HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI, 2008


Ndugu Wananchi;

Ninayo furaha kwa mara nyingine tena kuzungumza nanyi kupitia utaratibu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa nchi yetu.
Jambo la kwanza ninalopenda kulizungumzia linahusu uzingatiaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na kuishi nchini.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 23 mwezi huu, nilimaliza ziara ya siku kumi Mkoani Kagera. Jambo moja nililoliona kwenye ziara hiyo ambalo sikufurahishwa nalo, ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.
Kwa muda sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini mwetu kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.
Wageni hao wamekuwa wanaingia na kuishi nchini isivyo halali. Sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo. Viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo. Hivyo basi, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki. Napenda kurudia kauli yangu niliyoitoa Mkoani Kagera kwamba ni marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

Ndugu wananchi;
Wageni wanaoishi nchini kwa kutumia vibali ambavyo havikutolewa na Idara ya Uhamiaji wanaishi isivyo halali. Wenzetu hawa wanatakiwa kufanya yafuatayo. Kwanza wajitokeze na kutoa taarifa kwa Maofisa Uhamiaji, Wilayani au katika vituo vya mpakani. Pili, iwapo watachagua kuishi nchini, wafuate taratibu zilizowekwa kuomba kibali cha kuishi nchini. Idara ya Uhamiaji ndiyo itakayoamua. Tunawapa siku sitini za kufanya hivyo. Baada ya hapo, hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawakufanya hivyo.
Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao. Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya nchini kwani inawezekana matatizo haya yanaweza kuwepo katika mikoa mingine.
Najua kwamba kuna Watanzania wenzetu wanaohifadhi wahamiaji haramu kwa kuwa wananufaika kwa kuwafanya vibarua au wafanyakazi wao. Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. Sheria za nchi, na sio manufaa ya mtu au watu binafsi, ni lazima zizingatiwe.

Ndugu Wananchi;
Jambo lingine baya linalofanyika katika mpaka wetu na nchi jirani Mkoani Kagera ni kuruhusu mifugo kuingia nchini holela. Hiki ni kitendo ambacho kinakiuka taratibu zinazotawala uingizaji wa mifugo kutoka nchi za nje. Pia ni kitendo cha hatari kwani kinaweza kupelekea mifugo yenye maradhi kuingia nchini bila kudhibitiwa na kusababisha maafa makubwa nchini. Kanuni na taratibu zimewekwa kisheria kutawala mifugo kuvuka mipaka na kuepusha hatari za namna hiyo zisitokee.
Jambo linalonishangaza ni kwa nini viongozi wetu hawa hawajifunzi kutoka kwa majirani zetu. Wakati wote tulipofanya zoezi la kurudisha makwao wakimbizi au wahamiaji wasiokuwa halali na mifugo yao wenzetu waliweka sharti la mifugo hiyo hiyo iliyotoka kwao ichanjwe kwanza kabla ya kuvuka mpaka hata kama mifugo hiyo ilitokea nchini kwao na kuja kwetu. Nilidhani hili lingekuwa fundisho kwa viongozi wetu hawa kuwa thabiti kuhakikisha kuwa mifugo kutoka nchi jirani inachanjwa kabla ya kuvuka mpaka kuja Tanzania. Lakini, hawajali kufanya hivyo. Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na viongozi na watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kuwa hakuna mifugo inayoingia nchini holela. Lazima sheria na kanuni husika zizingatiwe.
Aidha, nimeelezwa juu ya kufahamika kuwepo vivuko haramu kadhaa mpakani. Nimesema nilipokuwa Kagera na narudia tena leo kwamba, maadamu vivuko hivyo vimejulikana lazima tuvidhibiti. Kadhalika tuanzishe vituo mpakani vya kupokelea mifugo na kila anayeingia na mifugo lazima apitie hapo na kupata idhini husika. Nimetaka viongozi wenzetu hao wasimuonee haya mtu yeyote anayeingiza mifugo nchini kinyume cha sheria na taratibu zilizopo. Kadhalika viongozi na watendaji wanaozembea wachukuliwe hatua kali za kinidhamu mara inapobainika kuwa mifugo imeingia kinyume na taratibu katika maeneo yao.
Kama ilivyo kwa uhamiaji usio halali, tatizo la kuingiza mifugo kinyume na utaratibu linaweza kuwepo mikoa mingine nchini. Hivyo, maagizo haya ni kwa mikoa yote na wilaya zote nchini. Pia yanaihusu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo. Lazima Wizara itoe uongozi katika jambo hili muhimu kwa usalama na maendeleo ya mifugo yetu nchini. Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu mifugo kuingia holela. Si vizuri Tanzania kuwa ndiyo nchi pekee inayofanya hivyo. Wenzetu na hata hao majirani zetu wanatustaajabu.

Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia ni matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia hivi sasa. Bado bei ya mafuta iko juu sana na kuathiri uchumi wa nchi zote duniani tajiri na maskini ingawaje nchi maskini zinaathirika zaidi. Hili si jambo geni kwetu. Napenda kurudia kauli zangu za siku za nyuma kwamba, hatuna uwezo mkubwa wa kujikinga na athari za bei za mafuta. Hata hivyo, hatuna budi tuendelee kuwa waangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta. Tuepuke matumizi yasiyo ya lazima.
Wakati huo huo tunaendelea na juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha). Juhudi hizo zikifanikiwa zitatusaidia kupunguza mzigo wa mafuta tunayoyaagiza kutoka nje. Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini. Mpaka sasa leseni 22 za utafutaji mafuta na gesi asilia zimetolewa na kazi inaendelea katika hatua mbalimbali. Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie rehema zake na sisi tujaaliwe kugundua mafuta mengi hapa nchini yatakayotosheleza mahitaji yetu na ziada ya kuuza nje.
Ndugu Wananchi,
Tatizo lingine kubwa linaloukabili uchumi wa dunia sasa linatokana na matatizo yanayoukabili uchumi wa Marekani. Uchumi wa taifa hilo ambao ndiyo mkubwa kuliko wowote duniani umekuwa unapita kwenye misukosuko kwa miezi kadhaa na katika wiki chache zilizopita hali ikawa ngumu zaidi. Kasi ya ukuaji wa uchumi imepungua na thamani ya dola imeshuka. Serikali ya nchi hiyo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na matatizo hayo. Lakini, kwa kuwa uchumi wa Marekani ndiyo uchumi mkubwa kuliko wowote duniani na uchumi wa nchi nyingi duniani una uhusiano nao, matatizo ya uchumi wa nchi hiyo huathiri nchi nyingi. Na sisi Tanzania hivyo hivyo.
Nimeelekeza wachumi wetu wafanye uchambuzi wa kina juu ya athari hizo na kushauri hatua za kuchukua kupunguza makali yake. Moja ya jambo ambalo liko wazi ni lile la kushuka kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Sisi tunaweka sehemu kubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni katika dola za Kimarekani. Ni dhahiri kwamba kushuka kwa thamani ya dola za Kimarekani kunatupunguzia uwezo wetu wa kuagiza bidhaa nchi za nje.

Uchunguzi wa Akaunti ya EPA
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ambalo nimepanga kuliongelea leo ni hili suala la ukaguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje na hatua zinazoendelea kuchukuliwa baada ya taarifa ya ukaguzi kutolewa.

Ndugu Watanzania wenzangu;
Kwa mara nyingine tena nawapongeza na kuwashukuru wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutoa taarifa ya kina kuhusu matatizo yahusuyo matumizi ya fedha za Akaunti hiyo. Nawashukuru pia Watanzania wenzangu kwa kuunga mkono hatua tulizochukua na tunazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, nasikitishwa na taarifa ninazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hili. Baadhi ya uvumi huo umekuwa unapotosha ukweli na kuwachanganya wananchi. Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo. Aidha, nawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.
Napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake ujulikane. Mwisho ambao utakuwa na maslahi kwa taifa letu. Pamoja na yote yatakayofanywa, tunataka kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa kinyume cha utaratibu zinarudishwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake, yaani Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wameanza kuchukua hatua. Nimewataka watoe taarifa kwa wananchi mara kwa mara kadri inavyowezekana pamoja na haja ya kuwa waangalifu kutokutoa mengi yahusuyo uchunguzi wanaoufanya ili ushahidi usiharibike.
Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo.


Ujio wa Rais Bush

Ndugu Wananchi;
Natumai mmesoma na kusikia taarifa katika vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katika nchi yetu kunako katikati ya mwezi Februari, 2008. Tunaendelea kukamilisha ratiba na itakapokuwa tayari tutawapeni taarifa. Hilo ndilo jambo langu la nne leo.
Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba Watanzania tumpokee mgeni wetu huyu kwa mujibu wa mazoea na desturi za ukarimu wa Kitanzania. Huu ni ugeni mkubwa na wa heshima kubwa kwa nchi yetu. Rais Gerorge Bush ameipa heshima kubwa nchi yetu kwa kuamua kutumia sehemu kubwa ya ziara yake ya Bara la Afrika hapa kwetu. Ameonyesha upendo mkubwa kwetu nasi tumuonyeshe hivyo hivyo. Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku hiyo kumpokea mgeni wetu huyo mashuhuri.
Ziara hii ni uthibitisho wa kuimarika kwa mahusiano kati ya Marekani na Tanzania. Mahusiano hayo mazuri yameinufaisha nchi yetu. Marekani sasa ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa misaada ya maendeleo kwa Tanzania. Tangu mwaka 2003 kwa mfano, imekuwa inatoa msaada mkubwa ambao umetusaidia sana katika mapambano yetu dhidi ya maradhi ya UKIMWI nchini Tanzania. Kadhalika, Marekani imetusaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini.
Ndugu Wananchi,
Wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji. Kwa msaada huo utakaotolewa kupitia Programu ya Mfuko wa Changamoto ya Millenia utatusaidia kutatua baadhi ya matatizo yaliyoonekana sugu katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
Pamoja na hayo, ziara ya Rais George Bush nchini mwetu itasaidia kuitangaza nchi yetu na kuinufaisha sana utalii na uwekezaji hasa kwa soko la Marekani na marafiki zake. Tayari katika miaka miwili hii tumeshuhudia ongezeko kubwa la watalii wa Kimarekani kutembelea nchi yetu. Hivi sasa Wamarekani ndiyo wanaoongoza kwa idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti. Naamini baada ya ziara ya Rais wao watalii wengi zaidi wa Kimarekani watakuja. Hali kadhalika, wawekezaji wengi wa kutoka Amerika watajenga imani ya kuja kuwekeza nchini.
Ndugu Wananchi,
Wapo watu miongoni mwetu na hata nje wanajaribu kueneza uvumi wa uongo na kuihusisha ziara hii na masuala ya Makao Makuu ya Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Ni uongo na uzushi mtupu. Ziara hii haihusu hayo. Masuala hayo si agenda na wala Marekani haijaiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa Kamandi hiyo. Nawasihi Watanzania wenzangu tupunguze hii tabia ya kuzusha na kueneza uongo. Tunajitia hofu wenyewe na wenzetu bila sababu. Haina tija yoyote. Nawaomba tujitokeze kwa wingi kumpokea mgeni wetu huyu. Aondoke nchini salama na arejee kwao akiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

