Msanii wa muziki wenye vionjo asilia vya kitanzania na ambaye alivuma nakibao cha Sumu ya Teja Vitalis Maembe akiwa jukwaani kuliongoza kundi zimala Maembe & The Bagamoyo Spirit wakati wa mwendelezo wa tamasha la utamaduniwa Mtanzania mjini Bagamoyo.


Msanii huyo alifanikiwa kwa kiasi kikubwakukonga nyoyo za kila aliyehudhuria onyesho lake kutokana na umahiri wake wakuimba nyimbo zinazoigusa jamii kwa karibu, vilevile wasanii anaoshirikiananao wengi wao ni vijana wadogo ambao waliushangaza umati uliojitokeza kwauwezo wao wa kupiga ala na kucheza.


Ni wazi kuwa Tanzania imesheheni vipaji lukuki kutoka kwa wasanii wenye uwezo wakuipeperusha bendera yetu vilivyo.Kinachohitajika ni kwa wadau kutoa sapoti ya hali na mali ili wasanii hawawaweze kufaidika na kazi zao ukizingatia kuwa wengi wao wamejiajiri wenyewehivyo kuipunguzia mzigo serikali.


Hivi sasa Maembe ametoa albamu yake yapili ijulikanayo kama Imbila na hivi karibuni itaingia sokoni hivyo endeleakufuatilia CHUZI NEWS kwa taarifa zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kila siku nasikia vionjo vya kitz,vionjo vya kitz,.Hivi vionjo vya kitz vikoje?Tuelezeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...