," alisema mbunge huyo na kuongeza kuwa wamekatishwa tamaa, kiasi cha kuamini kuwa hata ikiwasilishwa bungeni hoja hiyo ingezimwa kama nyingine.

    Naye Hamad Rashid Mohammed alionya dhidi ya tabia ya viongozi wa Tanzania kutoishi na kuheshimu viapo ambavyo waliapa wakati wakiingia madarakani na kukumbatia maovu.

    Alisema kutokana na kukosa aibu na utii kwa viapo vyao, ndio maana wamekalia kimya tuhuma za ujenzi wa minara pacha ya BoT ambayo imeiingizia nchi hasara inayofikia dola milioni 600, lakini hakuna kiongozi anayejali au kusumbuliwa na suala hilo.

    Aliongeza kuwa hata wakaguzi wa hesabu wamenyimwa taarifa muhimu hivyo kutia mashaka juu ya suala hilo.

    Alidai kuwa BoT bila ruksa, uhalali wowote imetoa mikopo inayofikia Sh30 bilioni bila dhamana , jambo ambalo alisema wataendelea kulipigia kelele kama ambavyo wanafanya.

    ReplyDelete
  8. chama kinachotumia jembe na nyundo kama harama unategemea kitaingoza nchi bila kuiburuza.... ukileta nyoro nyoro unapigwa ngundo afu jembe linakuzika...... duh jamani tanzania tutafika kweli....

    ReplyDelete
  9. Tatizo ni spika wa bunge na atakapostaafu utasikia kusema ohoo!! kweli tunahitaji marekebisho,umemsikia juzi yule spika a zamani msekwa na warioba naye ana dai kuikosoa serikali baada ya kuona hawana kitu ndani ya serikali.

    ReplyDelete
  10. Hoja ya Zitto hii http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/8/16/makala1.php

    Sioni alichosema UONGO maana Waziri alishakiri kuwa kweli alisaini mkataba UK

    ReplyDelete
  11. unayedai sura ya KARAMANGI, HEBU JARIBU KUTAZAMA HUYO ALIYESIMAMA JUU YA KABURI YA NYERERE.

    TENA MZUKA WA NYERERE UKIPANDA, WEWE KARAMANGI UTAIPATA. NADHANI KWANZA NYERERE HUKO ALIKO ANA HASIRA NA WEWE ULIVYOSAINI MKATABA BILA KWENDA KWENYE KABURI LAKE.

    ASANTE MASOOD KIPANYA. NA WEWE MASOUD WAKIKUANZA HOOOOOHH!!! HAO WANYONYA DAMU WA CCM NI NOMA ati

    ILA HUYO KARAMANGI AKILI ZAKE ZIKO OK KWELI? MBONA ANATOA SABABU ZA WATOTO WA CHULE YA VIDUDU?

    NAOMBA KUTOA HOJA WAHESHIMIWA

    MAWAZIRI WAPIMWE MAGONJWA YA AKILI KABLA YA KUAPA KIAPO CHA UONGOZI.

    THEY PREACH WATER THEY DRINK BEER.

    SINA LA KUSEMA, NCHI INA BORE SANA, NDIO MAANA HATUTAKI KURUDI. MAANA ROHO INAKUUMA CHA KUFANYA HAKUNA.

    ReplyDelete
  12. Wangejua ndio wamempa umaarufu Zitto wasingesema. I'm sure wanajuta kimoyo moyo, sema hawawezi sema.

    maana hata wasiomjua sasa wanamjua.
    na ukizingatia ishu yenyewe madini, basi kila mtu inamgusa, maana ni mambo ya chapaaaa, achana na mambo ya pesa bwana. Wakristu wanakubaliana nami kuwa zilimuuwa Jesus.

    ila jamaa ccm ni wanga usipime siku huyo mganga wao akifa jamani, nadhani sisi ndio tutapona.siku yao inakuja kama chama cha KANU, hakuna kisicho na mwisho jamani.