Hali ya Kenya

Ndugu Wananchi;
Jambo la tano ninalotaka kulizungumzia ni hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani na rafiki ya Kenya. Kwa kweli inatusikitisha na kutuletea simanzi kubwa. Mioyo yetu inauma kuona na kusikia yanayotokea nchini humo. Jitihada yangu ya kuzungumza na pande zote zinazohasimiana pamoja na zile zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na wenzetu wengine bado hazijazaa matunda. Sisi hatutachoka na wala hatutaacha kuzungumza na pande zinazohusika kuhusu kuacha uhasama, kuacha na mapigano na kutafuta maridhiano kwa njia ya mazungumzo.
Tunaahidi kuendelea kuiunga mkono Kamati ya Mhe. Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa na Mama Graca Machel. Viongozi wetu hao wanaifanya kazi hiyo kwa niaba ya Umoja wa Afrika wanastahili msaada wetu na kuungwa mkono nasi. Aidha, tutaendelea kushirikiana na viongozi wenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kusaidia juhudi za upatanishi. Napenda kutumia nafasi kurudia tena yale maombi yangu kwa viongozi wa PNU na ODM na wananchi wote wa Kenya kuyapa mazungumzo nafasi ya kumaliza tofauti zao. Mapanga, marungu na hata bunduki zisipewe nafasi, kamwe hazitasaidia.
Tutenganishe Uongozi na Biashara

Ndugu Wananchi;
Jambo la mwisho ninalotaka kulizungumzia linahusu maadili ya uongozi nchini. Hususan napenda kulizungumzia suala la viongozi wa siasa Mawaziri na Wabunge kuwa pia watu wanaojihusisha na shughuli za biashara moja kwa moja. Upo ushahidi wa kuwepo migongano ya maslahi kwa baadhi. Lakini, pia, hata pale ambapo hakuna dalili za wazi, hisia za kupata manufaa yanayotokana na nafasi zao hutawala. Matokeo ya yote hayo ni watu kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wa viongozi wetu.

Ndugu Wananchi;
Nchi za wenzetu hasa zile za kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizo. Wenzetu wanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake. Unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo. Anapoacha uongozi wa siasa kama atapenda atachukua tena mali yake na kuendelea na shughuli zake.
Ni makusudio yangu kuwa utaratibu huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au Ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo.

Ndugu wananchi;
Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi tarehe 29 Januari, 2008 na tumeelewana. Ni matumaini yangu kuwa sote tutaunga mkono.

Mwisho, nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu. Tuendelee kushirikiana kuijenga na kuiendeleza nchi yetu.
Asanteni sana kwa kunisikiliza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. BLAH BLAH BLAH

    ReplyDelete
  2. JK Kweli anataka mabadiliko. Yaani amnikuna sana na kipengele hiki:

    "Ndugu Wananchi;
    Nchi za wenzetu hasa zile za kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizo. Wenzetu wanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake. Unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo. Anapoacha uongozi wa siasa kama atapenda atachukua tena mali yake na kuendelea na shughuli zake.
    Ni makusudio yangu kuwa utaratibu huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au Ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo.

    Ndugu wananchi;
    Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi tarehe 29 Januari, 2008 na tumeelewana. Ni matumaini yangu kuwa sote tutaunga mkono." Yaani hapo tunakuunga mkono na miguu 1000%

    ReplyDelete
  3. I support the idea of MP's giving up there businesses and concentrate on their ministerial jobs.Lakini nahisi wata EVADE kwa kuandikisha familia kuwa business owners.

    ReplyDelete
  4. Hii issue ya kusambaza uwongo (speculations) itaendelea as long as hakuna uwazi serikalini. Tumeshangaa jana Chiligati anadai issue ya Mafisadi ilikuwa ya serikali ila Slaa ameiwahi tu!

    Pili, nashangaa mpaka Raisi aende huko Kamachumu kanyigo ndo aundue kuwa kuna waahamiaji harama! Mhh! Hii kubwa nayo! Mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya, Waziri na wengine wote hawana habari!?? Nadhani Kikwete sasa una kazi baba.

