HABARI TOKA DODOMA SASA HIVI ZINASEMA KUWA SPIKA WA BUNGE MH. SAMWEL SITTA AMETANGAZA KWAMBA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AMEAMUA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU.
MH. SPIKA BAADA YA KUTANGAZA HILO AMESEMA MJADALA WA RIPOTI YA RICHMOND, NA SIO MJADALA WA LOWASSA, NDIO UENDELEE. NA NDICHO KINACHOFANYIKA HIVI SASA HUKO BUNGENI.
HABARI ZAIDI ZINASEMA KWAMBA MH. LOWASSA AMESEMA KWAMBA INGAWA HAJAMTAARIFU JK UAMUZI WAKE HUO, AMEAMUA KUJIWEKA KANDO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 101 mpaka sasa

  1. Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaat!!!! Is this for real? OMG! what is going on there?

    ReplyDelete
  2. Asante kwa kaka Edo kuonesha initiatiave. Na wengine wafuate nyayo, Nazir, Ibra, Arthur na wengineo wote waliotajwa.
    Pia warudishe hela zetu. Tuna machungu sana.

    Michuzi big up kwa kutupa "livescores". Nakukubali sana kaka.

    Bado ripoti ya BOT- EPA na madini kina Zitto.


    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. HUREEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE! Mungu wangu nchi yako tunakufa maskini kwanini?!! Jamani, hata aibu alikuwa hana!

    ReplyDelete
  4. Nilishangaa! Alikuwa anasubiri nini toka jana?! Ni ajabu sana kwa kweli. Wengine wa chini wana hali mbaya sana. Kikwete kweli ni kiboko!

    ReplyDelete
  5. Sio sababu,

    Wala Hajakwepa bado,

    Tutakutana nae huko huko mitaan na mahakamani

    ReplyDelete
  6. Hureeeeee, uamuzi wa busara sana huo Mr. Edo, kama inawezekana jiuzulu na ubunge tu

    ReplyDelete
  7. imekaa vizuri hiyo, hawa watu walishatakiwa kuachia ngazi sio leo. na hao akina Karamagi na Msabaha wanangoja nini mpaka sasa hivi? waondoke haraka sana na baada ya hapo tunachosubiri ni kuona wanapelekwa mbali zaidi ya hapo. watu tunateseka kila kukicha kwa sababu zao hawa fisadizi. naona kaamua kumpunguzia kazi JK, au anatuyeyusha tu inawezekana kamwambia japo sio kwa maandishi maana ni mshikaji wake. Aluta continua, wadumu akina Slaa wanaojua kuibua mambo bila woga

    ReplyDelete
  8. I tell you this is more than GOOD NEWS na bado ni lini tuanze kumfilisi. kikwete should know that the man was a spoiler.Congrats to Dr. Mwakiembe and the Team

    ReplyDelete
  9. Haya ndio tulioyategemea haya safari njema wasalimie Kighoma.

    ReplyDelete
  10. Eheee mambo yamekuwa mambo... Kujiululu kwa Lowassa hakutoshi...bado wengine wengi wanatakiwa kufanya hivyo na vile vile wanatakiwa wafidie gharama tunazoingia watanzania kwa kuingia mikataba feki..

    ReplyDelete
  11. Kweli Lowasa amefanya uamuzi wa busara.
    Ninachumshauri Mwakyembe akihadhari na lolote lile litakalotia doa umaarufu wake. Ninakumbuka suala la Prof.S.Mbilinyi (alikuwa waziri wa fedha) lilivaliwa njuga na Mh. Iddi Simba, baadaye Mh. Iddi Simba naye akavaliwa njuga na akina Mzindakaya naye akajiuzulu.
    Bila kusahau hadithi niliyoisoma nilipokuwa mdogo ya: "Mtego wa Panya huingia waliomo na wasiokuwamo" kutoka kitabu cha hekaya za Abunuasi.
    Mungu ibariki Tanzania na watu wake

    ReplyDelete
  12. Ni uamuzi wa msingi kwa heshima yake binafsi, ya mwenza wake JK na CCM kwa ujumla.Bado, wengine.

    ReplyDelete
  13. kachukua uamuzi wa busara mie sikuona namna yeyote ambayo angeendelea kuwa hapo alipo kutokana na kashfa hiyo tena ilitakiwa jana hiyo hiyo ajiuzuru na wengina nao wote wawajibike kama yeye.

    hata kiwira waliohusika nao wachukuliwe hatua na hata hawa wa uungo gesi wanaolipwa pesa ya bule wachukuliwe hatua huwezi klipwa bila kudeliver mambo ya kihuni bayo

    ReplyDelete
  14. Ebwana eeh!Michuzi unatisha,you r just so current.
    Siwezi kusema natoa pongezi kwa Mh. kuamua kujiuzulu..No way..he already has accumulated lots of wealth for himself and the entire family..wacha akapumzike after all he has never been that much of a mchapa kazi.

    Shemejio M.M

    ReplyDelete
  15. nakasikia ka wimbo ka AKUDO kwa mbaaali"ukisikia nimejiuzulu usifanye msiba ila sheherekea kwasababu nina roho mmbaya"...Oops nimekosea wimbo!!!!

    ReplyDelete
  16. boys 2men imesambaratika.Kwa kweli mlitufanya wajinga umeme tulipie bei kubwa kwa ulafi wenu hizo pesa nani kakwambia utakufa nazo? Na washikaji wako waombe msaada ktk tuta kama wewe.

    ReplyDelete
  17. Ngoja niwe wa kwanza kuchangia!!
    Michu nimemsikiliza vizuri sana EL wakati wa hoja yake ya kujiuzulu! Nimeamini Tanzania kweli hatutaweza kupambana na rushwa, jamaa anagoma kwamba ahusiki! Anadai kwamba amesingiziwa! Hivi ni kweli? Mbona kila kitu kilikuwa wazi? Kamati ile ilifanya kazi yake bila upendeleo na yeye anadai kwamba wanamwone wivu na uwaziri mkuu wake!!!!!

    ReplyDelete
  18. kwa nini mjadala kuhusu Lowasa usiwepo? Kwani Richmond ilijirich yenyewe?
    mbona mjadala ulikuwa juu ya kuunda tume kuhusu Buzwagu ukageuka na kumuhusisha aliyeleta hoja mpaka akasimamishwa?
    Kama mimi ni mbuge nisingekubali kirahisi ningependa rohasa aseme yeye anavyohusika au kutohusika tusikie to kinya chake.

    Pili hili si tu suala la kustep down ni mtuhumiwa kuanzia sasa hivyo afikishwe mahakamani.

