MH. HARRISON MWAKYEMBE


MBUNGE WA KYELA NA MWENYEKITI WA KAMA TEULE YA KUCHUNGUZA MADUDU KAMPUNI YA RICHMOND, MH. HARRISON MWAKYEMBE, DAKIKA TANO ZILOPITA AMEHITIMISHA KUSOMA RIPOTI YA KAMATI YAKE KWA UWAZI NA UKWELI KWA MUDA WA DAKIKA TAKRIBAN 80.




KAMATI TEULI HIYO IMEBAINI KWAMBA MKATABA WA RICHMOND ULIFIKIWA KWA UPENDELEO, RUSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI, NA KWAMBA LICHA YA USHAURI WA KITAALAMU NA HALI HALISI WAKUBWA WALILAZIMISHA USAINIWE. hIVYO PAMOJA NA MAMBO MENGINE KIBAO IMEPENDEKEZA MIKATABA YOTE YA NISHATI IPITIWE UPYA KAMA ILIVYO MIKATABA YA MADINI




KAMATI TEULE HIYO KUPITIA MDOMO WA MH. MWAKYEMBE IMETO MAPENDEKEZO KAMA 15 HIVI, BAADHI YAKE YAKIWA:




1. WAZIRI HUSIKA WA WAKATI HUO (MH. DR MSABAHA) NA KATIBU MKUU WAKE WAKATI HUO WAPEWE ADHABU KALI




2. WAZIRI WA SASA WA NISHATI NA MADINI MH. NIZAR KARAMAGI NA MWANASHERIA MKUU WAWAJIBISHWE KWA KUWEZESHA MKATABA WA RICHMOND KUHAMISHIWA KAMPUNI INGINE




3. UONGOZI WA TAKURU (SASA TAKUKURU) UFANYIWE MABADILIKO HARAKA KWA KILICHODAIWA KUTOA TATHMINI ISIYO SAHIHI JUU YA MAZINGIRA YALIYOUZUNGUKA MKATABA WA RICHMON.




4. MKATABA WA RICHMOND AMBAYO IMEIPASIA KAMPUNI YA DOWANS UCHUNGUZWE UPYA.




5. MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI




AIDHA JUHUDI ZINAFANYIKA KUIPATA RIPOTI YOTE HIYO NA KUANGALIA NAMNA YA KUWEKA HADHARANI ILI HADHIRA IJUE KILA KITU KWA UWAZI NA UKWELI.




PSSST! SASA TUNASUBIRI RIPOTI YA MADINI YA KINA KABWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. HUUUURRRAAAAAAYYYYYY!!!!!!!!!,

    Hayo ndio tuliokua tunayataka,

    sasa nimejua kwanin Rais yupo Dom.

    Unajua huyu jamaa (Mr. Mwakyembe) alishawahi kusemaga kua yeye ni mbunge tu lakin sio mwanasisa, sasa nimeamin kauli yake.

    Ila namba tano hapo nahisi michuzi umesoma vibaya,

    imeandikwa (nanukuu),

    MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI BUNGENI AMBAE PIA NI WAZIRI MKUU awajibishwe kwa kuutetea mwanzo.

    ReplyDelete
  2. Hey Michuzi,
    Pamoja na kukupongeza kwa kazi nzuri unayofanya kutupasha habari motot moto na mara tu zinapotoka-we are laways the first to know, sisi washabiki sugu wa Blog yako.
    Shukrani nyingi, na tunaendelea kusubiria what ever un-folds katika hii saga-Mwakyembe ni kifaa,namuaminia alikuwa mwalimu wangu wa sheria pale UD... miaka ileee..

    Keep up the good work..Michuzi kwa manufaa ya sisi tulioko mbali na home.

    Mimi shemeji yako. M.M

    ReplyDelete
  3. Chuo kikuu tupo wasomi kibao na watu safi huo uwaziri tunaumudu, achana na hao mafisadi. Msomi Chuo kikuu UDSM

    ReplyDelete
  4. Naona hiyo ripoti ina kasoro. Mfano angalia hii sehemu ya ripoti:

    "KAMATI TEULI HIYO IMEBAINI KWAMBA MKATABA WA RICHMOND ULIFIKIWA KWA UPENDELEO, RUSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI, NA KWAMBA LICHA YA USHAURI WA KITAALAMU NA HALI HALISI WAKUBWA WALILAZIMISHA USAINIWE"

    Halafu tena kamati inatoa ushauri huu:

    "MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI"

    Hebu niambie Michuzi, adhabu itakuwaje endapo mmoja wa viongozi waandamizi waliolamizisha mkataba usainiwe ni WAZIRI MKUU Mwenyewe ama hata Mwenyekiti wa AU?

