Barrick Gold Tanania yatimua wafanyakazi 900
Oktoba 29, 2007
Kampuni ya Barrick Gold Tanzania leo imetangaza kuwa imewasimamisha kazi wafanyakazi takribani 900 katika mgodi wa wa Bulyanhulu uliopo Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga.

Wafanyakaazi walioathirika na kusimamishwa kazi ni wale waliojisusisha na mgomo batili ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (TAMICO) jioni ya tarehe 24,October,2007.

Menejimenti ya mgodi wa Bulyanhulu imetoa taarifa kwa wafanyakazi wote ikiwaataarifu kuwa, wafanyakazi wote walioshindwa kurudi kazini kama walivyoagizwa wamesimamiswa kazi na nafasi zao zitatangazwa upya.

Menejimenti pia imefafanua kuwa waajiriwa wote wa hapo awali hawatabaguliwa kwa namna yeyote na kwamba kila mmoja anayo haki ya kuomba kazi kwa nafasi zitakazo tangazwa upya.

“Nasikitika sana kwamba TAMICO hawakuwa wastahimilivu, tumejaribu kwa kiasi kikubwa kutafuta suluhisho ili kuzuia vurugu za aina yeyote lakini wenzetu wa TAMICO wakafanya maamuzi kwa nia isiyo njema” alisema Greg Walker, Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu.

Hasara iliyopatikana katika Mgodi wa Bulyanhulu kutokana na mgomo huo inakadiriwa kuwa zaidi ya dola za kimarekani USD $ 5.2 milioni. Hasara hiyo inategemewa kuongezeka mpaka pindi mgodi huo utakapoanza kuendeshwa kwa ufanisi kama hapo awali.

Kipaumbele kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mgodi unarejea kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili kukidhi na kutimiza wajibu wetu kwa jamii inayozunguka mgodi, wafanyakazi wetu, wabia wetu kibiashara na serikali kwa ujumla.

Ili Shughuli zetu ziendelee kufanyika katika hali ya amani, Uongozi wa mgodi wa Bulyanhulu unaona haja ya kutekeleza marekebisho ya mfumo wa uendeshaji ambayo yatainufaisha kampuni na wafanyakazi wake.
Kuhusu Barrick Gold.

Barrick Gold Tanzania inaendesha migodi mitatu ya Bulyanhulu, North Mara na Tulawaka, ambapo hivi karibuni itaanza ujenzi kwenye mradi wa Buzwagi.
Maeneo ya migodi ya Barrick inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye sekta hii muhimu ya madini nchini Tanzania, huongeza nafasi za ajira, ukuaji uchumi na kuboresha huduma ya elimu na afya kupitia miradi inayobaki kuwa endelevu.

Kampuni ya Barrick ni mchangiaji mkubwa katika hazina ya Serikali, kupitia mishahara, mrahaba na kodi.
Imetolewa na;
Teweli Kyara Teweli
Uhusiano & Mawasiliano
Barrick Gold Tanzania,
Plot 1736, Hamza Aziz Road,
Msasani Peninsula
P. O. Box 1081, Dar es Salaam
United Republic of Tanzania
Kwa mawasiliano zaidi;
É +255 22 2600604
È +255 767 308600
*
tteweli@barrick.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hala hala jamani...... Naona Bro' Michu umetuletea hiyo moto. Kwa kweli mimi naona hao jamaa pamoja na kwamba wameamua kuwasimamisha ndugu zetu 900, lazima pia tuangalie swala muhimu sana ambalo hapo nyumbani linafumbiwa macho, kipengele kinachosema "sitajihusisha na mgomo wowote batili" kwenye mikataba ya kazi. Bahati mbaya ni kwamba wengi hatusomi hapo, sasa ndio mambo yenyewe haya!! Na hata tukisoma, nani kasema ukienda kuomba kuandamana kupinga pesa ndogo ya mishahara utapewa ruhusa, hivyo hakuna mgomo usio batili!!

    Ombi:
    1. Wizara husika tuliangalie hilo!
    2. Vyama vya wafanyakzai tuungane na kuwa na nguvu
    3. Wafanyakazi wenzangu, jamani umoja ni nguvu - tukigoma tugome wote na sio kuwa na mamluki!!!

