Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Watalaam wa uchumi hivi exchange rates huwa zina-reflect hali halisi ya uchumi wa nchi au ni kitu gani??.
    Mfano 1USD=106JPY(Japanese Yen)=7.9ZAR(south africa rand)=3,500Zambian Kwacha=550Congolese Francs=1,170TZS,n.k.Practically,uchumi wa Zambia na Tanzania unazidi vibaya sana uchumi wa congo(sina data,sina uhakika natumia 'kwa kufika na kuangalia' basis).Je uchumi wa SA una nguvu kuliko wa Japan??Tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Hapana David, exchange rate haionyeshi hali halisi ya uchumi ila inaonyesha mwenendo wa shughuli za kiuchumi katika kipindi husika. Kwa maana nyingine exchange rate inaonyesha mtu anavyotembea, haionyeshi alikofikia.

    Hivyo basi $USD inaweza ikashuka thamani dhidi ya Tz sh, hii ina maana kwamba katika kipindi husika ela ya Tz inapendwa zaidi ya USA, yaani watu watauza $USD watanunua Tz sh. Hii haina maana kwamba uchumi wa Tz unakuwa kupita wa USA.

    Hitimisho: exchange rate ni kiashirio tu cha mwenendo wa shughuli za kiuchumi sio kipimo cha moja kwa moja cha kukuwa kwa uchumi.

    ReplyDelete
  3. bwana ndumba nangae umetoa vitu siyo kawaida, thanks. David pia thanks kwa swali, limetufaidisha wengi.

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu hili ni swali zuri sana, kwani huwa linachanganya watu wengi sana pamoja na mimi. Lakini uelewa wangu so far ni kwamba exchange rate ni makubaliano kati ya mtu anayehitaji dollar na mtu anayehitaji shillingi (demand and supplier). Kwa mfano kama dollar ikipanda bei maana yake ni kwamba siku hiyo kuna watu wengi walizihitaji Dollar, au shillingi ikipanda bei maana yake ni kwamba watu wengi wamehitaji shillingi instead of dollar on that day. Kitu ambacho usije kuchanganya ni inflation rate na exchange rate sababu they have almost same concept but they are not the same.

    ReplyDelete
  5. Jamani exchange rate ni moja kati ya vitu vinavyo-determine uchumi wa nchi zinazohusika, vitu vinavyo-determine uchumi wa nchi vipo vingi ni pamoja na exchange rate, ili swali umnaweza kujibiwa vizuri kama mtamuuliza google.com na kufunuwa vitabu vitabu vya economics, finance and banking, pia mtaweza kujuwa jinsi gani exchange rate inakuwa calculated, mtaona sasa zile hard currencies kama £ na $ zimeshuka dhamani ni kwa ajili ya hali mbaya ya uchumi wa dunia/ credit crunch inayoendelea sasa. VITU VINGINE VINAVYO-DETERMINE UCHUMI NI PAMOJA NA:- EMPLOYMENT, PRODUCTIVITY, INFLATION RATE NA VINGINE VINGI TU.

    ReplyDelete
  6. kama walivyosema baadhi ya wadau juu, viwango vya kubadili fedha za kigeni ni moja ya viashiria uchumi lakini haiwezi kutoa picha kamili ya hali ya muda mrefu ya uchumi wa nchi. Mi si mtaalamu lakini naomba niseme machache yafuatayo:

    1. Wachumi hutumia vigezo vipingi kupima kiwango na ukuaji wa uchumi; mfano, pato la ndani la taifa kwa kaya; wastani wa bei za rejareja; mfumuko wa bei; riba za dhamana za serikali na mabenki; kiwango cha elimu na uwezo wa kutoa huduma za muhimu kama maji, afya, n.k.

    2. Bei za kununua/kuuza fedha za kigeni hutegemeana na matakwa yaliyopo katika soko. Iwapo kutakuwa na mahitaji makubwa ya fedha za kigeni, basi viwango vyake vya ununuzi vitapanda.

    3. Katika biashara za kimataifa, serikali/makampuni inapoagiza bidhaa/huduma toka nje, mara nyingi hulipa kwa fedha za kigeni (hususan dola ya kimarekani, lakini pia sarafu nyingne zenye viwango madhubuti na zisizoshuka thamani mara kwa mara mfano Euro na Pauni ya Uinregeza hutmika pia).

    Hivyo basi, nchi inayoagiza beidhaa toka nje kuzidi kiwango inachozalisha na kuuza nje (trade deficit) hulazimika kununua dola (au sarafu nyingine) ili iweze kulipia bidhaa zake; hii husababisha thamani ya sarafu ya nchi husika kushuka ikilinganishwa na fedha za kigeni.

    3. Wafanyabiashara na wawekezaji katika nchi changa ambazo thamani ya sarafu yake huwa zinabadilika mara kwa mara, hupendelea kuwa na akiba kubwa ya fedha za nje.

    Pia katika nchi zenye hali tete ya kisiasa, hofu ya vita na kubadilika kwa hali ya amani (mfano inapokaribia uchaguzi; kunapokuwa na vuguvugu la mapinduzi, n.k.) hupelekea wawekezaji katika nchi hiyo kupenelea kuwa na akiba ya fedha za kigeni, kusudi thamani ya sarafu ya nchi husika inaposhuka, akiba yao ithiathirike.

    4. Sera ya serikali na benki kuu juu ya hifadhi ya fedha za kigeni pia huathiri kwa namna moja au nyingine upatikanaji wa-, na bei za ununuzi wa fedha za nje.
    ---------------------------------

    Baada ya kusema haya machache, nikiri kuwa mi binafsi, pamoja na wadau waliotangulia hawajaweza kujibu kiini hasa cha swali la mdau Villa. Anochataka kuju mdau ni kwa nini thamani ya Yen ya Japan ni takribani Dola 1 ya Kimarekani kwa Yen 106; wakati shilingi ya Kenya ni Dola 1 ya Kimarekani kwa Shilingi 74; ilihali Japan imeizidi Kenya kiuchumi katika karibu kila nyanja.

    Swali hili ni rahisi na haiyumkini wengi tumeshajiuliza lakini jibu lake hatujalipata. Nimefungua mjadala wa majadiliano juu ya maada hii katika blogu ya UCHUMI NA FEDHA. Bofya Hapa: http://uchuminafedha.blogspot.com/2008/09/question-on-foreign-exchange-rates.html tujadiliane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...