    JK ana kazi sana pole kini ndio ukuu kwa hili utajijengea heshima.

    ReplyDelete
  19. Hii ni habari njema kwangu!

    ReplyDelete
  20. SASA NIMEKUMBUKA HAYATI BABA WA TAIFA KUWA KAMA UNAMPENDA MTU NENDA KANYWE NAE CHAI KWENU.
    KWA USHAURI MH.RAIS HILO BARAZA LAKO WENGI NI WABABAISHAJI ONDOA. KIDONDA CHENYE USAHA LAZIMA NZI AKIFUATE.

    ReplyDelete
  21. Napenda kutumia fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Edward Lowassa (Mb) kwa uamuzi mgumu na wa ujasiri aliouchukua wa kujiuzuru wadhifa mkubwa aliokuwanao. Ni jambo la nadra sana kwa viongozi wa bara letu kufikia uamuzi wa jinsi hii. Nasema hivyo kwa sababu pamoja na kuwa ripoti ya kamati ya Dr Mwakyembe haikuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuhusika kwa Mh Lowassa katika kuibeba kampuni ya Richmond bali ushahidi wa kimazingira tu, bado Mh Lowassa ameamua kujiuzuru ili kutoa nafasi kwa Mh Rais kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi.

    Tutaukosa sana uzoefu na uongozi wa kijasiri alionao Mh Lowassa. Hata hivyo Mh Rais kwa uzoefu wake na kwa jinsi anavyoufahamu utendaji kazi wa kiadilifu wa Mh Lowassa, pengine akamrejesha katika serikali yake.

    Ni hayo tu kwa sasa

    ReplyDelete
  22. Mmmmmm! mimi chimo kabicha

    ReplyDelete
  23. Mungu ibariki TANZANIA na watu wake

    ReplyDelete
  24. aaa..sipati picha katuni ya kesho ya KP...

    Ene wei..Safari moja uhanzisha nyingine.

    Ni matumaini yangu mawaziri wengine wiki hii watafuata nyayo za Edo.

    Ene wei,Tutafika tu

    ReplyDelete
  25. HILO HALIKWEPEKI NAOMBA WADAU MNISOMESHE.BADO TUNAWEZAJE KUCHUKIUA HATUA ILI KIRANJA HUYO APATE STAHILI YAKE?MDAU UK

    ReplyDelete
  26. Amelazimishwa kujiuzuru. Ngoma ilikuwa ngumu kwake. Kama anavyosakamwa Balali kwamba arudishe mali zetu, Lowasa naye arudishe. Hatuwezi kupandishiwa bei ya umeme wakati wachache wanaitafuna Tanesco.

    ReplyDelete
  27. huyu mjamaa lazima ajiuzulu kwani ripoti imesha sema wizara yake imehusika sana,sasa hakuna mjadala tena we umeme unapanda bei kama vile hatuwezi kutumia vibatali bwana,na wengine lazima wafuate tu hakuna kuoneana haibu sasaivi,na bora walikua wamerekani nasasa wapopo wakijua tu kuna mazoba bongo lazima watakuja na ya kwao.....

    ReplyDelete
  28. MICHUZI NAOMBA NISHAHIHISHE USEMI WAKO, TENA KWA HERUFI KUBWA KABISA. HAJASEMA KWAMBA HAJAMTAARIFU RAIS, KASEMA KAMWANDIKIA BARUA RAIS YA KUJIUZULU, NA BADO HAJAPATA MAJIBU. SASA KAMA BARUA IMEANDIKWA LEO ASUBUHI KABLA YA KWENDA BUNGENI, UNATAGEMEA MAJIBU YA RAIS YAWE YA HARAKA KIASI HICHO.

    KWA KIFUPI JAMAA KAJIUZULU....TUNAMSHUKURU SANA KWA KUTUIBIA PESA ZETU. UBAYA UNALIPWA HAPA HAPA DUNIANI. MAMBO YA MBINGUNI NI MENGINE.

    ReplyDelete
  29. Du Hatimaye tembo kaanguka. Naipongeza tena kamati teule kwa kuweza kuweka mambo hadharani mapka kisiki kikang'ooka. BIG UP Mwakyembe and your Team. Kwani huyo jamaa kujiuzulu ni nini? Aende zake tumechoka, tuna majiko ya umeme tumogopa hata kutumia kumbe yeye ndiyo mpandishaji umeme

    ReplyDelete
  30. GOOD RIDDANCE!! ANNA MAKINDA FOR NEW PM.

    ReplyDelete
  31. Akafie mbele, fisadi mkubwa.

    ReplyDelete
  32. Watanzania tumeamka sasa, nawashangaa sana hao wabunge wanaomtetea Lowasa, mwacheni aondoke, we are tired the the shames

    ReplyDelete
  33. Michi kazi safi endelea kutuma news maana wengine tuko makazini hakuan Radio wala Tv. Vipi yaliyojiri Dodoma kwa JK?

    ReplyDelete
  34. Hongera Michuzi kwa kuwa 'sharp' katika kutupa habari wasomaji wa blog yako. Bila shaka hii habari ya Waziri Mkuu umeipata katika chanzo ambacho si 'credible' kwa kuwa inatofautiana kidogo na taarifa halisi.

    Waziri mkuu ametangaza mwenyewe kujiuzuru baada ya kudai kuwa kamati ya Dr. Mwakyembe imemtuhumu bila kumpa nafasi ya kujitetea. Na kwamba ameshamwandikia Rais uamuzi wake huo, ambao alisema Rais bado hajaujibu.

    Kutokana na mkanganyiko huo, spika amelazimika kusimamisha shughuli za bunge hadi saa 11 jioni, si kwamba bunge linaendelea kama ulivyoandika.

    Pamoja na kasoro hizo bado nakupa hongera!

