
SALOME NANCY MAKANI
01/01/1978 - 26/08/2000
Mtoto wangu Salome , mdogo wa Reena Cleo, dada wa Austin, David na Anthony, wapwazo Nicola, Natasha na Shola, Babu Kitipwatipwa msk, shemejio Harry Hare, wifizo Becky, Lilly, Lulu, MARAFIKI WEEEENGI MNO umeniachia utajiri wa watoto(marafiki zako) mashallah.....
Ukoo wa Makani wote na wa Makwaia... jirani wa Upanga, ni miaka 8 (minane) tangu mrembo huyu atutoke hapa duniani....mwaka huu ndio angetimiza miaka 30 tangu azaliwe.... lakini leo tunakumbuka miaka 8 tangu atwaliwe......
ni kama jana tuu, namshukuru Mungu kwa kuwa ndiye mtoa faraja... bila ya hivyo duuuh, chaoo umeniachia majonzi makubwa sana mwanangu,
najaribu kufarijika kwa kuwa ulikuwa hodari hadi kifo kilipokufika 'infact' wewe ndio uliye waambia watu kuwa, mwambieni mama yangu mie karibu nitakufa na nipo tayari....
maneno mazito kwangu nitayakumbuka na kunitia moyo hadi tutakapoonana....
Naamini upo katika raha za milele, kwani uwepo wako nasi ni wa dhahiri, na ndio unaonifuta machozi mwaka hadi mwaka.
Basi endelea ku - RIP
Mama yako Mpenzi
Mama yako Mpenzi
Beatrice P. Makani
bite_makani@yahoo.com
pole sana mama maneno yako ni ya majonzi sana............R.I.P dada yangu ulikuwa mdogo bado.
ReplyDeletemacrol, kuala lumpur
Jamani salome, yani utadhani jana tu. Haupo nasi kimwili ila kiroho bado tunakukumbuka ucheshi wako na mapenzi yako mungu aiweke pema roho ya marehemu Salome.
ReplyDeleteAmeen
dah kweli majonzi makubwa nilikuwa sijui kama salome makani katutoka nakumbuka alikuwa akija salenda kunua ndizi za kuchoma na dada zake kweli wacheshi hawadumu R.I.P Salome ..
ReplyDeleteCHULU..THE NETHERLAND
Rest in Peace my little sister. We really missed you.-Fau, Espoo.Finland
ReplyDeleteNiliuwa simjuhi marehemu lakini naelewa majonzi anayoyapata mama yake kwani najua wish ya mzazi ni kuona mtoto wake anakuwa na kuacomplish ndoto zake na ikiwezekana hata kuchukua maumivu au kifo cha mtoto wake. Pole sana mama Salome na ufarijike kwa kujua kuwa mtoto wako amelala pema peponi na sisi sote tunaelekea huko ila ni kwa muda mbali mbali. Siku moja utaungana naye. Uko hamna uzuni, shida, njaa wala vifo bali ni raha na heri ya milele. Mungu abariki familia yako na awape faraja na malaika wa kuwaongoza katika maisha yenu. RIP Salome
ReplyDeletePole familia ya marehemu na Mungu awape heri na nafuu ya maumivu na pengo la mtoto wenu. Alisoma wapi marehemu?
ReplyDeleteSimjui huyu binti wala mama ake wala ndugu zake, lakini meseji ya mama imeni-touch. Poleni sana.
ReplyDeleteMdau
Ohio, USA
"We shall not say that you are gone, Too final is the sound. We'll say instead, you've gone ahead - where heavenly joys abound." REST IN PEACE LITTLE COUSIN. I WILL ALWAYS LOVE YOU!!! DA KUKA
ReplyDeleteningependa kutoa pole zangu wa Familia ya Makani na kumbuka mama makani alipo kuja kuniangalia pale muhimbili mwaka 1989 nilipo fanyiwa operation ya mguu, na pia nilipo kuja kumwaona Salome kabla ya kuja Texas,pole ni sana Mwenyezi Mungu awabariki
ReplyDeletengungu yenu wa Upanga
Maneno ya Mama Makani yamenikuna sana na kunitoa macho sio mpaka uwe mngoni ndo uwe na kipaji cha kuliza watu, binafsi nilimfahamu marehemu salome na kwa bahati mbaya alipotutoka nilikuwa tayari sipo nyumbani tanzania, daima tutamkumbuka kwa ucheshi wake siku zote roho ya marehemu isistiriwe mahali pema panapostahili
ReplyDeletealisoma muhimbili primary school baadae akachaguliwa forodhani sec school ndipo aliposoma marehemu
ReplyDeleteJamani pole sana mama,siwafahamu ila nimeumia, sina la kusema, sijui alikumbwa na nini hadi mauti yake naamini kila jambo mungu anamakusudi yake, jipe moyo mama utashinda, tunakuombea wakati huu mgumu mungu akutie nguvu wakati huu unamkumbuka mtoto wako mpendwa.