    Nashangaa pia kusema kuna vivuko fake vya mpakani, wakati kule Mbozi na Ileje kuna watu wanaishi Malawi wanasoma TZ na vice versa! Je na ile Maasai inachunga ndama wake kule Loliondo kuelekea Kenya na kurudi at random bila VISA utadhibiti vipi?! Hiyo ilikuwa porojo tu mheshimiwa rais.

    Tatu; hii issue ya kudhibiti viongozi wasifanye biashara ndo kali zaidi! Bongo hii Darisalama?!??!?!?!? Ni sawa sawa na kujaribu kuogelea kwenda pemba kutokea Tanga.

    ReplyDelete
  5. Hongera Mheshimiwa JK. Hii speech yako ni nzuri na inajenga imani kwetu. Tunakuombea mungu aendelee kukuzidishia ujasiri katika uongozi wako na wale wachache wanaokuzunguka ambao wana nia mbaya nawe washindwe. Udumu JK

    ReplyDelete
  6. Kama kuna mtu alibahataka kumuon JK kwenye TV wakati anapresent hii hotuba...utakubaliana na mimi kwamba huyu jamaa ni CHARISMATIC...hiki ni kipaji chake alichozaliwa nacho...sasa kama hajijui basi shauri yake.....yaani ana ulimi wa kuweza kumtoa nyoka pangoni...na ile smile isiyomtoka pale usoni mwee!!....Manake alivyokuwa ANANYENYEKEA....AKABEMBELEZA...AKAWA ANATOA STAHA YA UFUNDI WA HALI YA JUU.....jamani tusimwangushe JK kwenye ujio wa Bush.....YAANI ALIVYOKUWA ANABEMBELEZA!!!!JOKA LINATOKA LENYEWE PANGONI

    ReplyDelete
  7. My reaction from the speech of Mr President J.Kikwete. Kwanza kabisa I am so please to get this chance to provides answers from Mr president speech.

    First, Mfumo mbovu ndani ya wizara ya mambo ya ndani kupitia kitengo chake cha uhamiaji kimesababisha madhara haya yote. Mipaka yetu iko wazi pasipo ulinzi wa aina yoyote, wakati viongozi wetu wanazidisha zogo kuhusu wanaingiaje. Swala la rushwa ndani ya uhamiaji limesababisha watu wengi kuishi kinyume ndani ya nchi. Hii ni pamoja na vigogo wapya wa TTCL ambao wameanza kazi pasipo vibali, vile vile raia wengi wa bara la Asia wameza kuishi ndani ya nchi pasipo vibali halali vya kuishi. Swali langu ni nini kinafanyika kuenforce kwa raia hawa wangi waishio miji mikuu ya Tanzania? Awali ya hayo nampongeza muheshiwa rahisi kwa kugusa swala la wakimbizi ndani ya nchi.

    second issue, World economy is intergrated in global manner as Mr President elaborated, however kuongezeka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hakuna effect kubwa sana katika nchi ambazo sitegemezi katika mafuta. Ni uweleo wangu kwamba Tanzania economy is relied on Agricalture for more than 50%, na wakulima hawa majority wanatumia jembe la pilau au mkono basi kuongezeka kwa bei ya mafuta hakuna much effect in our economy. Tanzania use mafuta sana kwenye cormercial uses and not business uses. So increases of gas price will affect individual people more than whole economy. Hii inadhihirisha ni kiasi gani wachumi wa muheshimiwa raisi wana focus more kwenye factor za uchumi wa marekani than their own economy.

    Tatu, swala la kusema uchumi wa marekani umekwenda chini, na uchumi wa marekani unaffiliate na world economy it's misinterplation of the real meaning. America economy inaaminika umekubwa na tatizo la subprime mortagage. Mortgage ina contribute about 47% of the total US economy, less than 5% of home owner are not capable to make their month payments, which cause this crisis to landers. Go to the point ya USA economy, uchumi wa marekani bado una contribute about 43% of the world market. Majority of index in the world are still bring more return, that includes S&P 500, Nikkei index, Russell 2000 and many others are still bring giantic returns, so all MR JK said is full of CNN and MSNBC lies. Kushuka kwa dolla kumeongeza nchi nyingi duniani kuinvest katika US market. Vile vile uchumi wa Tanzania ni mdogo sana kuweza kuathirika kwa kushuka kwa dolla, sababu hakuna vitu vingi tunavyouza kwenye soko la dunia, the different side ni kwamba consumer in Tanzania are benefit more from goods coming from USA.

    Swala la Bank Kuu, muheshimiwa Raisi J. Kikwete ameshindwa kuzungumza lolote la maana kuhusu bank kuu, alichoweza kuelezea ni kuwataka watu wafumbie macho kuhusu swala zima la Bank Kuu. Muheshimiwa ameshindwa kujibu tuhuma za US embassy kuitaka serikali ya Tanzania kumuomba Balali awe deported kutoka US kurudi Tanzania ili aface Justice. Vile vile muheshimiwa ajazungumzia lolote kuhusu why report ya Enerst & Young hajawekwa public so every Tanzania could benefit from analysis.

