rais george w. bush wa marekani na baraza lake la mawaziri

Michu,
Ukitazama kwa makini idadi ya kabineti ya Rais George W. as we call him in the U.S utaona ni namba ndogo lakini yenye ufanisi wa hali ya juu! ;
1. Je ,Tanzania haijaweza mpaka leo tangu ipate Uhuru kufikia uamuzi wa wizara ngapi ziwe ni "kiwango kipimo" yaani (standard) cha kutosha kwa ufanisi wa Maendeleo yake?
2. Je, Rais wa Tanzania mbona hatumii Nembo yake ya Urais kama inavyotumika kama ya Rais wa U.S?
Ukiangalia kwanza utaona kanembo ni kadogo sana. Kila mahali Rais anapokwenda kutoa hotuba ni lazima nembo hiyo iwepo kwenye podium au meza anayosimamia rais kuzungumza!!!
naomba uniwakilishie mjadala huu...

Mdau, North Carolina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Jamani mimi niko USA lakini mbona tunajipendekeza sana. Bush kaondoka USA kuja Africa lakini nobody knows about it. Acheni ushamba akija mheshimiwa siyo kwamba hali itabadilika hata kidogo....acheni ubishi. No one cares for Africa in this end but Africans. Siyo Yesu au Mtume. lakini he is the most powerful man in the world...I agree lakini ni ushamba mtupu mpaka JK

    ReplyDelete
  2. Wewe unayetaka waweke nembo kwani Picha zao zitawekwa wapi?...mbona hujiulizi kwa nini kila Ofisi nchini ina picha ya rais Ukutani utadhani yeye ni Sultan.
    Huo ndio Urithi wa Ujamaa kumtangaza rais kwa kila njia.

    ReplyDelete
  3. Sioni nini serikali ya Bush ilichofanikisha kwa raia wake, I mean American tax payers zaidi ya majonzi kila siku. Kama serikali ya Bush yafanya kazi kwa ufanisi, kwa nini hadi leo New Orleans bado wanahangaika? Watu hawana nyumba, shule wala sehemu ambayo yapasa kuishi binadamu. Serikali ya Bush inashindwa ku-provide huduma ya afya ya bure kwa kila mwananchi wake. Kama wewe huna kazi ya maana au ya kukupa kipato cha kuweza kujilipia huduma za afya basi huna tofauti na wabongo. Asie na kazi ndio basi tena. Serikali imeshindwa kuwapatia nyumba hao wanajeshi waliotoka Iraq kwa sababu za magonjwa, hebu niambie hiyo kweli ni serikali bora??? Tembea ndugu yangu Scandinavia au nchi tajiri western Europe ndio utajua kweli kuna marais wa dunia wanaojua kufanya kazi kifanisi. Sie huyo Bush, au kwakuwa anajua kupigana vita? Mie Marekani hata kwa rungu siji kuishi, kwanza ni dhiki tupu, mwisho wa mwezi ukifika mshahara wote waishia kwenye bills, na kama utabakia na pesa basi ujue umefanya udanganyifu huko ndio ukapata pesa nyingi zaidi. Wamarekani kuuwana kila siku. Maisha magumu yamewachanganya wamarekani akili.

    Asante sana kaka Michuzi kwa kazi nzuri.

    Oxford University - UK

    ReplyDelete
  4. Ninachojua mimi ni kwamba pale anapokwena Rais wa Tanzania anakuwa anasindikizwa si na nembo ya raisi, bali na jamaa mmoja alivalia magwanda kabisa ya kijeshi yenye nembo kibao.....

    ReplyDelete
  5. Mleta hoja, samahani nisije nikajikuta ninatamka visivyo juu ya ushauri au maswali yako isivyo kawaida yangu.

    US haijawahi wala kamwe haitakuwa kipimo cha uendeshaji wa serikali za dunia yote wala haiwezi kuwa hata mfano wa lazima wa kuigwa katika uwasilishaji wa alama za utambulisho(mfano nembo n.k)

    Ingawa nakubali kuwa baraza letu la Mawaziri bado ni kubwa kidogo (yaani lingeweza kupunguzwa zaidi), kamwe sikubaliani kuwa sasa tujiwekee namba fulani inayofanana na ya US ndipo tuonekane kuwa tu wafanisi.

