RICHA ADHIA NDIYE MISS TANZANIA 2007 BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA USIKU HUU KWENYE FAINALI ZA VODACOM MISS TZ PALE LIDAZ KLABU. MSHINDI WA PILI NI LILIAN ABEL AMBAYE KAMA RICHA KATOKEA WILAYA YA KINONDONI. WA TATU NI QUEEN DAVID AMBAYE NI MISS TEMEKE. TAJI LA BALOZI WA REDDDS AMBASSADOR LIMENYAKULIWA NA VICTORIA MARTIN AMBAYE NI MISS TANGA NA MISS KANDA KASKAZINI. HII NIMARA YA KWANZA TOKA MISS TZ IFUFUKE MWAKA 1994 KWA MBONGOMWENYE ASILI YA KIASIA KUNYAKUA TAJI HILO.

SUBIRI MASNEPU KIBAO MUDA MFUPI UJAO....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 82 mpaka sasa

  1. maybe a change might work who knows.anyway all is good ,but wasnt my favourite choice
    mpenda nchi

    ReplyDelete
  2. Ama kweli!Nakumbuka aliposhinda Miss Kinondoni na kufanya mahojiano na bongocelebrity.com wananchi walichonga sana..Imebidi nisome tena yale mahojiano..bado siamini lakini.

    ReplyDelete
  3. Majaji wamehongwa, hana sifa yoyote ya kuwa Miss Tanzania hana uzuri kama washiriki wengine ambao walimwacha mbali sana katika field hiyo. Kuna haja ya wanaohudhuria sherehe hizi kuanza kuzomea maamuzi ambayo hawakubaliani nayo.
    Kama wanachagua rangi basi wamatumbi WARIE TU!

    ReplyDelete
  4. Utabiri wangu ulikuwa sahihi, nilijua kuwa huyu dada atakuwa Voda miss TZ 2007. Hongera Richa kwa kufunika.

    ReplyDelete
  5. Watabiri wa hali ya hewa waliisha sema mmanga ndo atanyakua taji hilo. Hongera bibie. She is pretty and deserved to win like any other tanzanians.

    ReplyDelete
  6. Waosha vinywa jamani inabidi muwe good losers.Badala ya kumsagia nibora kumtakia binti huyu heri katika shindano la miss world. Hongera bibie, sikutaka ashinde but ameshinda na nampongeza sana

    ReplyDelete
  7. uwiiiii subiri waosha vinywa wakiamka!!!!!

    ReplyDelete
  8. Hongera Richa Adhia kwa ushindi wa Miss Tanzania 2007.

    ReplyDelete
  9. Hongera sana Richa, umestahili kushinda kuwa Miss tanzania 2007.
    Nakutakia kila la heri katika majukumu yako ya Mrembo wa Tanzania.

    ReplyDelete
  10. Congratulation Richa......ninategemea utaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

    ReplyDelete
  11. NDAKI NA MAJITA LAZIMA NYIE NI WACHAWI.KAMA SIYO HIVYO BASI NINYI NI WAPIGA RAMLI MAARUFU SANA.HAIWEZEKANI UTABIRI WENU UKAWA HIVYOHIVYO KWA 100% NDAKI ULITOKA NA KUMTANGAZA MSHINDI KWA MAMLAKA ULIYOJIPA MWENYEWE NA MAJITA ALIANZA KWA KUTOA HOJA ZA KUHOJI UHALALI WA HUYU BINT RICHA KUWA MISS TANZANIA.NAWAPA SHAVU WANAKIJIJI WAONA MBALI KAMA HAWA VIGAGULA VYA HAPA KIJIJINI.
    mkunwakunwa

    ReplyDelete
  12. Sio siri sijafurahia ushindi wa huyu Dada, asili yake ndio sababu.
    Mimi nilijua kama huyu dada alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda, kwasababu tunatabia ya kubabaikia watu weupe, sasa huku kwenye Miss World akisema kutoka Tanzania ,watatushaanga sana.
    Tulikuwa na kila sababu za kumuacha huyu na kumchukua mweusi akawamshindi, ilitujivunie rangi yetu.
    Nimechukia sanaaaaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Richa, ila sijafurahia uwakilishi wako wa Tanzania kwenye Miss world.

    ReplyDelete
  14. Huyu alitangazwa sana, na nilijua atakuwa mshindi kwaajili ya hiyo rangi, pumbavu kabisa.

    ReplyDelete
  15. Mimi sijaona uzuri wowote wa huyu Richa, ila rangi yake ndio iliyompa ushindi, ninaona yupo kawaida kama watu weupe tunaoishinao huku.
    Bora hata mngempa Miss UK hilo taji kama mlikosa wa kumpa?.

    ReplyDelete
  16. WAHINDI WA TANZANIA aka WADOSI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
    nA MWAKA UJAO MREMA ATAKUWA RAIS WA TZ MTAJIJU

    ReplyDelete
  17. Acheni unafiki nyie! Tangu lini wahindi wakashiriki katika shughuli yoyote ambayo wao hawatafaidika!? Huyu kaona kuna opportunity ya kupata umaarufu Tanzania halafu akaenda kuutumia kwao India na Ulaya. Hivi mnafikiri mmatumbi anaweza kuruhusiwa hata kushiriki kwenye Miss India!? Mpaka leo wanajitenga kwa kuishi 'uhindini' na kuwa na misikiti yao. Leo wameona Miss Tanzania na wao wanajifanya Wabongo sana! Fumbueni macho muone kiini macho.

    ReplyDelete
  18. Hongera Richa , nime mfuatilia huyu binti toka kwenye Miss Dar Indian Ocean na nilijua alikuwa mshindi ingawa alipata ushindi wa pili. kwani tulijua wazi Lilian alikwua amesha hakikishiwa ushindi kwenye kitongoji hicho na nilisema Lilian watch out for Richa, na kweli , tukaona kweney matokeo ya Miss Kinondoni na sasa Miss Tanzania .
    Richa ana sifa zote, kwa walio hudhuria shindano hilo na walio hudhuria yote aliyo shiriki Richa watajua alikua na sifa zote za kushinda , ingawa ushindani ulikuwa mkubwa kati yake na Lilian.
    MIss Redds ambaye ni Victoria Martin, alikwua nitegemeo kubwa kwa walio hudhuria kuwa ataibuka mshindi ,mbaka pale alipopata kiguugumizi cha ghafla pale alipo takiwa kujibu swali na hiyo ilimuangusha kwa kisai kikubwa.
    Kwa ujumla, oneysho lilikuwa zuri , stage ilikuwa nzuri , lights zilipendezesha , parking zilikuwa zimepangiliwa vizuri.
    Kikuwa nilicho kiona hakikuandaliwa vizuri ni kwamba table zilikuwa ni hazina number so ilikwua mbaka uangaike kutafuta sehemu ya kukaa, ingawa hakuna aliye kosa kiti.
    Hongereni sana Kina Lundenga pamoja na Voda kina Mafuru na wote mlio andaa oneysho hili na dhani sasa mmeshajua kuwa Ubora ni muhimu na kweli mmetuhakikishia kwa hili ,kwamba Tanzania tunaanza kujua Ubora ni umuhimu na sio kubana bana tuu hela ili kufanya kitu , ili mradi hela ibaki na kuiweka mfukoni,na pia mmejua hela yenu milio toa imetumikaje, kwakweli ni mwanzo mzuri na mmetupa moyo kwa sisi tunao taka kuandaa maonyesho kwani tume jua nani wa kufanya nao kazi na wana thamini ubora.