    Last, muheshimiwa ameonyesha kutufundisha watanzania kufikiria kuhusu nini tufanye pindi muheshimiwa G.W. Bush atakapofika. Ni haki ya watanzania kuwa na freedom of speech pasipo vizingiti vyovyote, vile vile ni haki ya watanzania kusema lolote kwa muheshimiwa rais wa marekani bila kuvunja mipaka ya kisheria. Hii iwe ni kumuomba muheshimiwa G. Bush kusitisha misaada kwa Tanzania au iwe ni kumuomba kuongeza scholarship kwa watanzania. Imefika muda muheshimiwa ache kutupangia nini wananchi tufanye.

    Mwisho, speech ya muheshimiwa bado haijazungumzia lolote, kuhusu ni mbinu gani mbadala zitakazo wasaidia wadau wa Tanzania, ni vugu vugu gani analotumia kuzuia Rushwa ndani ya serikali yake. Ni kwanini anazidi kuwafunika mawaziri ambao wamekula rushwa na kuitia Tanzania katika Billion of dollar loss.
    Thanks
    Mdau wa USA

    ReplyDelete
  8. Rais, ameongea kuhusu habari za Balali kuwa kuna watu wanaeneza uzushi! ilitakiwa atoe mfano wa uzushi wenyewe hata mifano mitatu hii ni ujajnja wakuwafanya wananchi wasio analyse mambo waone kuwa yanayosemwa si kweli. mifano ya uzushi ni muhimu ye kama rais kuitaja pia alitakiwa atuambie kuwa balali yupo wapi? angalau aseme wao kama serikali wanajua alipo na anarudi lini. si kuongea juu juu na kuwaacha wananchi bila uwazi. hivi ni kama kuwatega watu!!! inabidi raisi huwe direct katika kusema. ni vizuri kwa nchi.

    ReplyDelete
  9. Ngonjera tu za kila siku...kuna siku tutazichoka

    ReplyDelete
  10. Mmmh hizi hadithi na hekaya zitatushinda!!!Watu wenye akili zao wanataka kuona matendo si maneno mengiiii.
    Huyo BushI anakuja kwetu maana wengine washamshtukia zamaniiii,hivyo anaparamia vioo tu sasa!!Pole zetu.

    ReplyDelete
  11. Porojo kibao, wala hakuna cha point hapo!

    ReplyDelete
  12. Tatizo la mtu kama hujui unaweza amini mambo mengi sana kutoka kwa wataalamu! Ila Mdau annon Feb 1:9:05 AM EAT wa TEXAS umeniosha sana. Asante sana kwa summary nzuri kuhusu economy za dunia hii.

    Nashauri Mara nyingi uwe unatembelea hii blog maana hizo zingine huko wanatuchanganya na mambo mengi, majority ukiwa uzushi au ya mitaani including dini!.

    Nashukuru kwa kuweka wazi kuhusu kushuka na kupanda kwa USD na Economy ya US na effects zake kwa sisi huku dunia ya nne.

    Maana mimi namsikia Kikwete kila siku analia na Mafuta kupanda bei lakini ukija nchi zingine kwa mfano hapo Kenya, Uganda na hata Ulaya hakuna anayeongelea hiyo issue. Wala hata bei ya vitu haijapanda. Sana sana imeshuka. Mifano ni Majirani zetu

    Sasa, mimi nashangaa, inakuwaje sisi mafuta yatuumize kwa maelezo ya mheshimiwa?! Sisi tuna nini na hayo mafuta mpaka yatuumize? Sasa yakipanda kufikia dola 250 kwa pipa ina maana uchumi wetu uta-crumble? Tusaidieni wachumi tumwelewe huyu Rais wetu. Anatuchanganya tu. Au inawezekana tuna mkataba wa kununua nchi fulani kwa bei kubwa zaidi ya ile ya soko la Dunia kama tulivyozoea?!

    Visababu vya namna hii ndo vinaongezea speculations mitaani.

    ReplyDelete
  13. Huyo aliyetoa majibu ya hotuba amenichekesha kweli, kwani umeambiwa utoe majibu au umeamua tu kutoa ujuvi wako humu kwenye blogu.

    Mie sina ujuzi wala si mtaalamu wa masuala ya uchumi lakini suala sio kutegemea bidhaa kutoka US suala ni kutumia US kuweka akiba ya nchi na hapo ndipo uchumi wa US ukitetereka na nyie wenye vi akiba vyenu kwa kutumia US dollars lazima mtetereke. Mfano mdogo tu kwa wanafunzi walio nje ya nchi kama UK halafu wawe wanapewa monthly allowance zao kwa US dollars, lazima rate itawaumiza kwa sababu kama US imeshuka na wao pesa yao watakapochange kwenda £ itakuwa ndogo na haitaweza kukidhi mahitaji yao. Huo ni mfano mdogo tu sana.

