Bwana Michuzi,
Mimi ni mdau wa hapa US, Ningependa kuingiza hoja binafsi kuhusu uchaguzi wa rais wa Marekani, ambao uko kwenye hatua za awali za kupata wagombea.
Kinyang'anyiro hicho kimeanza leo katika jimbo la Iowa ambalo huchukuliwa kama jimbo muhimu katika historia ya uchaguzi hapa Marekani kwa sababu anayeshinda katika uchaguzi huo huwa katika msimamo mzuri zaidi wa kushinda majimbo mengine, kwani inamuongezea confidence hali kadhalika media attention. Nikitoa utambulisho huo, Seneta Barack Obama, mgombea kwa upande wa chama cha Democrat ameshinda jimboni humo dhidi ya wapinzani wake wa karibu John Edwards na Hillary Clinton.
Ushindi huu ni wa kihistoria ukizingatia kwamba Iowa ni jimbo lenye wazungu wengi kuliko weusi, kitu ambacho kimeishangaza dunia kwani Obama ni mchanganyiko wa Mkenya na Mmarekani...hivyo huchukuliwa kama mweusi.


Lengo langu kuleta picha hii ya hatua za awali za uchaguzi wa urais hapa US ni kufungua mjadala na kukaribisha inputs za watu katika uchaguzi huu, na dunia ijue.


Mdau Jacob

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Kaka Jacob mambo ni mazuri,kwani Historia inataka kuweka Uthibiti kwamba Ipo siku mtu mweusi atakuja kuwa Rais wa Nchi hii kubwa Duniani.Sote Tunasherehekea Ushindi Mkubwa wa Obama huko Des Moines (Iowa),Lakini ukweli wa mambo ni kwamba safari bado ni ndefu mno.Na bado inaonekana Mama Clinton ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa na GOP itakayokutana huko Denver June/2008.Wale Wabantu wenye Uraia wa USA.Tumpigie kura Mkuu Obama ikiwa atachaguliwa na GOP.

    ReplyDelete
  2. Mimi nimeangalia huo ushindani wote kwa makini sana. Obama hata akipata kura nzuri za maoni hatapita hata kidogo katika kinyang'anyio cha urais. Sababu ni kwamba mabali ya kuwa mweusi anakasoro moja nayo ni kupendwa na wanyonge na wala si matajiri ukiachia mbali Oprah. Bado hajasema lolote kuhusi Matajiri wa nchi hii ambao wana uwezo wa kuamua nani awe kiongozi. Kumbuka kwamba Marekani ni nchi ya Kibepari wala socialist country. unyonyaji ni sela ya Marekani na watu kuwa matajiri ni fahari ya nchi wala si socialism. Ndiyo tatizo kubwa sana la Obama. Kosa kubwa alipo sema kwamba ataya 'tax' sana makampuni yanayo export jobs hii ime weka macho ya mabepali kuwa makubwa sana kumwangalia Obama kwa jina la Mchawi. Obama hata shinda urais Ng'o.

    ReplyDelete
  3. Waafrika bwana, tunakosa kujadili namna ya kuisaidia Africa yetu, tunaijadili America. Kenya jirani zetu wanaungua hapo watu hapo mnaleta mjadala wa Obama. Akishinda akishindwa ni USA its non of our business! Lets concetrate on what we can do for our Tanzania and Africa.

    ReplyDelete
  4. Iowa caucas haina historia kubwa sana, imeanza miaka ya kati kati ya 1970. Washindi wa caucas asilimia 50% wameweza kuwa wawikilishi wa uraisi kwa vyama vyao, na asilimia 50% nyingine hawakuweza kushinda. Tazama mtu kama Bill Clicton, yeye alishika namba tatu pale Iowa, then akapoteza pale New Hamshire, na akaenda kupata ushindi wa kwanza pale Georgia, then mbio zikaanzia pale.

