50 cent na tony yayo wakitoka kwenye mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliopita.

kwenye maongezi yake amesema ana hamu sana kutembelea sehemu mbalimbali kila anakokwenda lakini ratiba ya waandaaji inamzuia kuona vitu vingine zaidi ya uwanja wa ndege, chumba cha hoteli na jukwaa la muziki.

ameeleza mipango ya kurejea bongo kama mtalii na kusema ana hamu sana kuona kwa macho yake mbuga ya serengeti na mlima kilimanjaro ambao amesema anatambua hauko kwa watani wa jadi.

amesema kwamba atalitilia maanani ombi la mwenyeji wake joseph kusaga kusaidia kunyanyua vipaji vya wasanii chipukizi wa bongo kwa kuomba propoza za afanye nini.

amesema kwa sasa anaelekea london, kisha los angeles ambako ana mradi wa filamu kubwa anayoshuti na mzee mzima al pacino. hakutaja jina lake ila itamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

wadau wengi wamefurahi kwa ujio wa 50 cent na kundi lake lote la G Unit ila wameiwekea alama ya kuuliza idara za utalii, uwekezaji na kadhalika kwa kukosa kuichukulia ziara hii kama moja ya promosheni ya nchi, ikizingatiwa kwamba wenzetu sauzi walimpeleka sehemu kibao ambazo amezitangaza kinoma, na pia kumuamkia mzee madiba.

wamewaponda sana maafisa husika kwa kukosa kuonekana sehemu yoyote, ikionesha ni jinsi gani JK alivyo na kazi ngumu ya kuwaamsha watu hao katika kuitangaza nchi. wengi waliuliza Mungu atupe nini bongo, donda???

habari hii hii imakaaje wadau??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2008

    Kwa kweli kaka michuzi umesema kitu muhimu sana "Tanzania ipewe nini?donda?"
    Maana wasouth walivyo makini walimpeleka 50 cent kuangalia mgodi wa platinum(100km kutoka johannesburg) ili ajue bling zake anazovaa zinapatikana vipi?halafu wakampeleka soweto akaone historia ya south afrika hususan wakati wa ukaburu.sasa can you imagine sisi tumeshindwa hata kumpeleka bagamoyo(less than 50kms kutoka dar) ajue historia ya utumwa maana ma african american wengi asili yao ilitokana na biashara ya utumwa.tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni system mbovu serikali isiyo penda nchi.50 cent mwenyewe kasema katika mahojiano kuwa ratiba haimruhusu kufanya hivyo sawa ni kweli lakini ukiangalia kwa undani kama serikali ingepiga hili dili na tigo/prime time promotions sidhani kama ingeshindikana kuchepuka kwenda bagamoyo unless kama jamaa kweli alikuwa anataka kurudi zake haraka mno.ni kweli tungesema labda angedai malipo zaidi lakini kama kuna fun flani asingedai hivyo vijisenti maana 50 cent ana pesa yake na siyo kwamba kaja bongo kuzikusanya kaja bongo kwa mapenzi yake mwenyewe na ndiyo maana katika shoo ya south alipangiwa ku perfomr for 90 mins lakini watu wakapiga mayowe jamaa akapandwa na midadi akaongeza dakika 40 nzima za performance.
    mdau sauzi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2008

    Tatitizo la mifumo yetu ya kazi watu hatujipimi kwa mafanikio yanayotokana na kazi ila tunapimana kwa mafanikio ya nyumbani kwa wafanyakazi; mtu ana gari za kifahari, nyumba nzuri, nyumba ndogo bomba n.k. tungezingatia mfumo wakupimana kwa output ya kazi ya mtu, nadhani kila nafasi tunayoipata tungeitumia vizuri. Tanzania ni tajiri ktk vivutio vya utalii ila bado utangazaji wake ni mdogo sana. Huyu jamaa ni maarufu na kijana hivyo kama angetumiwa kuitangaza nchi vijana wengi ulimwenguni wangeitambua tanzania kwa haraka zaidi kuliko hata wanavyofanya mabalozi wetu. Siyo, siri mimi nipo ulaya lakini watu ukiwasikia wakizungumzia afrika yenye vitutio vya utalii lazima waitaje Afrika kusini. Wenzetu pamoja na kutangazwa na mandela lakini bado wajua umuhimu wa watu maarufu pamoja na michezo ktk kutangaza nchi. Siyo akina bush pekee yao ila hata hawa washikaji wataweza kutusaidia kuitangaza nchi. Nadhani hiyo ni challenge kwa watu wa utalii

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2008

    Jamaa wanauliza je wao watakula ngapi cha juu? Maana ndio washazoea!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2008

    tatizo ni CCM.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2008

    Ni kweli,watu kama hawa ni kuwavutia zaidi ili warudi na kuleta mpunga...aka mapesa.ingawa wengine wanayachota hayo mapesa na kuyaita vijipesa.
    mshikaji keshasema atarudi kama mtalii..ni ishara nzuri.
    big up kusaga na wengine,endeleeni kuleta vitu kama hivyo..ndugu zetu wa uganda na kenya wanaaalika sana hawa watu;sasa ni zamu yetu.

    big up michoouuuuzi kwa jitihada zako za kutuhabarisha.

