Aiseee , issa.


Tafadhali mtafute huyo jamaa hapa watu wamechanga euro 126 maana miye nilikuwa kwenye tafrija fulani hapa niliingia kwenye mtandao watu wamecheka sana huwezi kukisia.
Basi nimechangiwa pesa hizo as such siyo kwa ajili ya matatizo ya huyo bwana ila for the joke of the year. maana watu wametafisiriwa kwa kila lugha (stomach!!!)


MWAMBIE HE MADE OUR WEEKEND THANKS MAY GOD BLESS HIM:
Ma'mdogo Ujerumani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2008

    mgawane, no discussion

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2008

    Lakini jamaa kachemka kwani sio ONE STOMACH bali SAME STOMACH au sio wadau?Unajua watu wengine kithungu hawajui!wao wanafikiria ni sawa na kingeredha akah!

    Kana Kane nyarubamba

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2008

    Huyu msela ametafsiri kiswahili moja kwa moja "Tumezaliwa tumbo moja"......kwa kiingereza amevuruga kabisa, sio sawa hivyo "born in one stomach" aha ahaaa! Lugha hiyo ngumu.

    JK - T. O.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2008

    Euro 126 / 3 = Euros 42. Kwangu, Kwako na Kwake, Kwangu kwa sababu nimesaidi Hisabati hapo.

    -BooSt3D.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2008

    Kana Kane nyarubamba kuzaliwa tumbo moja si Same Stomach, kibiolojia mimba haikai tumboni na hivyo hatusemi stomach (mfuko wa chakula) tunasema 'Womb' (tamka 'wum')
    waweza sema 'grown in the same womb' au 'born of the same womb'
    Inapendeza sana kijana alivyofanya, Ametimiza maana hata 50 angesoma angeelewa, mi tu ngeli ya kubambia na nimeelewa. Lugha ni maana na si usahihi!
    Apakati_ya_chembe_au_kidevu@yahoo.com

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2008

    Du!Huyu jamaa kanikumbusha stori ya 'My Milk is standing!,so big money you give me'.'Not flat flat'.Aise,mboona shida ndugu yangu?Born one stomach hiyo kali mze,sishangai Ujerumani kama walikufa mbavu!Aya,kidhungu mtadhungumdha wenyewe jamani?You can imagine how the unfortunate Tanzanians are desperate to forge ahead and be like anybody else no matter what!Usikate tamaa ndugu yangu ipo siku Kidhungu kitakubali tu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2008

    YAANI HIYO NIMEWEKA SCREEN SERVER KWENYE DESKTOP YANGU,KILA MTU AKIINGIA ANACHEKA HANA MBAVU SIKU YA JANA KILA NIKIMUANGALIA JAMAA ILIKUWA KICHEKO KWA KWENDA MBELE.WASHKAJI NDIO USISEME.THATS WHY I MISS MY BONGOLAND, WATU WANA VITUKO KIPAJI BWANA .BIG UP SANA JAMAA YAANI ANACHONIFURAHISHA JAMAA YUKO COMFORTABLE KABISA HANA SHOBO WALA NINI NA MASELA WAKE KWA NYUMA WANAMPA KAMPANI NA INAVYOONEKANA JAMAA WALIMSAIDIA HADI KUANDIKA.PEACE MICHUZI.
    DANNY MWANDUPE,INDIA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2008

    Cut it Short, Few Questions to ask ?

    Do we really understand the HIP HOP and RAP music in its entirety.

    Does the trip serve its purposes, improving the music talents of our own and Tanzania image abroad or a pure performance stunt on our part?

    Following recent flogging of HIP HOP performances from revered US Hip hop artists in Tanzania, do they really understand a little bit of us as people, culture, music and general aspect of our life. The reason I am asking this question(s), is because many of our Rap stars are not rooted the same way as Majority of their counterpart in US, ie. Ghetto life, total isolation from establishment, institutionalized/branded projects, different cycological and mental background, different way of thinking. So, are we the fans and our stars idolizing something blindly or we have firm understanding/knowledge of all these characteristics ?

