watani wa jadi simba na yanga leo wamezabwa faini ya shilingi 500,000 kila mojakutokana na timu hizo kufanya vurugu wakati wa mechi yao iliyochezwaJumatano iliyopita mjini Morogoro.

katika mchezo huo ambao Simba ilishinda bao 1-0 mashabiki wa Yanga waliwekavizuizi vya viti kwa lengo la kuzuia magari ya viongozi wa Simba nawachezaji tukio ambalo lilisababisha kushambuliwa kwa mawe, chupa za maji navimiminika vingeni gari la wachezaji wa Simba na mchezaji Haruna Moshialijeruhiwa.

yanga imepigwa faini ya shilingi 500,000 na imetakiwa kulipa gharama za uharibifu uliotokana na vurugu hizo ikiwa ni pamoja na matibabu ya mchezaji Haruna Moshi baada ya kuwasilishwa na kuthibitishwa na tff.

simba, ambao nao walihusika na vurugu kwa kurusha mawe, chupazilizojaa maji na vimiminika vingine na kusababishwa mchezo kusimama nayo imetozwa faini ya shilingi 500,000 na faini hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 31(1) na 66 ya tff.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. vimiminika vingine!

    ReplyDelete
  2. Hiyo sheria ifanyiwe marekebisho haraka sana.
    Sh 500,000/= haiwaumizi hawa simba na Yanga! Inatakiwa iwe sh. mil.5 as a minimum ili iwe fundisho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...