    ReplyDelete
  2. HAYA NDIYO MOJA YA MAMBO AMBAYO YANATURUDISHA NYUMA KILA SIKU HALAFU SERIKALI INAKAA KIMYA TUU.. IMAGINE HAPO FAMILIA NGAPI ZINAKUWA HAZINA KIPATO? WATOTO WANGAPI HAWATAENDA SHULE KWA KUKOSA ADA? HIVI KWELI WATU HAO WOTE WALIKUWA WAJINGA KUGOMA?,TENA KUPITIA CHAMA CHAO? LAZIMA HAPO KUWA WALAKINI . CHA AJABU MWAJIRI AMABAYE NI MMOJA YA WAWEKEZAJI WANAOTETEWA NA SERIKALI HAONI HATA AIBU KUFUKUZA WATU WOTE HAO!!! AMA KWELI TUTAENDELA KUIBIWA UTAJIRI WETU HIVIHIVI TUKIONA. HAPA NI KUONGEZA MAJAMBAZI TUU MITAANI. NAAMINI KABISA HAO JAMAA LAZIMA WALIKUWA NA POINT SI HIVIHIVI. SERIKALI KWELI INAONA SAWA HAYO YOTE?? HIVI SERIKALI IKO KWA AJILI YA NAI HASA?? IKO KWA AJILI YA WAWEKEZAJI TUU??????

    MZOZAJI

    ReplyDelete
  3. Mwenyekiti CCM Urambo azikwa

    Na Hastin Liumba,Urambo

    MAMIA ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakazi wa Mkoa wa Tabora wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Kapteni Jaka Mwambi, wamemzika aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Urambo marehemu Twaha Ngoso aliyefairiki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali aliyopata akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya mwezi uliopita.

    Marehemu Ngoso alizikwa jana saa 10:05 jioni katika Kijiji cha Usindi Kata ya Ushokola Tarafa ya Kaliua wilayani Urambo.

    Mwili wa marehemu uliwasili kwa ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) saa 7:15 mchana katika msafara ulioongozwa na na Bw. Mwambi.

    Katika mazishi hayo Bw. Mwambi, alisema CCM imempoteza kiongozi shupavu ambaye bado alikuwa akihitajika na chama hicho kimepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa.

    Aliwataka wanaCCM na wakazi wa Urambo na Mkoa wa Tabora kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao

    Katika salamu zake za rambirambi CCM imetoa sh milioni 1 kwa ndugu wa marehemu wakati CCM Mkoa wa Tabora ilitoa sh. 477,000 na Serikali ya Mkoa ilitoa sh. 300,000.

    Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Abeid Mwinyimsa, Wakuu wa Wilaya za Sikonge,Tabora na Urambo.

    Kufuatia kifo hicho idadi ya watu waliofariki katika ajali hoyo iliyotokea Septemba 24 mwaka huu katika Kijiji cha Usindi Kaliua imefikia wanne.

    Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni diwani wa Kata ya Ushokola Marehemu Haruna Shamshel, walinzi wa Waziri Kapuya marehemu Ramadhan Waziri na Khalfani Kiloko.

    http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4344

    ReplyDelete
  4. Jamani jamani watanzania LETS JOIN FORCES TOGETHER TO KICK BARRICK OUT OF OUR COUNTRY.

    Hawa wazungu wameshatufanya watz mazezeta sana tumeshachoka.
    Wanachuma uchumi wetu, wanatunyanyasa, wanasign bogus treaties with corrupt ministers etc
    LETS KICK THEM OUT

    ReplyDelete
  5. Michu,unatuangusha ndugu yangu kutokana na ukereketwa wako wa CCM.Yaani unajifanya kama hujaskia kwamba akina SLAA wamelipua bomu jingine kuhusu mafisadi!!!Acha kuangalia upande mmoja tu wa shilingi ilhali wasomaji wako tulio nje tunakuamini kuwa u miongoni mwa vyanzo bora vya habari za huko nyumbani.Ile ya orodha ya mafisadi kule Temeke uliikaukia,na hii ya wikiendi nayo umeichunia.ACHA UNAZI WA KISIASA.

    ReplyDelete
  6. Hivi jamani kuna tetesi kwamba hawa barrick katika hiyo migodi yote mitatu kwa pamoja kodi wanayoilipa serikali ni chini ya wanayolipa makaburu kwa kampuni moja tu ya bia!
    Je wapi duniani bia ina thamani kuliko dhahabu?! labda kwa bongo tu!Au wabongo twabugia laga kwa kasi ya umeme!Ama kweli wajinga ndio waliwao!

