mtangazaji mahiri wa michezo wa clouds 8.44fm ibrahim masoud 'maestro' (pili kulia) akiwa anakula stori na masupa staa wa soka wa enzi hizo. toka shoto mohamed hussein 'mmachinga', edibily lunyamila na thomas kipese. wachezaji hawa wote wanajishughulisha na kusaidia vijana kukuza vipaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mzee, Michuzi, big up for the pic. Mimi kama kijana ninayependa kabumbu na mshabiki mkubwa wa Yanga, nimekulia nikiwaangalia hao - Chinga, Lunya na Kipese. Yaani leo umenikumbusha mbali, hasa Yanga walipochukua kombe la Afrika Mashariki na Kati. Kizota yuko wapi jamani?

    ReplyDelete
  2. jamani mbona hao kinakaka wazuri hivyo lakini hawawezi kuchomekea mashati????jamani ustaarabu kidogo basi
    ili wadogo zenu waige!!

    ReplyDelete
  3. katika wote hao, kipese alikuwa winga teleza, nilimkubali, mohammed hussein alikuwa anasubiri mipira ya kukutana nayo apige manduki, lunyamila sifa nyingi mpira mdogo

    ReplyDelete
  4. Wanasaidia Vijana gani? Wana Ofisi zao ambazo tunaweza kuwasiliana nao? Halafu mdau hapo juu umeliza kuhusu Kizota, ni kuwa Kizota hatunaye tena. Alifariki baada ya Kugongwa na daladala akitoka taifa kucheki mechi ya Taifa Stars na Ghana

    ReplyDelete
  5. Hi Bro Michuzi, kama alivyo sema hapo juu jamaa, yaani umenikumbusha mbali sana kuweka picha za hawa vinara, kuhusu kandanda la bongo, hasa jamaa huyo Mzee mzima mheshimiwa Lunyamila, nilikuwa nampenda sana alivyokuwa akikung'uta ball. Ninawasalimu sana tena sana wazee waheshimiwa. Mimi kama mshabiki wa Yanga ninawashukuru kwa yote waliyo yafanya. Pia jamaa ameuliza hapo juu kuhusu, Kizota yupo wapi? Sio alisha fariki? Sina uhakika kamili ila nilisikia hivyo.

    ReplyDelete
  6. Kizota tumeshamzika.....huyu mohamed hussein mmachanginga alikuwa balaa...yani mpaka leo yanga hatujapata natural striker kama mmachinga...maana mnaweza usimuone dk 60 uwanjani lakni ukija kumuona ni wakati anashangilia bao alilofunga...sana sana mmachinga

    ReplyDelete
  7. Anon wa kwanza (juu kabisa, Saidi Mwamba Kizito hatunaye tena duniani (RIP).Hapo katika picha huyo Thomas Kipese (uncle Tom), namkubali haswaaa, hiyo ilikuwa winga ya maana we acha tu. Lunyamila chenga nyiiiingi (mchoyo sana), sifa tu ila soka la maana hakuna, Mohd mmachinga yeye ni magivu meeeengi akili kidogo kwenye soka!Ila watabaki kuwa katika kumbukumbu za soka tanzania!

    Bablii

    ReplyDelete
  8. ndugu hapo juu uliyeuliza kizota yupo wapi....dah imeniuma ila aksante mchuzi kwa blogg coz namjibu kuwa KIZOTA MWAMBA SAID alishatangulia mbele ya haki(NI MAREHEMU) kwa sasa ...ingawa sina hukakika wa Lugha niliyoitumia...Marehemu au HAYATI.SORRY

    ReplyDelete
  9. we anon wa juu nadhani humjui lunya kipindi kile yanga wametoa kombe la afrika mashariki lunya alitisha mpaka mashambiki wa nchi nyingene walimkariri mashindano yalivyoanza tena mwaka uliofuata alisajiliwa simba kwahiyo aliichezea simba.basi la simba lilivyofika wakamuona mashabiki wote wakaanza kuimba jina lake (lunya lunya lunya)alafu wewe ndo unasema mpira mdigo aacha utani wewe.ukisikiwa uarabuni unanyongwa

    ReplyDelete
  10. we unaesema lunyamila mpira ulikuwa mdogo sijui unamzungumzia lunya yupi,nenda kampala leo halafu ulizia habari zake.