    ReplyDelete
  35. Bwana Michuzi kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuwa shapu sana kutuwekea habari mbichi kabisa.Nimekuwa kwenye mjadala mkali na wadau wenzangu huko nyumbani juu ni nini kitafuatia baada ya report ile.Hata kwenye blog yetu ya hii ya jamii jana nilitoa maoni na kuelezea nini watanzania wategemee.Sasa kama dakika 20 zilizopita kuna mdau alinitumia sms alinijulisha kuwa Mh.Waziri Mkuu Lowasa kajiuzulu.Kwa kuwa nipo nakamua book kufukuzia nondoz kando na computer yangu ikiwa ni saa 9.30 usiku kwa hapa Ohio-USA, nimekuwa nafungua blog yetu kila baada ya dakika ili nione kama kuna breaking news kuthibitisha kama ni kweli.Hatimaye nakutana na maandishi mekundu kwa herufi kubwa yakithibitisha hilo.Sasa hatua ya Mh.Lowasa kujiuzulu.Kama kada wa CCM nampongeza kwa uamuzi huo ambao kimsingi ni mzito sana na ambao pengine wengi hawakuutarajia.Napongeza kwa kuwa likuwa ni lazima kufanya uamuzi huo mchungu sana ili kutuliza hali ya mambo ambayo dhahiri,shahiri ilikuwa inakipeleka chama na serikali yetu mahali ambapo tusingepatarajia kabisa.Kama alivyosema kwenye taarifa yake kuwa sasa wabunge waijadili Richmond na sio Lowasa,ni kweli kabisa.Maana nina hakika kabisa joto lake sana limeshuka kabisa na inawezekana kabisa siku 2 walizotengewa wabunge kuijadili report zikawa ni nyingi.Nasema hivyo kwasabu sitegemei kuona kama bwana mkubwa amejiweka pembeni mawaziri wake wabaki.Ndio kusema mapendekezo ya kamati yameanza kuzaa matunda kiasi cha kuuzima mjadala.Ndio,maana inajadili nini tena wakati wahusika wamekubali kuwajibikika? Ndio maana nasema mjadala haupo tena.Labda kutoa maangalizo kwa siku sijazo.Nampa pole sana Mh.Lowasa,maana ni ukweli kwamba matatizo yanampata binadamu.Na kwa kweli,kwa wanaCCM tunapaswa kulia wote.Waswahili wanasema "mchuma janga hula na wa kwao".Kwa hiyo hatuwezi kufurahia jambo hili japo katika mantiki yake ni uamuzi busara kwa maslahi ya taifa na kukirejeshia chama heshima,hadhi na imani kwa watanzania.Mzee wangu JK,naomba uupokee uamuzi wa Mh.Lowasa kwa ujasiri bila hofu yoyote.Najua ni majaribu makubwa sana.Hatahivyo,jipe moyo mkuu.Chukulia kama ni changamoto kubwa na muhimu katika utawala wako.Mungu aliyekuinua kuwatumikia watu wake ana makusudi mema nawe.Kumbuka umma wa watanzania wana imani nawe sana.Na hao ndio ulioingia nao ubia wa kuongoza nchi na kuwatumikia.Tunatambua nia yako ilikuwa njema kabisa,lakini unapofungua dirisha kuruhusu hewa safi iingie,sio ajabu kuona inzi na mbu wakiingia pia.Hakuna kurudi nyuma.Songa kifua mbele kwa ukakamavu wananchi tuko nawe.
    Mungu Ibariki Tanzania
    Mungu mbariki Rais wetu!

    ReplyDelete
  36. Namuonea huruma sana muheshimiwa kikwete kwani sasa ile kasi mpya na ari mpya inabidi ibadilike anyway ni uamuzi wa busara muheshimiwa kujiuzulu unfortunately tunataka na ufatiliaji wa tuhuma hizo huku ulaya zinaanzishwa probes kuchunguza hizo tuhuma.

    Na sio kutaarifiwa basi mtu kajiuzulu then anaendelea kula kuku tu lazima afilisiwe na kama ikiwezekana kufungwa kabisa!!!!!!!!!! Tuwe kama Thailand, Malaysia, Singapore kwa kasi kikwete tuko Ulaya sio tunamalizia nondo zetu tunakuhakikishia tunairudisha Tanzania katika ramani ya dunia kiuchumi na kimaendeleo
    Kaza Buti Mzee JK
    Usirudi Nyuma
    Tuko nyuma yako
    Wako
    Mwenye uchungu

    ReplyDelete
  37. Karamaji na mwenzio Msabaha , haya mfuaate upesi kujiuzuru, hahahaha, karamaji safari imewadia sasa, Mkuu ameshaanza usijifanye kuzuga wewe mfisadi mkubwa!!1

    ReplyDelete
  38. Kwakweli Sasa Hii ndio Tanzania tunayoitaka;
    Tanzania Blia Mafisadi
    Tanzania Bila Rushwa
    Tanzania Bila Wezi ;
    Mungu Ibariki Tanzania

    Watu WeeeeeeeWeeeeeeeeeeeee

    Afadhali sana huyu jaamaa kajitoa maneke kulikuwa na Fununu anataka kugombea urais mwaka 2010 kwa kumpika Chini Jakaya katika kura za ndani ya CCM,
    na alikuwa ameshaaandaa kambi nzito ;

    Swali JE ATAENDELA KUWA MBUNGE AU NDO NAUBUNGE GOODBYE??

    ReplyDelete
  39. kwa kweli waendeleekujiuzulu hawa ni wanyonyaji wasio na huruma hata kidogo mtu unamyonya mpaka mfupa ,wale kidogo wabakizie na wenzao
    mimi bill pale nyumbani nalipa postpaid, nilikua nalipia tshs 30,000 per month hapo situmii jiko la umeme wala birika ,wala ni pasi mafridge matatu, tv na feni moja tu basi mwaka huu jan
    matumizi haya haya nimepata bill ya elfu 92,000/= kwa kweli nimechanganyikiwa taa zetu ni tube light, nasema hivi sbab mimi ni mtanzania wa kawaida tu
    bei imepanda mno jamani

    kikwete akae akijua kua mimi sina imani nae tena ,anatumia kodi zetu kwenda nje kila siku,
    nasema hivi watu wameelevuka kwa sasa tumechoka na kuibiwa ,tunaishi maisha ya kuhangaika, kwa ajili ya manufaa ya watu wachache

    mlioko ulaya komaeni hukohuko huku serikali hii ni ya wezi wenye njaa kali

    ReplyDelete
  40. JAMANII NGOJENI WAOSHA VINYWAA NA WADAU WAAMKE WAANZE KUTAPIKAAA??

    ReplyDelete
  41. Hivi kwani kujiuzuru na ubunge haiwezekani? asijitetea chochote, ni bora ameachia ngazi..kama mbwai,mbwai bwana!

    ReplyDelete
  42. SIKU ZOTE TUNAONGEA KWENYE BLOG HII. KUNA WATANZANIA WENGI VIONGOZI MAFISADI NA WASIO WAADILIFU. WATU WAMESAHAU KABISA MAMILIONI YA WATANZANIA WANAOKUFA KWA KUKOSA "BASIC SERVICE" KAMA HUDUMA ZA AFYA NK.

    NDIYO MAANA TUKIFIKIA HATUA KAMA YA KENYA KWENYE UCHAGUZI UJAO SITASHANGAA. MAANA WANAIBA KURA KUINGIA MADARAKANI WATUIBIE.

