mtoto samuel nkya akiaga leo uwanja wa ndege wa julius nyerere kabla ya kupaa kuelekea mumbai, india kwa matibabu ya uso wake

mwenyekiti wa kamati ya kuchangia gharama za matibabu ya mtoto samuel akimsindikiza
emmanuel nkya, baba mzazi wa samuel, akiongea na waandishi juu ya safari hiyo ya mumbai
david sawe akiongea juu ya safari ya matibabu ya mtoto samuel nkya
mama mzazi wa samuel akiwashukurui wasamari wema waliojiyolea kwa hali na mali na kufanikisha safari ya matibabu ya mtoto wake huko india. jumla ya sh. 13,616,900/- zilipatikana kutokana na michango iliyoanzishwa na globu hii ya jamii na kufunguliwa akaunti maalumu na adu kadhaa. ni siku ya furaha sana kwa wadau wote kwani mwisho mwema unafurahisha ati


Mtoto Samuel ambaye amekuwa akipigiwa debe la matibabu kwenye uso wake na vyombo vya habari vya ektroniki na vya kawaida leo ameondoka kwenda India katika hatua nyingine ya uponyaji wa kidonda chake.

Debe hili lilianzia kwa mdau David Sawe ambaye aliunda kamati ya kuchangisha fedha za matibabu akishirikiana na wapiganaji Athumani Hamisi na Mkuu wa Wilaya ya nanihi na baba mzazi wa Samuel.

Hali kadhalika, mdau Jimmy Kihwele wa Wichita, Marekani, ambaye mara baada ya kuona tangazo la mtoto Samwel kwenye globu hii ya jamii, alianzisha blog maalumu na kuweza kufanya harambee huko aliko ambayo pia imechangia kujazia katika gharama za matibabu. Tovuti ya mdau Jimmy ni http://www.jifunze.com/FundRaising/

Akiwa uwanja wa Julius Nyerere mtoto huyo alitoa shukurani nyingi kwa watu waliokuwa wakimsaidia kufanikisha matibabu yake.

Pia baba wa mtoto huyo Emmanuel Nkya kwa niaba ya familia alizungumza machache kuhusu mtoto wao huyo na jinsi tatizo lilivyoanza hadi hapo na pia mama wa mtoto alizungumza; pia alishukuru blogu mbalimbali na vyombo vya habari vingine vya print na elektroniki vilivyofanikisha tiba za mtoto huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera Blogu ya Jamii kwa kazi njema!
    naomba salaam zangu za pongezi ziende na kibao changu kinaitwa
    TEN COMMANDMENTS OF MARRIAGE
    ~~~~~~~~~~~~~

    Commandment 1 : Marriages are made in heaven, but so again, are
    thunder and lightning.

    Commandment 2 : If you want your spouse to listen and pay strict
    attention to every word you say, talk in your sleep.

    Commandment 3 : Marriage is grand -- and divorce is at least 100 grand!

    Commandment 4 : Married life is very frustrating. In the first year
    of marriage, the man speaks and the woman listens. In the second year,
    the woman speaks and the man listens. In the third year, they both
    speak and the neighbors listen.


    Commandment 5 : When a man opens the door of his car for his wife,
    you can be sure of one thing: Either the car is new or the wife is!

    Commandment 6 : Marriage is when a man and woman become as one, the
    trouble starts when they try to decide which one.

    Commandment 7 : Before marriage, a man will lie awake all night
    thinking about something you said. After marriage, he will fall
    asleep before you finish.

    Commandment 8 : Every man wants a wife who is beautiful, understanding,
    economical, and a good cook. But the law allows only one wife.

    Commandment 9 : Every woman wants a man who is handsome, understanding,
    economical and a considerate lover, but again, the law allows only
    one husband.

    Commandment 10 : Man is incomplete until he marries. After that, he
    is finished.
    ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    mdau,
    mnyalukolo

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli Balozi Mithupu unastahili pongezi japo michango hii imechukuwa muda mrefu sana, nadhani tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ingekuwaje kama kungekuwa na deadline ikipita mgonjwa anakufa?? inabidi tuhamasishane kwa mambo ya msingi na ya kibinaadam. Namuombea Samy apone haraka.
    Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  3. Napenda kutoa shukrani kwa blog ya michuzi na media zingine zilizosaidia kupatikana kwa gharama za kumpeleka kwenye matibabu mtoto Samuel.
    Pili namtakia afya njema kwa mtoto Samuel.
    Samahani Michuzi nje kidogo; Hivi Da Rehema Mwakangale ameolewa?Hizo picha kama anatu'beep' hapo chini ya msalaba siyo siri.

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Balozi MICHUZI kwa hili la mtoto Samueli kuwezesha wana jamii kuchangia Tshs 13 Millioni nakupa hongera sana, tena sana, yote haya malipo yake utayapata kwa mwenyezi mungu kwani ndiye pekee anyeweza kulipa fadhila kwa kila mja wake. AHSANTE SANA na kazi njema.

    Q

    ReplyDelete
  5. HONGERA SANA MICHUZI...LAKINI HII MICHANGO IMETUMIA MUDA MREFUU JAMANI TOKA HUYO MTOTO AKIWA MDOGO MPAKA SASA NAONA KAVAA NA SHATI KABISA...MICHUZI MICHANGO WEKA DEALINE PLEASE...

    ReplyDelete
  6. MUNGU ATAMSAIDIA APONE MTOTO ANATIA HURUMA ASANTENI KWA MICHANGO YAKUMFANIKISHA MUNGU UWABARIKI NA AWAZIDISHIE ZAIDI WOTE WALIOJITOLEA MIMI NI MDAU TU SINA UNDUGU NA HAWA WAHUSIKA ILA NIMEGUSWA NA JUA UCHUNGU WA MTOTO na SHUKURANI ZA DHATI KWA KAKA MICHUZI

    ReplyDelete
  7. This is indeed a great achievement by your blog! Next time you should set a deadline kama wadau walivyochangia au kama deadline sio busara basi tuongeze jitihada kwenye uhamasishaji.

    Secondly, Nahisi hizo hela ni kidogo due to nature of the problem unless kuna source nyingine za fund.
    Once again congratulation.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...