    Ndg. yangu ufanisi (both Allocative efficiecy & Productive efficiency) inapimwa kwa vitu vingi sana sio tu uchache wa Mawaziri.
    Hivi unajua hao jamaa wanatumia kiasi gani cha fedha za bajeti yao kutengeneza siraha, kwenda vitani na kujilinda (isivyo lazima) kwa kuishi maisha ya hofu?

    Hata kama wangekuwa na waziri mmoja tu, kitendo cha kwenda na kuanzisha vita Iraq kwa visingizio visivyo vya kweli na bila hata kuwasikiliza UN na sasa kusababisha mauaji ya watu (Wairaq & Wamarekani na washirika wake) ambao mpaka sasa idadi yake haijulikani kamwe hakitasahaulika na ni imani yangu kuwa siku moja watu watafikishwa katika vyombo vya haki kujibu hayo.


    Ukubwa wa Baraza la mawaziri utafuatana na mahitaji yetu halisi(ambayo yanaweza kuwa yanabadilika kutegemeana na mabadiliko mbalimbali) na pia miundo yetu ya utawala na majukumu ya mawaziri kama ambavyo tunaona inaleta ufanisi na si kwa mujibu wa utaratibu wa US!

    ReplyDelete
  6. Huyu mdau wa OXFORD naona anahitaji kwenda TUMAINI ili aelimike vizuri. Pamoja na kudai kwamba yuko uko OXFORD bado anashindwa kutumia resources zinazomzunguka kuangalia emigration ya waingereza to "GREENER PASTURES" abroad? Waingereza ni wajanja kuliko wewe.. Kawaulize wakueleze why statistics za emigration zinazidi kuongezeka.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  7. Mtoa mada nafikiri picha yako ina affect your logical way of thinking,mimi nasoma uingereza nanimetoka kufundishwa how American system works.Umesahau kua USA ni kubwa,ina states tofauti na hizo states zina governers ambao wana separate rules from the federal state,kwahiyo ukipiga hesabu ya hao mawaziri plus governers unajaza diamond jubilee(i'm only joking)but my point is you cannot compare a big state like America with Tanzania,nchi yetu ni mtoto ukilinganisha na USA kwahiyo lazima viongozi utawaona ni wengi wakati kumbe the number of cabinet ministers is directly proportional to the ministerial position available lakini kwa vile tunawaona mara kwa mara tunaona wengi.Ma gavana wanaoneka kukitokea disaster au campaign za kura wengine i'm sure hata huwajui na unaishi huko US.

    ReplyDelete
  8. Usifananishe serikali ya US na ya TZ ni vitu viwili tofauti. Hao wana states ambazo zinajitegemea mpaka katika sheria, ndio maana utakuta kwenye states hii sheria ni tofauti na states nyingine. Sasa hiyo ni central govt ambayo inaangalia kwa ujumla masuala ya United States na katiba yao. Lakini hilo li muungano wa states lilivyo kubwa kama wangekuwa wanafuata mfumo wetu wa utawala sidhani kama nao wangeweza.

    Msipende kulinganisha vitu vilivyo tofauti kabisa!

    ReplyDelete
  9. Hili ni somo kwa JK.

    Ebu JK piga hesabu kwa harakaharaka: US with the land that is more than 30 times larger than TZ and with a population that is 10 times larger than TZ (Hapo bado hujaweka idadi ya illegals) has the cabinet which is half that of TZ. How do you interpret this?

    It is not too late to make changes bro!!!!

    ReplyDelete
  10. Natoa pongezi kwa Mr. Michuzi. Nasoma sana sana kuhusu Tanzania kenu blog ya kwako. Nafikiri rias kutmie nembo inatigemea system ya nchi pia preferences.

    Asante sana sana Michuzi.

    Mungu bariki Tanzania na watu yake.