    It is not over yet, na hii sio victory kwa Obama, bali ni momentum ya yeye kwenda kufanya vizuri New Hamshire, North Carolina na Nevada soon this january. Obama anapesa za kumfanya afanye state campain, vile vile amedhihirisha kwamba the battle is just beggining.Lakini usimunder estimate mama Clinton, huyu mama anapesa ya kutosjha kufanya kampeni usiku na mchana.

    Republican side is a mess, Rommeny anamillions of dollar lakini amechapwa vibaya na Mick Huckabee, then more to come New Hamshire sababu Mc Cain analead kwenye polls, inatisha kwa Mitt.

    American Politics, I love it. Just imagine mtoto wa masikini kabisa baba Mkenya mama Kutoka Mashambani Kansas huko lakini ameweza kusearch for American Dream, Kuanzia degree yake pale NY, then kwenda pale Havard school of Law, then kwenda Chicago, then kuingia kwenye senetor two years ago na sasa kuwa mgombaniaji wa kinyang'anyiro ya urais USA kupitia democratic. This is only in America where people who are working hard does not get back pet, but they get reward. I love this country. As Obama said " It's only in America where hard work is rewarded". That is true

    ReplyDelete
  5. Anayeuliza na kuhisi kama kushinda kwa Obama leo hapa IOWA ni dili huyo mtu sio tu hajui siasa za USA bali pia hamjui Obama na nguvu zake kisiasa
    Pia labda haijakaa vizuri kaka Michu,hiyo deal kushindwa kwa Obama kwenye nomination hizi ni deal zipi hasa?
    Obama ni mmoja wa wana siasa wenye mvuto sana kwa karne hii kupata kutokea nchini USA,Alijiingiza kwenye siasa miaka 12 iliyopita akigombea na kushinda mfululizo kama seneta wa jimbo la Illinos,na baadae mwaka 2004 kwa vehemently majority akashinda kuwa US seneta akiwakilisha Illinos,huku akimgaraza vibaya sana Republican kwa zaidi ya asilimia 81 za kura zote na kuwa seneta wa kwanza kuingia kwenye US congress kwa kura nyingi kwa zaidi ya miaka 140 toka babu Lincoln Abraham alipomshinda vibaya Stephen Douglass kwenye uchaguzi wa upande mmoja mwaka 1856
    Obama,msomi aliyesoma kwenye shule za kutukuka huku akihitimu vyema elimu yake ya sheria sio mtu mbabaishaji na alijidhirisha hivyo alivyokataa mapema sana mpango wa Rais Bush wa kuivamia Iraq,tukio hili ni mtaji wake mkubwa sana wa kisiasa kwa sasa
    Kumbwaga mtu kama Mama Clinton aliyesaidiwa sana na mmeo wake Bill sio jambo la dili,ni ushupavu mkubwa sana wa kisiasa
    Jana Obama kaishangaza dunia,kashinda kwa asilimia zaidi ya 36 ili hali alitabiriwa atashinda kwa asilimia 32 tu,kumbwaga kingunge kama Edward na heavy spending yake ile sio kitu kidogo
    Obama akishinda,natabiri atakuwa Rais wa kwanza minority kupata kutokea USA,Na kama eti atashindwa na Huckabee"huck"au Roomney wa Republicans kwa sababu tu eti Obama ni mweusi ni mawazo mgando na yamedhihirika jana kama hayana msingi wowote
    Je kuna jimbo lina watu wabaguzi wa rangi na conservatives zaidi ya IOWA na New Hamphire ambako Obama anaongoza kwa kura halisi na kura za maoni??
    Obama for America,Obama not only for blacks,Obama for All,Might Sir God bless him

    ReplyDelete
  6. Usisahau kuwa ni maraisi wawili tu waliowahi kushinda kwenye Caucases na kuendeleza libeneke kwenye uchaguzi mkuu,mmoja ni huyu Joji Kichaka,mwingine homework kwako.
    Inapendeza Obama kushinda lakini kushinda urais,piga ua.White America isn't ready yet for a Black president.Na ukifuatilia kwa karibu matokeo ya Iowa,utagundua furaha ya Republicans kuona Obama amepata atokeo mazuri kuliko Hillary kwa vile wanafahamu kuwa ni rahisi kwao kumbomoa Obama iwapo atapitishwa kuwa mgombea wa Democrats,kuliko kumshinda Hillary.
    Only Democrat anayeweza kupambana na mbinu chafu za Republicans (backed by corporate America) ni Hillary.UKIONA ADUI YAKO ANASHEREHEKEA USHINDI WAKO BASI UJUE ANA MANUFAA NAO.