    ReplyDelete
  19. WABONGO ACHENI KUCHONGA HUYO DADA NI MZURI AND I DON'T CARE WHAT YOU THINK. MTASEMA SANA MWISHO MTACHOKA..RICHA ANASTAILI HILO TAJI HATA KAMA ANA ASILI YA KIASIA LAKINI SI NI MTZ? SHE GOT IT GOING ON AND SHE DESERVED THE CROWN...AMBAO HAMPENDI MLIE TU MPAKA MWAKANI...
    mfkasera
    kansas city

    ReplyDelete
  20. HUYO DEMU NI MZURI ANA KWELI ANASTAILI HILO TAJI....KILICHOBAKI NI KUMPONGEZA NA KUMSUPPORT AS NEEDED..
    johnson county,ks

    ReplyDelete
  21. Lakini si mhindi uyo, sasa hapo identity ya Tz iko wapi? au ndo mambo ya soko huria, who knows.anyway kwa uzuri mzuri anafaha ila pale tutakopokuwa na wahindi wawili miss world wa India na Tanzania ndo kizahazaa kitakapoanza

    ReplyDelete
  22. i raised my eyebrows...calling a spade a spade, ningefurahi zaidi kama angukuwa mswahili...kama vipi tuwaone kwenye u-cabin crew air tanzania, tuwaone wanachanganyika nasi kwenye "shule za msingi", tufanye nao kazi mawizarani, watujazie magari mafuta sheli, wengine wawe trafiki mabarabarani watusimamishe...wengine wawe wanajeshi, wengine wakasomeshe mwananyamala siyo wabaki almuntazir na mzizima tuu...wengine wakaruke as cabin crew precissionair, tujae nao vituoni kwenye madaladala...wanaoonekana zaidi sehemu hizi nionavyo mimi ndio watakaotoa best picture ya mtanzania...isiwe utanzania huu ujitokeze kwenye masilahimasilahi tuu...

    ReplyDelete
  23. jamani sasa itabidi bendera ya tanzania tuiongezee rangi nyeupe au sio??????????????????manake black inarepresent watu wa nchi sasa huyu mbona kama mfilipino mh ni sawa na pilau ule na kisamvu.

    ReplyDelete
  24. Michuzi binafsi nakupongeza kwa kuweza kutuletea habari hii.inaonyesha jinsi gani unatujali. Umeweza kutupa vituuzi vya uwanja wa taifa na miss Tanzania.Hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya unavyofanya wewe bila malipo yoyote.

    ReplyDelete
  25. Victoria Martine Amestahili Kuchukua REDD'S Fashion Ambassador 2007-2008 Kwa Kua Alikua Na Vigezo Vyote!

    Kuhusu Miss Tz, Hakuna Ubishi Wahindi Walijipanga Vizuri Kumsupport Ndugu Yao!....Pia Anao uwezo Wa Kujielezea!...Katika Ulimwengu Wa Sasa Kukubali Changes Ni Ngumu Sana Lakini Itabidi Iwe Hivyo! Mbele Ya Macho Ya Ulimwengu Tutaonekana Hatuna Ubaguzi!

    Izz Wa

    ReplyDelete
  26. Nimefurahi sana kwa kuwa atapeperusha bendera ya nchi yetu na kulipa jina Tanzania. Hasa kuzua gumzo kwa wenzetu wa Afrika mashariki na kati kuona binti mwenye asili isiyo ya kiafrika kuwa miss TZ. Italeta picha kuwa nchi yetu haina ubaguzi wa rangi wala kabila. Ila binafsi sikufurahi ashinde. Pia nahisi mwenye ShivaCom anaundungu na huyu binti, maana wamefanana!!!

    ReplyDelete
  27. du haya utajiri ameongezewa gari hela wakupewa wakupewa tu nilivymuona victoria martin nilikuwa na rumaini sana ila kila heri miss patel TZ nilichonga sana sasa maji ya mafika shingoni

    ReplyDelete
  28. Miss India, Oooops!, Miss Tanzania 2007, umeniudhiiiiiiiiiiii.

    Sijafurahia ulivyoshinda lakini ntafanyaje?

    Sikupendi.........!

    ReplyDelete
  29. Tumemuona MISS INDIA? lakini naona mwaka ujao atakuwa Mchina!Redd's ambassador was my best followed by Queen..kweli tumejionea Utafouti na Vodacom..Halafu tuacheni kuidanganya public wale Twanga were not the one supposed 2 be there,wanaimbwa wakina aisha wakati wako uingereza..ThT were the best in Performance!

    ReplyDelete
  30. Jamani eh, kwani hakuna uwezekano wa sijui katiba ama taratibu za kutafuta hawa warembo wetu kubadilishwa kidogo, I mean badala ya kuwa yanafanyika mara moja kwa mwaka, basi mwaka huu yafanyike baada ya miezi mitatu labda......, I mean huyu Miss mpya akabidhi taji hilo kwa mwengine labda by January? Hebu tujaribu na isipofanya kazi, basi tutarudi kwenye utaratibu huu wa sasa, lakini baada ya huyu kuwa amekabidhi taji hilo.
    Na pia basi vimakosa vilivyofanyika kipindi hiki visirudiwe tena jamani manake uuuwiiiii! naogopa kusema saaana.

    Ni wazo tu jamani, mi nalia hapa sasa, uwiiiiiiiii.

    Waandaaji na majaji kwenye shindano hili mmenikera kweli kweli.

    ReplyDelete
  31. ...ni sawana miss south africa kuwa mzungu!!...kuna dada zetu wangapi apo sauz mpaka 'misi' wao awe mzungu!...kaka issa i had my fingers crossed but naona umenitoa hapo juu...haya mambo ya 'kuonekana hatuna ubaguzi' hivi kweli seriously kuna mtu dunia hii ya leo anaamini hakuna ubaguzi?...lengo mojawapo la umisi hivi siyo identity jamani? mpelekeni mpanda mkamtambulishe MISI TANZANIA HUYU!!! moune watu watavyowakodoleeni macho with complete confusion...richa is the odd one in that group...my sister once accidentally happened to be in a place where there was a quiz conducted by dstv...all maswali centered within channel za dstv...she got ALL questions right, ALL...'mshindi' (who got away with a dstv decorder plus accesories) missed some...organizers walibabaika sana and it was a big embarrassment and lots of maelezo given and wakamwambia aende "ofisini kufuatilia"...she never bothered to go...matokeo ya kupangwa hayo!...i hate this all misi thing, wanadhalilika sana dada zetu kufukuzia nyumba na hivi vigari

    ReplyDelete
  32. kweli namsapport anayesema tuiedit bendera yetu ya Taifa tuweke rangi nyeupe ziwe tano!Miss Tz this time iko Kihindi zaidi!Inaniuma sana I think next time tujaribu Mamiss wawe judged by Votes not by judges!I wish Miss Redds Ambassador atuwakilishe Miss World!Nadhani Tz tunaongoza duniani kwa kuwatetemekea watu weupe!