    Mdau,
    Bergen,Norway

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2008

    Michuzi na wewe kwa lugha yako inaelekea unababaikia hawa wanamuziki kutoka Marekani sana.Kwani 50Cent ni nani zaidi ya mwanamuziki tu?Inawezekana Tanzania kujitangaza kwa njia zingine na sio lazima kupitia muziki peke yake.

    Tusiwalaumu sana watu wa utalii saa nyingine..wanafanya kazi yao..matangazo kwenye mabasi London,matangazo kwenye Cnn nk.50Cent wenzenu wanamjua kama mwanamuziki mhuni tu.Ndio maana kila siku analilia kuitwa kwenye kipindi cha Oprah mpaka akaanzisha beef naye.Kwa hiyo ninachotaka kusema ni kwamba kama Tanzania hawajajitangaza kwa kumtumia 50Cent..wewe Michuzi kwanini usiwasaidie?Wewe si mtanzania?Au ndio kusubiri mpaka mfanyiwe..do your part bro.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2008

    Wabongo kwa kupenda misaada.bwana.Eti 50cents ataSAIDIA(keyword) kukuza vipaji vya wasanii wa bongo.Hivi wabongo mtaacha lini kudanganyika kitoto namna hii huyu mtu ni mfanyabiashara anachotaka yeye ni ulaji sio kusaidia mtu.Fifty anafanya maonyesho kama haya na zaidi ya haya duniani mnadhani anajali kitakachoendelea mara baada ya kuondoka stejini?
    CHA AJABU- wabongo mnawapiga vita ombaomba wa katikati ya jiji na Wakati huo huo mnaomba misaada kama ombaomba.Anavyosema kuwa atawasaidia wasaidia wasanii wa bongo ni sawa na sisi wanaume kumwahidi demu vitu kedekede ili mradi umpige jiti.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2008

    We anonymous wa Tarehe May 05, 2008 12:41 AM inaelekea ni mtu mnoko fulani kwa kizungu wanasema nerdy au straight headed! sababu unampangia michuzi namna ya kujadili maoni yake wakati upo katika blog yake.
    kwanza naomba kukusahihisha michuzi hajasema kuwa ni lazima kwa Tanzania kujitangazakwa njia ya muziki.
    kama una macho,masikio na uwezo wa kuelewa nadhani utajistukia kuwa unachemka kumkosoa michuzi namquote
    "wadau wengi wamefurahi kwa ujio wa 50 cent na kundi lake lote la G Unit ila wameiwekea alama ya kuuliza idara za utalii, uwekezaji na kadhalika kwa kukosa kuichukulia ziara hii kama moja ya promosheni ya nchi"
    amesema wadau wengi wameweka alama ya kuuiza idara za utalii....
    mjumbe hauwawi wewe!
    michuzi achana na wasafisha vinywa endelea na moyo wako mzuri wa kutupa latest kutoka bongo!
    isitoshe huyo senti hamsini kuja bongo ni kitu kizuri katika kujenga ramani yetu hata kama ni mwanamuziki mhuni(according to you)lakini he is big so coming to bongo kuna impact kubwa tuu
    "Hate it or love it" he is still on top!keep on hating!
    mdau sauzi!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2008

