alex gwebe nyirenda jnr. akiwa na picha ya marehemu babu yake na wajina alex gwebe nyirenda leo kwenye makaburi ya kinondoni ambako shujaa huyu aliyepandisha mwenge wa uhuru kilele cha mlima kilimanjaro amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika mazishi ya kifamilia yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki katika makaburi ya kinondoni, baada ya misa katika kanisa la mtakatifu columbus.
msalaba wa kaburi la marehemu alex gwebe nyirenda
binti wa marehemu akipewa pole na waombolezaji wakati wa mazishi waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu alex gwebe nyirenda
jeneza likishushwa kaburini
mjane wa marehemu akiweka mchanga kaburini
ndugu jamaa na marafiki wakimzika marehemu alex gwebe nyirenda
sura za huzuni wakati wa mazishi
mjane wa marehemu akiwa na waombolezaji wakati wa mazishi. mbele ni mzee ally sykes nyuma yao ni brigedia jenerali mstaafu hashim mbita
baadhi ya waombolezaji wakisubiri mwili wa marehemu uletwe kwa mazishi. toka shoto ni mzee said el maamry, meja mstaafu kashmir, hamza kasongo, george kritsos na kanali mstaafu julius mbilinyi. alietupa mgongo hakuweza kutambulika mara moja
ANGALIA VIDEO YA SEHEMU YA MAZISHI HAYO KWA
KUBOFYA HAPA

WASIFU WA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA

Nyirenda alizaliwa tarehe 2 Februari 1936 Karonga Malawi, wakati wazazi wake wakiwa katika likizo ndefu ya Krismasi kutoka Tanganyika.
Alisoma shule ya msingi ya Mchikichini Dar- Es-Salaam na baadae shule za Sekondari za wanaume za Malangali (mkoani Iringa) na Tabora, hadi 1957.
Baada ya kuchaguliwa kuendelea na amali ya kijeshi, alijiunga na Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst kama Afisa Kadeti mwaka 1958 na baada ya kufuzu alirejea Tanganyika kujiunga na King’s African Rifles mwaka 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Afisa Kamili katika jeshi la wananchi la Tanzania na aliondoka jeshini kama Luteni-Kanali Agosti 1964.
Ilikuwa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliyempa heshima kwa kumpandisha cheo cha Brigadia pamoja na marehemu Brigadia mstaafu Moses nnauye.

Alikuwa Mtanganyika wa kwanza kuhitimu kutoka Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst, akiwa katika kombania ya Waterloo. Alikuwa afisa wa kwanza Mtanganyika katika King’s African Rifles 1960.
Alipewa heshima ya kupandisha bendera ya Tanganyika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro taRehe 9 Desemba 1961, ambapo wakati huo huo bendera hiyo ilikuwa ikipandishwa Uwanja wa Taifa katika mji mkuu wa taifa jipya la Tanganyika, Dar-es-Salaam.

Brigadia Alexander Donald Gwebe- Nyirenda alikuwa mwanachama wa Rotary Club, mzee wa kanisa la Kipresbiteri la Mtakatifu Kolombas, na mwanachama wa Gideons International.
Alikuwa mcheshi na wote waliomfahamu watamkumbuka kwa hilo. Alikuwa mwanamichezo hodari na alicheza Squash na Golf, mbali na Raga- amabayo aliacha kucheza akiwa na miaka 40- na soka- ambayo aliiacha akiwa na miaka 45!

Brigedia Nyirenda alifariki 20 Desemba 2008 mnamo majira ya saa 12 na dakika arobaini. Ilibainika alikuwa anasumbuliwa na saratani ya umio kutoka Februari 2008; ugonjwa huu ulimdhoofisha hadi alipofariki kutokana na malaria kali.

Alimuoa Hilda Simkoko na walibarikiwa kupata na watoto 5 ambao ni pamoja na Marehemu Alexandra Katie Katinda, Suzyo Maimba Leziya, Atupiye Tima Hope, Alexander Nkutondwa Foti na Tiwonge Buchizga Andrew.

Aidha walikuwa na wajukuu kumi ambao ni marehemu Kanyanta Sampa, Mpumelelo Malumo, Hilda-Katie Miller,Thungo Kuwani
Mkuzom Kuwani, Alexandra Gwebe-Nyirenda, Ethan Gwebe-Nyirenda, Naomi Nkumbula na Jordan Nkumbula.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI SHUJAA WETU HUYU
AMINA
UNAWEZA KUSOMA MAHOJIANO YA MWISHO YA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA NA BONGO CELEBRITY KWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mh. japokuwa sipo huko nyumbani, lakini kumbukumbu zangu zinanionesha kuwa askari kijana na mkakamavu Julius Mbilinyi (squash game preserver) ni Brigedia Generali na bado hajastaafu jeshi kwani amepanda ngazi hiyo hivi karibuni. Kama kumbukumbu zangu siyo sahihi mnaweza kunirekebisha.

