Home
Unlabelled
tanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tanga School, nadhani ndiyo shule kongwe kuliko zote katika Tanganyika.
ReplyDeleteDuh ili gazeti hata baba wa taifa hajazaliwa, yaani miaka 11 kabla ya kuzaliwa Nyerere, sasa mbona gazeti ilikuwa inachapishwa kwa lugha ya kijerumani?...Nitajiju baba CI
ReplyDeleteLakini walilisoma kweli hao watani wetu. Ninavyowafahamu ni wavivu sana wakusoma hata kajitabu sembuse ligazeti lote hilo.
ReplyDeleteViko wapi sasa????....
ReplyDeleteKuna mtu aliniambia kuwa tatizo kubwa kwa waTZ wa sasa na wa zamani ni kwamba wakifanikiwa kwenda juu, wengi huwa wanashindwa kubaki huko. wachache ndio humudu kubaki juu miaka nenda miaka rudi.
hii hali ndio naiona inayotokea ktk huu mkoa wa tanga. Mambo mengi yalianza huko lakini sasa hivi hayapo tena.
Nani alaumiwe? serikali au wananchi?
Kubwa la Ma-Anonny
Wanaobidi walaumiwe kwa Mkoa wa Tanga kutokuendelea sasa hivi mbele ni wanawake wa Tanga sababu wanawake wa Tanga wanawalea Wanaume kama wanawake wawe waume zao au watoto wao wa kiume.
ReplyDeleteUkitaka ulelewe kama mwanamke kaoe Tanga kama wewe ni mwanamme.Uoe kule uone kama siku si nyingi hujaanza kuongea kaa bibi na kuwa goigoi kama mwanamke.
Raisi Kikwete kapigilia msumari kwa kuteua wanawake watupu kuwa wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Tanga.Mkoa uliojaa goigoi wengi Sasa hapo pataendelea?
Anon wa 1:56:00 PM EAT
ReplyDeleteKULA 5! Hapo umesema kweli! Na hii ya Rais nilikuwa sijaiona.
SASA HAKUNA CHA COSTAL UNION wala AFRICAN SPORTS.
MICHU LEO UMENIKUMBUSHA MBALI SAAAANA!!!
ReplyDeleteUMENIKUMBUSHA SHULE YANGU YA ECKERNFORDE TANGA!!!
NAIKUMBUKA SANA TANGA KUANZIA BARABARA YA 1-21.
MIKANJUNI,MAGAONI,MABAWA,KISOSORA,CHUMBAGENI,KWA MINCHI,SAHARE.
NAKUMBUKA SANA WEEK END MAMBO YA RASKAZONE!!! DU
ILA TA KWA VISHEREHE KILA WEEK END MAULIDI AU HARUSI!!!
KWELI WAJA LEO WAONDOKA LEO!!
MPO WAPI MLIOSOMA ECKERNFORD,GARANOSI,SAHARE,POPA,JUMUIYA,TANGA SCHOOL?
Hebu acheni umbea hapo juu, mimi nimefika Tanga na kule Lushoto watoto wengi wa vigogo wamesomea au wanasoma kule.
ReplyDeleteMkapa kahamia Lushoto.
Watanga wavivu, nani anasema hivyo, Saruji Tanga, viwanda vya sabuni Tanga, hata soda za Tanga zilikuwepo, Anjari soda ni ya Tanga Vyakula mnavyokula Kariakoo asilimia kubwa inatoka Tanga, kama ni wavivu mngepata mboga na matunda?
Na wasiojua ni kwamba kiwanda cha kwanza cha uchapaji east africa nzima kilikua Lushoto Tanga, Soni pale.
Wasambaa walikua kabila la kwanza Tanzania kuandika vitabu kwa lugha.
Akaja Nyerere akairudisha nyuma, Mwinyi akaendelea, Alichofanya Mkapa ni kuhamia kule.
Na kama hawasomi, mlimpataje Makamba ambaye ni msambaa kuja kuliongoza jiji la nchi Dar es salaam.
Hamuujui uzuri wa Tanga, bali kusifia wanawake tu.