    Mzungu
    Chelteham - England

    ReplyDelete
  11. Sasa ndugu wadau mnaofanya comparison ya baraza la mawaziri wa bongo na kulinganisha na ukubwa wa baraza la mawaziri la US na hapohapo mkasema kwamba kwa kua US ina tawala za "states" tofauti na kusema kwamba kwa sababu hiyo basi mnapata conclusion kua baraza la TZ ni dogo, Mimi nafikiri mnasahau kitu kimoja muhimu. TZ kuna ngazi kibao za utawala, kuanzia serikali kuu ambako ndiko kuna mawaziri na manaibu hamsini na kitu; Jumlisha na makatibu wakuu zaidi ya 20. Hapo bado hujaweka wakurugenzi wa wizara maana kila wizara ina idadi kubwa ya watu hawa (say wakurugenzi 20 kila wizara x 20 unapata wangapi?). Then from there uje sasa katika tawala za mikoa. Hapo ndio unaweza kufananisha mikoa kama "states" za US. Huko utakutana na Mkuu wa mkoa ambaye anatambulika kama ni Rais wa mkoa. Huyu mkuu wa mkoa ndio unaweza kumlinganisha na Gavana wa majimbo (states). Then huyu mkuu wa mkoa ana mlolongo mreeeefu wa wasaidizi amba nikiwalisti hapa ntakua najaza blog ya michuzi. Mwishoni kabisa katika listi ya mkuu wa mkoa unamkuta katibu tarafa, then diwani, then balozi, then wengine wengi ambao siwezi kuwakumbuka kwa harakaharaka.

    Hivyo basi, mimi naungana na watoa hoja ya kwamba serikali yetu imejaza sana watu ambao wanaongeza gharama kwa walipa kodi. We angalia nafas hizi mbili; Makamu wa Rais na waziri mkuu... Unaweza kuniambia kwa sasa hivi hapa kwetu TZ hivi ni kweli tunahitaji kuwa na makamu wa rais? I think ingekua bora kuvunja cheo iki maana nacho kina mlolongo mkubwa wa watu wa kumpa tafu makamu wa rais ambao ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi.

    ReplyDelete
  12. Kikwete ni kijana mwenzetu lazima tumsaidie kwa mawazo ili afanikiwe zaidi na uozo wote ulio ota mizizi huko nyuma kwa manufaa ya waliozaliwa ili kutawala wengine mpaka mwenyezi Mungu awachukue uozo huo ung'olewe na kutokomezwa kama magugu mashambani.NI KWELI KWAMBA BARAZA 'JIPYA' LA MAWAZIRI BADO NI KUBWA KULIKO ILIVYO STAHILI.Bila shaka anatambua kwamba UKUBWA WA PUA SIO WINGI WA KAMASI.Na Panya wengi hawachimbi shimo.Baraza lile la Mawaziri lipunguzwe hadi lifikie hadi Mawaziri angalau 20 kwa sasa kama siyo chini ya hapo.Miongoni mwa Mawaziri walioteuliwa karibuni bado wamo wenye kukabiliwa na tuhuma za ufisadi.Bado wamo ambao wamekuwemo toka utawala wa Nyerere,WHY?Hatuna watu wengine waadilifu na wenye uwezo zaidi ya hao kila kukicha wao ndiyo wateule?Mawaziri wengine hawafai na hawataziweza Wizara mpya walizo kabidhiwa.Wanajulikana wazi.Wizara za Viwanda,Nishati,Madini,Mipango na Fedha zimekuwa zikipewa Sura za ajabu ajabu tu,sijui kimshiko au vipi.Mageuzi gani yatakayo patikana na viongozi wa aina hiyo?Hivi ni lazima Waziri atokane na Wabunge?Is it the rule of the Thumb?Hata kama tuna Watanzania wenye upeo na uwezo mkubwa zaidi wa uongozi waliopo nje ya Ubunge au wigo wa siasa?Ni lazima atoke Chama Tawala katika mazingira yetu ya Kitanzania?Au tunafuata mkumbo tu bila kujua madhara yake katika muda mrefu?Hivi kweli kuna sababu zipi zinazo mfanya Kikwete awateue watu waliokwisha chaguliwa kuwa Wabunge na kuwafanya wawe Wakuu wa Mikoa sehemu zingine zilizo mbali kabisa na majimbo yao ya uwakilishi na kutarajia watazifanya kazi zote hizo mbili zenye majukumu makubwa na mazito ya kila siku kwa ufanisi unaotakiwa?Au vyeo vinatolewa kama zawadi hapa nchini bila kujali athari zake?Bila hata haja ya kujilinganisha na nchi kama Marekani nafikiri ifikie mahala viongozi watambue kwamba Watanzania wa kizazi cha leo sio maamuma au mazumbukuku.Wanatambua ujinga wote unaofanywa na viongozi wao wenye upeo unaoishia ncha za pua zao!Ni vyema wajirekebishe wenyewe kabla ya kuumbuliwa na watoto wadogo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...