ReplyDeleteSalome alisoma Immaculate Nursery school. primary school Muhimbili Secondary Foradhani High School Mwenge Open Academy...tuition Tambaza Secondary School... akafanyakazi Alpha Bureau de change...alifariki akiwa na umri wa miaka 22 na miezi minane... Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Mpwenda wetu peponi amen
ReplyDeleteAlisoma Upanga Immaculate nursery school, muhimbili primary school, forodhani secondary school na Mwenge Open Academy- high school tuition tambaza secondary school akafanyakazi Alpha bureal de change
ReplyDeleteMama makani, pole sana.
ReplyDeleteJamani Salome hatutamsahau uchangamfu, upendo wake daima.
Watanzania wenzagu, kifo cha Salome, kitukumbushe kufahamu kuwa sisi wote ni wasafiri katika dunia hii.
Mungu alisema kufa hakika mtakufa, haijalishi umri mdogo au mzee sana.
Namuomba Mrs. Makani amtegemee Mungu katika maisha yake, ajitoe kwa Mungu ajitahidi kutenda mema ili siku moja aonane na binti yake mpendwa huko makao ya milele ambapo kifo kitakomeshwa. Wabongo wenzangu, Salome alikuwa na mapenzi sana na mama yake na nikiwa shahidi jinsi alivyojitahidi kila siku kumsaidia mama yake kwa shida yeyote aliyokuwa nayo na aliyoweza kumsaidia mama yake alifanya kwa heshima na mapenzi makubwa. Mimi ni shuhuda maana mama makani niliwahi kushare naye ofisi.
Salome umetangulia, nasi tunafuata nyuma kwa zam zamu, Mungu atusaidie wote ili nasi tuimalize salama safari yetu hapa duniani,
Anna
ak_abduel@yahoo.com
Pole sana mama, maneno uliyoyasema hata mimi yameniuma moyoni kanakwamba namjua marehemu. Hakika machozi yananitirika napoandika salamu hizi.
ReplyDeleteMola aiweke roho ya marehemu Salome mahala pema peponi- Amein.Na pia awape nguvu ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa marehemu salome, najua fika kipindi kama hiki ni kigumu sana kwenu.
pole sana mama yangu beatrice,maneno yako yamenichoma kiasi cha najiuliza wewe kama mama unajisikiaje rohoni mwako.lakini naomba nikuambie kuwa mshukuru mungu kwa kila jambo,na bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.na bwana akujaze faraja moyoni mwako ,na la muhimu kabisa muombee sana ,mkumbuke kwa sala na ibada.
ReplyDeletendimi mwwanao
mariana kaloli
Pole sana uchungu wa mwana aujuae ni mzazi. Hakuna mwenye kuweza ziba pengo la binti yako kwani yeye alikuwa ni mtu special uliyepewa na Mungu. Please be strong na uko kwenye maombi yetu
ReplyDeleteMAMA SALOME, UMENIFANYA NILIE
ReplyDeletePOLE SANA MAMA
MAY SALOME'S SOUL REST IN ETERNAL PEACE, AMEN
Mdau, Japan
Pole sana sana mama. Simfahamu bintiyo wala pia wewe. Ila kimeniuma hadi machozi yamenitoka.
ReplyDeleteIt is really hard moment you have gone through, hasa kumpoteza kijana katika familia. Naamini Mola atazidi kukupa nguvu mama Salome pamoja na familia yako.
Naamini Mola aliyemchukua anampenda zaidi yetu, na hiyo ni njia yetu sote, ila tu ni swala la wakati.
Pole sana mama Salome,
and RIP SALOME!!