Honesty, Watanga wavivu waelimu. Mashule mengi lakini wanaosoma wote wametoka nje ya Tanga. Hawapendi kuchangamsha ubongo wao kabisa. Well, wanaweza kuwa wanafnya mambo ya viwanda n.k, lakini meneja ni mtu kutoka nje. Mameneja wa mashamba ya chai wote uliza wametokea wapi?
ReplyDeleteWale wanaoifahamu vizuri Tanga hawawezi kundika vitu vya ovyo-ovyo kama baadhi ya watoa maoni hapo juu.
ReplyDeleteMimi kwetu ni Kigoma na nimeishi tanga kwa mara ya kwanza miaka kumi iliyopita kikazi. Wakazi wa Mkoa huo ni wakarimu na wacheshi. Kwao wao mgeni ni sehemu ya jamii. Katika kukaa kwangu pale sikujisikia kama nipo mbali na nyuymbani kwetu ambako nilipazoea sana, nimepata marafiki kadha wa kadha wazee kwa vijana. Sasa hivi mimi kule tanga najihesabu kama ni nyumbani kwangu kwani nimeweza hata kujenga nyumba na baadhi ya ndugu zangu wanaishi huko na kufanya shughulizao na familia zao. Wakati nikiwa na mapumziko mafupi nyumbani kwangu ni Tanga.
Nilipata bahati ya kuongea na wazee mbalimbali ju ya mabo tofauti ya Tanga, waliniambia kuwa hapa sio mahali pa kubaguana, kwa mfano miaka ya nyuma Tanga iliwakilishwa bungeni na wabunge ambao Tanga sio asili yao Kama Marehemu Alhaj Omar Muhaji toka Kondoa, Marehemu Austin Kapera Shaba toka Mtwara. Hawa watu hadi leo hii wanahesabika kama ni wanatanga halisi.
Lakini historia ya Tanga inaonyesha kuwa Tanga kabla na baada ya ukoloni ilikuwa ni moja kati ya maeneo yaliyotoa ajira nyingi katika nchi hii, nchi za jirani na hata sehemu nyingine duniani.
Hili lilikuwa linadhihirishwa wazi na kilimo kikuu kwa wakati huo cha zao la Mkonge. Kwa wale waliokuwepo miaka hiyo nadhani ni mashahidi katika hili.
Tanga katika kuijua kwangu, nimeona ni mkoa wenyewe maingiliano na makabila mengi, mbali ya watu wenyeji wa wa Mkoa wa Tanga, kuna watu wengi sana waliohamia na kuzagaa katika mkoa mzima kutokea Burundi, Kongo, Kigoma , Tabora, Mwanza, Sumbawanga, Shinyanga, Njombe, Mtwara, Lindi, Ruvuma nk. Na hao wote niliowataja wako katika generations tofauti, kwa maana kuwa nyumbani kwao ni Tanga.
Pia maelezo ya wazee hayakuishia hapo, kutokana na umaarufu wa zao la mkonge, shughuli za kiuchumi zilikuwa ziko juu sana na hata ilikuwa ni rahisi kwa vijana wenye vipaji kupata fursa ya kuviendeleza. Kwa mfano, wanamuziki wengi mahiri wa miaka iliypita walitokea Tanga, kama Mzee Frank, Mzee Mdimu, andugu wawili Rajab Khalfan na ndugu yake Issa Khalfan (Jamhuri Jazz Band / Simba wa Nyika) Wilson Peter na George Peter (Jamhuri na Simba wa Nyika). Mzee John Kijiko, Hemed Maneti Ulaya, Komandoo Hamza Kalala na wengine wengi.
Vile vile kulikuwa na wachezaji mpira mashuhuri kama akina Omar Zimbwe, Omar Mahadhi, Abdallah Luo, Omar Mwabuda, Makunda, Mbwana Abushiri, Jalala, Mohamed Salim, Salim Amir, Salim Omar nk.
Katika kuzungumza na wazee hatasahau kukuelezea Mwalimu wake baba wa taifa Mwl Nyerere, Mzee Augustine Makame. Huyu Mzee yupo hadi hii leo, yeye alimfundisha Mwalimu Nyerere.