    Hapa bado samaki wakubwa watafichwa na wadogo kama kina Msabaha watamezwa.

    Hiki ni kiini macho tu, labda tumngojee Kabwe na Ubuzwagi.

    ReplyDelete
  5. MAMBO MENGINE NI SAWA LAKINI SASA ANGALIA HITIMISHO NDIO UCHEKE.

    5. MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI


    MBONA WEZI WA MIFUKONI AU HATA TU WAVUTA BANGI WANAPOKAMATWA NA KWA USHAHIDI KAMA HUU HUWA PROVISIONS ZA NAMNA HII ZA KUSUBIRI HEKIMA YA MTENDAJI MKUU WA SERIKALI HAZIPO???

    MTU AKIGUNDULIKA NI MWIZI TENA ALIYEATHILI MAISHA YA WATANZANIA KWA KIASI HIKI SHERIA ICHUKUWE MKONDO WAKE.
    A. KWANZA ANAONDOLEWA UWAZIRI MARA MOJA
    B. AFIKISHWE RUMANDE KAMA WATUHUMIWA WENGINE HATARI BILA DHAMANA (MAANA ANATAKA KULIFUTA TAIFA LETU KATIKA RAMANI KWA KUWAUA WANANCHI NA NJAA NA MARADHI NA KILA AINA YA KARAHA.

    C. KESI IANZE NA MASHAHIDI WOTE WAKIWAMO NINYI KAMATI YA BUNGE MAANA MMECHUNGUZA NA KUPATA USHAHIDI MSAIDIANE NA POLISI KUWATIA HAWA WATU HUKUMINI.


    AIDHA HATA SUALA LA TAKUKURU SIO TU KUBADILISHWA NAO WATUHUMIWE NA KUSTAKIWA KAMA WATU WALIOJARIBU KUFICHA UKWELI (KUSHIRIKI KATIKA KUWAPA UKIMBIZI WEZI), MAHAKAMA NDIO IWAACHIE HURU WAKIONEKANA KUWA HAWANA KOSA HILO!


    MBONA YAKIFANYIKA HAYA TUNAANZA SASA KUTAFUTA KADI ZETU ZA CCM AMBAZO TULIKUWA TUMEZITUPA STOO SIKU NYINGI!!!

    KABLA SIJASAHAU HATA HUYO MTENDAJI MKUU MWENYEWE NAYE ANATUHUMIWA NGOJA TUSUBILI TUONE SKANDALI ZOTE ZIAINISHWE HALAFU TUTEME SUMU!

    ReplyDelete
  6. Michuzi nimeingia kazini mchana huu kila kona hiyo report imekuwa gumzo, sisi tunasubiri uamuzi kutoka kwa Rais mwenyewe.. patamu hapo...
    kwa kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni.
    na huo ni mwanzo tu!
    na bado, yaani mwaka huu mafisadi wanalo!
    big up kuuubwa kwa mwakyembe, huo ndio ujasiri tunaoutaka katika kutetea haki yetu kama watanzania na kama wazalendo HALISI wa nchi yetu!
    I AM SO CURIOUS ABOUT WHAT IS GOING TO HAPPEN NEXT!!

    ReplyDelete
  7. Ni kama naota vile na nikiamka hii ndoto ndo ivo, kwisha pia!
    Wote waliohusika aidha kwa kutoa shinikizo au kukubali shinikizo achieni ngazi..
    Na ikibainika kweli kulikuwa na rushwa wahusika wote wachukuliwe hatua kali na mkataba uvunjwe..

    Tanzania si maskini kama tunavyochukuliwa, tumebambwikwa huu umasikini na viongozi wetu na maswhiba wao mafisadi.
    Aluta continua comrades!!!! Slaa upo?