    ReplyDelete
  13. unajua kikwete alipo ingia madarakani alikuwa na kasi mpya sana! na kwa siku 100 tu kama rais,aliweza kuwaumbua viongozi wengi lakini kwasasa kasheanza kudorora kabisa.
    Inakuwaje mtu anatoa hoja! then bila uchunguzi mnamfuta kazi! thts bull s***t, wangefanya uchunguzi kwanza, lakini walicho fanya! ni UDIKTETA! mi mwenyewe ccm lkn walichofanya si vizuri kabisa! zombe ni shujaa! wa Watanzania wote kwani hoja yake ilikuwa kwa manufaaa ya Watz wote!

    ReplyDelete
  14. Daaaaaaaaaa
    Mh.Kabwe,ZITO
    Kigoma Kaskazini

    ReplyDelete
  15. Just simple logic connecting variables; Karamagi hakuwa ziarani na Rais ng'ambo wakati akisaini Contract? Mkataba haukupata baraka ya baraza la mawaziri kabla? Mwekezaji mkubwa kiasi hiki anaweza kuwekeza nchini bila kiongozi wa nchi kupenda/kujua/kubariki? Waziri hamuogopi boss wake? Share holders wakubwa wa CASPIAN (wanaoshinda kila tenda za kufanya kazi na wawekezaji ktk madini) ni kina nani? Kwani mawaziri takribani 60 si ni wabunge bungeni? Mke wa spika si ni waziri? Haongelei SIRI za Baraza la mawaziri hata kwa mumewe? Kwani wabunge wote wa CCM si lazima wafahamike vizuri na vikao vya CCM na hata mwenyekiti wa chama? Sasa unategemea nini hoja ya Kabwe na nyingine "NYETI" Zipite Bungeni? SITASHANGAA MICHUZI USIPOIWEKA HII.

    ReplyDelete
  16. Michuzi!

    Naomba waandishi wa habari wewe wanasema BAADHI YA WANANCHI WANAMLILIA KABWE! NA HUYO ANAESEMA PUBLIC ANGER please naomba wawe specific binafsi, huyo ZZK (ZITTO ZUBERI KABWE) awe bungeni asiwe, sioni tofauti ya utawala kwa hiyo sijachukia wala sina uchungu wowote na suspension yake. Kwanza alizoea hizo suspension toka alivyo kuwa shule sasa hakuna jipya kwake hapo.

    Hao wabunge wanaojidai kumchangia hizo pesa wakati katika majimbo yao akina "Kayumba" wapo kibao nawashangaa sana waache kufuata mkumbo, ACHENI HIZO!!!

    Serikali yetu akiamua imeamua hapa ni kutiana hasira tu. MWACHE aende huko kwenye Migodi alete data kamili sio kuumiza vichwa vya watu! Ongeza mjadala ZZK magezeti yauze then wakupe %

    ReplyDelete
  17. Kabwe ni kKiboko yao
    kama mnavyojua hii ni nchi ya Wadanganyika ndo maana serikali ishazoea kuwadanganya kama watoto. Wamesahahu kama wabunge wa sasa ni wasomi na hawaogopi. Tuache kuwa wadanganyika tuungane na Kabwe kuiokomboa nchi yetu tuache bla bla. Wabeba boksi rudini tujenge nchi.

    ReplyDelete
  18. Nimesoma hoja aliyoiwasilisha Kabwe, aisee kijamaa kimeenda shule na kimesoma documents zote. Inaelekea hata shuleni huyu alikuwa book worm. he understands what he is talking about. Hakuwa na jazba alipowasilisha hoja. The wording was perfect. Nadhani huyu ni kijana moto sana. Mh, unahitaji ulinzi wangu Zitto.

