Gari ambalo alikuwa akisafiria Athumani Hamisi, Hery Makange na Anthony Siame namba T 961 AGT baada ya kupata ajali.
Herry Makange akimsaidia Athumani mara baada ya kumtoa katika gari
Baadhi ya wananchi waliofika katika tukio hilo. Inasikitisha majeruhi waliibiwa baadhi ya vitu vyao vikiwamo fedha na simu za mkononi.
Athumani Hamisi akihamishwa wodi jioni 12-9-08. Athumani aliyepata ajali asubuhi leo amelazwa katika wodi ya Sewahaji 17 wakati mipango ya kumhamishia katika wodi Maalum inafanyika. Madaktari wanafanya kila jitihada kumhudumia mpiganaji huyu ambaye hadi tunaondoka wodini alikolazwa mida ya saa mbili usiku alikuwa anaweza kuongea na hata uji aliweza kunywa kwa kusaidiwa. analalamika kuwa na maumivu makali shingoni na utosini.

Herry Makange (kushoto) na Athuman Hamisi.

Wapigapicha za Habari wa tatu wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo wamenusurika kufa katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi wakiwa njiani kelekea Kilwa katika futari maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kupitia Voda Foundation.
Wapigapicha hao ni Athumani Hamisi wa Daily News na Habarileo, Herry Makange wa DTV na Channel 10 pamoja na Anthony Siame wa New Habari Cooparation.
Halizao zinaendelea vyema isipokuwa Athumani aliyepata majeraha kichwani tumboni na mkononi baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka mara kadhaa kabla ya kutua nje ya barabada.
Athumani amesema walikuwa katika mwenzo wa kawaida na walipokaribia Kibiti sehemu ambako barabara ina changarawe juu ya lami, gari iliyumba na kuserereka na kuanguka.
Globu hii ya jamii inamuombea mpiganaji huyu apate nafuu ya haraka. Pia inatoa shukrani kwa msaada wa hali na mali ambayo Vodacom inatoa kwa majeruhi, pia asante ziende kwa Ruge Mutahaba wa Clouds FM ambaye alihakikisha gari inavutwa hadi Dar ambako imeegeshwa kituo kikuu cha kati cha polisi.
Vile vile shukrani za pakee ziwaendee pia Herry Makange aliyebaki kulinda gari na vifaa vya kazi ambavyo vyote vipo salama, na Anthony Siame ambaye hakubanduka ubavuni pa Athumani hadi anafika Muhimbili.
Picha zilipigwa na Siame, na hiyo ya hospitali ilipigwa na bernard rwebangira na pia zipo katika
mrokim.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. kaka hiyo futari mbona asubuhi wakati tumezoea huwa jioni? mungu awape wepesi wa kukabili matatizo waliyonayo na wapone haraka

    ReplyDelete
  2. Oohh jamani Poleni sana Mungu atawasaidia mtapona haraka

    ReplyDelete
  3. Pole sana Athumani, na wenzio.

    Upone haraka!


    M.
    www.marekani.com

    ReplyDelete
  4. Poleni sana. Nawaombea mpone haraka mweze kurudi kazini na kuendelea na kazi nzuri mliokuwa mnafanya.

    ReplyDelete
  5. POLENI SANA!

    michu!!! Hii idea ya kuwa gari limepinduka mara tatu? nani aliileta? maana hata pikipiki siku hizi ikipinduka utasikia, mara tatu? au mara tatu ndo kiwango kikubwa kabisa?

    Let us be realistic. Nani huwa anakaa kuhesabu hayo magari yabapobingirika au ndo uzushi tu?

    ReplyDelete
  6. Ebwana nimeona picha za ajali kwa Father Kidevu hakika inatisha na kusikitisha, Mungu awajalie afya njema wote. Pitieni www.mrokim.blogspot.com

    ReplyDelete
  7. Poleni sana na tunawatakia speed recovery
    Mbona kama Kilwa ni mbali sana? Kwenda kwa ajili ya Futari tu au kaka yetu hujatumalizia hadithi yote?
    Anyway I hope you guys will get well soon

    ReplyDelete
  8. poleni na nawatakieni speed recovery. Hata hivyo michuzi heading kidogo inababaisha "wapiganaji" nilidhani ni wanamasumbwi vipi wapiga picha unawaita wapiganaji?

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wapiganaji. Tunamuombea Bro Athumani apone haraka na kuendelea na kazi.

    ReplyDelete
  10. Mbona hamtuambii hiyo ajali imetokea wapi exactly? Mnafikiri sisi hatuijui Kilwa ama njia ya kusini? Ndio kwetu huko mwe jamani.