    ReplyDelete
  33. Moja ya sababu zulizowafanya Ma-miss waliopita kutofanya vizuri kwenye Miss World ni kushindwa kujieleza na kutojiamini. Nadhani majaji wamemchagua Richa kwa kuwa ana sifa hizo zaidi ya washiriki wengine. Mamiss wote waliowakilisha Tanzania katika Miss World walienda kama watanzania ni sio kwa kuwakilisha maeneo waliyotokea kama Temeke, Kinondoni, Dodoma....n.k....hivyo nategemea Richa ataenda China kwenye Miss World kuiwakilisha Tanzania na atabeba bendera ya Tanzania. Inaweza kuuvutia sana mataifa mengine kuona kwamba Tanzania pia ni "land of opportunity" na "anybody can make it" Nchi zilizokaribisha mataifa mbalimbali zimeendelea na zinazidi kuendelea kutokana na kuwapokea na kuwatumia wageni wenye mawazo na vipaji tofauti. World Cup, Ureno ilikuwa na wa-brazil zaidi ya wawili kwenye timu yao. Ni wakati watanzania kuamka na kupambana na wenzetu kwa vigezo vya akili na vipaji na sio rangi.

    ReplyDelete
  34. acheni ubaguzi wa rangi!kuweni kama nchi za wenzetu!kama ni raia ana haki zote kama wa Tz wengine!

    ReplyDelete
  35. Tusidanganyane jamani mhindi mhindi tu mbona basi hawakubali kuolewa na waswahili na wakifanya hivyo wanatengwa, mbona hatuwaoni wakijichanganya na waswahili kama kweli ni Watanzania, kwaniini wanatumia passport za nchi mbili? India kuna waswahili mlaikini hata siku moja hutachaguliwa kuwa waziri au mbunge hata kuingia kwenye hao mia bora sahau.Imefika wakati tukubali tusikubali Utanzania kwanza wala si ubaguzi kama watu wanavyofikiria ila ni Identity yetu sisi kama waafrika.Wingereza wanawatu wa mataifa yote lakini muingereza halisi anahaki zaidi na siku hizi ndio wanaliongelea sana hilo sasa kwanini sisi pia tusiliongelee. Kwa kifupi tu mss Tanzania ni biashara ya wahindi huyo ndugu yetu Lundenga msindikizaji tu wala sishangai hata kidogo. Watanzania muamke sasa mtaliwa mpaka mkome.

    ReplyDelete
  36. YOU DESERVED TO WIN RICHA.... You are one of the most beautiful girls in TZ....I am confident you will represent TZ well in the Ms. World Pageant... CONGRATS!!!

    ReplyDelete
  37. I’m speechless. Kwanza swali alilopewa kujibu katika kuwania taji la miss TZ, aliulizwa ‘which is your favourite color’, akajibu WHITE! Na akaendelea kuisifu rangi nyeupe na jinsi gani anavyoipenda, kuwa ni pure… Automaticaly inaonyesha jinsi gani anavyoona rangi nyeupe ni bora kuliko zote. Anatamani na bendera yetu ingekuwa na weupe kudhihirisha sisi ni nchi yenye amani. Rangi nyeusi in many generations BC and AD imekuwa ikifananishwa na giza, misiba, mashetani na kila kitu kisichokuwa bora. Na imejengeka katika fikra zetu kuwa mtu mweupe ni bora kuliko mwenye ngozi nyeusi. Na mastereo type wanaendeleza hiyo fikra, kuwa mtu mweupe ni mzuri kuliko mabinti zetu wenye ngozi nyeusi. I’m so %*#@?^!!$...

    ReplyDelete
  38. Hivi mbona hatulalamiki kuwa na wabunge wahindi na waarabu???Mohamed Daewji,Rostam na Arfi wa Mpanda ni wabunge waliochaguliwa na wananchi kwa kuwaona wanafaa.Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwachagua Jamal,Derek Bryson na Alnoor Kassam.Hao ni wahidni na mzungu waliokuwa kwenye baraza la mawaziri.Bryson alikuwa kipenzi cha watu wa kinondoni na watu hawakuangalia rangi yake.Leo hii tumeanza kuwabagua ndugu zetu kwa kusema ni wahindi au wazungu.La msingi ni kwamba mtu akiwa mtanzania ana haki zote bila kujali rangi yake.Leo tukianza na wandi kesho tutabaguana kwamba wewe ni mkurya au msukuma au mhaya,tutafika kweli??Kubwa ambalo tunajivunia watanzania ni umoja na upeo wa kufikiri tusichochewe na wachache wasio ona mbali.Sweden kwenye baraza lao la mawaziri Minister wa integration ni mweusi tii kutoka Congo anaitwa Nyamko Sabuni .

    ReplyDelete
  39. Duh, alishariki katika mashindano ya dunia na akachemka vibaya, sasa wamempa tena nafasi nyingine ya kutuaibisha, Bongo bwana!

    Alishiriki mashindano ya Miss Earth 2005 akitokea Miss Beauty Queen ya Maria Sarungi Tsehai.

    Tatizo akina Lundenga hawalengi au kusaka mrembo atakayefanya vizuri katika mashindano ya dunia, bali anayetoka katika familia ya wenye nazo kama huyu ili asiwasumbue wakati wa maandalizi ya Miss World... Aah, siongei tena!

    ReplyDelete
  40. jamani acheni ubaguzi, tanzania ni nchee pekee ambayo imefanikiwa kuwa na makabila ya rangi tofauti kwa amani, sasa mkianza mambo ya rangi tutaishia kama rwanda na burundi, binti yuko bomba na kinachotakiwa ni yeye kujivunia ubongo wake, Richa go on and fly the flag!!

    ReplyDelete
  41. MDAU MWENZANGU MKUNWAKUNWA!
    NASHUKURU KWA KUNIPA PONGEZI ZA KUTABIRI KUWA MISS PATEL NOO... I MEAN MISS RICHA KUWA ATAKUWA MISS TANZANIA.