    Lakini hata hivyo ningependa swali kulielekeza kwa Brigedia Generali Julius Mbilinyi vipi squash jamani mbona inafifia? tunakutegemea sana katika kuidumisha squash.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa na mungu amlaze pema peponi.

    Wasifu wa marehemu unaonyesha alikuwa ni nyota inayongara tangu ujana.

    Mtoa habari hakuelezea alipostaafu jeshi akiwa na umri wa miaka 28 tu mwaka 1964 akiwa afisa wa cheo cha juu yaani luteni kanali, Je marehemu kuanzia mwaka 1965 baada ya kustaafu jeshini mpaka 2008 alipitia ktk masuala gani zaidi ya kuwa mpenda spoti.

    ReplyDelete
  3. HAMNA CHUO CHA KIJESHI CHA KIFALME KATIKA U.K. MARA NYINGI MAJINI HUWA HAYATAFSIRIWI KUTOKA LUGHA MOJA KWENDA LUGHA NYINGINE NDO MAANA CHAMA CHA MAPINDUZI KITABAKI CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA LUGHA YOYOTE ILE, WEWE UMETAFSIRI SANDHURST ROYAL COLLEGE OF CADETS KAMA CHUO CHA KIJESHI CHA KIFALME HIYO SI KWELI. AFTER ALL ROYAL DOES NOT MEAN MFALME/KIFALUME. KING NDO MFALME

    ReplyDelete
  4. poleni jamani Suzio na Foti

    ReplyDelete
  5. hivi kuonyesha picha hadi makaburini, maana yake nini?

    ReplyDelete
  6. ni ajabu kwamba hakuna hata kiongozi yeyote wa kiserikali aliyekuwepo mazishini.Hii serikali yetu balaa.
    NB- Hivi ni kwa nini Tanzania hatuna makaburi ya serikali.Watu kama hawa wangezikwa kwenye makaburi special.
    Anyway najuwa kuna mtakaosema "kifo cha mlalahoi na poshi ni sawa" lakini pangetakiwa pawe na sehemu ya Kumbukumbu kwa waliochangia Taifa kwa hali na mali.Kupanda na kusimika Bendera na mwenge si jambo dogo.
    He was our HERO.
    RIP

    ReplyDelete
  7. R.I.P. Shujaa Nyirenda. Amen.

    SteveD.

    ReplyDelete
  8. Sura za serikali ziko wapi, wanajeshi wako wapi? ama kweli bongo tambarare! Yaani shujaa amesahaulika??

    ReplyDelete
  9. Wewe anonymous was December 25, 2008 12:15 AM ni mtu wa jabu sana. Wewe kila kitu ni criticism tuuu, does it mean that wewe uko perfect by 100% kama Mungu? Whether Royal means Mfalme au King au vinginevyo wewe sio professor wa dunia unayekosoa kila kilichoaandikwa. Wewe mwenyewe umetumia kiswahili kibovu kuliko vyote lakini unakimbilia kukosoa wenzio tu kila wakati. Sometimes kama huna hoja unakaa kimya. Hata kama unaishi Uingereza ukibeba maboksi na kujifanya wewe uingereza yakwako, basi tuache na tafsiri zetu mbovu na wewe ubaki na za kwako ambazo ni sahahihi. Mdau

    ReplyDelete
  10. Michuzi,

    umewateremsha vyeo hao askari wastaafu. wanaweza kuwa wakali kwelikweli kwa kitendo chako hicho.

    hapo kuna COL.KASHMIR ilikuwa awe CDF wa kwanza wa JWTZ lakini suala la rangi likamponza.

    mwingine ni BRIG.GEN JULIUS MBILINYI.

    MZEE SAID EL-MAAMRY naye zamani alikuwa Polisi. sifahamu alistaafu akiwa na cheo gani.

    Kulikuwa na Mwakilishi wa JWTZ ktk msiba? Amiri Jeshi Mkuu alituma salamu za Rambirambi?

    ReplyDelete
  11. Poleni sana wafiwa.

    Na wewe anon hapo juu mbona wachekesha? Hivi weye hujui kuwa kisiwa cha Uingereza ni cha kifalme? Queen Elizabeth II is the head of state and she is the head of British Forces. Mfalme mtarajiwa lazima apate mafunzo hapo na Prince Charles alishapitia zamani, wanae (Prince William and Harry) ambao wako kwenye royal lineage nao wamepitia chuo hicho alichosoma Mzee Nyirenda.

    Queen ndio anayefunga sherehe (graduation) za chuo hicho, akistaafu basi mfalme/malkia ateyekuwa madarakani ataendelea na system hiyo.

    Maofisa wote wa kijeshi wa ngazi za juu nchini Uingereza wanapitia/wamepitia hapo toka enzi za British Empire. Hata Idd Amin wa Uganda naye alisoma chuo hicho cha kijeshi nchini Uingereza.

    ReplyDelete
  12. MICHUZI NAONA NA WEWE UMEKWENDA KULA XMAS PIA MAANA NAONA HAKUNA MPYA YOYOTE YA LEO HAYA BASI XMAS NJEMA

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa Balozi,
    Kwanza natoa pole kwa familia nzima ya Mzee Brig. Nyirenda.