    Pili kama umesoma uchumi na unajua jinsi uchumi wa dunia na nchi yetu unavyoenda (tangu enzi ya Nyerere uchumi unasimamiwa na so called donors/ donors countries kumbuka IRD- Intergrated Rural Devt, SAPs za World Bank, na sasa kuna Livelihoods Approaches na sijui MDGS, Poverty whats whats ambazo hizo zote ni donor driven) budget yetu itagemea kwa kiasi kikubwa pesa kutoka nje kupitia hayo mamilolongo chini ya neo colonialism. Sasa unapokataa kuwa kushuka kwa uchumi wa donor mmoja hakuwezi kukwamisha uchumi wetu unawafanya wachumi walioko TZ na wengine nje ya TZ hawajui kitu, wewe kwenye uchumi wa US umeona hicho kinachokugusa moja kwa moja ambayo ni mortagage vingine sio rahisi kuviona. Hivi unajua kuwa China imeshikilia uchumi wa US kwa sehemu kubwa. (Soma world economy inavyoenda Wamarekani wengi wanajua kinachowazunguka humo ndani mwao basi). Na soon kutakuwa na economic recession kama hizo measures walizotoa hiyo serikali ya US itafail. Niambie kwa nini watu wa Mexico wanarudi kwao? Kwa nini Construction Industry imedoda sasa hivi? Na ajira zimepungua kwa kiasi kikubwa waliokuwa wanafanya kazi 2 mpaka 3 sasa hivi wamebaki na moja au hawana kabisa.

    Kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta, anayebisha kuwa mafuta hayajapanda wakati yanaonekana kwenye soko la dunia yamepanda, basi tena huyo ana yake. Sasa yakipanda kwenye soko la dunia nyie mtauziwa kwa bei ya chini? Mnafikiri kwenye hilo soko kuna mjomba mjomba? Hii inaaffect sio uchumi wa Tz peke yake bali uchumi wa dunia nzima, ndio maana GB alienda kuongea na waarabu wapunguze bei ya mafuta na sijui kama imesaidia pamoja na kuwa kwake Rais wa US. Mafuta yanunuliwe pipa moja kwa dola 100 halafu msione madhara yake kwenye uchumi wa nchi na bei ya mafuta isipande? Watu dunia nzima wanatafuta alternative source of fuel.

    Ni rahisi sana mtu kusema kazi ya mwenzie ni upuuzi kumbuka kuna washauri wa uchumi na mambo mbali mbali wanaomwandikia huyo Mheshimiwa hotuba yake kutokana na qualifications zao. Sometimes kujifanya kujua kila kitu kunaweza kudhihirisha uwezo wa ufahamu wa mambo wa mtu.

    ReplyDelete
  14. Wewe uanyesema bei ya vitu Ulaya haijapanda wacha kudanganya watu, usilete maneno ya vijiweni hapa. Bei ya kila kitu imepanda hakuna kilichobaki kuanzia nauli ya basi, treni na vitu vya kutumia kila siku mpaka mkate. Matumizi yangu ya kila wiki yameongezeka tofauti na siku za nyuma. Vitu vile vile nilivyokuwa nanunua kwa £ 10 sasa vinanicost £15. Labda ukiwa hufanyi budget na ukienda shopping mradi unajinunulia tu vitu huangalii expenses zako ndio utasema kuwa bei ya vitu havijapanda. Tena basi wanavyojua kupandisha kishakji kitu cha pence 20 kinakuwa 30, cha pence 50 kinakuwa 69, nimetoa mfano huu wa pence ndio waswahili wengi wanaenda kununua vitu £1 shop au 99 pence.! Wacheni kudanganya watu humu.

    ReplyDelete
  15. Am bit confused!! What a nice speech with a plethora of propaganda and realistic in positivism perceptiveness. There are some gaps of underpinning assumptions and theories in the whole speech.

    Nevertheless, How could a president use the rocket science approach to confuse the main stakeholders of speeches ( wakulima wa jemebe la mkono kule Mbwinde, Ungwande, Nakenjilili, Mpute, Kishimundu, Njoro, Kyela, Kajibunde few to be mentioned).

    The honoroble Predident has used both of inductive and deductive methods in addressing the critical issues face our country, however, he has been very generalisable in certain domains.

    To comprehend with other arguments, certainly I concur with some of issues and enormously disagree with other matters. Like the issue of American economic recessions has effect globally,Babu zangu si mnafahamu hata nyangumi akifa, wengi watakuwamo, baharini kuna viumbe vingi ati!Je ni nani atabisha September 11 haikuleta madhara, mnafahamu ni jinsi gain Bima za ndege zilivyopaa juu. Undeniably, American issues are determinants of global economic structures. Thus, I vigorously critique the aforementioned argument that no effect of what has recently happened to USA.

    Paradoxically, it seems that is not easy to locate the where in particular there were misinformation, again am confused as well. I want to say if someone wants a technical report should ask for the detailed information from reliable department.


    I think that we should organise a symposium for discussion critically the way forward, aspiration, desire for our nation with our individual commitment which should trigger to team work spirit. So Discussant should come with his/her view thereafter, the conclusive remarks will bring us to affirmation.

    More confusion is where, maafisa watendasji wanapojichukulia mamlaka ya idara nyingine, lakini hii ladbda inatokana na Lack of Clarity.Ama kwenye barua zao za ajira hazikuwapangia majukumu ya kufanya, ni chagamoto kwa Idara kuu ya Utumishi. Do you have employment policy, What does it articulate on employing new staff!I think there is lack of something behind.