Kwahiyo wanaoiangalia Tanga kwa kutazama "wanawake" ndiyo wavivu wa kufikiria kwani hajafanya zoezi la kutosha kujua how Tanga is potential kwa economy ya Tanzania.
Wote tunafahamu jinsi zao la mkonge lilivyoanguka Duniani, sehemu kubwa ya mkoa wa Tanga ilikuwa ni mashamba makubwa ya zao hilo la Mkonge, kwa hiyo kuanguka kwa za la mkonge kuliendana sambamba na kuanguka kwa uchumi wa mkoa wa Tanga. Kwa maana hiyo hata zile activities zilizokuwepo wakati kwa ajili ya nguvu za uchumi haziwezi kuwepo tena.
Lakini Tanga inabaki kuwa potential kwa uchumi wa Tanzania kwa kipindi kirefu kijacho na inaweza kurudi ahali yake ya zamani endapo mpango wa muda mrefu wa kujenga bandari mpya huko Tanga utatekelezwa.
Mimi sasa hivi ni mwana-Tanga halisi, kwani ni mahali pazuri pa kuishi maisha ni nafuu ninaweza kupafananisha na Morogoro.
Kwa uvivu ni wavivu haswa! kasoro wanaotoka Lushoto lakini kuanzia korogwe kurudi nyuma mpaka ufike Tanga mjini hapana kwakweli.Kwa wanawake hali kadhalika mtaa huo wa wavivu ndio hao hao wenye bidii maana hawana kazi ya kufanya zaidi ya kufundwa.Viwandani nenda kafanye tathmini utagundua asilimia 75 ni wageni sio wenyeji upo hapo shenanihii?
ReplyDeleteMnaosema Tanga naona hamjui tu. Kwa mfano nendeni kule Lushoto muone wasambaa wanavyojishughulisha na vitu kama biashara za bongo na matunda n.k. Biashara ndogo ndogo wanazo na kwa Tanzania hizi zikipewa sapoti zaidi basi tutapiga hatua zaidi kama taifa.
ReplyDeleteWewe mtu wa kigoma unayetetea wanawake wa Tanga hufai kuwatetea kwa sababu hayo makabila yote yaliyohamia Tanga walikwenda kama manamba kwenye mashamba ya Mkonge baada ya mkoloni kuona kuwa wakazi wa Tanga ni wavivu mno akaamua kuagiza wafanyakazi manamba toka mikoa ya wachapakazi kama Kigoma na Iringa.
ReplyDeleteTatizo la nao manamba walipofika Tanga wakaoa wanawake wa Tanga wakalowea hasa watu wa Kigoma.
Watu wa Kigoma ni kama watu wasio na kwao wakifika mahali.Ni lini uliwahi kuona mtu wa kigoma anasafirisha maiti kwenda kuzika kigoma kama kafia mikoa ya mbali?
Mtu wa kigoma akifika mahali naye habanduki na hasa akiwa mwanaume,na akapata mwanamke wa Tanga hapo ndiyo kabisa!! Mtu wa kigoma kafika.
Mimi nilioa Tanga mwanamke akawa ananipeleka kuniogesha bafuni.Akaja kufariki baada ya kukaa naye miaka 10.
ReplyDeleteAlipofariki mimi kuoga mwenyewe ilikuwa shida.Nilikuwa mvivu kuoga kupindukia.
Sasa ikatokea nikaja oa mwanamke wa Kichaga baadaye.Nikamwambia awe ananipeleka kuoga sababu mimi sijazoea kuoga mwenyewe akanipa kipigo ambacho sitasahau.
Nikamshitaki kwa ndugu zake wakanitukana kuwa dume zima limekaa kama senge.
Ikabidi nijirekebishe.Nianze kukakamaa.
Malezi ya wanawake Tanga ni kweli wanawalea wanaume kama wanawake.
Tanga kuna tatizo la Mfumo jike.Wanataka hata wanaume wawe kama wanawake kwa kuongea na tabia.
