mh. mizengo pinda akisalimiana na wabunge wal.na iohudhuria semina ya uwajibikaji wa ukaguzi wa mahesabu ya serikali mei 3, 2007 ukumbi wa ubungo plaza wakati huo akiwa waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa. na chini mh.pinda akitoa hotuba ya kushukuru uteuzi wake sasa hivi bungeni dodoma.
BUNGE LA JAMHURI DAKIKA CHACHE ZILIZOPITA LIMEMTHIBITISHA MH. MIZENGO PETER PINDA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUCHUKUA NAFASI YA MH. EDWARD LOWASSA ALIYEACHIA NGAZI JANA. MNAOJUA IDADI YA MAWAZIRI WAKUU WALIOPITA PAMOJA NA MAJINA YAO NA MIAKA WALIYOKUWA MADARKANI NAOMBA MTUSAIDIE WENZENU



MH. PINDA AMEPITISHWA RASMI NA WABUNGE KUWA WAZIRI MKUU MPYA KWA KURA 279 ZA NDIO AMA ASILIMIA 98.9 WAKATI KURA MBILI ZIMESEMA HAPNANA NA MOJA IMEHARIBIKA.

KUANZIA DAKIKA HII MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA NDIYE WAZIRI MKUU WETU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Michu Dola zangu 500 zi wapi?? Nilipatia kwa kusema huyo Mizengo Peter Pinda ndo atakuwa PM.

    ReplyDelete
  2. Hongera muheshmiwa sana.

    Mie naomba kukumbushwa vile Lowasa yeye alishinda kwa asilimia ngapi vile? wakati ule alipopigiwa kura na bunge hilo hilo!

    ReplyDelete
  3. kama huyu pinda ni msafi kazi yake ya kwanza ni kumchambua huyo mbunge wa Kwela,mkoa wa Rukwa Mh Mzindakaya(pichani hapo juu) alipata wapi pesa za kujenga kiwanda cha kusindika nyama?hayupo katika list ya BOT kweli?
    mawaziri wakuu wa zamani include
    Mwalimu J.K.Nyerere
    Mzee Rashid Mfaume Kawawa
    Hayati Edward Moringe Sokoine
    Dk. Salim Ahmed Salim
    Joseph Sinde Warioba
    John Samuel Malecela
    Fredrick Sumaye
    Edward Lowassa a.k.a Richmonduli
    Mizengo Peter Pinda
    Harisson Mwakyembe - next PM

    ReplyDelete
  4. haya Mr.Nyooka sijui Mr.Pinda, na ukanyooke haswa huko bungeni usiende kupinda,mana ukileta janja ya nyani,tume zitaundwa and you will be lowasalised....Hongera, je una mke? we dini gani? waweza kuoa mwingine...umenivutia....

    ReplyDelete
  5. its too a early to make a comment on the new Pm(Mizengwe isiyoPinda), lets see, hope the cabinet ll ivolve over 50% of new faces and reduced its number to 40 or less, Mr JK we ve already seen that >60 ministers is too much to handle we need few ministers who can delver something to the society,,, god bless tanzania and no where else

    ReplyDelete
  6. Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Nampa Hongera sana Mh. Mizengo Peter Pinda. Tusogezee gurudumu la maendeleo.

    ReplyDelete
  7. Hivi Jk kafikiria nini mpaka kumteua huyu jamaa, ok, anazo sifa na experience ya kazi za kisiasa, ila mmh jamaa ana miaka 60 mwaka huu, hivi kwanini hatuangalii na umri..miaka 60 kwa bongo si ni mingi mno, si ndio watu wanaanzaga kuchoka na kuumwa mara miguu, mara pressure, kisukari etc,,au kwa vile wanakuwaga na pesa hawa (FISADILIZATION) ndo mana huwa hawaugui na kuhangaika kama wenzangu na mie...anyway, labda wenzetu wanaendaga check ups ulaya,,,ila mmh miaka 60 jamani, wangekuwaga wanatazama na umri jamani kwenye nyadhifa kama hizi, tusije mpa kazi halafu kila leo sick leave, then akatibiwe marekani, gharama kwa wananchi, kwa hiyo tunarudi palepale, UFISADI NGUMU SANA KUISHA TANZANIA..anyway, tutaona...