    Anyway, let keep our eyes more on the speech and soon we will evaluate the performance.


    Dr. Confusion

    ReplyDelete
  16. TUKIGUNDUA MAFUTA MAMBO NDIO YATAKUWA WORSE ZAIDI, TUMEGUNDUA DHAHABU WAJANJA WAMETUPIGA BAO MAFUTA WATATUKAMUA ZAIDI. NAOMBA WASIONE MAFUTA KABISA WAKUTANE NA MAJI TU.

    ReplyDelete
  17. kwanini hujaongelea la kuondoa show room za magari mtaani. ni vema showroom wapelekwe sehemu moja na Bank wawekeeni huko mjini watuache tujenge nyumba za kuishi

    ReplyDelete
  18. DR COMFUSION I SALUTE. NAFIKIRI HIYO SYMPOSIUM(MAJDALA YAKINIFU) UFANYIKE KWENYE BLONGU HII TUKUFU

    "I think that we should organise a symposium for discussion critically the way forward, aspiration, desire for our nation with our individual commitment which should trigger to team work spirit. So Discussant should come with his/her view thereafter, the conclusive remarks will bring us to affirmation."

    ReplyDelete
  19. Sisi inasema hii yote ni kiswahili mulefu hakuna action. Watu kwisaondokana na mineno mingi. Hii Tanzania President haiko serious kila siku nasunguluka dunia.

    ReplyDelete
  20. Hili swala la viongozi kuchagua jambo, ni muhimu sana. Wenzetu waliangalia mbali sana. Mfano kunabaadhi ya serikali haziruhusu ndugu kuwa ktk baraza la mawaziri sababu tu wanawezaleta maswala ya kifamilia ktk baraza hilo

    ReplyDelete
  21. Hii kwa kweli inavutia sana kwa sisi watanzania. NAdhani wengi sana tuko myopic ndo maana tunavutwavutwa tu.

    Tuanze na huyu annonn Feb 1 1:41yuko UK. Wewe annon na mabox yako unadhani kwamba bei ya vitu inapanda kwa mafuta tu? Kuna sababu nyingi sana zinaweza sababisha bei kupanda. Katkka mwaka mmoja nimesafiri nchi 16 Duniani, tano za Africa. Zote hizo hakuna nilikoona bei ya vitu imepanda kwa sababu ya mafuta. Kuna factors nyingi sana. In Fact kule Hongkong na Malysia, nauli imeporomoka zaidi. Sasa hawa wananunua mafuta wapi, au unataka kusema wanayo yao?! Pale pale Saudia, kodi haishikiki mwaka mmoja huu. Wao ni moja ya watoa mafuta wakubwa Duniani. Fikiria.

    Dr. Confusion uko confused zaidi. Nakuonea huruma. Sasa wewe unasema baada ya september 11 insurance zilipanda sana kwa mashirika ya ndege, hapo bongo kuna shirika gani hasa ambalo linaweza kuleta effects kwa watumiaji (ambazo sijui ni wangapi) kwa ujumla? Auguments zako zina work kwa nchi kama SA, Nigeria labda na Egypt lakini si kwa bongo. Hatuna direct interacion na US kiasi cha kwamba recession yao ituathiri sisi!

    KUna annon Feb 1:34 unaanza kwa kusema huna ujuzi na uchumi. Hiyo ilitaka kunikatisha tamaa kusoma gazeti lako, lakini nikajitahidi. Kwa kifupi ni kweli uchumi uujui kabisa ulitaka kuandika tu. Suala la Kikete kuwa-consult wachumi wake ni kweli. Lakini unafahamu kuwa huyo huyo KIkwete aliwa-consult wataalamu kuhusu Richmond? Pia akaingizwa mjini na watalaamu hao hao pale airport siku mahujaji walipotaka kuondoka kwenda Macca? Sijui kama unafutilia haya mambo. Nimekushangaa comments zako hazina kichwa wala tumbo!.

    Hata hivyo kama ulivysoma, huna idea zozote za uchumi. Inawezekana huna ideas zozote zile. Ulitaka kuandika tu.

    Tuwe makini wabongo. Tunadike kwa data na ufahamu. Hii blog tunasoma wengi sana, wanaoelewa na wasiolewa haraka. Dr. Confusion na wenzake mambo yao ni ku-confuse watu. Mki-confuse nyie wenyewe msihamishie kwa wengine!

    ReplyDelete
  22. Ninachoona mimi ni kuwa hotuba za maraisi za mzee Ben wa ANBEM na huyu tuliyenaye, hazina tofauti. haziongeleagi issue iliyopo kwenye jamii. kukiwa na issue ya kuua raia
    kwa kuwahisi kuwa ni majambawazi, raisi anazungumzia korosho. kukiwa na issue ya kwa nini Balali harudishwi nchini, raisi anazungumzia ujio wa Bushi basi ilimradi ni Blah Blah tu....