    ReplyDelete
  11. Nyie wote mnaomkandia Edibily Lunyamila hamjui mpira naona mlikuwa washabiki wa kusikiliza redio tu,ila kama mlikuwa mnaenda pale neshno stadium msingesema huo utumbo wenu,TZ mpaka leo hatujapata winga kama huyu,pia winga ndio kazi yake kukaa na mpira ili washambuliaji wajipange golini kabla hajamimina majalo(cross)ili watu wacheke na nyavu.
    Nawakumbuka hawa wachezaji kwa kuchezea timu zote mbili kongwe za bongo (Yanga na Simba) kwa vipindi tofauti Yanga na

    ReplyDelete
  12. hao jamaa walikua mwisho,ila jamani nauliza hivi kwanini wachezaji wakibongo soka linakufa mapema yani wamejitahidi ni miaka 4 ona hao jamaa walicheza na nonda lakini mwezao bado yupo kwenye dimba wao imebaki histori tu nini hasa tatizo bongo

    ReplyDelete
  13. KINACHONIFURAHISHA ZAIDI HAPA NI KUWA HAWA WACHEZAJI WOTE WALIANZA KUCHEZEA YANGA KUTAFUTA MAISHA NA MWISHO WAKAFUATA MAPENZI YAO KWA KWENDA SIMBA....HUYU MEASTRO NAYE SIMBA BLOOD...

    ReplyDelete
  14. kaka hapo juu ndio mliokuwa mnampa sifa nyingi lunya bila mpangilio, mpaka akaondoka kwenda kujaribu kucheza bundesliga ujerumani, hehehe bundesliga utachezaje striker una kilo 60? unatafuta kuumia bure, mpira kwetu upo lakini sio serious, afya za wachezaji wa afrika mashariki mzozo!

    ReplyDelete
  15. Mohammed Hussein Daima "Mmachinga", Edibilly Jonas Lunyamila "Lunya" na Thomas Mourice Kipese "Uncle Tom". Yani hapo Simba akiingiza mguu Tatu aibahatika 2. Ilikuwa ni raha tupu. Watoto walikuwa wakali, fedha ilikuwepo. Watoto wkiingia Taifa utadhani Arsenal, Sharuks! Sharuks! Ah hebu mi niache nisije nikalia!!

    ReplyDelete
  16. Na kama wachezaji hawa wangekuwepo kipindi hiki ambacho wabongo wanaipenda timu yao ya taifa,nina imani huenda tungekuwepo Ghana .Hawa jamaa vipaji vilikuwepo,sikuhizi naona soka bongo hamna kabisa,Yanga limebaki jina tu.

    ReplyDelete
  17. Hawa jamaa walichezea Yanga kwa mapenzi makubwa yao halafu wakaenda Simba kumalizia kutafuta senti zao za pensheni.

    ReplyDelete
  18. Ni kweli kabisa kwamba wanaosema Lunya hakuwa na kiwango ni wazushi.Kama sivyo basi hawajui soka.Ni kweli hawa walikuwa wanaishia kumsikiliza Ahmed Jongo wa RTD akiwatangazia tu wala hawakuwahi kumshuhudia Eddy.Huwezi kuamcha kumtaja Edibily miongoni wa mawinga hatari sana waliowahi kuwepo Tanzania.Na napenda niungane na mdau aliyesema hatujawahi kuwa na winga ya kushoto kama Eddy.Huyu bwana alikuwa hakabiki.Mabeki wengi walipata tabu sana kumkabili Lunya.Wanaolijua soka la Afrika Mashariki wanatkubaliana nami kwamba Paul Asule wa Uganda alikuwa ni beki mahiri sana katika eneo hili Afrika Mashariki miaka hiyo.Lakini aliwahi kukiri kwamba katika maisha yake ya soka hakuwa kuadhiriwa na mshambuliaji yoyote katika ilivyowahi tokea kwa Eddy.Nina amini kabisa kama Lunya asingerubuniwa na akina Gulamali kufikia hatua ya kuacha zoezi la majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Ujerumani na kwenda kwenye pambano la watani wa jadi mjini Mwanza,basi angekuwa mtanzania wa kwanza kung'rara katika anga la soka la kulipwa barani ulaya.Mimi kama shabiki wa simba kwa wakati huo tukikutana na Yanga hakuna mtu alikuwa ananipa homa kali kama Eddy.Umaarufu wa washambuliaji kama kina Mohamed Hussein,Kizota,Tungaraza"boli zozo" na wengine nia matokeo ya kazi aliyokuwa akiifanya Eddy.Harafu leo mtu anatokea kumkandia.Acheni mzaha nyie!!! Yaani kama kuna kipaji ambacho kimetoweka bila kuleta matunda yaliyokuwa yapatikane,basi ni Eddy.Inasikitisha sana! Anyway,ndio soka la bongo!

    ReplyDelete
  19. Chuki binafsi yaifaiee tuiacheni jamani italeta tafarani jamaa walikuwa wazuri katika soka hakuna cha maguvu wala nini pia mpira unatakiwa nguvu sasa unakuta wachezaji wengine hata kumaliza nusu kuku na sahani ya chips wawawezi watawezaje kuwa na nguvu Mmachinga upo juu mtu wangu

    Katochi)

    ReplyDelete
  20. Kiboko ya lunyamila alikua Kassongo Athumani,

    Wakikutana ilikua ni kama Christian Ronaldo na Ashley Cole enzi zile yuko Arsenal,

    Palikua hapatoshi uwanjani.

    Kipesse alikua bishoo sana wakati Machinga alikua kiruka sna sama-soti pamoja na kitambi chake,

    Sijui siku hizi bado anaweza??