    ReplyDelete
  19. SITA NDIO KAISHIWA KABISA,YANI HATA HAJUI ANALOLIFANYA,NIMESIKILIZA MAHOJIANO YAKE NA BBC,HAKIKA SIKU ZA UHARAMIA ZINAHESABIKA,SITA UNANIUDHIIIIIIII,NA WEWE MUDHIHILI KAMA NIKUKUTA KWENYE GIZA NITAOMBA DK 5 THEN WATU WATASEMA KUWA UMEPATA AJALI,NA HUYO KALAJONGI SIJUI NDIO HATA SITAKI KUMSIKIA,KWA KWELI INAKERA SANA

    ReplyDelete
  20. Duh kwa spidi hii tutakuwa na msamiati mpya hivi karibuni... "ku-kabwe". Huyu kijana watamkabwe hao nyang'au wa CCM bwana. Hicho ni chama cha Nyundo na Jembe, ukileta matata wanakutia nyundo kisha jembe linachimba kaburi lako.

    ReplyDelete
  21. Zitto anajaribu na vijana tunatakiwa kumuhunga mkono ktk uchaguzi wa 2010 na lazima watu wawe ccm kuleta mabadiliko na kama blair alivyofanya labour lazima kuwe na new ccm kwa mwendo huo wazee wote tutawazika maana wamefikia kustaafu ila wanataka kufia bungeni sasa inamaana gani bunge sio sehemu ya kusubiri kufa ni mahala pa kutunga na kulinda maslahi ya nchi.
    Mimi binafsi nina toka mikoa ya kusini mbunge aliyetoa wazo la kuwa zitto afungiwe ni mjinga ajabu na toka apate ubunge hakuna shule wala dispensarly iliyojengwa ktk utawala wake na ni mshirikina ajabu,kama mnakumbuka ndio alikuwa mmiliki wa mchinga sound na kwa kutokuwa na akili na upumbavu wake na una invest ktk music wakati watu wako awajui kusoma ni akili kweli hiyo michuzi?
    Nitajaribu kuwakilisha picha za jimbo la mchinga ili watu mjionee wenyewe na mtajua huyo jamaa ni mjinga kiasi gani na mpumbavu wa kutupa.
    Sina nia mbaya na nchi yangu ila kama kijana nina asira sana na hali ya siasa kwa ujumla na njia muafaka wa kutoa hawa wazee & wajinga ktk siasa ni amani ikishindikana ni kuingia msituni tu na sio kwa ajili ya kumwaga damu ila kuwa mafia wa siasa na kuondoa mmoja baada ya mwingine na kuweka hali sawa ndio njia sahihi.

    ReplyDelete
  22. Unajua kwenye mikataba kunasemaga wenye madini wanufaishe wananchi wanaozunguka migodi, lakini sijawahi kusikia wamejenga shule nzuri ya kisasa, hospitali au basi zahanati ya kisasa au kitu chochote kikubwa katika machimbo yote kulingana na faida kubwa mno kupindukia wanayo ipata.Hakuna mtu wa kuwabana wajenge akisha pewa 10% basi anatulia wanataka wakiugua wao ndio waende south afrika wakati wananchi wavuja jasho wafie kwenye hospitali hatarishi. Vile vile msisahau karamagi ni mfanya biashara mkubwa tu mwamba ngoma huvutia kwake, pamoja na kwamba JK anataka ushahidi kama wa kukamatwa ugoni hata mpata mtu ataishi akitazama (kama ule wimbo wa waluteri ni ujumbe wa bwana)yatakuja kuibuka makubwa wakiondoka madarakani kuliko ya Yona na Mkapa subirini

    ReplyDelete
  23. Mi ni mwanaCCM na tatizo lenu nyie hamjui nini kinaendelea hayo mashimo yote ni mali za vigogo wa CCM na ila kijana anataka kutuumbua uchunguzi wa nini? kaa bila kazi Sisi na familia zetu tunafaidi nini kujali watanzania shauri zao ngoja wafe na njaa na magonjwa.wanangu wanasoma nje natibiwa nje, mi na mke wangu ni wabunge sasa shida ya nini kidumu chama cha mapinduzi oyeeeeeee mlie tu.