    MUNGU WABARIKI HAWA:-
    1. Mhesh. SLAA, ZITTO KABWE, Mch. MTIKILA nk.

    2. DAKTARI MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE YOTE.

    3. WABUNGE WOTE WALIOONESHA UCHUNGU SAFARI HII KATIKA MIJADALA MBALIMBALI.

    4. WATANZANIA WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO.


    Anony,
    MAREKANI KWA BUSH.....

    ReplyDelete
  43. SIKU ZOTE TUNAONGEA KWENYE BLOG HII. KUNA WATANZANIA WENGI VIONGOZI MAFISADI NA WASIO WAADILIFU. WATU WAMESAHAU KABISA MAMILIONI YA WATANZANIA WANAOKUFA KWA KUKOSA "BASIC SERVICE" KAMA HUDUMA ZA AFYA NK.

    NDIYO MAANA TUKIFIKIA HATUA KAMA YA KENYA KWENYE UCHAGUZI UJAO SITASHANGAA. MAANA WANAIBA KURA KUINGIA MADARAKANI WATUIBIE.

    MUNGU WABARIKI HAWA:-
    1. Mhesh. SLAA, ZITTO KABWE, Mch. MTIKILA nk.

    2. DAKTARI MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE YOTE.

    3. WABUNGE WOTE WALIOONESHA UCHUNGU SAFARI HII KATIKA MIJADALA MBALIMBALI.

    4. WATANZANIA WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO.


    Anony,
    MAREKANI KWA BUSH.....

    ReplyDelete
  44. HALELUYA, HALELUYA, HALEYUYA HALELUYA HALELUYA. Mungu Mwenyezi ametutendea mema HALELUYA!!! Niacheni niimbe HALELUYA KUU japo ni wakati wa KWARESMA mana nimefurahi sana.Kweli mambo ya Mungu ni ya poleple lakini akiamua kujisdhihirisha, matendo yake ni makuu na yanatisha kama nini. Ah KAKA KAJIUZULU AMA KWELI HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA!! Ngoja niwahi zangu nikajipongeze na kuhitimisha furaha yangu kwa kitimoto na ndovu baridi pale JJ SINZA MAPAMBANO.Karibuni sana wadau wote mliofurahishwa najambo hili. Mapambano bado yanaendelea na Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  45. SAMAHANI ANON HAPO JUU WA ohio samahani tena ila naomba nikwambie kwamba nchi yetu inazidi kuwa maskini kwa ubinafsi na uzandiki wa watu wachache wenye mawazo yako. Lowassa is a thief simple! Big time theif! Yaani huyu jamaa na kodi zetu anazolipwa marupurupu na mishahara mamilion bado anatufanyia haya madudu? eti kafanya uamuzi wa busara? which uamuzi, hapa kinachofuatia apelekwe kwenye vyombo vya sheria! This is way too much.

    Au mkubwa kwa vile uko OHIO hujui machungu ya watanzania hapa nyumbani? mtu analipwa mshahara wa elfu sitini halafu taifa linamlipa Million 152 kila siku Lowassa kupitia kampuni yake hewa? eti tumuonee huruma? Huyu ni muuaji zaidi ya INTERAHAMWE!

    Eti hakupewa nafasi ya kusikilizwa? Mwakyembe alitutangazia watanzania wote wenye chochote/maoni waende kwenye kamati yake! Mbona hakwenda? People wote sio wajinga kama mnavyotufikiria. Huu UFISADI wa kuiweka mbele CCM kuliko taifa letu ndo unatufikisha hapa!

    Nasema hivi, Lowassa na wote waliotajwa waondoke na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Watanzania tumechoka, kuibiwa na watu wale wale, siku zote. Mpaka wengine wameshaamini kwamba walizaliwa wawe maskini! Mdau wa Ohio Iam sorry I thought because you are in western countries ungekuwa na uelewa zaidi ya huo, but unfortunately you are worse off!

    Lowassa has done more damage and He has proved right Nyerere aliyetwambia kwamba huyu jamaa si muadirifu! YAMETIMIA.

    Tanzania ni ya watanzania wote, masha bora si kwenu tuu watoto wa wakubwa na viongozi! CCM watch out, watu tuna hasira na nyinyi...Iko siku kitaeleweka tu, ngoja tusake nondo!

    ReplyDelete
  46. Hongera lowasa kwa kujiuzuru

    Nimepokea kwa furaha sana kwa kujiuzulu mh lowasa ni jambo la kujiheshimu sana, na kukbali matokeo, ni ushujaa na mapenzi ya dhati ya kuwajibika ktk nchi ili kutoa nafasi kwa watu wengine kufanya kazi kwa mapenzi ya dhati toka moyoni ktk nchi hii

    Sikuona sababu ya kusubiri report ya Mwakyembe ungeachia ngazi mapema sana tangia mwanzo

    Ulizoiba zinatosha nenda katumie na mke wako sasa kwani maisha bora ya lilenga zaidi ktk mfuko wako binafsi. sijaamini kama mtu kama wewe ulikuwa unaitumbukiza nchi ktk janga la kifo namna hii,maisha yamekuwa magumu sana kila mahali nchini Tz, wewe unashika uchumi wa nchi hii ktk mikono yako.

    naomba uombe msamaha kwa wananchi wa wazawa wa Tanzania, kwani kila kilio chao hutobaki salama kabisa.

    Mungu ibariki Tanzania

    Email:moshaalexus@yahoo.com

    ReplyDelete
  47. Tuwalinde Mwakyembe na Michuzi dhidi ya Tindikali

    ReplyDelete
  48. mimba tayari tumeanza kuona watoto na badooooooooo!!kwani wako wengi sana,kajitoa kigogo wao bado vifaranga sasa!!!!!WADANGAYIKA OOOOOOOOOOOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE MUKAMA~SEOUL

    ReplyDelete
  49. KIKWETE ANAPONZWA NA USHKAJI NA WAKO WENGI WATAKAO KUANGUSHA.....
    ANGALIA KAKA JIPANGE TENA
    "Haya Edward sisi tulikupenda lakini Richmond wamekupenda zaidi...wasalimie Kighoma"

    ReplyDelete
  50. ALL IN ALL KIWETE IS THE BEST TO ME HOW MANY PRESIDENTS HAVE PASSED WHAT HAVE THEY ACHIEVED THAN RUSHWA ANGALIA ANAVYOPAMBANA WAZI ALIWAAAMBIA ALIVYOANZA TU KAMA UNAFANYA KAZI KAMA INAVYOSTAHILI ULL STAY UNLESS OTHERWISE ULL BE KNOCKED OFF SASA HAYO MAJIMAMBO.JAMANI WATANZANIA TUJALINI AMANI PIA OHHH HAYA MAMBO YANATISHA SANA ASWA WALALA HOI MAANA NDIO WANAKUWAGA WABAYA SANA KWASABABU YA HAKI YAO.NDIO MAANA UJAMBAZI BONGO KILA SIKU WATAHAWANA NJIA YA KUISHI