    ReplyDelete
  7. Kampeni na Spichi yake ilikuwa kali sana na ya mvuto. Anafaa sana kuwa rais wa US lakini ukweli ni kwamba nijuavyo dakika za mwisho Wamarekani (wa Democrats) watamtanguliza mke wa Clinton. Inauma sana lakini ndivyo itakavyokuwa na sababu yake itaelezwa na wengine wanaoniunga katika hili.
    Matokeo ya IOWA ni ya muhimu lakini huwa hayamaliziki hivyo hivyo kila wakati soma historia ya uchaguzi wa US uone.

    Mkata issue

    ReplyDelete
  8. not all blacks are my friends;not all whites are my enemies .Take that into cosideration.

    ReplyDelete
  9. Hilo jimbo lina wapiga kura ambao ni wachache mno katika majimbo ya Marekani wenyewe wanaita single digit percent of voters ambazo ukweli wa mambo hazikuwezeshi kushinda uraisi wa Marekani.

    Hivyo kama ulivyosema ni kweli linawapa confidence hasa wagombea wapya kuendelea kupoteza pesa zao kwenye kampeni mbele kwa mbele kwenye majimbo mengine baada ya kujiona kama na wao wamo vilevile!

    Obama si tajiri ukilinganisha na wagombea wengine waliopo na wale waliowahi kutangulia kabla yake wawe wazungu au wafrika,hivyo nafasi yake ya kushinda ni finyu mno.

    Iowa si jimbo la matajiri hata kidogo kwa tafsiri za Marekani ni moja ya majimbo malofalofa marekani.Kuna Majimbo ya matajiri atakayoenda atakiona kilichomnyoa kanga na atajua kugombea uraisi ukiwa lofa marekani ni hasara juu ya hasara unapoteza hata kile kidogo ulichonacho.

    Akishindwa uraisi ajiandae kupoteza na ugavana kwenye uchaguzi wa jimbo lake kama akithubutu kugombea.

    Marekani wachague Raisi mweusi au chotara ni ndoto za mchana.Watu weusi endeleeni kumwaga pesa zenu barabarani kwenye Kampeni za Obama watu wazile halafu wawaache mnalia bila Kupata Raisi mweusi na hela imekwenda!

    ReplyDelete
  10. who cares?, kwa nini usilete hoja zinazohusu nchi yako au jirani zako wa Kenya?hata kama una greencard, USA siyo nchi yako, and waachie wenyewe wajadili nchi yao.

    ReplyDelete
  11. Sasa Kibaki si aachie tu madaraka??

    Unajua hata akiendelea kung'ang'ania haitakua na nguvu kwan hana wabunge wengi.

    Kila atakachokieongea watakipinga, kuna tetesi kua eti Kibaki anaandaa Njama za kuvipiga viberiti vile vituo ambavyo ODM walipata kura nyingi,
    Hii ni katika kupoteza ushahidi ili hata wakirudua kuhesabu ionekane ameshinda,

    Hizi ni tetesi tu jamani

    ReplyDelete
  12. MNAOSEMA HII HOJA HAITUHUSU MNAONYESHA UFINYU WA MAWAZO. KUSHINDA KWA OBAMA KUNAONESHA WAMAREKANI KUTAKA MABADILIKO, INAONESHA KWAMBA HAWARIDHIKI NA HALI ILIYOPO SASA MAREKANI AMBAPO: MASKINI WANALIPA KODI ZAIDI KULIKO MATAJIRI, WAMAREKANI MILLION 47 LEO HII WAKIUMWA HAWAJUI MATIBABU WATAPATA WAPI, NCHI INATUMIA MABILLION KWA VITA YA IRAQ ISIYO HALALI ILHALI WAMAREKANI WENGI TU WANASOMA SHULE KAMA NGUMBARU, N.K, N.K.