    ReplyDelete
  8. Mhh safi sana Mh. Mwakyembe, nimefurahishwa sana na huu ushauri no. 5, lakini japo mwakyembe alishasema yeye sio mwanasiasa lakini hapa kaleta siasa:

    MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI,
    alitakiwa kusema hivi:

    MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUJIUZULU NA KUACHA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, hiyo ingeleta maana zaidi

    ReplyDelete
  9. Michu...najua hizi nyuuzi ni bado mbichi na huenda hauja tafakari kabla ya kuongea hapa bloguni...mie nauliza swali kwako na kwa wana blogu wote, hapa kweli kuna uwazi? ni uwazi gani ambao hauwataji kwa majina hao viongozi wa juu waandamizi waliohusika? na kwanini kamati isitoe mapendekezo km kwa mfn, KAMATI INAPENDEKEZA KILA MKUU WA IDARA AU WIZARA ILIYOHUSIKA KWA KUANZIA AJIUZURU, then ndio sheria ifuatwe?Na mbona hakuna kipengele cha watalipaje fidia za mabilioni yaliyopotea kwa kuingia mikataba mibovu?Huku wadanganyika wakifa kwa kukosa dawa za maumivu au wakiugua zaidi kwa kwenda hospitali na kulala sakafuni na kuumiza mgongo na kupata other deadly infectious diseases?WAJIUZURU WOTE!!!
    Ngoja tumwangalie JK.....

    ReplyDelete
  10. Mnyonge mnyongeni....... huyu jamaa JK ana chapa kazi kwelikweli,namfuatilia sana!si binadam wa kawaida,hapumziki,hachoki, kila siku njiani. schedule zake zinatisha hata wewe michu ungekuwa yeye, wiki moja tu ungeenda Milembe kupumzika.MUNGU MJALIE AFYA NJEMA RAISI WETU TUZIDI KUPATA MATUNDA MEMA TOKA KWAKE.AMIN.

    ReplyDelete
  11. KWANZA KABISA MBUNGE MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE NI WAADILIFU WAPEWE KAZI.HASA ZA UWAZIRI SIO HAO WABABAISHAJI KAZI KULA BILA HURUMA. HIVI NYIE MAWAZIRI FEKI SHULE MMESOMA WAPI HAMJUI UTU. WASOMI UDSM TUPO NA KAZI TUNAIWEZA KAMA TUNASUKUMA MLEVI SIO HAO WABABAISHAJI.

    ReplyDelete
  12. Waziri mkuu naye ajasalimika ...

    Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.

    ReplyDelete
  13. KINA KAYUMBA TUNATESEKA KINA MSABAHA,MWANASHERIA MKUU NA WAZIRI MKUU MNAKULA KUKU KAZI HAMZIWEZI MSAADA KTK TUTA ACHIA KABLA JK HAJAKUTOSA.

    ReplyDelete
  14. JK BARAZA LAKO BAADHI NI WABABAISHAJI UNAKAA NAO WA NINI? UNAWAONEA AIBU JIFANYE KAMA VILE UWAONI WATOSE.

    ReplyDelete
  15. Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni jamani. Nimeisoma ripoti yote kaka Michuzi kama ulivyoiweka hapo juu. Na si hii ya muhtasari uliyoiandika kwa wino mwekundu. Asante sana kwa taarifa.
    Licha ya kuwa wengi mmemsifu Mwakyembe kwa hili, ni sawa, kila mtu ana akili zake. Na jazba pia kila mtu ana yake, inaruhusiwa.
    Mimi binafsi sioni kama huyu Mwakyembe ni mwalimu wa sheria, maana, hata sisi ambao si wasomi wa sheria, tunashangaa yaani mtu atoe maelezo ya kiapo, na baada ya hapo aende nje na kusema mambo yake anayoyataka ambayo si chini ya kiapo na Mweakyembe na wenzake wayavalie njuga na kuyajengea hoja kiasi cha kuyafanya ni halali, ni maajabu. Kwa nini Msabaha kama kweli hamuogopi Mungu kwa kusema uongo alisema majungu nje ya kiapo? Si angesema chini ya kiapo? Tunashangaa kwa hili. Sasa ndiyo hapo wanapokosea na kuonyesha nia ovu. Ninayasema haya kwa faida ya Mwakyembe na wenzake. Kila kitu chenye hila huwa hakifanikiwi.
    Watu kwa upande mwingine wanajua Mwakyembe ameyafanya haya kwa manufaa ya nani. Wasije wakaona watu ni wajinga. Furahini ndugu zangu, lakini furahini kwa busara. Na hayo majungu ingekuwa mimi ningeyafanyia kazi nikaja na evidence, haikuwa hivyo. Sasa Mwakyembe anasemaje? Hawa watu ndani ya jumba la duara jamani, waoneni hivyohivyo wamevaa suti, kila mtu ana lengo lake na matamanio yake!!
    Pili, kwa nini hawakumuita huyu Mheshimiwa kumhoji na wao kujiridhisha? Au walikuwa na agenda zao tayari kichwani. Angepewa haki ya kujieleza na yeye chini ya kiapo ingeleta maana. Jamani, muogopeni MUNGU! mtakwenda kusema nini huko mbele, au mnafikiri sisi ni watu wa hapa duniani siku zote? Tutaondoka tu. Huko tunakokwenda, hakuna kupigiwa makofi wala nini, utasemaje?
    NDIYO MAANA NASEMA, MNYONGE MNYONGENI, LAKINI HAKI YAKE MPENI.