    ReplyDelete
  51. "Because I have been linked to this scandal, I have decided to write to the president asking to be relieved of my duties," Edward Lowassa told MPs.....vp kuhusu kuturudishia mkwanja wetu??? kujiuzuru siyo issue kwa wananchi tunataka asongeshwe mbele na afilisiwe

    ReplyDelete
  52. Wakubwa! msimpe huyu jamaa sifa za bure! Huyu hakujiuzulu huyu! Jana usiku kuliwaka moto huko kwenye vikao vyao vya ndani vya sisi-M! huyu atakuwa ametakiwa AANZE kwa kwenda mbele!

    Waziri mkuu mzima utaachiaje ngazi kwa maneno unayosema ni ya kusingiziwa!!!
    Take five, Mhesimiwa Mwakyembe!!
    good riddance!
    Haya, na wengine waanze kutia maji mabichwa yao...!!! I am SOOOOO happy!

    ReplyDelete
  53. Thanx Bro Michu for this info. Sasa kilichobaki ni kuwaunganisha Lowassa,Karamagi,Yona,Mkapa,Msabaha nk kwenye kuadabishwa,they should be accountable.

    ReplyDelete
  54. Ahsante sana Bwana michuzi kwa habari hizo.Mh.Lowassa na wote waliohusika sio kwamba wanapaswa wajiuzulu bali wanapaswa kukamatwa moja kwa moja kutoka jumba la bunge nakufikishwa katika vyombo vya sheria.Accounts zao kuzuiwa pia mali zao wakati sheria inachukua mkondo.Hii itafanya kwa kila kiongozi yeyote kua makini anapokua madarakani,kwani ikiishia kujiuzulu tu kutampa nafasi kiongozi yeyote kujichotea mapesa na baadaye kujiuzulu na kuendelea kutumbua pesa zake alizozipata kwa ufisadi.KUJIUZULU HAKUTOSHI,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  55. JAMANIII.....NASKIA RAHAAAA..UTAM!! ME NASUBIRIA ZE COMEDY WATAKAVYOHARIBU..HA HA HA HAAAA!!! UUWIIII..

    NIMEFURAHI SANA JAMANI, YANI NIMEPIGA KIGEREGERE KIKUBWA SANA, HAWA WATU WAMETUFANYA MAHANITHI SANA!! YANI NINA MACHUNGU MIE JAMANI SIJUI NIKAWARIPUE NA GOBOLE LANGU WOTE?? NAFUU MUANZE KUVAA KIZUIA RISASI!! PUMBAFFFF..MICHU USIBANE!!

    ReplyDelete
  56. Wapendwa Hizi ni Habari Njema. Narudia HABARI NJEMA. Kwani Imeandikwa 'NI LAZIMA MTU MMOJA AFE KWA AJILI YA WENGI' 2010 SI MBALI, ccm wameshatoa kafara tumeliona, lakini si lazima tulikubali. mafisadi wako wengi, tunataka mikataba migine pia ipitiwe hasa wa buzwagi.
    HILI PIA NI CHANGA LA MACHO. ili tuseme wanafanya kazi na tuwachague tena, hatutaki kufukia mashimo wakati viazi vimeshaliwa, tunataka tule viazi wote, haisaidii chochote, bado hawa jammaa ni wazembe, Kikwete mwenyewe a step down, najua naye anahusika tu. si bure. pesa zinarudi vipi? akijiuzulu inatosha? afungwe tu ili anangalau asizitumie tena. Tena nasikia aliiba mashine za kufulia za hospitali akkanzisha dry cleaning business, arudushe zile mashine mount meru hospital pia. Jamaa ni MWIZI kabisaaaaa.
    SAmaki Mmoja akioza Fridge bovu mwaga wote nunua ingine. Tuwamwage wote na fridge CCM bovu, 2010 tupigie Kura wengine Yaani Upinzani, Chadema, NCCR au wengine wowote.

    ReplyDelete
  57. SASA NEXT PM NI NANI WADAU?

    ReplyDelete
  58. afadhali amejitoa, mi mnaniudhi sana, haya na wengine jitoeni, mana nina hasira na nyie, UFISADI WENU NDO UNATUFANYA WENGINE TUNAISHIA KUBEBA MABOKSI NCHI ZA WATU....bila ya hivyo, tungekuwa nyumbani kwetu tunaishi kwa raha musratehe, ila kila tukifirikia namna ya kuanza kusettle nyumbani ni headache kubwa, wenyewe wachache wamejilimbikizia mali, nchi wameishikilia utadhania ya kwao binafsi...watoto zenu tumesoma nao huku nje, wamemaliza mmewaambia warudi upesi, bado mko kwenye system mtawasaidia, haya wamesharudi mmewapa kazi, nafasi nzuri nawao wanajijenga, tumebakia watoto wa mbwa, tunabeba maboksi tu ughaibuni....
    SINA HAMU, WATANZANIA KAENI CHONJO, UCHAGUZI 2010 KUNA VITA KAMA YA WAKENYA YAJA........

    ReplyDelete
  59. we blog yako sasa leaves much to be desired. uliyobreki newzz partly ni kweli partly si kweli. Ni kweli kuwa amewasilisha barua ya kujiuzulu. lakini bunge limesitisha kikao hadi saa 11 jioni ili kuamua ni namna gani bora ya kuendelea na mjadala. mind you kwa mujibu wa katiba ombi lake likikubaliwa ina maana nafasi za mawaziri ziko wazi kwahiyo hakuna serikali bungeni.its advisable kuwa uwe na namna ya kupata taarifa sahihi.

    ReplyDelete
  60. Waapsss jamani wamemuonea Lowasa kijana wa watu mbona hawakumhoji akatoa kile alichokuwa nacho moyoni?This is not fair kabisa Lowasa is innocent na saga hili aliingizwa mkenge tu.

    ReplyDelete
  61. BOOOOOOOOOOOOM!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  62. UKIPORA HAKI Ya maskini Mungu atakutandika hapa hapa duniani.Ndiyo maana mijizi mingi na mifisadi ina migonjwa kama visukari,BP,na haiwezi kula chumvi wala sukari Mungu kaikomesha kaachia sukari na chumvi wafaidi maskini wanaowaibia kodi zao.