Si ajabu kukuta mwanaume Tanga anakuna nazi au anampaka hina mkewe kwenye vidole.
Na kwa malezi hayo Tanga kuna wanaume wapaka hina wengi na wanaotembea barabarani wakiwa wanarembua macho na kutikisha viuno na kutafuta mabwana kama wanawake kwa sababu kwao wanaona mfumo jike ndio unafaa sana na hawaoni aibu hata uwaambie vipi kuwa mwanaume hatakiwi kukaa kike kike.
Hoyce Temu: Richa hakustahili
ReplyDeleteTanzaniaDaima jumatano, 5 Septemba 2007
na Mwanne Sekuru
HOYCE Temu, mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, amesema hapingi taji la Miss Tanzania kwenda kwa Richa Adhia kutokana na rangi au asili yake, bali mrembo huyo hana sifa na vigezo vya kuvikwa taji hilo.
Hoyce alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Haidery Plaza, ikiwa ni siku tatu baada ya kufanyika kwa shindano hilo na Richa kuvikwa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007.
Muda mfupi baada ya Richa kuvikwa taji, Hoyce alifikia hatua ya kububujikwa machozi kwa kile alichosema na anachoendelea kusisitiza kuwa, mrembo huyo hakustahili kutwaa taji hilo.
Kitendo hicho cha Hoyce kilitafsiriwa kwa maana mbalimbali, huku wengine wakimlaumu kwamba mrembo huyo wa mwaka 1999, ameonyesha ubaguzi kwa sababu anampinga Richa kwa asili yake.
Akifafanua msimao wake jana, Hoyce alisema hampingi Richa kwa uasili au rangi yake, bali hakustahili kuvikwa taji hilo, isipokuwa mrembo namba mbili hadi wa tano.
Walioshika nafasi hizo katika shindano hilo lililofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club ni Lilian Abel, Queen David, Victoria Martine na Khadija Sulla.
Hoyce alisema kilichotokea katika shindano hilo, kinatishia kutekwa kwa maudhui halisi ya uwepo wa shindano hilo nchini kutokana na baadhi ya wadau kujali zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali.
“Sikuona kigezo chake cha kumfanya achaguliwe kuwa Vodacom Miss Tanzania mwaka 2007, kwani inaonekana wazi wadau kuangalia zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali baada ya kuipa kipaumbele lugha yetu.
“Napenda nieleweke kuwa simpingi Radhia kwa uasili au rangi yake, bali ninahoji vigezo vilivyomfanya hata akavikwa taji kwa sababu hana hadhi aliyopewa ya kuiwakilisha nchi katika shindano la kimataifa,” alisisitiza Hoyce huku akionyesha masikitiko.
Alisema kilichomliza siku ya shindano, si suala tu la Radhia kutangazwa mshindi, pia ni kuona shindano zima la safari hii lilivyokuwa na upungufu mwingi.
Hoyce miongoni mwa upungufu huo, anasema ni kukosekana kwa vazi la ubunifu wakati kila wakati imekuwa ikisisitizwa kuhusu suala la ubunifu wa vazi la taifa.
Alisema, hofu yake ni kwamba, kama hali hiyo itaendelea hivyo ya warembo kutoshindanisha ubunifu wao, kuna hatari hata utamaduni halisi wa Mtanzania ukamezwa na ule wa kigeni.
Alisema dosari nyingine ni utaratibu uliotumika katika kuuliza maswali, kwani kwa kawaida kapu la maswali linapopelekwa mbele, huwa halirudi nyuma hadi wote wamalizike, lakini safari hii wakati wa kujibu swali kwa mrembo Victoria Martin, kapu liliondolewa na baadaye karatasi ikatolewa tupu.
“Sipo hapa kwa ajili ya kutaka kumvua taji Richa, isipokuwa nipo kwa ajili ya kurekebisha haya, ili yasije kutokea miaka ijayo.