    ReplyDelete
  24. Huyu kijana Zitto ni Hatari sana kama anakuwa na uwezo wa kufichukua jambo kubwa kama hili basi anatufaa sana! Na huyo Spika wa Bunge jamani awajibishwe mbona tangu aingie yeye bungeni kila siku kuna matatizo kwa kweli Demoksrasia bungeni imepotea ajiulize mbona mambo kama haya yalikuwa hakuna wakati wa Pius Msekwa?

    ReplyDelete
  25. MICHUZI
    Mimi nafurahi unavyowapa news za home hawa wadau wa mbele 'abroad' lkn mbona wanajifanya wao wanajua sana...kuna jamaa anasema ndio maana hataki kurudi bongo kisa viongozi wazushi, sasa kuna bill kuhusu dual citizen washkaji kama hawa unaona wanastahili coz wanonekana vimeo. isue ya kabwe ni ivi mh katoa hoja ila wabunge wa ccm wana utamaduni wa kufanya kazi kwa pamoja kama walivyokubaliana kwahiyo hawawezi kumsuport zito, tukichukulia demokrasi ya kweli haiwezi kupatikana bungeni mpaka vyama vya upinzani viwe imara, walau wapate 40% ya viti bungeni...beside mh zito alipoambiwa ajitetee akajibu ''NIMESEMA NILICHOTAKA KUSEMA, BUNGE LINA KANUNI ZAKE NA SPIKA NI MWANASHERIA NATUMAINI LITANITENDEA HAKI' japo alisema revolutinary ideas cant burn...inaonesha kabwe alijua amechemsha ndio maana akasema anajua atatendewa haki, kwahiyo msiwe mashabiki kiivyo, muhimu ni kwamba wadau washinikize serikali ipeleke huo mkataba uchunguzwe kuona kama una mapungufu kama mikataba mingine ya madimi inayolalamikiwa siyo eti mkataba umesainia london...wadau ehe juzijuzi nilikuwa geita yani makaburu wanavyosafirisha matani ya vito ni isue wa2 wangu yani jk akimaliza ngwe ya 2 itakuwa mahandakizzz.....
    DUAL CITIZEN,,,wadau wote mliojilipua mbele 'abroa' ndio maana hamtaki kurudi home, bill ya dual cit itakwamishwa coz mnaonekana siyo wazalendo ndio maana wengine mmebadili uraia 'nyie ni matraitor'..kama ni ajira mbona kuna washkadau wanakula mipunga ya maana na life inaendelea, mbona tulikuja kwenye miss tz uk mbona kuna washkaji wamechoka hata bongo inatia hamasa rudini bwana kuwa abroad siyo isue kama ndivyo mnavyoishi wazee....can pls have a moment of silence or let pour some liquor kwa wadau waliotangulia mbele ya haki.

    Kha, mji mkongwe

    ReplyDelete
  26. We bwege hapo juu, hujui unachoongea!

    ReplyDelete
  27. Anon. wa August 18, 2007 5:35:00 PM EAT, Kha mji mkongwe, tafadhali nenda ukajifunze kuandika. Hiyo shule uliyosoma inabidi ifungwe... nimeshindwa kukuelewa kabisa.

    ReplyDelete
  28. Wabongo wabongo wabongooooo,mnatishaaaaa.Lol nakumbuka miezi si mingi Zitto alikuwa anatukanwaaaaa kooote,yaani ilikuwa issue nzitoooo.eh kuna mtu hapo juu kadiriki kusema we love you zitto.Jamani muwe na msimamo mkimtetea mtu iwe ni hivyo akikosea si wooote mnamgeukaa,yaani mfanye for better or worse.Ah namlilia Mheshimiwa Amina Chifupa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...