    Na ndiyo maana mingi inaishia kuadhirika.Kweli Mungu si Athunmani.Hawafanani kabisa na Athumani.

    Hongera mheshimiwa Mungu kutusaidia kupigana na mifisadi.

    ReplyDelete
  63. "Kioo, kioo, alikivunja nani, sijui sijui, wa mwisho akamatweeeee!".

    Nadhani sasa Mh. JK atakapokuwa katika ziara za kikazi nje ya nchi, akiulizwa mbona nchi yako ina kila namna ya nanihii, lakini nyinyi mko nanihii, sasa atakuwa na jibu.

    [Vyungu vinatokota Buzwagi na EPA, ambayo ni maeneo madogo tu].

    Lakini naamini kwa asilimia kubwa tu, kuwa kuna Waandamizi fulani fulani katika wizara nyingi tulizonazo kwamba sasa hivi matumbo yako MOTO!.

    Ombi kwa Bunge Tukufu, and of course kwa Mh. JK, tumalizane na hizo kwanza halafu wapinzani waibue na nyingine, nazo mzishughulikie. Heshima itarudi tu.

    Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote................

    ReplyDelete
  64. ANNA MAKINDA ndio the next PM.
    Nakubaliana na anony mmoja hapo juu.
    Nyie subirini tu

    ReplyDelete
  65. Hiyo nimekubali. Sasa tuanze mahakama haraka sana. Takukuru nao wawemo!

    ReplyDelete
  66. SAMAKI mmoja akioza basi wote latika kapu wameoza.Haitoshi kujiuzuru kwa waziri mkuu pekee yake,RAIS naye anatakiwa kujiuzuru kwani ni yeye alie wateua hao watenda kazi wake.Wamemlet down basi naye aondoke jukwaani ili kupisha waigizaji wengine.

    ReplyDelete
  67. ANNA MAKINDA ndio the next PM.
    Naungana na anony mmoja hapo juu.
    Nyie ngojeni tu!

    ReplyDelete
  68. Wana Blog, yaani hapa Univ of Dsm wanafunzi wanaandamana na kuimba Lowassa rudisha hela zetu, huku wameshika mabango mengi sana yanayoorodhesha mafisadi wa Richmond. Zaidi ni kuwa Kilio cha mafisadi! Mimi natamani nijiunge nao maana bei ya umeme inanitatiza. Usiku nikisikia hata feni limewashwa nawagongea mlango watoto wazime maana ugali utakuwa haupatikana kwa jinsi Richmond anavyonitafuna kwa nguvu! Aondoke na arudishe fedha zetu na wengine wote waliohusika.

    ReplyDelete
  69. Historia inajirudia: Hii ni mara ya pili sasa! Mara ya kwanza yalimkuta Ndugu Rashid Mfaume Kawawa na MV Rajpar! safari hii yanamkuta Manywele na Richmond Development!

    MtiMkubwa.

    ReplyDelete
  70. Kwa kweli yametufika sasa ni wakati wetu sasa UAMUZI WA KUJIUZULU NI POA

    ReplyDelete
  71. Kama wazungu wanavyosema it is about the time. Kwa wale ambao mnadhani Lowassa asinge jiuzulu nawasupport kabisa kwani hii ni shock news, hasa kwa wengi wetu tulio nje ya Tanzania. Going back kwenye point, Lowassa hakuwa na ulazima wowote wa kuhojiwa, however yeye ndie aliyekuwa mstari wa mbele kutetea scandal yote ya Richmond, kumbukumbu zangu zinaniambia aliwaambia wabunge wa CCM wache kushangilia swala la Richmond.

    Hii ni move nzuri sana kwake, kwani nina baadhi ya wadau wenzangu tulikuwa tunaplan kufanya maandamano hapa ughaibuni tukiomba Muheshimiwa ajiuzuri. Again, point yangu sio kusema kwamba bwana Lowassa is guilty, kwani hakuna litigation zozote zilizo failiwa, point muhimu ni kwamba muheshimiwa waziri alishindwa kufanya maamuzi muhimu pindi swala hili la Richmond lillipo lipuka. Kama muheshimiwa Lowassa angekuwa wa kwanza kuomba bunge liunde tume pindi tuu swala hili lilivyo bumbuluka basi leo tungekuwa tunaongea mengine.

    Hongera zangu ziende kwa Dr Mwakyembe, kwani ameonyesha ufanisi wa juu kabisa katika kuorganize the whole report spectrum. Vile vile Prof Tenende wa pale Houston, Texas kwani aliweza kuonyesha doti hadi doti la majambazi hawa wa Richmond. Hili ni swala la kitaifa, i hope JK atavunja baraza zima la mawaziri kwani wananchi hawana imani nalo. Vile vile napenda kuwashukuru wandishi wa magezeti mbali mbali ya hapo nchini, ndugu michuzi kwa kutupa snap shot of what happening in day to day basis. I believe each Tanzanian who participate on this movement needs special Thanks.

    Hakuna maendeleo pasipo mabadiliko.More to come, i believe we will see Zitto report about Madini which will be a slum dunk.

    The next thing i believe ni sheria kuchukua mkondo wake. This people creaple our country, our economy, our hearts, our moral and our respect on global manner. They need to stand infront of Judge. I am so Happy leo. This is our time, this is our Era, Tanzania the Come back Kid,
    Mdau wa US

    ReplyDelete
  72. Yap yap, aibu kubwa, watoto wake huwa wanajidai mno, at least sasa hivi watanyamaza kimya, serikali inastahili kurudushiwa hela yote na hawa mafisadi, ianzishe tume ya kusaka mali na fedha zinazohusiana na hizi hela za wizi kwani wnaoiba sasa hivi hawana wasiwasi hadi wakamatwe. Bila kuwa na tume maalum wizi wa fedha za serikali utaendelea.

    ReplyDelete
  73. eh kwa kweli hii inatuonyesha kuwa maombi ya watu wa mungu yanajibiwa,maombi yaliyomguruma uwanja wa taifa kabla ya mwaka huu yalikuwa kiboko,tumemwona mungu nchi hii ipate viongozi waadilifu Rwakatare kachomoza tayari,Rais kikwete wape watu kama hawa wizara nyeti hawatakubali mlungula,kwa kweli watanzania wengi tulio hapa Oslo tunaipongeza kamati ya mwakyembe kwa kazi pevu ,nzuri na ya kina,Bot nayo tunaomba wengine wapewe kadi nyekundu sio balali tu
    Rugaitika Revocatus

    ReplyDelete
  74. jk usipokuwamakini utatupeleka kenya hayo mambo ya kupeana kisa friend of mine yatakutoa hata wewe kwenye upresident nadhani kwenye hilo umejifunza chagua kiongozi kwa kuzingatia sifa sio sura wa urafiki

    ReplyDelete
  75. Heads will roll, kudadeki. Na bado!