    Inaonekana tatizo ni system ya nchi; inaonekana hakukuwa na ushirikiano kati ya watu wa TIGO na wizara ya utalii. Huku ughaibuni makampuni mengi hutangaza bidhaa zao kama COCACOLA kwa kuwatumia "maselebrite". nashauri kuwe na policy (ya nchi) itakayowezesha mkakati wa kuwatumia watu maarufu (maselebrite)kuitangaza nchi yetu kwa kuwaalika kuja kutembelea sehemu zenye vivutio nchini kwetu. Isiwe wanamuziki tu ( yaweza kuwa watu wetu wizara ya utalii wamemchukulia 50 cent kama mhuni tu kwa kuwa ni mwanamuziki, kitu ambacho ni makosa walipaswa kujali umaarufu wake, proximity yake na media na pia influence aliyonayo na waondekane na dhana potofu kuwa muziki ni uhuni kama remmy ongala alivyowahi sema kwenye moja ya nyimbo zake). pia isiwe wanamuziki tu; wizara kwa kushirikiana na makampuni kama TIGO, CELTEL, KAMPUNI YA BIA na KAMPUNI YA SIGARA wawe na utaratibu wa kuwakaribisha watu maarufu wenye ukaribu na media kama Oprah,David beckham, lewis lennox, dezel washington na wengineo wengi. ieleweke kwamba hawa hawaji ku-perform hivyo serikali ikubali kuingia gharama, lazima tukubali kutumia pesa ili tuweze kupata pesa hapo baadaye. na hao maselebrite waelezwe kuwa wamepewa mialiko hiyo ili wakirudi kwao watusaidie kuitangaza Tanzania.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2008

    watanzania tumezidi ushamba sana na ndo maana hata watani wetu wajadi wametuzidi hata kutuchukulia lugha yetu ya kiswahili kusema ni yao. 50 cent angetakiwa kupelekwa sehemu ambayo yeye mwenyewe angekubali na ndo njia kamili ya kuitangaza tz. imefika wakati sasa watz tuchangamkie tenda. next time mtasikia denzel anataka kuja kushoot movie mtamyima eti muda... hee lets wake up watz.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2008

    Huwezi kparamia marketing Strategy za watu kila kitu na wakati wake. Kama 50 analipa leo kesho je?
    Chema chajiuza chenyewe. Bush kaja hilo ni tangazo tosha, jay Z kaja. Tunachotakiwa kufanya kukuza utalii ni sisi wenyewe kuwa watalii pia. Mtalii si Mzungu au Mmarekani peke yake.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2008

    Bongo hakuna fosi kingi cheza drafti taratibu nyie wote walugaluga tu msizani mambo yenu ya utoto basi na sisi mabosi tuwapo!tutatofautishwaje?Who is Who?Chezeni ngoma ya kitoto,pia msitafute ujiko kwa nguvu ili gavumenti iwainue nanyi mtakua kama mafisadi katika nyanja yenu.Tulizeni bolu,fanyeni yanayowahusu yasiyowahusu waachieni wenyewe.shauri lako Isa hata ukiamua kutoposti lakini siku moja utafikisha ujumbe.Tchao!mie nilianza kwenye chipukizi,halaiki heshima kulia zote najua,shauri yenu!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2008

    hakuna kitu,ingekuwa 50cent anamapenzi kweli na africa,angekuwa anajua kuhusu sulivan maana huu mkutano ni wa marekani weusi wnaotaka kuinvest na kuitangaza africa,tumeona wanamuziki kibao wenye mapenzi na africa wakichangisha pesa kwa ajili ya mkutano utaofanykia arusha,tumeona wakina oprah,boyz 2 men na waigizaji kibao,labda kama ilikuwa nia ni yeye atembee au tumpe contact ya kututengenezea matangazo,lakini sio useme kaja kwa mapenzi yake.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 06, 2008

    Niwapongeze wote mliotoa maoni hapo juu! yote nimeyasoma na mengi yamebeba maana nyingi sana.

    Kila kitu na kila nchi zina mfumo wake wa ueneshaji, kama ilivyo majumbani kwetu pia ndio hivyo ilivyo. wachache wetu huwa tunakuwa na strategic plan za miaka mitano mbele na kuzivunja vunja katika malengo madogo madogo, na wengi wetu huwa tuna rapid plans ambazo kinachotokea sasa ndio hichohicho cha kutolea macho. Na ndio maana mtu akija na ubunifu wa kufungua internet cafe basi baada ya miezi mitatu zinakuwa 50, mwingine akianza biashara ya magari basi baada ya miezi miwili kuna showrooms 100.

    sasa niseme tu kuwa, wizara ya utalii kama wizara ina taratibu zake za kazi na plans endelevu za miaka kadhaa zikiwa zimevunnjwa vunjwa katika vipande vidogo vidigo. 50 cents ni kama mtalii mwingine yoyote na hawezi kupata attention ya wizara nzima otherwise tutakuwa watumwa. hivi ni ma celebrebrity wangapi wamekuja kwenye utalii kimya kimya bila hata ya sisi kujua? ni mpaka tusome kwenye website za nje ndio tunajua kuwa George clooney alipita serengeti, alipajuaje? sio wizara jamani? mimi nimeshuhudia John legend kaja bongo mwezi wa kumi 2007 kwa ziara ya UN akaenda hadi tabora kwenye Millenium villages (mratibu akiwa Dk. Sempeho wa UNDP) lkn sidhani kama iliandikwa kwenye press...bado siilaumu wizara kwa sababu tu imeshindwa kumkirimu 50 cents.....kama alivyosema ndau mmoja hapo juu, kuwa 50 ni mfanya biashara kama walivyo wengine, akiondoka hapa kashatusahau.