    NGOJA NIJIPANGE ILI NIWASILISHE HOJA NZITO ILI NYUMA YA HUU USHINDI NATAK NIKUSANYE DATA ILI MISOUP ASIJE AKANIZITO KWA MADAI YA KUM-KALAMAGI HUYO BINTI.

    ENE WEI TUTAFIKA TU

    ReplyDelete
  42. Hongera Richa you deserve!!!!

    Kuhusu swali, amejitahidi sana hata Lilian Abel alijibu vizuri na bila kubabaika ila hatuwezi kujua mambo mengine walipokuwa kambini.

    Mimi naamini alikuwa mwema sana kule kambini ukichukulia kuwa alikuwa Mhindi na anawapinzani wengi toka amekuwa miss kinondoni hivyo kwa vyovyote vile alijitahidi kutengeneza tabia nzuri, kwa kila mshiriki na kila mtu hapo kambini ili ajinyakulie point.

    Tusilalamike sana mradi atabeba bendera ya Tanzania na sio ya India basi huyo ni wetu. Walimu wajitahidi kumtrain ipasavyo

    ReplyDelete
  43. WATA SEMA SANA, KISHA WATA LALA!!! WENYE WIVU WAJINYONGE!!You were the most beautiful contestant Richa, forget all the negative things some people are saying about you. You are TANZANIAN, you have equal rights as all the rest.... whether black or white.... WISHING YOU ALL THE BEST IN YOUR REIGN AS MISS TANZANIA, and all the years to come...!! Guys, all that negative things you say about RICHA wont change the outcome, she is the winner!! she is our beauty ambassador, accept it and support her...

    ReplyDelete
  44. Hongera dada, shughuli yako pevu na unastahili taji hilo.

    Kwa wale wabongo wenye kuchonga, mara ooh huyu ni mhindi na si mtanzania, mbona akina Halle Berry, Michael Johnson, Carl Lewis, Thierry Henry,n.k wanawakilisha mataifa ambayo kiasili si ya kwao?, acheni ulimbukeni wa mwaka 47, kuna watanzania wengi tu ambao ngozi zao zi nyeusi.

    Mbona hamkumnanga Mwisho Tumpambe wa Mwampamba, Kali Ongala na wamishenari kibao ambao wanakuja Tz na kuishia kuchukua uraia kutokana na mapenzi yao kwetu?

    Hongera Richa mambo yako hevi

    ReplyDelete
  45. Jamani, mbona kuna wa Tanzania wengi, wenye asili ya kihindi, ambao wame suport sana wachezaji wetu wa Taifa Stars walivyojitahidi na kuwafunga Msumbiji!!! Na wala siongelei suppport ya ushabiki tu!! Hata kabla ya mechi hiyo, walipewa suppport nyingi sana.They represented our country well, and made us proud!! Kwanini leo hii, watu wanachonga sana na wanashindwa kumsupport Richa, Mtanzania mwenzetu, hata kama ana asili ya kihindi??? We are with you all the way Richa, you have our support, am sure you will represent TZ well.. and you too will make us proud!!! You deserved to win...! Hongera Sana.

    ReplyDelete
  46. wahaya,wagogo na wachaga
    Kwao wao mtu ambaye hatokei kabila lao si mtu:Kyasaka na Mkonongo; wahaya sijui wanamwitaje?
    Japokuwa sio mambo mazuri ila kuna wakati two evils r facing u at a time,u better opt for a lesser evil!
    Nadhani MAMISS wanapokuwa wanaelekea Miss Tanzania, vitu vyote vinavyowapa popularuty huwa ni mwiko, but the gal went to sell herself thru BONGO CELEBRITY. In my Mind this was enough ground to disqualify RICHA, ila kwa kuwa alikuwa ameandaliwa ashinde, waandaaji wakajidai kufumbia macho.
    Michuzi naomba namba ya Mchunx MTIKILA nimpe hii ground of appeal ya kusafisha uzawa.
    CHAKULA CHA WATOTO UNATUPIA MBWA!!!
    NO OFFENCE INTENDED,JUST QUOTING THE BIBLE.

    ReplyDelete
  47. Hatulalamiki kwamba sio mzuri, ni mzuri hasa anafaha, lakini when comes to represent nchi tungependa the true african, ndio asili yetu jamani, huo mfano wa wabunge na nk hatukatai, ndio maana hata uchumi wa nchi wanashikilia wao. Hivi akiambiwa uyo avae traditional dress atavaa nguo ngani? ya kihindi au ya kimasai? Hivi akiambiwa aeleze culture za kibongo hataeleza nini? labda akalilishwe.hayo mambo yangekuwa yanaendeshwa humo kwa humo nchini hakuna noma, but when comes to international representation uafrica uwe paramount, ni sawasawa na mimi mweusi tii nikawakilishe china kwenye miss world!! nina wasiwasi hata kiswahili anajua vizuri huyo.It is time to call a spider a spider, fatilia marekani wanavyowasha moto kwa OBAMA regardless kuwa ameonyesha uwezo wa hali ya juu na kwamba US ni mixture ya makabila yote. ''Africa is for Africans, black Africa'' (quote from Idd Amin Dadaa)

    ReplyDelete
  48. MISS NORWAY NI MFILLIPINO 2007!NINI AJABU?KINACHOMETA NI UZURI TUU,

    ReplyDelete
  49. Wengi wanasema wahindi wanaubaguzi, wanataka wawe wizarani, kwenye ndege nasijui wapi tena, nawauliza hivi hawa wabaguzi weusi wanakaa wapi?
    [Wizarani] Zakhia Meghji, wabunge wapo, na huyo anayesema kwenye ndege sijui amepanda ndege ngapi za air Tanzania.
    Umbea umewazidi tu hawa wabaguzi, wahindi wakisaidia jamii kama mambo ya mpira basi hakuna anayesema [baniani mbaya kiatu chake dawa]
    Wahindi wakijenga wakitoa misaada hospitalini kutusaidia SISI WEUSI hakuna anayelikemea hilo.

    Kila mtu hapa anasema wana ubaguzi lakini nikiingalia hizi post zenu hapa basi sioni tofauti kabisa na hao mnaowasema wana ubaguzi.

    Kama mnakumbuka katika kinyang'anyiro cha miss world Afrika wakati ule Sumari alipochukua taji, SA afrika iliwakilishwa na msichana wa mwenye asili ya kihindi anayezungumza kizulu, kiingereza na kiafrikaans
    Watu wa SA afrika hawakua malimbukeni kama wengi wa watu hapa.
    Kama dunia hii ingeangalia asilia ya mtu ndio awe miss basi watu wenye asili ya afrika kamwe wasingekua miss Ufaransa, Holland USA, hizo nchi zote nilizotaja basi watu wenye asili ya umatumbi waliziwakilisha nchi hizo.
    Africa is for african, black african (Idd Amin Dadaa) Labda wewe unayemfuatilia Idd Amin ujiulize kwanini aliivamia Tanzania? na asiende kuivamia India? na kama tutafuata theory zake basi itakua hivi; Europe is for Europeans {white Europeans} na tutaendelea hivyo hivyo mpaka tutakaposema Tanzania sio ya wamasai, wangoni nk.