    ReplyDelete
  76. Nyani haoni shaurile, walivyomsakama Zitto bila kumpa nafasi ya kujitetea hawakuona hilo sasa umefikia kwake ndio imekuwa hivyo. waht goes around always comes back around. Ukikosa bora ujinyamazie taratibu usiseme hovyo mwisho utasema na visivyo kuwepo maana hata kama unasingiziwa ndio unazidi kuonekana mwongo, achukue desa kwa Ben na makelele yote kanyamaza kimya hataki bugudha mzee wa watu. Kujikosha ndio kunawafanya watu waseme ambayo hata hayapo kwa kutaka kuonekana hawana hatia.

    ReplyDelete
  77. MIMI MAMBO YA KUJIUZULU BILA KUCHUKULIWA HATUA SIPENDI.HUYO KIONGOZI WA SERIKALI NA KUTUHUMIWA KWENYE UFISADI LAZIMA APELEKWE MAHAKAMANI HILI HELA ZA WANANCHI ZIRUDI NA YEYE APEWE ADHABU KWANI WOTE HAO WALIKULA KIAPO KUTUMIKIA TAIFA LETU KWA UKWELI.MAMBO HAYA KUJIUZULU TU NA KUKACHIWA NDUGU ZANGU HAWA SIO MAKOCHA WA MICHEZO AMBAO TIMU IKIBORONGA TUNA WAFUKUZA AU WANAJIUZULU NA KOCHA MWINGINE ANALETWA TIMU INAENDELEZA LIBENEKE.HAPANA HAWA NI VIONGOZI WA NCHINA WASHITAKIWE.

    ReplyDelete
  78. Oh hii ni habari nzuri sana yenye uzuri kupita kiasi, sasa naona Watanzania wameamka. Ukweli ni kwamba wakubwa walizidi kula na kasahau wananchi wao sasa ni wakati wao wa kuwajibishwa. Na sisi wananchi tunaomba awajibishwe kama wengine walivyowajibishwa. Na pia umeme upunguzwe bei ili watanzania wote waweze kutumia umeme, umeme ulikuwa unatumiwa na wao wenyewe tu maana ulikuwa bei juu sana kumbe zilikuwa ni hela zao za mifukoni. Na kama walivyopiga kelele kuhusu Balali na kudai alipe, tunaomba na Mh. Edo alipie hasara yote aliyoisababishia taifa. Tunaamini hasara si hii tu kuna mengine yatakuja mengi tu huko siku za usoni. Mfano mwingine kijana mh. wa watu Kabwe walijifanya kumpa adhabu eti kwa kusema waziri ni "muongo" ikapitishwa apewe adhabu ya kuacha kuwatumikia wananchi wake kwa uwakilishi wake bungeni, je sasa na hawa waliosababishia hasara kubwa ya mabilioni serikali pamoja na kuwatesa wananchi ambao ndo waliowaweka hapo walipo kwa kulipia umeme bei za juu zisizo halali, je apewe adhabu gani ya kufanana na alichokitenda??

    ReplyDelete
  79. Jamani Watanganyika wenzangu,mnaonaje hapo tukamweka JOHN POMBE MAGUFULIII????

    ReplyDelete
  80. Ndugu wadau wenzangu mliobobea kweny masuala ya sheria
    Huku ng'ambo kuna mashitaka ya abuse of power
    ambapo adhabu yake ni kurudisha mshahara woot tuliomlipa au kufilisiwa kiki ambatana na kifungo jela
    sasa hili suala mnalionaje kwani ni wazee wetu ndio wanaoumia mpaka sasa kwa ufisadi wake

    ReplyDelete
  81. Vema kajiuzulu, waziri mkuu ajaye asitoke kwenye recycling plant. JK unao watu wengi wenye uwezo na nia ya kuijenga nchi si kama JK alivyosema enzi zake hapakuwa na wasomi na wanasiasa wakutosha

    ReplyDelete
  82. Haitoshi kujiuzulu..inabidi ahukumiwe na kurudisha pesa za walalahoi na wananchi wenye kuvuja jasho wa Tanzania. Baada ya hukumu pia bila kujali kuwa alikuwa waziri mkuu wa nchi mlafi..ahukumiwe na akakione cha mtemakuni huko jela! Vilevile afilisiwe ili uwe mfano wa viongozi wengine wafisidi na waroho wenye kukalia viti ili kujaza matumbo yao!
    Nawakilisha ....Kudumu Kujenga Nchi!
    Serikali ya Valafi hoyiiiiiiiiiiiii!

    ReplyDelete
  83. Je mkataba wa richmond hausitishwi baada ya kuthibitika kuwa walidanganya kwenye zabuni? Tutaumizwa mapaka lini. Au nchi imekuwa ya vichaa kujifunzia kunyoa?

    ReplyDelete
  84. Magufuli si ndiye aliyemwomba rushwa Karamagi wakati wa uchaguzi wa NEC kule kwao, eti awagawie tumadini kidogo watu wa jimbo lake ili wamchague?? Rose Garden ameiwekea kifua.HAFAI ananuka turushwa tudogotudogo

    ReplyDelete
  85. Mungu atupe nini tena.....labda aendelee kuwafichua.Maana mpaka kujitoa keshaona hali mbali.Tanzania we need to be serious na nchi yetu esp makini katika uchaguzi.

    ReplyDelete
  86. eeeeeebwanaeeeeeeeeeeeeeeeee duuuuu sasa boys 2 men imebaki sijui tuseme "boys 1 men" au vipi? na je huyu JK jamaa Lowassa si bonge la swahiba wake na tuone atamfanyaje, TZ kumekucha sasa na hii ni "kazi kwelikweli"

    ReplyDelete
  87. mmoja mmoja ataondoka, mafisadi nyie, sasa Raisi si na wewe ujitoe maana uliwachagua mafisadi ina maana ulikua unapata cha juu
    na wewe tunaomba ujiuzulu tumekuchoka, hatuoni maisha bora wala nini
    patachimbika mwaka huu