    ReplyDelete
  8. kaka ni hivi huyo jamaa nae si sahihi nikiwa na maana si safi si alikuwepo serikali ya mkapa? au watu mmesahau?

    ReplyDelete
  9. HONGERA MP MPYA
    Nimeridhika na uteuzi ila cha msingi sasa Pm ni kuondoa uozo wote maaana umesihi Ikulu muda mrefu sana unayajua mambo yote ya serikali sasa Baraza nalo twangoja nani IN/OUT tunaomba na baraza liwe na mawaziri wasiokuwa na mali nyingi na wazitangaze kama ilivyofanya kwenye maelezo yako .Tunahitaji kuona Jeshi Jipya la Mhehimiwa JK linapambana na kila aina ya mchezo mchafu tunataka serikali safi ,tusifikishane mbali kama kwa wenzetu KENIA

    ReplyDelete
  10. Yes! wanaingiaga katika nyadhifa hata na 99% lakini mwisho wake huwa 0%.

    I don't care who is in, I count who does what we agreed upon.

    Kwako PM ninachotaka kuona mimi maskini ni :-

    1. Tanesco (na EURA) wateremshe viwango vya bill za Tanesco kuwa ilivyokuwa manzoni mara moja vinginevyo sakata lote lilifanya hata ukapata nafasi hiyo halina maana kwa maskini.

    2. Wote waliohusika na wizi au kutuletea hasara au kutetea wezi tukianzia na EX- PM, BALALI, MEGJI, SPIKA 6, KARAMAGI,WAHUSIKA NA MAKAMPUNI YALIYOCHOTA TOKA BOT n.k wanafikishwa mahakamani mara moja, wafilisiwe na wafungwe katika magereza yanayoongoza kwa kazi ngumu sana na mazingira magumu mno!
    Hapa unatakiwa uwe na roho ya paka maana itabidi wakati mwingine hata utofautiane na JK aliyekuteua, potelea mbali maana Mungu aliyemkuu na nguvu kuliko JK atakuwa nawe!

    vinginevyo na wewe usipoangalia kama Richmonduli utamaliza au kukatishwa kipindi chako tukikwita,

    Mizengwe wa ku- Pinda Pinda.

    Ukipewa nafasi kama hiyo at this defining moment kwa nini usiandike historia kwa kusafisha mafisadi na kurejesha demokrasi na haki. Nakwambia hutaishia tu hapo hata Maraika Gabriel atapendekeza jina lako uwe kiranja Mkuu tukutanapo huko mbinguni! Samahani nilikuwa nimesahau kuwa huko hakuna cha sheria!

    ReplyDelete
  11. All I can say, it is tooo early to say anything regarding to the new PM; to date, nobody knows his wrongdoings or if he ever involved himself in any scandalous issues so far prevailing. Let's give him the benefit of the doubt, though we all cheered for previous ones and what we found out later were rather astonishing and embarassing. By the way,mdau Kijiwe Said I like the term "Richmonduli", whos knows may be that's what it means. later

    ReplyDelete
  12. Kama huna mke nakusubili nami sina mume, halafu napendeza kuwa mke wa waziri mkuu mwambie mchu akusaidie kunitafuta.nataka nikae na Mama Salma Kikwete karibu ili tusaidine kuinua maisha ya kinamama , watoto na jamii kwa jumla.Queen of the Jungle.

    ReplyDelete
  13. mmmmm, sina neno na uteuzi wa mheshimiwa but I thought we truly needed something NEW here. The mheshimiwa has been around since...my GOD!... enzi za Nyerere!...and then Mwinyi...and then...Mkapa...amd then JK!! Ni kweli tunaweza kujiaminisha kabisa kuwa kutakuwa na jipya hapo?? MUNGU
    ibariki TZ.