    Hebu kueni naepukeni na fikra zenu za kijinga.

    By the way, mimi ni mweusi kama mpingo lakini namsapoti huyo mhindi.

    ReplyDelete
  50. Hajui chochote kuhusu Tanzania huyu. Ukimuuliza akutajie makabila manne makubwa Tanzania hajui. Ukimuuliza chakula kikuu cha Watanzania wengi hajui, si ajabu hata ukimuuliza akutajie baraza la mawaziri halijui.Halafu mnataka kusema naye ni Mtanzania! Mbona hatuwaoni kwenye majeshi yetu au kushangilia Taifa Stars ukiondoa wale wachache wanaotoa bulungutu wanajua litalipa!? Jana mbona sikuwaona pale National!? au wao hawaoni fahari kushangilia timu ya Taifa ya Tanzania!?Kama ilivyo Tanzania majuu pia wanajitenga hivyo hivyo! Acheni hizo let's call A SPADE by its real name A SPADE!

    ReplyDelete
  51. Michu hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya. Unatufanya tuwe home wakati wote. Sijui kama malipo yoyote unayoyapata, anyway keep it up! Awali ya yote ninaipongeza Taifa Stars kwa kazi nzuri walioifanya ya kufungu iwanja wetu kwa ushindi. Natumai kupitia uwanja huo tutaendelea kuwa washindi. Nafikiri ni vizuri tukamkumubka aliyefanya jitihada zote kuanzia wazo mpaka ujenzi wa uwanja wetu kukamilika, kama ni mzee wetu Mkapa tuna kila sababu kumpongeza na kufanya kila jitihada kuweka kumbukumbu hiyo ili iwe sehemu ya historia ya michezo nchini mwetu.

    Pili mampongeza miss TZ 2007 pamoja na mawazo mbalimbali yanayoonesha kupinga ushindi huo kisa asili yake lakini siyo utaifa wake. Mimi nafikiri kwanza tunahitaji kuelimishwa umiss duniani objectives yake ni nini? Wahindi nchini mwetu wakuwepo siku nyingi sana kabla ya uhuru. Hata baada ya uhuru kuna watu walitaka kujaribu kutoa mawazo kwamba waondolewe lakini baba wa Taifa kwa kutumia busara zake alikataa kabisa hayo mambo wakawa raia, na wamekuwa raia wazawa. Tuachane na ubaya wa rangi, hiyo concept imeshapitwa na wakati. Duniani kote ulishapigwa vita vya kutosha. Kujaribu kuongelea ni kutaka kuwaoneshea udhaifu mkubwa huko wenzetu wameshatoka. Huko Ulaya tunakozungumzia ni kwamba haki yako ni haki yako. Na hasa ukiwa tu raia haki yako ni kwa mujibu wa sheria hilo halina utani. Ubaguzi kwa kiwango tunachotaka hauwezi kuisha hata siku moja. Kjijini kwenyewe tunabaguana, makazini bongo tunabaguana. Usitegemee mhaya au mchaga akakuchukulia wewe ambaye siyo mhaya au mchaga kama mhaya au mchaga mwenziye kumbukeni kashfa ya TRA kuhusiana na ukabila.

    Cha maana huyo dada awakilishe nchi yetu abebe bendera yetu, kwa njia hiyo nchi yetu inatangazwa kimataifa, tukuimbuke kuwa Tanzania haijulikani sana duniani.
    Angeshinda ndiyo pale amabapo watu wa mataifa mbalimbali wataanza kufuatilia hii Tanzania iko wapi watakuja utalii, watakuja kuwekeza uchumi unakua ndicho tunachokitaka.Nchi nyingi duniani zimeendelea kwa kuwa na muingilano wa mataifa mbalimbali. Mzee wetu Mandela anasifika sana duniani na ni majuzi tu salamu yake ilizinduliwa London kwasababu pamoja na kukaa gerezani miaka 27 hakulipiza chochote kwa wazungu. Kwa hili wazungu wamejifunza vitu vingi. Tusilipe ubaya kwa ubaya. Sisi tuoneshe upendo kwa watu wote watajifunza kutoka kwetu. Tena mimi nimefurahi huyo dada ana asili ya kihindi tunafundisha ulimwengu mambo mengi. Ukifuatilia historia unaweza ukakuta wahindi wengine walifika bongo kabla hata ya makabila yetu mengine kuhamia bongo. Hatuhitaji ubaguzi wa aina yoyote huyo ni ufinyu wa mawazo. KAMA wazungu wanabagua sio lazima na sisi tubague. Mzumgu akifanya upumbavu sio na sisi tufanye upumbavu halafu tunajitetea kuwa mbona na wazungu wanafanya. Wazungu kuna vitu wanajifunza kutoka kwetu hata kama hawawezi kusema waziwazi. Wakichemka sisi tunafanya tofauti wanajifunza.

    Hatuoneshi utaifa wa Tanzania kwa rangi, utaifa maana yake ibaki kama ilivyo na kamwe si rangi. Umiss ni mchezo kama michezo mingine kuna kitu gani special kuna umiss tofauti na michezo mengine? Mbona huko ulaya kwenyewe mnakosema tunaona waingereza weusi, wamarekani weusi na juzi tu huko Osaka, Japan M-Qatar mweusi ambaye ana asili ya kenya akapeperusha bendera ya nchi hiyo baada ya kushinda? Waingereza na wamarekani wangapi weusi tumewaona ktk michezo hii ya Osaka wamepeperusha bendera za nchi za Amerika, Asia na nchi za Ulaya? Je umiss una nini cha ajabu na cha ziada zaidi ya kuwa bujrudani? Tupeni jibu jamani? Umiss ni nini?

    ReplyDelete
  52. Watu wote wanaompinga huyo dada kuwa MISS Tanzania based kwenye rangi ya ngozi yake au her ethnicity wana matatizo ya akili . Mimi nikiwa mmoja wa watu ambao nimeshaexperience ubaguzi sita kubali hata siku moja kukubali hizi mbegu za chuki zipate nafasi katika nchi yetu .

    Mimi nadhani tumpinge huyu dada kama kutokana na vigezo vya umiss na sio rangi yake . Huyu dada ni mtanzania kama watanzania wengine na akila sababu ya kuliwakilisha taifa lake.

    Napenda kumpa hongera na kumtakia mafanikio mema katika kuliwakilisha taifa letu.

    ReplyDelete
  53. anon wa 4:37 tumia akili bwana,,Mtu wa Norway na mfilipino rangi zao za ngozi tofauti yake ni ndogo sana..hemu kaa chini umfikirie mtanzania na mhindi tofauti yao ni kubwa kiasi gani,,unadhani Miss Tz 2007 angekuwa na asili ya kenya,ghana au msudan watu wangeumia sana? NO,wewe kama unakaa Norway na kama ni mwanamke, hemu jaribu 2008 kuomba nafasi kwenye mashindano uone kama utapewa..labda utapewa ya kusafisha holi yatakapofanyikia mashindano.