    NI SABABU KAMA HIZO HIZO ZINAWAFANYA WAKENYA WALIO WENGI KUTAKA MABADILIKO KWAO, KUKATAA STATUS QUO, UCHUMI UNAKUWA 6% LAKINI ASILIMIA 50 BADO WANAISHI KWENYE UNASKINI WA KUPINDUKIA, MATABAKA YANAZIDI NA UFISADI NDIO KWANZA UNAONGEZEKA, KIBERA NA MATHARE WANAISHI KAMA WANYAMA!

    NI SABABU HIZOHIZO KWETU TANZANIA LAZIMA TUWE MACHO: LEO HII VIONGOZI WETU WENGI WAMEBATIZWA, WANAITWA "MAFISADI", UCHUMI UNAKUWA, LAKINI MALALAMIKO YA UGUMU WA MAISHA YANAONGEZEKA, MAJI, UMEME, AFYA, ELIMU MATATIZO. WIZI UNAZIDI: RADA, RICHMOND, IPTL,BOT, MIKATABA YA AJABU....YOU CAN GO ON FOREVER!

    KWA HIYO MUAMKO HUU WA BINADAMU KUTAKA KUISHI KAMA BINADAMU UPO SI BONGO PEKE YAKE, NI MPAKA KENYA, CHINA, USA NA KWINGINEKO DUNIANI. NDIO MAANA WATU KAMA OBAMA WANAOONEKANA KUJALI HALI ZA WANYONGE WANATOKEA KUWA MAARUFU. KAMA ATASHINDA AU HAPANA HILO NI JAMBO JINGINE REFU NA TOFAUTI KABISA.

    ReplyDelete
  13. Tunaacha kujadili hali ya Kenya tuko busy na Obama! Hii ni serious!

    ReplyDelete
  14. wewe anonymous 2:50:00 una akili finyu kidogo kwa taarifa yako marekani ni nchi ya wahamiaji na kila mtu anaweza kua mmarekani aijilishi kitu ni nchi ya kila mtu hata kama ni weupe ndio wengi na ndio wananafasi ya kupata uraia zaidi.che muhimu kuhusu uraisi wa marekani ni muhimu kushikwa na mtu mwingine na inajalisha sana hata kwa maendeleo ya afrika hata hapa uluya maeuropean yana interest zao na raisi wa marekani kwa sababu ya maslahi yao,na kama marekani itapata raisi anaejali africa na akakemea unyinyaji wa aina yeyote na hapo ndio itakua njia ya waafrika kunyanyuka.huyu rais wa taifa hilo ni muhimu kwa watu wote duniani,viongozi wetu wa africa tunajua wanavyofanya kazi kwa mawazo ya mgando kutegemea mambo ya maraisi wa uluya,mkapa kikwete nimeudhuria vikao vyao mkiwauliza maswali kuhusu maendeleo watakujibu wakubwa hawajaaamua na wakubwa wamegoma kwa hio lazima ujue huyo raisi wa marekani haitumikii marekani tu dunia nzima inamwaaangalia,kwa hio mtoa mada ana hoja.aksante

    ReplyDelete
  15. Obama nayeye si mkenya na nyie tena ndugu yake raila huoni kuwa inapendeza wajaluo wawili kugombea urais mmoja Afrika kwingine America? kwanza itakuwa jambo la fahari sana mwafrika kuongoza america ingawa mambo yanaweza kumtokea kama yalivyo mtokea Mbowe wakati wa uchaguzi. wamarekani weue hawawezi kukubali kuongozwa na mwafrika tena anayejulikana kwao ni wapi kiulaini bila kuchambua historia yake ya DNA

    ReplyDelete
  16. "The Audacity of Hope"...Tusubiri New Hampshire in a few days.