“Na tunachotakiwa ni kuangalia Nancy alipungukiwa vigezo gani hadi kushindwa kuchukua taji la ‘Miss World 2005’, ili tuweze kuchagua ambaye ataweza kujazia vigezo hivyo na kurudi na taji hilo na si kurudi nyuma tena,” alisema kwa uchungu huku akionekana akitaka kulia.
Aidha, alisema kuwepo na utaratibu wa kutangaza mataji, kwani unapotangaza mapema mrembo aliyeshika taji jingine kabla ya taji la Tanzania, unamnyima haki yake ya kupigania taji lake, kwa kuwa atajua hataweza kushinda tena.
Vinginevyo anasema watangaze utaratibu wa kuwa mrembo anaweza kushinda taji la Miss Tanzania hata kama katangazwa kupata taji lingine.
Pia alishauri kwa wanaopewa kazi ya kusimamia kambini wanatakiwa kuwa makini kuangalia warembo ambao wanatakiwa kushika taji hilo kwa uhalali.
Mnanishangaza mimi.
ReplyDeleteKama ni wavivu je yake mavyakula mnayonunua Kariakoo anayeyazalisha ni nani?
Kama ni hio RTD sasa imekua Usambara town kwani kila leo ndio hao hao.
Kwa taarifa yenu nikwamba pamoja nakufujwa au kuachwa nyuma lakini Tanga iko juu.
Muulizeni Mkapa.
Hawasomi!!? Acheni tusilete orodha ya wagosi wanaonyanyasa serikalini.
Hasa hao wasambaa hawakuitwa wasambaa bure.
Kariakoo sasa yote imekua ya wagosi sasa, kama vile wahindi na kisutu.
Kama unaona wanaume wa Tanga goigoi mwazime mkeo uone kama atakutaka tena.Acheni hizo,Tanga is best from those days
ReplyDeleteWewe annomy uliye-type comments zako bila ya kufikiri na kusema 'Well, wanaweza kuwa wanafnya mambo ya viwanda n.k, lakini meneja ni mtu kutoka nje. Mameneja wa mashamba ya chai wote uliza wametokea wapi?'
ReplyDeleteHuenda unakatatizo kidogo, hivi umesahau kwamba hii nchi ya Tanzania ni kwa ajili ya watanzania wote?
Unaelewa nini juu ya huu usemi unaosemwa 'fursa sawa' oau 'equal opportunity'
unataka kuwafundisha nini watu wa Tanga, Ubaguzi?
Mbona mimi ni mtu wa Tanga na ninaongoza shirika hapa hapa Mwanza, je watu wa Mwanza niwaiteje?
Acha ujuha, mmmeonyesha vitendo vyenu vya kibaguzi dhidi ya miss Tanzania 2007 kumbe bado sasa mnataka wenyewe kwa wenyewe mbaguane?
Ukweli ni kuwa wa Lushoto ndio wanaojishughulisa lakini kwingine ni wavivu.
ReplyDeletemajority ya watu wanaoshughulika Tanga sio wenyeji wa hapo na hata mtu akiishi tanga akirudi likizo unamwona kawa kama mrenda vile.
Gazeti linasema USAMBARA, kwahio linaongelea maendeleo yaliyokua kule Usambara kwa wasambaa.
ReplyDeleteWanaosema watu watanga hawasomi ni wavivu nataka kuwauliza je mnawajua watanga ambao wako serikalini? Je mnamjua Makamba ni nani? Mshangama ni nani? ni wengi tu kama tukitafuta majina ila nimewapa haya majina ambayo pengine yatamifunua macho kidogo. Kuna pia Shekilango Road, je mnajua kwanini ilipewa hilo jina na Shekilango alikua nani?
Tanga inafujwa lakini bado itazidi kuongoza.
Mgosi, Bambo, Mangi, NG'NAWANE, MTANI,,,,Na wengineo sina Mbavu...mnaniacha hoi na huo ubishi wa Tanga...Acha tuuu vitu vingine vinakaribiana na ukweli jamani, kama hilo la JK na wakuu wote wa jinsia sina mbavu...hivi kweliee...