Dada T
I AM THE YOUNGEST BROTHER OF SALOME MAKANI (ANHTONY)TO BE HONEST FROM THE MOMENT DADANGU AMETUTOKA,MAISHA HAS NEVER BEEN THE SAME,SHE HAS LEFT SO SO MANY FRIENDS THAT SOME WANAKUJA JUST KWA KUNIANGALIA SURA YANGU TU WANANIULIZA WE SI MDOGO WAKE SALOME? AND START TELLING ME AMAZING STORIES ABOUT HER,I WISH I KNEW MY SIS THE WAY WATU WENGINE WANAVYOMJUA,IT JUST BRINGS BACK ALOT OF MEMORIES. OUR MOTHER'S MESSAGE HAS TOUCHED ALOT OF PEOPLE AND FILLED THEM WITH SYMPATHIES AND YET KUMKUMBUKA MUNGU KWAMBA ITS HIM WHO GAVE IT AND HIM ONLY WHO CLAIMS IT BACK..MY KIPENZI SISTER I AM CRYING AND SHAKING RIGHT NOW WRITING THIS LITTLE PIECE OF MY HEART.. SIMPLY BECAUSE I AM JEALOUS THAT YOU ARE IN PARADISE AND SOONER OR LATER WE SHALL ALL REJOIN...KEEP BUILDING THAT CASTLE WITH DAD ON YOUR RIGHT HAND FOR US..WE LOVE YOU LIKE WE HAVE ALWAYS DID..there so many to write ila i think macho yangu yamejawa na machozi i cant write more..all i can say jamani AHSANTENI SAAANA SAANA FOR YOUR COMMENTS..TUOMBEANI AMANI NA UPENDO..LOVE YOU SISTER SALOME NANCY MAKANI..LOVE ALWAYS LITTLE BRO ANTHONY MAKANI (uk)
ReplyDeleteSiwajuhi hii familia. Kwa kweli maneno ya mama yanasikitisha sana na kutupa mwanga wa "not to take life for granted" Hamna chochote tulichofanya kutuwezesha sisi kuwepo na huyu msichana mzuri kuchukuliwa na Mungu kwa kweli ni mapenzi ya Mungu na ashukuriwe kwa kila jambo. Sisi tuliopewa muda zaidi tugunduwe kuwa hatujuhi siku wala saa. Tuishi maisha yetu kama leo ndiyo ni siku yetu ya mwisho. Tupendane, tuheshimiane na la zaidi tumpende Mungu. Sijuhi kilichosababisha kifo cha marehemu lakini inaonyesha kuwa yeye alibarikiwa kujua saa ya mauti yake kwa hiyo kama alikuwa na lolote la kutubu alitubu. Familia ya marehemu ifarijiwe na ibarikiwe na sis iwote tunaosoma blogu hii Mungu atubariki ili tuelewe thamanai ya maisha tuliyopewa. Tuyatumikie na kumtumikia Mungu vema na mwisho wa siku tukumbuke kusema asante baba kwa yote na kwake tujikabidhi.
ReplyDeletemy the load rest her soul in peace our beloved sis.i did pray with watoy leo to sen our blessing...we will always love you even though i never had the chance to meet her.....love ayisha gugu...from birmingham
ReplyDeleteSalome jamani salome jamani !!! rafiki yangu wewe rest in peace my dear.
ReplyDeleteI will never forget your the day that I came to see you at the hospital. Ulikuwa una maumivu sana, lakini uliweza kuongea na mimi so well!! jamani salome I can still close my eyes and see your pretty face , I can still close my eyes and see you saying " thanks for coming jamani!" ..salome you are such a beautiful woman ! yes you are and not you were. Nalia i cant write anymore
Im really sorry about wot happend , i was so young when she went and i didnt understand but as i grew older i understood. I also learned then even though we cant see her she is still in our hearts Its been eight yrs and we all really miss her. May the Lord bless her and let her rest in peace. I miss her terribly even though i had only seen her for a short time, my mum says she has the qualitys of my sis so she might be gone but atleast i know how she is like. I wish her all the best up in heaven .... Lord bless her.... Nicola ( niece) Love you lots xxxxxxxxx
ReplyDeleteSorry about it.Just remember that we are all behind yyou. I miss you auntie and i almost cry everyday . But thank god u r safe in heaven . I wish she was here with me. I love her with all my heart . I'll keep prayin for her . Love u lots Natasha (niece)
Tony baba you and your mum have made me cry so much this evening, I had to take some time to compose myself before I could find strength to write.