    ReplyDelete
  88. umenichekesha sana BABU MZEE REVO wa 2:12,,kawimbo katamu sana....
    kioo,kioo alikivunja nani....sijui sijui ,,waongo ndio wote....PITENI,PITENI...wamwisho akamatwe,atiwe gerezani..
    kawimbo kaminikumbusha mbali,,kanafaa sana hapa....
    INFWAKT MANY OF THE TOP GOVERMENT OFFICIALS, NEED TO LOWASALISE THEMSELVES, BEFORE ITS TOO LATE.
    OOH, GO LOWASA ITS YOUR BADDAY..
    GO KARAMAGI ITS YOUR BADDAY, GO MSABAHA ITS YOUR BADDAY...AMAKWELI ZA MWIZI 40

    ReplyDelete
  89. Inasikitisha lakini ili kupata maendeleo ya kweli lazima haya yatendeke vinginevyotutakuwa tunafanya kazi bure, ikiwa unahusika mtu anahusika na uhalifu kweli hatua zichukuliwe kwani huyu moja kwa moja ni mbadhilifu wa mali ya umma hatufai , na hapo Rais anakazi kweli kwani Kuchaguliwa kwake mara ya pili kutategemea busara yake katika uamzi wa suala kama hili, akifanya kinyume amevunja imani ya Watanzani, Naomba Mungu utumie hekima na busara katika kuamua hili, ikiwa kunauhakika katika tuhuma za viongozi basi wapewe sitaha zao. Maana wanastahili na walikusudia kufanya hivyo. Kwani nini wasiwajibishwe hakuna kutazamana usoni, mmoja atoke mwingine apone na wewe unayetoka jilaumu mwenyewe na tamaa yako, na wala usianze kuunga vikosi vya ujambazi na kuwadhuru wengine haitasaidia.

    ReplyDelete
  90. ASANTE MUNGU, WASHINDWE NA WALEGEE VIONGOZI WOTE WEZI WANAOTUIBIA HAKI ZETU, UWALEGEZE MUNGU KWANI WAMETUFANYA TUISHI KIMASIKINI SANA KWA WIZI WAO, WAONDOSHE VIONGOZI WOTE WEZI KWA NGUVU ZAKO MUUMBA, MUNGU KWELI U MTUPI KIUMBE WAKO, HII NDIYO HASA WATANZANIA TULIKUWA TUNAOMBA, ONDOKENI WEZI WOTE MUWAACHIE VIONGOZI WAZURI WAONGOZE NCHI KIMAENDELEO, BADO MOTO SASA UNAWASUBIRIA MAANA KUIBA NI DHAMBI KUBWAAAAAAA.

    ReplyDelete
  91. nadhani prof mark mwandosya anafit ktk position iyo ya PM,wadau mnaonaje?

    ReplyDelete
  92. mambo hayooooooooo, mafisadi wote matumbo joto

    ReplyDelete
  93. kwakwakwaaaaaaaa...ahahahaaaaaaaaaaa. jamani jamani jamani. sasa nadhani watachaguliwa wenye akili zao timamu. Watakaoangalia maslahi ya kila mtanzania na si maslahi ya kila kiongozi wa CCM. Hahahahahahaaaaaaaaaaaaaa!! Acha nicheke mieeeee!!!!!! wameumbuka haooooooooooooooo. na JK ndio atajifunza. Kwanza kwa nini bunge linaendelea wakati waziri mkuu kajiuzulu. Au sheria za bunge nazo zimejiuzulu jamani. Waziri mkuu ndio kiongozi wa bunge tukufu. Kama hayupo, that means na bunge lisiwepo hadi hapo atakapochaguluwa PM mwingine. hahahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaa!! AIBU!!

    ReplyDelete
  94. Mungu ni mwema sana!!! Sasa JK amepata nafasi ya kuchagua baraza la mawaziri ambao hawana biashara za kishenzi za kuwaumiza wananchi.

    Namuwaza sana Salim Ahmed Salim...

    ReplyDelete
  95. Dr. Asha-rose Migiro ndio awe the next PM!! Mama yule yupo serious na kazi yake.

    ReplyDelete
  96. KUNA POSSIBILITY MHESHIMIWA BENALD MEMBE(MB) WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIKIANO WA KIMATAIFA (MFAIC) KUWA WAZIRI MKUU, MTANIAMBIA

    WABILLAH TAWFIQ

    ReplyDelete
  97. TANGAZO LA KAZI..... VACANCY

    NAFASI NYINGI SANA ZA UWAZIRI. TUM CV KWA MH JAKAYA jakayak@hotmail.com

    CLOSING DATE TAR FEB 09TH 2008

    ReplyDelete
  98. baba wa taifa alisema tukome kuchagua "mahandsome boy "mnaona sasa ??

    ReplyDelete
  99. Kikwete give me hug,jamaa msela wako lakini kachemsha umemwaga,powa kishenzi. Na wewe Lowasa mwanaku........yo mwanaku......na umenifanya kwa njaa nije ulaya nijilipue, na sasa kusugua mavi na kuosha vibibi vizee, ili niweze kuleta pesa za kumuhudumia mama yangu. wewe umekaa ma.......u juu ya kiti umestaree kwa wizi, wenzenu tunateseka huku jamani,baridi, ubaguzi. tunatamani kurudi kwetu lakini tunashindwa kwa hali ngumu ya nyumbani.

    ReplyDelete
  100. Anon feb 8, 12:35 ingawa umetukana kidogo ila nimecheka sana nimeweza kupima hasira iliyomo kifuani kwako, hata sisi tunauchungu sana pale unapoenda tanesco na kulipa sh 94 elfu kwa mwezi au zaidi eti unalipa umeme pekee bado mengine unakua na vyombo vya umeme unavirundika kabatini jikoni na kuvifungia ili watoto wasivitumie kwa hofu ya kushindwa kulipia umeme. huona wivu sana nikienda nchi jirani na kukuta wenzetu wanatesa na umeme hiter zinawaka kila kitu umeme kwa sana,

    Mh. tusubiri sasa hiyo kesi ya ngedele ilopelekwa kwa nyani.

    kwa kupendekeza mi ningefurahi wangefilisiwa ili iwe fundisho kwa waroho, walafi wengine wote

    Sijui hela nyengine wameshazimovuzisha wameshaficha mivunguni mwa vitanda vyaoooo???

    Hichi ndo kile kisa cha mwanambuzi tunalipa fidia kwa kosa la mwengine.

    ReplyDelete
  101. Kwa kweli hili suala la waziri mkuu kuhusika katika ufisadi uliofanyika katika mkataba wa richmond ni kitendo cha aibu na ambacho hakina uzalendo kabisa. Kusema kweli mtu kama lowassa hafai kabisa kusika nyadifa yoyote kwa sababu ya kuweka maslahi mbele kuliko ya wananchi. Viongozi bora uwa na legacy ambayo inadefine uongozi waka na kama ni nzuri basi itakumbukwa na daima na vizazi vijavyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...