    ReplyDelete
  21. Wana-blog, yaani habari za Said Kizota zimenigusa kusema ukweli. Dah, sina la kusema. Sijui nilikuwa wapi...

    Na hao watu wanaokurupuka na kumuongelea Lunya kama walivyofanya, nawapa pole. Kaulize SA,Uganda na Kenya; jamaa amewakimbiza sana mabeki tokea yuko form 3 au 4, wakati huo bado mwili wake ni mdogo. Yaani mi' mwembaba kinoma, lakini baada ya kumuona Lunya akikimbiza mabeki nikapata moyo - na kuwakimbiza mabeki nawakimbiza sana tu.

    Huwezi 'amini Moh'd Hussein alikuwa anamweka Nonda benchi!

    ReplyDelete
  22. Hii picha inaonyesha tofauti kubwa kati ya watoto wa mjini na wa vijijini.Angalia mtoto wa mjini Tom alivyovaa tofauti kabisa na hawa ma-country boys lunyamila na chingaboy.Hata kama hujui watokapo utatambua tu kuwa Muokota korosho(chingaboy) na muuza matunda(lunyamila) hawajakulia dar.
    Halafu wanaosema Lunyamila alikuwa mchovu wana lao jambo.Huyu kipese alikimbia Yanga baada ya kusikia Lunyamila anasajiliwa sababu alijuwa atasugua benchi kwa sana.Na wanaosema kuwa lunyamila alikuwa ni mtoka nduki labda hawajui kuwa WAHA ni waendesha baiskeli(phoenix,Swala nk) kwa sana na huwa wanaziendesha kwa kushindana na kubishana ni jadi yao.

    ReplyDelete
  23. Hawa wote walikuwa wazuri sio Lunyamila peke yake.Si sahihi kusema kuwa ata akina Mohamed Hussein walipata Umaarufu kupitia Edibily.

    Mohamed Hussein ameanza kuwika akiwa Bandari ya Mtwara ambako Yanga na Simba zikicheza na Bandari wakati huo lazima zichezee magori na ndio maana majina kama Mohamed Hussein na Eddiphonce Amlima yalikuwa common kutoka pande za kusini.

    Kuna tofauti kidogo na Uncle Tom,yeye nadhani alianza cheza mpira zamani kidogo ukilinganisha na Eddibil.Amecheza mpira na akina Makumbi Juma na Hamis Gaga(Gagarino) na akina Sanifu Razzaro(Tingisha),Athumani Juma Chama(Jogoo),Salumu Kabunda(Ninja),Issa Athumani na Aboubakar Salim(Sure boy) to mention a few.

    Namkumbuka vizuri kwani mwaka 1993 wakati simba ilipokutana na Yanga walipigwa bao tatu kwa moja na mfungua mlango alikuwa Makumbi Juma,Lapili liliwekwa kimiani na Uncle Tom namlango wa mabao ulimaliziwa na Sanifu Razaro.

    Gaga alichezea Simba na kwa mara ya kwanza alikosa penati wakati Golikipa Patrick Mangwata akiangalia nyavu iliyochanwa kwa shuyi kali la Makumbi Juma.

    Ukweli unabaki palepale kwamba hawa wote walikuwa vinara.Chamsingi ni kuwa bado soka yetu hailipi sana.Waweza sikia mtu kama Eddibilly,Mohamed Hussein au Uncle Tom hawana ata nyumba ya kulala.Siku moja nilikwenda Bagamoyo nikakutana na Steven Nemes ambaye sasa anaitwa Aboubakar lakini maisha aliyonayo siyo ya mtu ambaye alikuwa ni tegemeo kwa Young African ya Dares Salaam.

    Nakumbuka wakati huo nilikuwa naipenda sana Pamba ya Mwanza TP LINDANDA.Ikiwa na akina John Makelele,Hussein Maisha,Razaki Yusufu,Fumo Felician,Ally Bushiri na Paul Rwechungura.

    Wakati huo Costal Union ilikuwa chini ya Idrisa Ngulungu,Ally Maumba

    Mpira ulikuwa unanoga ata ukienda Zenj utawakuta akina Ubwa Makame (mzungu),Rashid Tall,Innocent Haule,Gharib Ratto,Juma Bakari Kidishi na wengine maarufu.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  24. bongo watu wanaweza kukupa sifa mpka ukajiona ushakuwa star hivi hivi, hawa watu wanaomsifu lunyamila ndio waliosababisha kijana wa watu akajiona anaweza kucheza soka la kijerumani, na kusababisha akapoteza nauli yake buree! angejua angezama tu abebe mabox! mi napiga soka zaidi yao wote hapo lakini nabeba tu hapa! watu wa bongo wanaweza kukurostisha hivi hivi unaona, wanakupamba mwisho unaishia kijiweni cheki sasa yuko kijiweni hapo ni mizinga tu!
    aangalie asiwe kama aswile mlimba scania , mizinga ya kufa mtu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...