    For the super stars from us, it is definitely they see a raw talent and creativity from our own, complementing their music, and that to them it is purely a market/franchise ploy to exploit, And I must say YOUTUBE and INTERNET play a bigger role on this. Now, from our own perspective, Our talents and stars, are they getting the same fan base, record sales, public exposure in the US, similarly or fractionaly of our US counterparts, or again is just a total business in Balance, probably will force to complain to World Trade Organisation(WTO)...LOL!!

    Or are we just imitating our counterparts achievement on this dip rooted music, just for the money, pride, talent or blind following. How does that relate to our own music ?

    Most importantly, where are we heading from here ?


    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2008

    duuh, wadau huyu jamaa unaweza kuwa sahihi endapo tu, kama "one stomach" ni jina la mji fulani example i'm born in dar es salaam at muhimbili hopital, hayo ndio matumizi ya ""born in"".you never know labda kuna mji unaitwa "one stomach"

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2008

    huyo jamaa anayejiita Mchangiaji amebwaga ung'eng'e hapo ili iwe nini sasa? Halafu stori zake kama za Kala Pina hivi? Tatizo bangi za chooni.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2008

    JAMAAA ALIKUA ANAJARIBU KUOMBA MTAJI KWA 50 BAHATI MBAYA HAJAMUONA ANGEMCHUKUA HUYU.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2008

    Oya Michu mbona huyo jamaa kama vile mnafanana sura? sio ndugu yako kweli huyo? hebu muulize fresh inawezekana mkawa ndugu mliopoteana kwa muda!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2008

    Anon 10.15, umesahau moja ya "go one by one.." (mtu anatoa directions hapo). We mchangiaji unaboa kama nini funga domo lako, alaa! Wewe unataka kuanalyze kila kitu una matatizo gani wewe, stop being so uptight.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2008

    Mchangiaji ananibore sana tu leo wacha niseme...kila siku unaandika kidhungu huku...hii blog ya waswahili...Kusoma kiswahili ujue lakini kuandika usijue .....ehhh bwana...samahani bwana lakini penye ukweli pasemwage.

    Wewe kama ujumbe wako unataka ufikie watu andika kiswahili...Wewe umeshaona huku watu wanasema Me and 50 born in one stomach ......sasa unategemea watajua hisho kidhungu chako...You are wasting your time my dear.

    Kwanza hata tunaojua ung'eng'e nikishaona mtu ameandika kwa kidhungu na skip....Niko na wadhungu 24/7 huku ...nikiingia huku nataka kusoma na kuandika na waswahili wenzangu sasa wewe tena na kidhungu chako...ndio iweje??? Aaaaa bwana acha hizo....

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 05, 2008

    Logic connection.Proof by Conter examples:If 2*2=square of 2=4
    Then 3*3=square of 3=9.
    Hao ndo watanzania.Mfano mmoja wanaconclude na kutangaza.
    Hudhurie tu miziki musiojua maana yake ila msiadike au kuimba hadaharani mtaumbuka.
    Uhuru na Kazi.
    Hekima ni Uhuru.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 05, 2008

    nimemzimia huyo kijana, alisahau sentensi moja, kwamba yeye na 50ct blood blood!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 05, 2008

    Mhindi aliwahi kuanguka kazini akazimia mhindi mwenzie akaniuliza kwa kiingezreza nimwambie kilichompata yule mhindi mwezie wakati kiingereza sijui sana.Ikabidi nitafsri neno moja moja kwanza kabla ya kumjibu.Nikajua

    "Kazi" kwa kiingereza ni "JOB"

    MIA kiingereza ni "HUNDRED"

    kwa hiyo "KAZIMIA" kwa kiingereza itakuwa ni "JOBHUNDRED"

    Nikamjibu JOBHUNDRED sir akaondoka akijua kuwa mhindi mwenzie kachoka tu kwa kufanya kazi mia moja akaacha mhindi mwenzie amezimia katoa macho kama chura na mimi nikaondoka zangu vibarua wenzangu wakinisifu kuwa najua kiingereza si mchezo pamoja na kuwa kibarua kwa mhindi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 05, 2008