    ReplyDelete
  7. bw. Tewelli sitakuandikia barua pepe ila nitakuomba ujibu swali moja kwa kupitia blog hii.naamini unaitembelea blog hii ndio maana umeleta taarifa hii humu.je ni kigezo gani kilichokufanya uandike kuwa mgomo huo wa wafanyakazi ni batili,na je nini kilihitajika ili kuufanya mgomo huo uwe halali?....zemarcopolo.

    ReplyDelete
  8. NYERERE HAKUWA MJINGA ALIPOSEMA TUACHE KUCHIMBA MPAKA TUTAKAPOKUWA TAYARI. SASA TUNAFANYIZIWA NCHINI MWETU BILA YA SERIKALI KUJALI. TENA WANAONEKANA HAWANA WOGA WA KUFUKUZA WATU WOTE HAO INA MAANA WANA BARAKA ZA SERIKALI HAWA!!! HII SIJAPATA ONA NI TANZANIA PEKEE NDIO YAWEZEKANA..

    ReplyDelete
  9. JAMANI TUWASAIDIE HAWA WATU, TUNABAGULIWA/NYANYASWA NDANI YA NCHI YETU WENYEWE NCHI INAHARIBIKA/HARIBIWA SLOWLY BUT SURE "TUNAHITAJI MIKATABA YA KUJENGA NCHI YETU SIO KUBOMOA NCHI YETU" .. KICK THEM M@T#E& FU%K$ OUT

    ReplyDelete
  10. Wadau wenzangu haya ya Barrick yapo karibu kila kampuni zilizopo Tanzania,si suala la kushangaa sana japo Barrick wamefika mbali sana,na hii ni kutokana na kusoma udhaifu wa kiutendaji kwa watendaji serikalini yetu. NBC, TRC,TWIGA CEMENT,ni mfano tu wa makampuni yaliyokua,au yapo kwenye migogoro ya maslahi na hali bora kazini. Watanzania hadi ukiona wamegoma ujue hali ni mbaya sana.Hawa wageni wanatufanyisha kazi wanavyotaka ni waliopo kwenye bodi au vyeo vya juu ndio wafaidikao. Hii naomba iwe changamoto kwa wizara ya kazi haya mambo si kama hawayajui au hawayasikii,tunaomba wapunguze kupuuzia jamani watu wanachoka kugeuzwa watumwa. Ikumbukwe kwamba serikari pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii wanakusanya hadi 28% ya mshahara wa mfanyakazi kwa ajili ya kodi na mafao huku mfanyakazi akibakiwa na wastani wa 70%ya mshahara kila mwezi. Sasa kwanini wizara haingilii kati matatizo ya wafanyakazi na vyama vyao dhidi ya hizi menejiment za wawekezaji hawa

    ReplyDelete
  11. Nasikia kichefuchefu! Itabidi NCHI nzima igome ili wote tufukuzwe URAIA.....

    ReplyDelete
  12. Eti "Kampuni ya Barrick ni mchangiaji mkubwa katika hazina ya Serikali, kupitia mishahara, mrahaba na kodi" Hivi huyu Teweli sijui, anajua mrahaba anaouongelea?? Au katumwa tu aongee vile??

    ReplyDelete
  13. Bwana Michuzi sielewi kwanini unanibania maoni yangu.. Hii blog inatupa opportunity ya kutoa maoni wewe unayabania kwanini? I just wanted to know, maanake si mara ya kwanza kw wewe kunibania maoni yangu.

    ReplyDelete
  14. haki ya nani hii nji kweli haiendi popote mpaka kiama, serikali ya vitambi vimelala tu vinadizi kuporomosha maghorofa ya rushwa.
    hawa watu inabidi wapate exposure what is wealth accumulation while the majority suffers????
    sirudi bongo hata kwa dawa,

    ReplyDelete
  15. Tanzania worker Union hawana nguvu za kujuibu mashambulizi, what they need ne strong worker union ambayo itazuia mtu yoyote kufanya kazi pasipo kujiunga na hiyo Union. JK need to jump in and help those 900 people.
    Where are Tanzania activists? You need to sleep on it

    ReplyDelete
  16. Mwanachi ya jana 29/10/2007 nayo yasema:

    Posted Date::10/29/2007
    Wafanyakazi 725 Kiwanda cha Nguo Urafiki watimuliwa
    Na Furaha Kijingo

    WAFANYAKAZI 725 wa kiwanda cha nguo cha Urafiki jijini Dar es salaam (TFC) wametimuliwa kazini kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya ogezeko la mshahara iliyotangazwa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati kwa sekta binafsi hivi karibuni.
    Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na uongozi wa chama cha wafanyakazi kiwandani hapo zinasema kuwa wafanyakazi hao walifukuzwa kazi kuanzia jana.
    Baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa wamefukuzwa kazi kwa mdomo baada ya uongozi wa kiwanda kuwaeleza kwamba usingeweza kuendelea kuwaajiri kutokana naongezeko la mshahara wa kima cha chini.



