Habari kutoka kwa A.Y ni kwamba msanii huyu mkali anatarajia kuzindua documentary “UNDANI WANGU”, Website www.ay.co.tz na Nguo zitazokwenda kwa jina la “A.Y COMMERCIAL WEAR”.
Tarehe 16/11/2007
Venue:Club Maisha
Wadhamini ni Straight Muzik wakishirikiana na Lips Entertaiment
DocumentaryInaelezea safari nzima ya maisha ya A.Y kama live shows zake,historia ya muziki wake,maisha nje ya muziki,ushauri na mitazamo ya wadau,maisha yake ya kimapenzi.
Clothing line: Pia AY anatarajia kutoa nguo zake week hii jumamosi zikiwa zinajulikana kwa jina la “ A.Y commercial wear”.Zina ubora wa hali ya juu kabisa na zitapatikana katika duka la Zizzou Fashion kabla uzinduzi huo.Washabiki na wapenzi wa A.Y wataweza kupata T.shirts za Kiume,Tops za Kike,Kofia za kike na kiume zenye nembo yake. Website.
Siku hiyo A.Y atazindua tovuti yake ya www.ay.co.tz ambapo atakuwa msanii wa kwanza kuzindua tovuti yake rasmi kwenye siku hiyo maalumu.Katika website yake kuna mambo mengi ndani yake.utapata kuona video zake mpya,habari zake,ratiba ya ziara zake za kimuziki,picha mbali mbali,pia kuna sehemu inayofanya shabiki ukawasiliana na A.Y kwa barua pepe na mambo mengine mengi ya kuvutia.
Wasanii wanaotamba afrika ya mashariki kutoka Kenya,Uganda na Tanzania wataosindikiza usiku huo watatangazwa kipindi kifupi kijacho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera kijana kwa jitihada zako tunakutakia kila heri ufikie mafanikio unayokusudia. Hata h ivyo ushauri wa bure ni huu; si lazima kila aitwaye celebrity aje na lebo ya nguo ili kufanikiwa. Siyo tu kwa sababu P didy , 50 Cent na wengineo wana lebo na KP kaanzisha basi kila mtu atataka kufanya hivyo. Tumieni mtandao na wataalam wa mambo ya biashara kubuni miradi mipya lakini siyo kuigana tu. Haya ndiyo mambo ya uswazi kila baada ya hatua mbili unakutana na genge, la nyanya, nazi kauzu na ndimu.

    ReplyDelete
  2. Tight sana hii. Out of big number of artists that exist in Tizii music industry, u're the one who always come with something which shows that u real want 2 take step ahead. Kuanzia mamega mix enzi zile, wengi wakafuata. Keep ya head up bro, milango itafunguka sooner than u think.
    Ariano, K'la.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...