ReplyDeleteTuache utani linalonikuna ni kutowekeza katika mazao ya matunda. Na kutokuwa makini ktk uwekezaji kwa jumla. NASIKIA WAJANJA WA NCHI JIRANI WANAJIZOLEA KIHOLELA NA KWENDA KUFANYA KWELI KTK VIWANDA VYAO NA KU-LEBO made in HUKO KWAO!!!! jamani masikini Wabongo,,,hawachukui Tanga tuu bali hata kule Manyara-vitunguu, Arusha-Tanzanite, Vinyago Kina CHINGA vya Mwenge, Ntwara nk, acha GOLD ya Bwana NYEPESI... Mi naona la msingi tuisukume serikali yetu na kupendekeza mikakati mipya ya kuwekeza katika mikoa na maeneo mashughuri kwa uzalishaji ili kuboresha maisha ya watu wetu,,,hata kina mama wa Tanga wakitupepelea tuta-furahia na kufanya kazi kwa bidii na Afya njema zaidi. Naamini mahaba na mapenzi ni SANAA Inayohitajiwa sana ktk familia na maisha ya mahusiano,,, ni SEHEMU YA UTAJIRI WA WATU WETU NA MIMI BINAFSI SI-UBEZI...NAUTAMANI, NAUFAGILIA,,,Kwangu ni kichocheo cha MAISHA BORA KTK NDOA. Bila Ndoa yenye FURAHA NA MAPENZI jamani, tutaweza wapi kufanya makazi haya mazito ya kuuondoa umasikini? KTK mahaba na ustawi wa kipato, utani utakomaa ktk nchi yenye kipato na ajira kwa wote. Wengi watapenda kufanya kazi yenye mapato mazuri.Hata kina mama tunaowanyooshea vidole ktk huu mtandao watakuwa tayari ku-ingia ktk soko hilo...lawama na kejeli hizi zitakuwa burudani baadala ya mzaha tuu ktk mtandao wa Bwana Michuzi.
La Msingi Bwana nasi Wagosi na watani wengineo tukipata kaupenyo kam mfano huko RTD alikotaja jamaa hapo juu au kwingineko basi tuwakumbuke na wengine tusiwafungie nje kabisa. WOTE WAJUKUU WA BABU MMOJA. NA MAMETU HUYU MTANZANIA. Inawasononesha wajukuu wa Babu Nyerere WANAPOFUNGIWA NJE SASA WANASHITAKI KTK MTANDAO!!! KAMA KWELI BASI KAZI YA MTANDAO HAPA KUREKEBIHANA MWENENDO.
Nilifungua blogu kufuatilia swala aliloandika jamaa kwenye GAZETI MWANANCHI JUMAPILI 18.11.2007; juu ya Dada YETU Miss TZN ku-kashifiwa ktk mtandao. Kwa kweli inauma sanaaaa wabongo sio vizuri...hata kama ana ngozi tofauti...mbona Babu Yetu Nyerere alishalaani mambo hayo? na alipigana kufa na kupona dhidi ya UOVU huo... Dhambi ya Ubaguzi haisameheki... Japo ANC wamejaribu kusamehe TUKIIANZA BONGO NI KAMA MTU ALIYEONJA NYAMA YA BINADAMU...kumbukeni maneno yake... leo Wabara... kesho Wazanzibara..kisha..Wapemba...Keshokutwa .... inaendelea kusambaa....
Nalaani kwa moyo wangu wote unyanyapaa wetu dhidi ya dada huyu. Namtakia kila la heri...Dada usikate tamaa...Ndivyo binadamu tulivyo.NAAMINI KWA MOYO WANGU WOTE KUWA ULISHINDA KIHALALI. mdudu rushwa hakuingilia maamuzi ya majaji.
Kuhusu namna ulivyochaguliwa...Kamati ya kina Lundenga myasikie hayo na kuyafanyia kazi.
Kila la keri MISS TANZANIA2007
Kila la keri Wagosi
Kila la keri Wamangi
Kila la keri Waba-mbo
Kila la keri Wana-wane, ngosha, bageshi na juu ya yote WATANI WOOOTE BARA NA VISIWANI!!!!
ASANTE Muhidin kwa nafasi hii.