    ReplyDelete
  17. I don't want to entertain the shortsighted contributors of this issue. Ati unasema tusiongelee siasa za Marekani kwa sababu ya Kenya? hujui kwamba siasa za Marekani zinaihusu dunia nzima? hujui nchi hii chini ya utawala wa rais Bush ndiyo imekuwa ya kwanza kama siyo pekee kuridhia matokeo haramu ya uchaguzi wa Kenya? au unafikiri hili halina impact? no..kama USA sasa hivi ingekuwa na kiongozi ambaye hajali maslahi yake na kuweka demokrasia mbele haya yanayotokea Kenya katu tusingeyasikia. Au je umesikia lolote kutoka kwa wakubwa hawa juu ya hali ya Kenya hivi sasa?, kama si kusububiri hali itulie kidogo na kumtia moyo Kibaki aendeleze sera zao?
    If Kenyans chose to commit suicide, that doesn't stop the moderation of other issues. Obama's victory in this 95% white people state is a deliberate sign that Americans are ready for a change!
    Hillary is good yes! don't talk about Edwards, coz running mate would deem fit for him, but Obama has proven some Dr. King's elements, a person whose dream dominates the USA to date.
    Obama can do it against Hillary, And he can do it against GOP...no doubt.
    Hatutaacha kujadili siasa za Marekani kwa sababu zinaihusu hata nchi yetu ya Tanzania, huku tukiwakumbusha wakenya kuhusu demokrasia na kuachana na dhana ya ukabila!
    Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki America!

    ReplyDelete
  18. Namnukuu marehemu mwalimu "PALE PENYE UTAJIRI WA KUNUKIA PANA UMASKINI WA KUNUKA" wangapi wanakumbukuka kauli hiyo

    ReplyDelete
  19. Anons wote mnaotia mashaka kuhusu uwezo na nafasi ya Obama kuwa Raisi wa Marekani naona ni watu msiojiamini kabisa.

    Kuweni ambitious nyie watu, la sivyo mtabaki kusindikiza tu kila siku.

    Mimi ninaamini Obama anaweza. na kura yangu nitampa

    ReplyDelete
  20. HE WILL NEVER GET THE MOST POWERFUL JOB ON THE EARTH.THE NAME OBAMA SOUNDS LIKE OSAMA TO MOST WHITE AMERICANS.THEY ARE NOT READY FOR THE BLACK FORKS AS WELL.BUT WE DESPARATELY NEED HIM TO TACKLE FISAIDISM(UFISADI)HAPA BONGO.IT WON'T BE PROBLEM FOR HIM TO GET WORK PERMIT WITH INVESTOR STATUS.

    ReplyDelete
  21. Michuzi, naomba uuhifadhi huu mdahalo, halafu u-ubandike tena next year this time wakati Wamarekani wanaapisha Rais wao. Halafu tuone who will be back and who will run away.





    --I support Barack and Michelle Obama----

    ReplyDelete
  22. In America, Rais wa nchi hiyo huwa regarded as a world leader. And what I know so far, American president must be suitable to parts with interests (Capitalists) I am sorry to say that, my Brother Obama is not yet to impress the Caps.
    But he is taking a good try though. Big up for Him.

    Katty.
    Wilmington, DE.

    ReplyDelete
  23. "Man gives a award and God gives a Reward"-by DW.
    Americans are ready4 a change, 'n May God bless them.

    ReplyDelete
  24. Mdau hapo juu anon Jan 4, 11:21, Ningependa kukuelimisha kuwa GOP ni jina la the Republican Party na sio wao watakaomchagua Hillary au Obama. Hawa watachujwa kwenye Chama cha Ma Democrat. Twamtakia kila la kheri Bwana Barack Obama.

    ReplyDelete
  25. Democrats stand for everything that Tanzanians are against..
    -Gay Unions
    -Social programs
    -Racism..Clinton is in the news for making stupid remarks on thursday
    Democrats can not defend their own, they cave to the radical facist Islams.
    -capitalism works and gives everybody a chance to advance (Ask dictactor Nyerere)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...