    Kama kweli kachangiwa pesa mpeni MSHIKO wake, maana yeye hakuogopa kuvaa hilo Tangazo wenzie waliona aibu.Amefanya kazi ya Entertainment bila kujua,kasaidia AFYA za watu wote waliocheka na kuinjoi this.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 05, 2008

    kuvuruga kwa mdau ndiko kulikomfanya ajinyakuliye euro 126 big up.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 05, 2008

    BTW, KWA ATAKEPENDA, nenda MEDIATAKEOUT.COM Ukaone vichaa wa Africa(ANGOLA) walivyomrukia 50CENT NA KUMPORA CHENI JUKWAANI. hiyo ni Gossip Web ya African-american.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 05, 2008

    MCHANGIAJI UMENIBOA,SIO KWA SABABU UMEANDIKA ENGLISH,SABABU SINA MATATIZO NA HIYO LUGHA,LAKINI SIPENDI WATU WANAOCHUKULIA KILA KITU IN NEGATIVE WAY,KILA MTU ANGEKUWA KAMA WEWE,TUSINGEPATA MAENDELEO YOYOTE...DAH HUYO KAKA KANIACHA HOI!!!!MA MDOGO UK

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 05, 2008

    jamaniee mwacheni mchangiaji wa watu labda ni shemejie na Michuzi kutoka Uganda au ni mtani wa Jadi sasa kiswahili hakipandi inabidi ateme ung'eng'e. Au pengine huwa anadesa mahali sasa kuanza kutafsiri inakuwa kazi kwake inabidi a cut na ku paste, maana sina la ziada la kusema haiwezekani hata mazungumzo ya utani ya kiswahili yeye awe siriasi na kidhungu, pengine hana bandama mwenzenu! My stomachi yake haina bandama ndio maana hajacheka hicho kituko kaenda kuleta desa.

    Mhu huyu mchangiaji lazima atakuwa mwanafunzi tu hapa anafanya mazoezi ya kuandika kwa ili akiandika desetashion yake awe ameshaweza kidhungu! Maana haiwezekani kila siku yeye mchango wake kama sehemu ya desetashion au essay ya darasani! Mwe unisamehe mie when I got out of my mom 'stomach' I forgot my brain in her bandama, I came out with two bandamas one in my stomach another one in mai hed!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 05, 2008

    We wachawi utawajua tu, ndo hao wanokula watu! "MGAWANE, NO DISCUSSION" Kwani wewe nani mwenye kauli ya mwisho? uchoyo tu! Kwani Ma Mdogo umemuona ananjaa sana au tapeli? hanuki shida na ndio maana kataka atafutwe "STOMACH" akabidhiwe. Ndo nyie hata mtu akikuuliza njia mnataka mganjiwe. Njaa tu, mtakufa mkila!!!!!!!
    Michuzi usiitie kapuni hii maana watu kama hawa wako wengi wasoweza kusaidia wenzao wala kufikisha amana ya mtu, nawakome, ntawacharaza bakora humuuuu!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 06, 2008

    TVZ Kicartoon asante kaka mimi ndie nilieandika kuwa''mgawane no discussion''nashukuru katika watu 22 ni wewe tu ndio umeona kosa hilo,UKWELI NI KUWA SIKUELEWA MESEJI KUTOKA MAMTONI,NILIFIKIRI YULE NDUGU AMECHANGIWA HELA NA HAKUWAZA KUMTUMIA 'STOMACH' sikuona sentensi kuwa amemwambia michuzi kuwa amtafute yule jamaa!! na ndio kukoleza nikamweleza wagawane nikimaanisha kuwa amatafute mr.stomach, bila kujua kuwa alimaanisha the same issue!

    Thanks for your lovely comment, though umeenda mbali, lakini pia imenifundisha kutokuwa judgemantatal maana kuna wakati hujuimtu alikuwa katika mood gani.

    nimejifunza pia kuwa mwangalifu kutoa comment, lakini pia UNISAMEHE KAMA ILE COMMENT WEWE ILI KUUDHI KIASI CHA KUTOA COMMENT KAMA ILE, KUWA ''MCHAWI'.