ReplyDeleteLosing a loved one is the hardest thing I have ever had to deal with, and it’s usually hard to everyone in the family to a point that nobody has the courage to bring up topic. I never knew you sister but I have read so many good things from people that new her; May Lord rest your soul in peace Salome.
My reasons for writing are not only to sympathise with you but also to thank both you and your mum for your courage to talk about your sister/daughter because as a mother I cannot even start to imagine my world without my baby. This show how much of a remarkable and strong woman you are Mama Makani; na Mungu ataendelea kukuongoza.
I pray for you and your family to continue to find peace and love in yourselves and I also pray to take with me your courage and share with it my family; to find more strength to talk more about the loss of our beloved father.
May God Bless You All
Joyce Kiwia (Manchester)
Solome nakukumbuka sana nakumbuka back then nilikuwa nafanya kazi ips building, salome alikuwa next door jirani yetu,sometimes nilikuwa siendi lunch kwa sababu mambo mabaya kibongobongo, yaani always salome alikuwa akiona nakata kwenda luch anajua sina hela and she always bought me lunch,i wish i could do something back to show her my appreciation but God has another plan for u, we love u but God loves u more jina la bwana lihimidiwe,i will always remember u.
ReplyDeleteG u.s.a
Mama Makani Mungu akutie nguvu!!
ReplyDeleteManeno yako yanachoma sana. Sikufahamu wala simfahamu Marehemu Salome lakini naamini alikuwa binti "tajiri wa marafiki" na "mtu wa watu". Mwenyezi Mungu alaze mahali pema.
Kwakweli maneno ya mama MAKANI yamenichoma mno jamani nimejisikia uchungu mno.Mungu akupe uvumilivu mama katika kipindi kigumu kama hiki.Simjui huyu dada lakini nimeguswa mno, msichana mrembo too young jamani pumzika kwa amani Salome!
ReplyDeleteANTHONY MAKANI, pole sana Mungu akupe uvumilivu nimelizwa na maneno yako jamani sote tuwapitaji hapa duniani kila mtu anayosiku yake ya kufa!
Nawatakia kila la heri familia yote ya mama Makani!
Sijui hata niseme nini...
ReplyDeleteInauma sana jamani... Inauma sana... tena sana...
Pole mama Salome. Mungu aendelee kukupa faraja mamangu kwani Mungu huyo huyo aliyemleta Salome duniani pamoja na sisi wengine, ndiye aliyempenda zaidi na hivyo kumtwaa. Siku moja na sisi tunaungana na Salome katika furaha ya milele... Tupo pamoja katika maombi mama.
Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu Salome katika Mwanga wa Milele... Amina.
Jackie... DSM
Salome, We miss you a lot!! You were such a wonderful person, loving, caring and a good friend. My prayers are with your family. May God rest your soul in peace.
ReplyDeleteJohn(USA)
Salome makani i cant believe it has been 8 yrs, i was young but i remember you very much since i grew up with Tony & our mothers were very good friends. May god bless u & may u rest in peace, say hi to your dad up there too.
ReplyDeletePole sana Mama ushauri!! Pole sana pia kwa wanafamilia wengine!! Unasoma messege ya mama Makani mpaka unalia. Salome kwa kifupi sana alikuwa RAFIKI WA KILA MTU!
ReplyDeleteHiyo ilijionyesha hata wakati wa msiba wake, kwa umati ule na umri wake unaweza kujua kuwa alikuwa mtu wa aina gani. Sisi tulimpenda sana Salome, lakini Mungu ndie aliempenda zaidi! Raha za milele umwangazie ebwana.....
R.I.P lil sis.
Kassim.
Salome, you remain and will remain a "Darling" to us all. Prepare the ground for us and we shall surely meet again. Rest in Peace Darling. Harry
ReplyDeleteDEAR SALOME,
ReplyDeleteIT WAS GOD'S PLAN TO LET YOU LIVE THE 80's, ENJOY LIFE IN 90's AND HE TOOK YOU AWAY TO THE ETERNAL PEACE IN THE MILLENNIUM.
REST IN PEACE.
AMEN.
mIMI SIMJUI huyu salome wala familia yake, ila maneno ya mama mfiwa yamenitia uchungu. mungu azidi kukubariki salome na mungu azidi kukupa nguvu na upendo mama na familia yako.