    ReplyDelete
  11. Duh wakuu Futari asubuhi toka Dar mpaka Kilwa kwa ajili ya futari mhhh!
    Mdau pepo

    ReplyDelete
  12. Poleni sana.Lakini wabongo tujifunze kwendesha magari kwa kutumia busara na akili.Sasa kama sehemu/barabara ina changarawe kwa nini mtu uendeshe 100mph?Unajuwa for the fact traction kwenye changarawe,mchanga,wet surface haiwi nzuri kwa nini uendeshe kwa fujo?
    Waendesha magari wote wakishajuwa haya na kuyatiria maanani ajali za barabarani zitapunguwa kwa asilimia kubwa.
    Nasema tena poleni ndugu zetu.

    ReplyDelete
  13. Watu wa Tanzania wana tabia mbaya sana gari ikipinduka tu wanakimbilia kwaibia waliopata ajali, ni njia zote za Tanzania, sababu ni nini? umasikini? na huu ni wakati wa mfungo wa ramadhani na wengi wa njia hiyo ni waislamu safi! hii tabia ikomeshwe jamani. mimi nilipata ajali kama hiyo baada ya Kilwa vijiji vitatu kuelekea Dar, nilikuwa katika Suzuki Grand Vitara V6 mimi na my wife wangu na abitia mmoja ni ajali mbaya kama hiyo, nilipata pancha tairi la mbele kulia mwanzo wa daraja nikagonga daraja baada ya gari kunivuta upande mmoja na kushindwa kuirudisha barabarani kwa vile tukio lilikuwa la ghafla baada ya hapo AIR BAGS ZIKAVUMUKA ZIKATUSAIDIA MIMI NA MKE WANGU KUTOGONGA MELE KWENYE KIOO AU MIMI KUJIBAMIZA KWENYA USHUKANI, tukaserereka kuelekea mbugani kwa mwendo wa kasi na kujigonga katika tuta na kupinduka cali pia tulikuwa tumefunga mikanda wote watatu, mungu mkubwa hakuna hata mmoja wetu aliyetoka hata chembe ya damu tulitoka wazima lakini gari ilikuwa nyang,anyang,a na written-off, cha ajabu wwenyeji walikuja kwa fujo wakijuwa tumesha kufa ili wapore kila kitu, mimi nikawahi kutoka ndani ya gari, nikawafunguliwa wenzangu wakatoka na nikawambia ni marufuku mtu kusogelea gari kila mtu awe mbali asiguse gari, nilikuwa na bastola ambayo naimiliki kihalali nikaitowa na kushika mkononi nikasema mtu aguse gari na akione cha moto, wakanywea wakaanza kuwa marafiki wakatusaidia kupata ulinzi wa kulinda gari anagawa si bure tuliwalipa, wakaenda kumwita taariki ambaye aliongozana na katibu wa taarafa, ambao nao walitaka rushwa ya laki 500, 000.00 ili waniandikie ripoti nikakata, wakaninyanganya leseni na insurance yangu, mimi nikaondoka nakaenda kumshitaki kwa mkuu wa mkoa wa polisi, wakanirudishia lesini yangu ila hawakuniandikia ripoti yoyote, hiyo ndo hali halisi ya Tanzania ni rushwa na watu kutojaliana tena utu haupo tena. nakumbuka nilipokuwa mdogo gar zilikuwa zinalazwa nje na asubuhi unaikuta salama, siku hizi jaribu utakuta haipo, mtu akikwana na gari watu walikuwa wanamsaidia kusuku bure, siku hizi ni hatari tupu, mtu hata maji ya kunywa unaweza kunyimwa ukiomba, kwa kweli huu si utamaduni wetu wa kiafrika.

    ReplyDelete
  14. Wow! inasikitisha kumbe watu wote tunawaona kwenye ajali zikitokea wanakimbilia kuiba.

    Nimeona huyo mtu aliyepata ajali pamoja na gari kupindika mara tatu lakini akatoka na laptop yake kiunoni. Inasikitisha lakini inachekesha sana.

    Na kuandikiwa report ya ajali mpaka hongo? Siku hizi camera ndio ziwe report basi.

    Ndio maana Obama juzi kwenye interview alikua anasema hata kuekewa simu Africa mpaka ulipe hongo.....hao viongozi wao kama wanatakakuw partner na sisi lazima wawe responsible.....tunatia aibu...hivi JK hayaoni hayo?

    Kwanini isiwe adhabu kali sana kwa watu wanaotaka rushwa....Mimi naona watu siku hizi waanze kuwire up voice recorder mahali unajua mtu atakupiga mkwala halafu unampeleka kwenye sheria.

    Ndio maana hata watu wanaofanya kwenye ubalozi wetu kitu kidogo wanakuzungusha kweli sometimes najiuliza hivi wanataka nini? Now I know.......wanataka rushwa....

    ReplyDelete
  15. HAWA SI WAPIGANAJI, BALI NI WALINZI WA RAISI, LABDA TU KAMA LUGHA HIYO IMETUMIKA KUWAKWEZA. NINAWAPA POLE MAJERUHI WOTE.

    ReplyDelete
  16. Duh,hili puto kwa kuliangalia tu lilikuwa kwenye mwendo mkali.Thanks to God kwamba walikuwa wamefunga mikanda(nadhani).Poleni sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...