    ReplyDelete
  14. Prime Ministers of the United Republic of Tanzania
    Rashidi Kawawa 17 February 1972 13 February 1977 TANU
    Edward Moringe Sokoine 13 February 1977 7 November 1980 CCM
    Cleopa David Msuya 7 November 1980 24 February 1983 CCM
    Edward Moringe Sokoine 24 February 1983 12 April 1984 CCM
    Salim Ahmed Salim 24 April 1984 5 November 1985 CCM
    Joseph Sinde Warioba 5 November 1985 9 November 1990 CCM
    John Malecela 9 November 1990 7 December 1994 CCM
    Cleopa David Msuya 7 December 1994 28 November 1995 CCM
    Frederick Sumaye 28 November 1995 30 December 2005 CCM
    Edward Ngoyai Lowassa 30 December 2005 7 February 2008 CCM
    Mizengo Peter Pinda 8 February 2008 CCM

    ReplyDelete
  15. MICHUZI HUU JAMAA MBONA KAFANANA NA KIKWTE ?

    ReplyDelete
  16. Sawa, wingine ndio! Hatufuatilii sana maboya siasa lakini nyie mnaosema kama hatumbuki mnaweza mkaelezezea zaidi?

    ReplyDelete
  17. Nahisi kati ya hizo kura mbili za hapana,moja itakuwa ya Lowassa

    ReplyDelete
  18. Goddam! Now we have a Handsome President and an Ugly Prime Minister!

    ReplyDelete
  19. ebwana

    Mwanaume ni Mkapa kaona BOT inakuja juu, akajitupia hapo kenya kusulihisha mgogoro by the time anarudi kuna ya lowassa mnasahau BOT hata pongezi hajatowa nimekubali mjanja kweli mzee mzima

    William

    ReplyDelete
  20. Sasa huu mwanzo tu je tume ya wakina kabwe ikimaliza kazi watajiuzulu mawazili wengine wangapi? Je scandal ya BOT itawanusuru wakina Meghji na wengine? Mimi naona Kikwete na bwana Pinda waje na sura mpya kabisa za mawaziri. Wasiwepo wa zamani hata mmoja maana wote ndio wale wale. Utavunja leo, kesho tena scandal zitawarudia.

    ReplyDelete
  21. IZ HE SINGLE ??

    ReplyDelete
  22. wewe pa-1 namna gani, kwani kila aliyekuwepo ktk serikali ya awamu ya 3 si safi? Kama unaamini hivyo, unatakiwa kusema pia hata mteuaji naye (Kikwete) tulifanya makosa kumchagua maaan alikuwa kwenye awamu ya 3.
    Hakuna mtu safi, ila wapo wenye unafuu kama huyo Mizengwe iliyopinda. Hata JK Nyerere alipokuwa anampigia debe Mkapa alisema katika wagombea wote BWM anaunafuu. Hivyo hakuwa 100% clean

    ReplyDelete
  23. Hongera Pinda.

    ReplyDelete
  24. Mhe. Pinda. Umeingizwa kwenye nafasi uliyo nayo sasa hivi kwa NGUVU ya UMMA. Usilisahau hili. Utumikie UMMA huo kama ulivyoahidi, nao utakuenzi. Ukifanya kinyume, si ajabu UMMA huohuo ukakutapika. Sasa ni wakati wa kujenga nchi na kuweka maneno na sifa pembeni.

    Kila la kheri Tanzania. Tunaomba Mungu yanayotokea Tanzania yapeleke amani na maelewano kwa jirani zetu wa Kenya na nchi nyingine zinazotuzunguka. Hongera Watanzania.

    ReplyDelete
  25. Haya tena mnaowania uwaziri sifa ni hizi hapa:
    1. Usiwe muongo kama Karamagi
    2. Usiwe mwizi kama Balali
    3. Usiwe mbishi kama Zitto
    4. Usiwe na makelele kama Makamba
    5. Usiwe mbabe kama Sitta
    6. Usihukumu kama Mudhihiri
    7. Usiue kama Ditopile
    8. Usidandie hoja kama Mrema
    9. Uwe na huruma kwa nchi kama Dr Slaa
    10. Usiwe na tamaa kama Lowassa

    Haya tena tumeni sivi zenu upesi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...