    ReplyDelete
  23. Anon Saturday, February 2, 2008 1:57:00 AM EAT, Mtoa Maoni:
    I don’t want to bring a debate over the issues, but I am much confused to see even some of people are not aware that, globalisation is the powerful configuration in world economy, there is one scholar asserts that Globalisation is not optional.We should develop the no-nonsense thinking. In light of few comments:
    The world economy is operating under matrix structure; I think we remember on David Ricardo theory: the principle of “comparative advantage” that explains how trade is beneficial for all parties involved, thereafter developed by famous Scottish economist, Adam Smith principle of “absolute advantage” he argues how a country can benefit from trade if the country has the lowest absolute cost of production in a good.

    Guys, Tanzania is now depending highly from Asia products and Dubai, U.K and other part of world. Are you ready to be confused!!. Thus, if any of the mentioned country has been got mild effect, definitely Tanzania will have the indirectly effect as it trades with those countries. Coming to the regional integration, Kenya is one country which is believed that has received an impact from recession, so how about the common market and other multilateral agreement within East Africa Community. Get a confuse.

    Kuhusina na suala la Bima ya ndege, nataka kukwambia hivi, tumia akili ndogo tu ya kuchanganya nakuchanganyikiwa utagundua kwamba Serikali ya Tanzani ilikuwa na ATC amabyo inapata kisai kikubwa cha ruzuku toka serikalini, kitengo cha Ndege za Serikali, Helicopter za Polisi, Madini zote hizo zinalipiwa bima, Fedha zilitokana na Public finace which is accented by president under the appropriation act, sasa kama fedha hizo zinakula na kupunguza allocation ya social budget, kama hospitali,mashule utaniambiaje kwamba Septembe 11 haijamgusa mtanzania wa kawaida, Je katika watanzania milioni 35 ni wangapi wanategemea madawa na shule za Jamii.Kwa nini asiguswe na fedha zinazopunguzwa kumeet hizo cost.There is BIG PICTURE, and focus to narrow view. You have got shortcoming in detail analysis, ha ha ha ha ha!!

    If you need more confusion tries to revise your knowledge on Medium Term Expenditure framework (MTEF), a budgeting model that has been triggered by WB.


    For the benefit of all: I sometimes part with the junior here,I dont want to mention, he has got focus thinking keep it up!! Let confuse those who are not willing to open up their minds.

    Dr.Confusion.

    ReplyDelete
  24. Mr. Confusin you seem to be totally confused and unware of the situation in Tanzania. I want to clarify some issue which you seem not to understand. One of the annon above have given you a true picture of Tanzania. I am surprised taht you still argues that Tanzania Government is heavily finaning ATC on Insurance. Dont forget that ATC during Sept 11 was under SAA. Kwa sasa ATC inajilipia yenyewe.

    idadi ya abiria na watumiaji wa ndege kwa bongo huwezi fananisha na US. Jamaa kasema wazi kabisa. Sijui kama umemuelewa kweli.

    Wewe kweli ni confused Dr. Pole sana kwa confusion

    ReplyDelete
  25. Dr. Confusion you appear much confused as you have always been. Always very condused! I am sorry for you.

    Most of the economic theories you have mentioned above do not operate in Africa. Every theory has to have a starting point. We mis a starting point in Africa.

    Therefore you should always not jump into European or American theory and try to plug into Africa! You dont need glass to see this. We have not moved where we are because we try yo apply those non-starter theories!

    I am sure you will remain permanently confused if you dont orient you thinging in the other direction.

    ReplyDelete
  26. It seems like JK twist many Tanzanians from that speech which had full of propaganda. I understand we are in globalization era, that things that affect US today have indirect effect in Tanzania economy. Ninachosema mimi ni kwamba mortgage crisis in US haina effect yoyote na growth of Tanzania GDP au GNP. Najua kwa past few month uchumi wa US umekuwa slow, lakini hii haijaleta implications kubwa kwa nchi ambazo hazijawekeza katika nchi hii. Kushuka kwa dollar kunaadhiri sana Saudi's and China sababu they own a big part of US debt. Lakini how about Tanzania?

    Tanzania is not industrial country, it doesnt export many goods. Tanzania it import everything from Asia and middle east. So, kuyumba kwa uchumi wa Asia kutakuwa na implication kubwa zaidi ya kuyumba kwa US economy. For those who knows economics 101, mtafahamu ya kwamba country GNP inadeal na production with in the country na viwanga vya hiyo nchi abroad, so what is the figure of GNP this month compare to Last month? So, kabla muheshimiwa haja develop arguments just give us the figure, usije kusema uchumi umeslow because of rising of gas price in world market, while Tanzania relie on cormercial uses of gas and not industrial uses. People we need to wake up.
    Mdau wa US

    ReplyDelete
  27. Ndugu waeshimiwa habari za uzushi zinatokana na kubania habari kwa wakubwa.
    Suala la kutangaza utalii sio la Bush ni la mabalozi wetu kama hawawezi warudishe home. Wapelekewe vipeperushi na ktk sehemu ya mapokezi wekeni tv zinazoonyesha mbuga zetu na mt kilimanjaro. Kenya airways wanatangaza mt kilimanjaro sasa ni wao na nimeliona hilikwa yeyote anaesafiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...