ReplyDeletemanchester, UK.
pole sana mama na Antony na wote! nimesikitishwa sana na maneno mazito ya mama na antony, simjui salome bali naujua ukoo wa makani na makwaia kwani mama yangu mkumbwa aliolewa na late joseph makwaia. na sura ya marehemu salome ni sawa na dada yangu elizabeth makwaia, nimeumia sana she was young. pole sana mama pole kwa maumivu mazito uliyoyapata yesu pekee ndio mfariji wako.
ReplyDeletemimi Kashinje Geneya, London
Pole Sana Mama yangu Mama Makene . I feel you. Mungu akubariki na akutie nguvu Msg yako ni nzito nainatia uchungu. I love you!
ReplyDeleteMama Salome na Anthony Mdogo wake Salome, POleni sana pamoja na ndugu wengine wote na marafiki. Mama wee, Machozi yananitoka Siwafahamu mimi pia ila, siwezi kuimagine Uchungu ulionao kwa kupoteza kipenzi chako, POLE SANA.ILA SALOME ALIPENDWA MAMA NA NI KWA SABABU YA TABIA NJEMA NA UPENDO ULIOMFUNDISHA KATIKA MALEZI, ULIFANYA KAZI KUBWA NA NZURI, HONGERA KWA HILO,Mungu akupe FARAJA zaidi na MATUMAINI.NDUGU TUENDELEE KUMUOMBEA ILI ANGAZIWE MWANGA WA MILELE.
ReplyDeleteH.TX
Poleni sana mama na wengineo wote. Salome alibahatika kupendwa na wengi popote alipokuwepo kutokana na ucheshi wake. Mimi nilimjua kupitia MOA High School akiwa classmate wangu darasa moja la ECA. nafikiri nilimzowea sana na pengine tulizoweana sana kama wananfunzi na ninakumbuka yeye ndiye alinifundisha/ tufundisha pale shuleni tofauti ya Uncle na Ako utani ambao tuliutumia sana darasani kila tulipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amin
ReplyDeleteMUNGU AWABARIKI NYOTE..... ASANTENI SANA NA POLENI SANA KWA KUTOKWA NA MACHOZI NAAMINI NI MACHOZI YA UPENDO MWINGI KWANGU NA FAMILIA YANGU.... GOD BLESS YOU GUYS..... Mama Salome(Mrs B.P Makani)
ReplyDeleteGone yet not forgotten, although we are apart, your spirit lives on within us, forever in our hearts. RIP dear Sister.....till we meet again. Mamu(Mombasa, Kenya)
ReplyDeleteHakuna tarehe 26 ya mwezi wa nane ambayo simkumbuki Salome hakuna-nabaki kumwombea na kukumbuka mazuri tuliyoyapitia as kids especially, she was my childhood na adulthood friend, nilisoma nae frm nursery to high school..Nakumbuka primary school tulikuwa tunapenda sana kuchoreana cards za birthday, na tulipenda kuchora pamoja..Hizo ndio memories ambayo nahold mpaka leo and forever.
ReplyDeleteNakupromise bibi Bite ntakuja hapo Upanga very soon, its been three years sijaja na mauwa yangu wa kumbukumbu ila napromise ntakuja!
We miss you Sally darling and love you lots!
D!
Pole sana mama na familia nzima, siwafahamu vizuri ila nakumbuka mwaka 1999 au 2000 nilisikia dada kama huyu alikuja Finland kwa matibabu, sina uhakika kama ni huyu, then later tukaja kusikia mungu ameamua kumchukua, anyway, kwa ufupi nimetokwa na chozi kwa maneno ya mama na kaka Tony, binafsi nimeshafiwa na mtoto, japo alikuwa mdogo na sikupata nafasi ya kucheza ama kuongea naye but INAUMA SANA, HAKUNA MFANO WAKE....Pole sana mama yangu mpendwa, tujipe moyo, watoto wetu wapendwa wako mahala pema peponi.Tusiache kuombeana faraja ya mwenyezi mungu, kwa maana katika miaka kadhaa niliyoishi hapa duniani, ´sijakutwa na kidonda kigumu kama hiki cha kufiwa na mtoto,RIP babies ,AMEN.
ReplyDeleteI had a dream about Salome Makani today. I have had not seen her since Muhimbili Primary School. In my dreams she looked as I last saw her but in short hair. She was a prefect. She did not say much but was there. Just wanted to share. May her soul rest in peace
ReplyDelete