    ReplyDelete
  16. We mtoa maoni hapo juu(February 6, 2008 4:37:00 PM) Kwanza hueleweki alafu inaonekana una ufisadi pia ndani yako.Nadhani msabaha ni mjomba wako manake unavyojaribu kumdefend kwa hoja hewa na kumtaja Mungu inaonekana hututakii mema watanzania wenzako.Sisi wote tuna akili na tunajua mema na mabaya kwa hiyo hii ripoti ni changamoto na iko sawa kabisa hamna majungu kama unavyodai labda kama majungu unayaanzisha wewe.Watanzania tumeamka Aluta continua bado zamu yako!!

    ReplyDelete
  17. Kuna mambo mengi yanazungumzwa hasa kuhusiana na namna ambavyo viongozi wakuu wa dola wanavyojaribu kumalizana kwa maana ya kutengenezeana kashfa kila kukicha,kama ambavyo anon wa saa 4:37:00 anavyojaribu kueleza.Lakini pasi shaka sidhani kama kamati teule ya bunge ilikuwa na nia ya kumhusisha na kashfa Mh.EL (Mb) kama si namna alivyoshiriki moja kwa moja kwa namna ya kipekee kuilinda kampuni hiyo mara tu baada ya kufanikiwa kupewa tenda.Hatujasahau namna ambavyo waziri mkuu alivyokuwa anashinikiza umma wa watanzania kuacha kujadili suala la Ricmond wakati maji yalikuwa yamekwishajaa katika bwawa la mtera na kidatu.Watanzania walikuwa na haki ya msingi kujadili kwasababu mkataba wa Richmond kama ulivyo IPTL,Songas na mingine ndiyo inayofanya TANESCO izidiwe na gharama za uendeshaji na hivyo kusababisha kupandishwa kwa tariff ya umeme ipande kila kunapokucha.Naamini mungu anaipenda nchi hii na asingependa kuona haya yanaendelea kutendeka bila wahusika wote kuanikwa hadharani.Mungu ibariki tanzania!

    ReplyDelete
  18. Wewe anon. wa 4:37, usiwe na wewe kichwa cha panzi. Huyo aliyesema kuhusu mnyonge mnyongeni, ameongea vizuri, na ninakushangaa kuwa unafikiri kuwa namtetea Msabaha. Hapa anayeongelewa ni Waziri Mkuu. Ni kweli kuwa kwa Waziri Mkuu hawakumtendea haki. Ukweli utabaki hapo hapo. Kwa nini Msabaha aende nje ya kiapo na kusema majungu na Tume wayafuate? Nini maana ya tume inayoapisha watu? Noa hilo bichwa lako na acha ushabiki wa kitoto.
    Na pia kwa nini hawakumuita Waziri Mkuu kumhoji na yeye, kama si kuendeleza majungu, bila shaka kwa akili za kawaida tu, wangemtendea haki kwa kumhoji, ndiyo waandike waliyoyaandika.
    Tumeshamshtukia Mwakyembe na tume yake pamoja na SPIKA!! Sisi Watanzania tunataka ripoti zisizo na majumgu na ufitini.
    Umeelewa wewe anon. unayesema kuwa Msabaha ni mjomba wa huyo aliyecomment hapo juu? Nenda shule ukafunguliwe macho!!!