    Kazi njema kaka mimi

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 06, 2008

    Wewe mchangiaji usituletee unoko wako hapa kama wewe hupendi RAP/HIPHOP kimpango wako.Wazungu huku wanapensa ngoma ya msewe na wala hawajawahi kufika Africa kwa hiyo wabongo wakipenda American RAP/HIPHOP waache tuu ni maisha yao usitake kujifanya kiranja mkuu hapa.

    ReplyDelete
  26. Mambo. I'm a contributing writer to Bang! magazine based in Los Angeles and also write for The Source Magazine, among others. I was out in Bongo last June. I linked over to these pictures at my blog:

    http://sufferboulevard.blogspot.com/2008/05/50-cent-in-tanzania.html

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 06, 2008

    It is like being told off by your own kids, and I am dad here. LOL.

    Sorry guys, if I offended your conscious, this post was meant to give a different perspective on RAP and hip hop music. It is purely my personal opinion about anything in here, and I do believe I am entitled to that, whether it is written in English, Nyamwezi or Swahili, I decided to write in English, the reason being first and foremost for larger audience, that include Tanzanians, Kenya, Uganda and all that may understand a few broken words of English, I do believe english is an official language of Tanzania, Someone can enlighten me on this. Therefore, I am not contradicting that fact. and Last and most importantly for my own personal reason.

    I would also like to iterate that, Michuzi has a full control of whats to be posted, and thats his own decision, but at the same time I have high respect for him in bringing this blog to all sorts of people, including myself, and he solely give me this chance to do just that, that is to post what my conscious tells me to post, again it is WORLD WIDE WEB, matumbu can go in read, and CROATIAN can go in read and hack it too(LOL!!), if he/she wants to, and thats the beauty of it.

    Going back to the point, I am not saying that an expert on Hip hop/RAP music, but I do like good music, I listen to 2PAC and others, who projectile their music positively whatever the public opinion may suggest, but I have a clear conscious on what I listen and what to pick from the lyrics, and take that message on board, some are doing that, and some are just following the lyricism to the tunes and bits, and thats cool also, and my message directed to the latter and the whole concept and understand of the music itself. Don't you think will be a good knowledge acquired, if understanding the root of the music, messages portrayed to the fans. I hope you all wont be emotional on the issue, and I do respect your opinions, whatever it may sound.


    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 06, 2008

    KUSEMA KWELI MCHANGIAJI YUKO SAHIHI.KWANI MIZIKI YA HAINA KAMA YA 50 CENT HATA WAMAREKANI WEUSI WENYEWE WAMEJIULIZA JE INAWASAIDIA WATOTO WETU AU INAWAANGAMIZA? NA NDIO MAANA UMEONA 50 CENT AMEMTUKANA ALICIA KEYS JUZI TU KWA KUPONDA MZIKI WA HAINA YAKE.WATU WENGI WAMETOKEA KUIPONDA MIZIKI YA HAINA HII DUNIANI NA NI KWELI WATOTO WENGI WANAKUWA WANAIGA KUTOKANA NA HAWA KWANI "MSANII NI KIOO CHA JAMII" mstari wa afande sele.
    KWAHIO MCHANGIAJI HANA KOSA NA HATAKIWI KUOFFEND MTU YOYOTE KAMA UTACHUKULIA MANENO YAKE KAMA MAONI BINAFSI,KILICHO WAUMA NI KWAMBA MANENO ALIYOYASEMA NI UKWELI MTUPU.
    by wakili

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 06, 2008

    Anon 6:40PM tatizo si anachokizungumza mchangiaji, tatizo letu ujumbe wake hautufikii, kwanza haivutii kusoma ujumbe mrefu tena wa kiingereza ukizingatia wengi wetu hiyo lugha haipandi kwani akiandika mafupi kwa kiswahili ujumbe si utafika. Mie siwezi kusema nampinga kwa sababu hata sijasoma alichoandika, nikiona tu mada ndeefu halafu tena kiinglish aah mwanawane naruka nasoma koment nyingine sasa fikiria ni wangapi kama mie wanaoruka? Saa nyingine hata hatumuelewi anasema nini, aah shauri yake bwana anatwanga maji kwenye kinu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...