    ReplyDelete
  54. hongera ila kwa kweli tulipenda zaidi mzawa,

    ReplyDelete
  55. anon wa 5:44 kumbe problem yako ni rangi?sio asili sio?mimi ni dume.na kama kuna demu mzuri na anafaa basi hamna shaka atapata hio nafasi,AMKA

    ReplyDelete
  56. ebu tuchukue mfano kidogo tu kuwakilisha ujumbe, hivi timu ya taifa ibahatike kuwakilisha nchi,golini yupo kumar patel, 2 jamal guwaj, hivyo hivyo mpaka no 11, wote watanzania ila wana asili ya kihindi, kweli itaeleweka hapo. lakin kwenye soka letu la kibongo hata timu nzima wote wawe wahindi,wazungu, wachina alimradi ni wa tz hamna noma. unapotoka nje jamani identity ya nchi comes to mind

    ReplyDelete
  57. Hapa kuna utata, Hii nchi ya Tanzania haina ubaguzi lakini ikfika katika mambo ya kuwakilisha Taifa kimataifa Basi watanzani wazawa asilia, wabantu wawe the top. Hivi huyu akishinda mtafikiri watasema mtanzani?, watasema muhindi huyu.

    Hebu angalieni hawa jamaa walivyo na ubaguzi, wakigundua muhindi mwenzao kaolewa na Mtu mweusi wanamtenga sasa hawa ni wenzetu kweli?, Na kwa nini wakati wa uchaguzi wanakimbia nchi yaani kama vurugu tuathirike sisi weusi. Poa kwa kuwa majaji na waafrica asilia wenzetu walikuwepo basi tumpongeze kuwa kafunika. Ila na madada zetu mchemshe akili sasa, sio kung'ang'ania poda na umbeya muende shule. Uzuri si sura tu bali na akili pia.

    Hongera Richa Kwa kuwa Miss TZ natumai utaukana na uraia wa nchi nyingine kama unao.

    ReplyDelete
  58. Mimi nadhani kwenye nchi yeyote kama upo pale kihalali au kama ni raia hiyo nchi ana haki zote. Kama ni mweusi na unaishi kwenye nchi ya weupe kihalali, nenda kashiriki kwenye mashindano ya ma-Miss na usipokubaliwa ndio unatakiwa kulalamika. Wengi wetu tunaosha vinywa wakati hatujawi hata kujaribu kufuatilia taratibu za kushiki U-Miss zinakuwaje....let's try....na tukishindwa au kuchujwa tusitafute mchawi...tuangalie ni wapi tumefanya makosa na jinsi ya kujirekebisha. Nchi yeyote utakubaliwa na kupokelewa kama utakuwa mwakilishi wao, kama tunavyong'ang'ania sasa hivi bunge letu lipitishe "dual citizenship" ili watu kama Kali Ongara watuwakilishe kimataifa. Richa, hongera na tunategemea utatuwakilisha vizuri kimataifa hasa ikizingatiwa una passport moja tu ya Tanzania(since we don't have dual citizenship)....kama unapassport mbili, hapo patakuwa na ulakini maana sheria bado iko jikoni haijapitishwa.

    ReplyDelete
  59. CONGRATS RICHA!! FOR ACHEVING WHT U WANTED! MS.TANZANIA 2007.
    well this is to all the haterz kama nyie mnafikiri kwamba 2 win the tittle of ms.tz is 2 b dark .. ur mistaken .. as u ol say black is beauty lakini as the judges said kwamba brains also matter n tht is something tht Richa is BLESSED with!!n the beauty she also has it .. i am shua she will b an icon in the Tanzanian histry 4 acheving a LOT!! well last year we had enuf of experience i can say gud 4 nuin experience .. wammemchagua wema.. wht did she do ?? except from apeearing in papers for god knwz wht!! tht really wasnt pleasing .. so we dnt want to go in another year of horrible appearence for tanzania n i asure u tht Richa will represent Tanzania ..she has olredy proved to us tht she is someone we can rely on .. as in previously wen she was ms.earth.. and most of all Ms.kinondoni .. serving the community n she wil do much more as Ms.Tanzania.. well jus sit bac n w8 2 c how she is proud of flyin the flag of tzee in china wer she is going 2 make history fo Tz..well mostly a huge percentage wanted the Victoria gul 2 win.. si did i .. but mhh she has ol the vigezoz but akili .. urojo!!PEOPLE SHE HAS OLREADY WONN U CAN HATE IF U WANT BUT SHE DOSENT NEED THT .. ALL SHE NEED NOW IS THE SUPPORT OF ALL THE TANZANIAN'S WORLDWIDE.

    TANZANIANZ ITS ABOUT TIME YOU ERASE THE RACIAL DISRIMINATION FROM UR HEADS .. WE STAND UP N SPEAK UP 4 EACH OTHA WE R OL HUMANS FOR GOD'S SAKE.. SHE OLSO HOLDS A TANZANIA PASSPRT .. JAMANI MBONA PRE WA SOUTH AFRICA 2006 ALIKUA MZUNGU ..MBONA HAMKUSEMA ???

    RICHA GUL U LEAD !! DNT LET ANYONE HOLD U DOWN BTW THEY HAV 2 FACE IT THT UR OLREDY MS TZ .. WE CNT TURN BACK TIME ... N U DESERVED IT!! GO N MAKE TANZANIANS PROUD!!
    - SABZY

    ReplyDelete
  60. NATUMA salaam za pongezi kwa Richa kwa kushinda taji la Miss Tanzania 2007

    WIMBO: 'MWENYE WIVU AJINYONGE' ulioimbwa na Saida Karoli

    UJUMBE: Kwa wale wote wanaompinga kwa ajili ya rangi yake, waburudike na kibao hicho cha Saida Karoli.

    ReplyDelete
  61. Tuna wasichana wazuri wengi tu wazawa wa Kitanzania, hatuhitaji majeshi ya kukodiwa kutuwakilisha kwenye Miss World/Universe. Hivi mnafikiri mmatumbi anaweza kuiwakilisha India kama Miss India si itakuwa kashfa ya hali ya juu!? Wao mpaka leo wanatubagua ndani ya nchi yetu! Fungueni macho wabongo!
    Oneni wao walivyo wabaguzi wa hali ya juu. Mtaona kama katika timu yake atakayoandamana nayo kwenye Miss World kutakuwa na mmatumbi atakayefuatana naye.