    Kweli ubinafsishaji wa mashirika una raha na karaha, ukigoma - batili, sirikali wakiongeza mapesa - kazi huna..........wallahi ndo twafwa hivyo watanzania.... Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!!

    ReplyDelete
  17. Bw. Teweli tafadhali jibu swali langu ili niweze kujua kama kundi nililokuweka linakufaa au nimekosea.mpaka sasa nimekuweka katika kundi la 'ma-Chief Mangungo wa kizazi hiki'.Watu kama nyinyi ndio mnakiandalia kizazi kijacho mazingira ya kuwa watumwa...zemarcopolo

    ReplyDelete
  18. Teweli ni msemaji tu. Anasema kile anachoambiwa na bosi wake; mwisho wa mwezi hela inaingia mfukoni mwake na anahudumia familia yake!
    Sioni sababu ya kumlaumu Teweli jamani, mtumikie kafiri ...
    (Hongera TT mara ya mwisho nilikuona ktk Luninga ndg!)

    ReplyDelete
  19. Wewe Anonymous wa Tuesday, October 30, 2007 3:40:00 PM EAT unasema Teweli ni msemaji tu si kweli bali Yeye ni afisa uhusiano wa kampuni, hivyo yeye ndo anayemshauri boss wake waseme nini ili UHUSIANO uendelee na siyo uvunjike.Kwa mantiki hiyo basi Teweli lazima AJIBU swali la Zemarcopolo.

    ReplyDelete
  20. wewe unayesema Teweli anaambiwa na bosi cha kusema hujajiuliza kwa nini huyo bosi hajasema mwenyewe na je kwanini Teweli asiende kumuuliza bosi wake jibu la kutoa. hili swali ni la msingi jinsi ninavyoliona, bw. Teweli tafadhali toa jibu.kama nakumbuka jamaa email address yake ni zemarcopolo@yahoo.co.uk mjibu hata kwa mail kama kazi yako hairuhusu kujibu hadharani, inaelekea The Marcopolo hili swala limemgusa sana. Kujibu hoja ni ishara ya kustaarabika.

    ReplyDelete
  21. TATIZO VIONGOZI WA TANZANIA WANAJIFANYA KAMA VILE HAWAISHI TANZANIA, WANAKUBALI WANANCHI WANAENDESHWA NA WAGENI KAMA PUNDA. VIONGOZI WAJUE KWAMBA LIKIHARIBIKA HAO WAGENI WATAONDOKA HARAKA, TENA KWA KUCHUKULIWA NA MAJESHI YAO, LAKINI HAO VIONGOZI WETU NA FAMILIA ZAO WATABAKI NA SISI HAPA BONGO, NA WAJUE KWÁMBA HAWAWEZI KUWA SALAMA KWENYE MAJUMBA AU MAGARI YAO KAMA SISI TULIOKO MITAANI HATUKO SALAMA. KIMA CHA CHINI LAZIMA KIJULIKANE, MARUPURUPU YOTE LAZIMA YALIPWE, ASIYEWEZA KULIPA AONDOKE, WANAPATA FAIDA SANA NA BADO WANAKATAA KUWALIPA WAFANYAKAZI, NA SISI TUMEKAA KAMA MIZUZU TU, KAMA NCHI HAINA WENYEWE...HEBU KAJARIBU HUKO KWAO CANADA, AU SWEDEN UONE! HUKO WANALIPNA MISHAHRA MIZURI, NA HATA WAKIJA BONGO WANAJILIPA VIZURI, ILA SISI NDIO WATUMWA! KWELI UJINGA UNETUZIDI SANA BONGO.

    ReplyDelete
  22. Hivi serikali uko wapiiii?kwanza huyu jamaa anadai amepata loss ya 5.2million dolla,jamani hiyo migodi ingekuwa chini ya serikali hivi tanzania tungekuwa tuna madeni na benki ya dunia?tuliwasaidia south afrika kufukuza makaburu heti sasa sisi tunawarudisha hivi kweli mnatania au? mpaka 900 wokers wamegoma means kuna big problem hapo not joke!ingekuwa kumi is another stoy but 900 HUNDRED!!!! jamani MAKABURU wamerudi. by msononeka Msufini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...