    ReplyDelete
  19. Sasa kumekucha.Mambo hadharani,kimeo cha Richmond kimewekwa wazi.Natarajia mjadala mkali sana bungeni ambao mwisho wa siku tutarajie tsunami ya kutisha na mabadiliko ndani ya serikali.Hilo halina ubishi,hakuna namna ambapo CCM kama chama tawala chenye serikali,tunaweza kudumisha na kuimarisha imani na heshima yetu mbele ya jamii ya watanzania kama hakutatokea mabadiliko.Ni kwa hatua hiyo tu ndipo tutauthibithia umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kwamba awamu ya nne imepenia kwa dhati kumtumikia mtanzania.Sina shaka wala hofu na Mh.Rais JK,ninamfahamu vema, ni mtu ambaye hata kama unaukaribu naye sana lakini kama uadilifu wako unatiliwa shaka,hachelewi kukugeuka.Najua atafanya kweli.Tusubiri tu.Vinginevyo,taarifa hii imenishtua sana kiasi kwamba mwili ulikuwa ukisisimka kila niliposoma yaliyo ndani yake.Ni ya aibu,ni ya kusikitisha sana.
    Tumsifu M. BGSU,Ohio-USA

    ReplyDelete
  20. Tisa kumi sheria itachukua mkondo wake? Brotha Michu inamachungu ile kinoma na nchi yangu. Hawa so called vingozi wetu hawana hiyana.

    ReplyDelete
  21. Eh kweli katika kundi la mamba kenge nao wamo!Yani kuna watu wanasahau wananchi wanavyopata shida wao wanaleta ushabiki mandazi.huyo anaecomment kwamba "Tumeshamshtukia Mwakyembe na tume yake pamoja na SPIKA" hapo juu ni mfano wa mbumbumbu wachache wasiojua uchungu wa wananchi.Kama huna hoja nyamaza.Wengi tunaona ripoti imetulia na mafisadi lazima wawajibishwe.

    ReplyDelete
  22. MUHESHUMIWA MMOJAWAPO MKUBWA ALILAZIMISHA GAZETI MOJA LA KENYA LIMUOMBE RADHI KWA KUMUHUSISHA NA SUALA HILI JE ATALIOMBA GAZETI HILO RADHI KWA KOSA LA KUOMBA RADHI ISIYO HALALI? MAANA RIPOTI HII IMETABANAISHA JINSI MUHESHIMIWA SANA HUYO ALIVYOUSIKA.

    ReplyDelete
  23. nadhani tubadilishe jina la hawa watu. sio mafisadi "MAHARAMIA" hawa ni hatari sana kwa uhai wa taifa letu. hawa wezi au maharamia washitakiwe. acheni kubebana. peleka mahakani. Kikwete ana wakati mgumu sana, lakini kajua ni kwa nini ripoti ilionyesha kuwa mawaziri hawakubaliki. nyingine nyingi zinakuja.

    lakini sasa sisi watanzania tufanye nini. Je hatuitaji mabadiliko?

    ReplyDelete
  24. Ndugu mtoa maoni wa 4:37:00 pm, inaonekana hujaielewa vizuri ripoti hii, tafadhali rejea kuisoma kwa mara nyingine na utaona sababu ya kamati teule kupendekeza waziri mkuu afikirie cha kufanya kama mtu mzima inatokana na ushahidi wa kimaandishi Tafuta sehemu ya ripoti ambayo tume imenukuu barua kutoka kwa waziri Msabaha kwenda kwa katibu mkuu wake ikisema "nimezungumza tena na mheshimiwa Waziri Mkuu leo juu ya bei......" zingatia neno TENA. Kwa hiyo utaona amekuwa akihusika kwa ukaribu kuliko unavyodhani.

    ReplyDelete
  25. mtoa maoni wa 6.45 pm na wewe ni mtoto wa FISADI.. unafaidi jasho la sisi walala hoi.

    ReplyDelete
  26. duh JK ana kazi kweli hapo wamemtega manake lowassa,rostam aziz,karamagi ni mabest zake sa cjui atafanyaje jamani hapo ndo tutaona uadilifu wake km ni kweli ana nia ya kupambana na rushwa na ufisadi au atawalinda kwa kigezo cha urafiki au kulipa fadhila kwani kumbuka walimpiga tafu sana kwenye kampeni,mh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...