    INTRO: SONIA GANDHI, THE LEADER OF INDIA'S CONGRESS PARTY, HAS
    RESIGNED HER POSITION, BUT SENIOR PARTY OFFICIALS IMMEDIATELY
    REJECTED THE OFFER. MRS. GANDHI -- THE ITALIAN-BORN WIDOW OF
    FORMER PRIME MINISTER RAJIV GANDHI -- ISSUED A LETTER SAYING SHE
    WOULD RESIGN LATE MONDAY, AFTER A CALL BY OTHER PARTY OFFICIALS
    FOR HER TO STEP DOWN. V-O-A'S JIM TEEPLE REPORTS FROM NEW DELHI.

    TEXT: THE DRAMATIC ANNOUNCEMENT BY MRS. GANDHI CAME AFTER THREE
    SENIOR CONGRESS PARTY LEADERS QUESTIONED HER ABILITY TO LEAD THE
    COUNTRY, SAYING ONLY NATURAL-BORN INDIANS SHOULD ASPIRE TO HIGH
    OFFICE IN INDIA.

    IN HER LETTER OF RESIGNATION, READ TO JOURNALISTS BY PRANAB
    MUKHERJEE, A SENIOR CONGRESS PARTY OFFICIAL, MRS. GANDHI REJECTED
    ACCUSATIONS THAT SHE IS NOT SUFFICIENTLY INDIAN ENOUGH TO
    PARTICIPATE IN POLITICS OR RUN FOR HIGH OFFICE.
    kuwa wabaguzi. Fungueni macho wabongo!

    ReplyDelete
  62. NYERERE AKIFUFUKA AKISIKIA MNA LETA MAMBO YENU YA UBAGUZI ATAWATIA WOTE BAKORA.

    ReplyDelete
  63. jamani watu mlalamika nini mnalamimkia rangi ama nini,nyie watu mko bongo ama wapi inaonekana mjatembea.Je ingekuwa wewe unakosa kazi kwa jili ya rangi yako ingawa ni mwingereza ungejisikiaje ,mimi sioni shida yoyote niMtanzania mwaashe ashinde anaaki kama wengine.

    ReplyDelete
  64. UWIII UWIII EHEHEHE!!! Naungana na Hoyce Temu kulia. Huyo mhindi hakustahili kabisa kushinda amebebwa na wahindi wenzake. Hana lolote.

    ReplyDelete
  65. HOYCE TEMU HUKUSTAHILI KUFANYA ULICHOFANYA MBELE YA UMATI WA WATU, WEWE UNAONYESHA UBAGUZI. THAT MLIMBWENDE DESREVED THE CROWN. WHAT MATTERS IS....ni Mtanzania tena kwa kuzaliwa. KASOME URAIA UJUE.

    ReplyDelete
  66. Duh, yale yale sijui anaitwa Richa Vithlani au Patel. Au labda anaitwa Richa Mehta. Kama ni hongo hizo pesa wamezipatia huku huku. I mean wametuibia sis Wabongo wakahonga na zawadi ikabaki huko huko kwao! Sasa akaunti itahamishiwa India au Canada. Watanzania sasa na tujifunze tuwaepuke waporaji wa nchi hawa.Hela za rada hizi.

    ReplyDelete
  67. hey rachel u rule!!!
    don worry bout the odds.. just shut them up by winning the miss world pageant .. u beautiful, descent and intelligent .. u deserved and appreciated.. go princess go ..

    ReplyDelete
  68. all the best rachel..don worry bout the odds .. just make tz proud ..

    ReplyDelete
  69. Hey,on this issue refer the article by Mahmoud Mamdani, When Does a Settler Become a Native? Reflections of the
    Colonial Roots of Citizenship in Equatorial and South Africa 11, Inaugural Lecture at the
    University of Cape Town (May 13, 1998) (Univ. of Capetown Dep’t of Communication,
    New Series No. 208, 1998) (transcript available at http://www.bard.edu/hrp/events2000/
    Mamdani1.htm).

    ReplyDelete
  70. ...FastFoward to China: "...and now,The Miss World 2007 iisss...Miss RICHAAA, the Miss Tanzania....of INDIAN ORIGIN!!!!!"

    ReplyDelete
  71. Kuna mtu alitulaani kisha akatupa hiyo funguo ya laana baharini. Inashangaza mno jinsi wamatumbi wanavyokazana kubabaikia weupe. tunagombana wenyewe kwa wenyewe kwa wengine kudai kuwa wengine ni wabaguzi. ajabu ni kuwa hakuna hata mhindi mmoja anayejitokeza kusema kuwa wanabaguliwa. Hio kazi wamewaachia baadhi ya wabantu ambao wako tayari kuwatukana wabantu wenzao ili kuwatetea wahindi. Tumelaaniwa. Waacheni Wahindi wajitetee wenyewe na sio nyinyi wabantu wenzetu kujifanya ma-PR wao.....ACHENI HIZOO!!!

    ReplyDelete
  72. Common Sense inasema kuwa wale watazamaji kule China watakaposikia Miss Tanzania wanategemea kuona binti wa Kimatumbi kutokana na uklwei kwamba wanajua kuwa TZ iko Afrika. Kwa hakika watashangaa sana na kujiuliza uwezo wetu wa kutafakari pale watakapomuona Miss Tanzania iliyoko Bara la Afrika akiwa ni Ponjoro.../

    ReplyDelete
  73. U-Miss 2007, ni vilio!

    2007-09-03 18:44:27
    Na Mwandishi Wetu, Jijini
    IPPMEDIA


    Kinyang`anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2007, kilichofanyika usiku wa kuamkia juzi, kimezidi kuzua malalamiko miongoni mwa watu ambapo wanadai kuwa mrembo aliyeibuka kidedea hakustahili.

    Baadhi ya watu walioongea na gazeti hili leo asubuhi wamedai kuwa walikuwepo warembo wengi waliostahili kuvishwa taji hilo ambao wana sifa nyingi kuliko huyo aliyeshinda.

    ``Unajua kushindwa kujieleza vizuri kwa Kiingereza, haimaanishi kuwa mrembo hana vigezo vingine,`` amesema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sauda Masoud.

    Mtu mwingine amesema Richa Adhia, 19, ingawa ni mrembo na mwenye sura ya kuvutia lakini hakustahili kuchukua nafasi ya kwanza.

    ``Sisi tulidhani atachaguliwa Mtanzania halisi na si huyo dada ambaye asili yake si hapa kwetu,`` amesema mdau mwingine aliyejitambulisha kama Aboubakar George.

    �Warembo walikuwepo tena wazuri sana na wenye vigezo vya kimataifa, lakini nashangaa wakampa mrembo yule� kwanza ni mfupi kuliko wenzake�pili inaonyesha ushindi wake ulipangwa mapema,�� akasema mtu mwingine aliyejitambulisha kama Neema Samson.

    Mtu mwingine amedai kuwa mashindano haya yanaonekana kama si ya taifa bali ni ya mtu mmoja.