    sipingi kuwa wizara ina matatizo yake, lakini siafiki kama 50 cents anaweza kutangaza ramani ya Tanzania...Tanzania ni kubwa sana zaidi ya ma celebrity owte hapa duniani, sawa ni masikini lakini tuna rasilimali, tusijishushe hivyo, bali tuendelee na mipango yetu na sio (rapid decision) na tu improve pale kwenye mapungufu.

    Niwashukuru wote waliofanikisa ziara ya 50 cents, watu walioenda wame enjoy, na sisi tuliobaki majumbani tumefarijika kuwa sasa mambo yanabadilika kila kukicha.

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 06, 2008

    Anonymous wa Tarehe May 06, 2008 8:48 AM na wabishi wengine mimi bado nawapinga ukweli bado ni kwamba huwezi kufananisha 50 cent na john legend hata kiduchu.
    Tukubali kuwa this guy 50 cent ana influence zaidi ya mr ordinary people.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2008

    Nashukuru anon wa May 06, 2008 1:12 PM kwa maoni yako.. inaweza ikawa kweli kuwa 50 cents ni maarufu kupita John legend, lkn mimi nilitoa mfano wa hawa wanamuziki wanaokuja na sikuwa nataka kufanya comparison..na sidhani kama hapa tunabishana bali kila mtu anatoa maono yake kuhusu mustakabali huu, cha msingi ni kuwa kila mtu ana uchungu na Tanzania, na si ubishi wala ujuaji. Sidhani kama michuzi aliweka blog hii kwa ajili ya kubishana bali kuelimishana na kutoa mapendekezo na kuheshimu ya wengine pia.

    Mimi bado sidhani 50 cents is bigger than Tanzanian governement kupitia wizara yake ya maliasili na utalii na ndio maana nika mention hao waliouja toka huko mwanzo..ni wengi tena zaidi ya sent hamsini wamekuja kimya kimya wakaingia mbugani, wakaenda kui look zanzibar wakasepa kimya kimya, tunakuja kusoma kwenye web au kwenye E news katika interview zao kuwa wameshawahi fika serengeti, zanzibar na sehemu nyingne kadhaa za utalii.

    Sikatai kuwa wizara ina mapungufu yake tena yanaweza kuwa mengi, lkn kukurupuka tu kwa sababu ni 50 cents, tena hata kama wangemtembeza ingekuwa pleassure yake kutangaza ama la (si official).

    La, pili ni kuwa waandaaji ndio walokuwa wanajua ratiba ya mgeni wao, so ilikuwa juu yao wao kuihusisha wizara katika mpango zima wa ziara, ninadhani hata alipoenda south africa wizara ilikuwa approached na waandazi wa onyesho. Kumbuka kuwa hata hao waandaaji wanatafuta faida(stricly business) sasa wangeanza kumkirimu kupita kiasi obvious wangekula hasara maana si 50 peke yake, ni lazima wa accomodate timu yake yote..gharaa za chini kabisa za serengenti kwa mtu mmoja kwenda tena kwa usafiri wa gari kutoka dar hadi kule na kukaa siku moja si chini ya dola 800. sasa kwa show moja sidhani kama ingewalipa kuweza ku afford mambo yote hayo pamoja na kuwa na wadhamini.

    mi nadhani ifikie wakati tuwe tunaangalia vitu hivi kwa mapana,tutoe mapendekezo endelevu kwa wizara yatakayo lenga si mwanamziki mmoja bali watalii wote kwa ujumla maana wengi wa watalii tunaowalenga wengi wo sio ma celebrity, tuzingatie u-imla na sio individuals. 50 cents baada ya miaka mi 3 umaarufu wake ni huu huu? Tanzania je? I do still blv that Tanzania is bigger than celebrities who are coming to our country.

    Mungu ibariki Tanzania

    Nimalize tu kwa kukushukuru mdau ulie challenge maoni yangu, nayaheshimu maoni yako maana kila mtu ana haki sawa ya kutoa maoni ndani ya blog hii. Tunaelimishana, si ndio jamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...