    ``Hao wanaoandaa mashindano hayo, hawataki kusikiliza maoni ya wananchi wala wadau wa urembo, sasa basi wayatafutie jina lao na wala yasiitwe Miss Tanzania,�� mkazi mwingine wa Jijini, Bi. Mwenda Kassim amedai.

    Imeelezwa kuwa wakati wa kutangazwa kwa matokeo hayo, Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999 Hoyce Temu alidondosha machozi kuashiria kupinga matokeo hayo, yaliyokwenda kinyume na matarajio ya wengi.

    Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya majaji, Dk. Ramesh Shah alinukuliwa mara kwa mara akisisitiza kuwa kigezo kikubwa kinachotumika kumchagua mrembo ni uzuri na uwezo wa kuwasiliana.

    Baadhi ya watu walinyanyuka ukumbini baada ya mrembo huyo kutangazwa kuwa mshindi. Wengi walimpa nafasi Lilian Abel ambaye alishika nafasi ya pili.

    Mwenyekiti wa majaji mhindi, sasa mnategemea nini!!

    Msije kushangaa timu ya yetu ya Taifa soon itakuwa kama hivi:

    1. Krisha Gopal
    2. Manoj Kumar
    3. Dharmendra Mehta
    4. Anil Khimji
    5. Singh
    6. Amitabh Dewji
    7. Suresh
    8. Fazal
    9. Nizar
    10.Manji
    11. Alibhai

    Rais wetu mhindi na baraza lote la mawaziri ni la wahindi hapo ndio walala usingizi mnono wadanganyika watakapofumbua macho, but that WILL BE TOO LATE!

    mnajifanya nyie sio wabaguzi, lakini ubaguzi wa wahindi dhidi yetu hamuuoni!

    ReplyDelete
  74. JAMANI SAMAHANINI SANA? MIMI UZALENDO UMENISHINDA. NI KWELI HUYO MISS TZ 07 SIO MTANZANIA NA BALI NI MHINDI.. SCANDAL NI KWAMBA MSHINDI ALISHIPANGWA NA HUYO SPONSOR SHAR AMBAYE NAYE NI MHINDI KWA HIYO MSISHANGAE.....MBONA WAKATI WA UCHAGUZI UJAO ANGALIENI KAMA HUYO MISS WENU ATUKUWA TZ AU INDIA....MSHINDI ANGEKUWA queen david....
    kasera
    kc,ks

    ReplyDelete
  75. Nani anayetoa Utanzania? Tuwache ubaguzi...kuwa mtanzania haina maana uwe mweusi wa ngozi au sio kuwa na nywele za singa..Huyu ni Mtanzania kama mtanzania yeyote, sizani kuna mizani ya kuwa mtanzania..

    ReplyDelete
  76. NINI KUWA MTANZANIA? Kama waandishi wenyewe ndio hawa Tanzania bado kuna matatizo..Hongera binti na usivunjwe moyo na Watanzania wenye fikra chafu za kibaguzi, wewe ni mtanzania kama watanzania wengine na umejitoa kuwakilisha Tanzania..Ahsante sana

    ReplyDelete
  77. Tatizo ni rangi?? Au asili?? Jamani, mbona timu ya taifa ya mpira Ufaransa, wachezaji wengi wapo ambao si wazungu, mbali na kuwa France is a European country??? Henry, Gallas, Saha... England pia, Sol Campell, Ashley Cole... !! Mbona hawana ubaguzi kama nyie!! japo kuwa si wazungu, lakini wanauraia ya nchi hiyo, basi wanastahili kupewa haki yao!! Mbona mpaka leo hamajalalamika kuwa Timu yetu ya Taifa ya Cricket, kunawachezaji wenye asili ya kihindi, ambao wana represent TZ!! Mbona hamjasema chochote?? Go Richa, go fly our flag!! All the best girl...

    ReplyDelete
  78. mimi naona next year mashindano ya umiss tufanye wenyewe wabatu hamna kuweka hao vodacom ,mshindi wa kwanza anachukua baskeli yake poa utaona kama kuna muhindi ataweza kushiriki wale mweupe yoyote hata yule wa mkorogo hatutamuona itakuwa shwari kabisaaa,hilo ni wazo langu je munasemaje wadau.

    ReplyDelete
  79. Hivi tatizo ni RAV 4 au kuna jingine? Je, taratibu za mashindano ya miss Tanzania yameelekeza washiriki wake ni lazima wawe weusi kama mpingo?
    Mbona sijasikia mkimwongela Victoria Martin Hans?
    tatizo nini rangi? nyeupe? kwa hiyo sisi wanyaturu weupe kwenye miss TZ no?
    Wewe Hoyce Temu usilete mambo ya ukabila hapa, inawezekana nyie ndiyo mnaoharibu mashindano ya Miss tanzania kila mwaka kwa kushawishi ushindi wape watu wenu.
    Kama Miss TZ staafu inatuashiria kipindi chako cha umiss ulikuwa unafanya shughuli zako kibaguzi kabisa.
    Ninakushauri ujitoe hadharani ukielezea kukanusha kwamba ulilia baada ya ya kusikia Richa ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha miss Tanzania.
    Vinginevyo kama hutaki kufanya hivyo, ni vyema ukauhakikishia umma kuwa wewe ni mbaguzi, mpendelevu, na labda mkabila au mdini au vyote kwa pamoja.
    Hivi umakumbuka siku ile pale Kilimanjaro Hoteli pool side siku ulivyotangazwa Miss Ilala, unadhani hukustahili? je na yule Dada mfupi aliye kuwa wa pili au watatu ulijisikiaje alipokutupia makombora kwamba hukustahili?
    Lakini mimi kama mpenzi wa fani ya urembo nilimdharau yule dada kwa kuona kwamba wewe Hoyce Temu ulistahili, na kweli ulistahili pia kuwa miss tanzania.
    Ni vema ukajifunza kwa undani elimu ya uraia, ujifunze uhusiano wa kimataifa, ili uwe mwanadiplomasia hasa na wala sio mbabaishaji.
    usipoangalia utabakia mpika majungu mwaka hadi mwaka.
    From USA

    ReplyDelete
  80. Hivi jamani seriously mwenzenu
    Nimekuwa na hamu sana ya kuwa na “Bibi” (girlfriend) wa KIHINDI.
    Lakini hawa Mademu inasemekana wagumu sana kupatikana kwa mswahili.
    Kuna Mdau yoyote anaweza kunipa mbinu za kupata girlfriend wa Kihindi jamani?
    Nisaidieni mwenzenu tafadhali!

    ReplyDelete
  81. We Pwiia ninauhakika ubongo ni mdogo mithili ya kidonge cha 'piriton'.
    Unawaza kuunganishiwa hadi leo, ama kweli akili yako ndogo na fupi, nani akufanyie 'ukuwadi'?
    Nenda India kama umataka mademu wa kihindi.

    ReplyDelete
  82. Hongera.Good. Keep it up.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...