    Pili nitajaribu kutohoa maana ya
    Royal Military Academy Sandhurst = Chuo Kilichotukuka cha Kijeshi Sandhurst = Chuo cha Kijeshi Kilicho ktk Mamlaka ya Kifalme Sandhurst = Chuo Teule cha Kijeshi Sandhurst = Chuo Bwanyenye cha Kijeshi Sandhurst = Chuo cha Uongozi Ulitukuka cha Kijeshi Sandhurst.

    ReplyDelete
  14. Nyie watu munamshambulia huyu mtu ambaye kwa namna moja yuko sahihi hakuna chuo cha kiflume cha kijeshi cha UK, ni chuo cha maafisa wa jeshi kuanzia wa cheo cha chini kabisa. kwa sheria ya UK sawa mkuu wa nchi ni HEAD OF MONARCH awe king au queen, it is a simble, hana power yoyote kiutendaji. na si kweli maofisa wote wa jeshi la UK wamesoma hapo, wapo kibao waliosoma vyuo vingine vya USA, CANADA, ISRAEL nakadhalika, na si kweli kwamba walio inline to throne be either King or Queen lazima apitiea hapo hayo ni matakwa ya individuals. Wafalme nyuma ya queen wa sasa ni wengi tu hawakupitia jeshi, someni historia ya UK toka Monarch ilipoanza msiropoke tu kwa ajili ya kumbishia mtu aliyetowa maoni yake. Kuna vitu vingi tu hapa UK vinaneno ROYAL so utasema ni vya kifalme? msichekeshe, kwa mfano; ROYAL BANK OF SCOTLAND, ROYAL COLLEGE OF MUSIC, yaani insitute nyingi tu zenye neno ROYAL so ni za kiflume. NAWAKILISHA CHANGAMSHENI AKILI NA MUWE WATU WA KUCHAMBUWA MAMBO KIUNDANI, It is just a name, sasa unataka kuniambia J K NYERERE INTERNATIONAL AIPORT YA DAR NI YA NANI? IT IS JUST A NAME NA NAME WAKATI WOTE ALITAFSIRIWI YUKO SAHIHI.

    ReplyDelete
  15. HISTORY YA CHUO CHA KIJESHI SOMA HAPO CHINI, KILIANZISHWA KWA AJILI YA WATOTO WA WANAJESHI NA BAADAYE MADHUNNI YAKE KUKUA.

    History of the Royal Military Academy Sandhurst


    Modern-day officer training at the Royal Military Academy Sandhurst is the latest in the lineage of establishments stretching back to the formal establishment of the Royal Military Academy Woolwich in 1741 and the Royal Military College in 1800.
    The various sites of officer training for the British Army in history:

    High Wycombe
    Great Marlow
    RMC, Sandhurst
    RMA Woolwich
    Addiscombe
    RMA Sandhurst
    Mons College, Aldershot
    WRAC College Bagshot

    The history

    The Royal Military Academy at Woolwich, known as 'the Shop', was established in 1741 to educate the military branch of the Board of Ordnance to produce officers for the Artillery and Engineers. The two corps were referred to as the Ordnance Corps until 1856. Because there was strong competition to be selected to be selected as an Engineering officer, due to the good career prospects and interesting appointments, it was very much in the interest of gentleman cadets to study for their commissions. As regiments and corps were spun off on their own, so they maintained the same competitive system: sappers, gunners, signals and the tank corps. The RMA, Woolwich, remained open until 1939.

    In 1939, on the outbreak of World War II, RMA Woolwich closed and its senior students were commissioned into the artillery, engineers and signals. The remainder were sent to the territorial Officer Cadet Training Units. (Up to 1939 both RMA and RMC were fee-paying establishments.)

    The Royal Military College (RMC), established in 1800 was intended by Maj Gen John Gaspard le Marchant to be an Academy of three parts: a senior department for staff officer training, a legion for the sons of soldiers in the ranks, and a junior department for the training of gentleman cadets.

    Interestingly, only the previous year (1799) a school had been set up in High Wycombe and was operated by a French officer, General Jarry, on what amounts to a private finance initiative. This school was to teach staff duties to junior officers. The Private Finance Initiative shortcomings soon became clear and the school eventually became the Senior Department of the RMC in 1801. It remained at High Wycombe until 1814, moving to Farnham for seven years, and thence to Sandhurst, becoming Staff College in 1858.

    The RMC's Junior Department opened in 1802 at Great Marlow, but it was soon clear that the accommodation was unsatisfactory. William Pit had recently purchased Sandhurst Park, on the Exeter coaching road. It would be far enough away from London to prevent cadets becoming "distracted" by the lights of London. RMC moved into its purpose-built building, Old College, in 1812.

    RMC, Sandhurst, closed briefly in 1870 when the system of purchasing commissions was abolished, as the purchase system had been the main reason for attending the RMC - its successful cadets obtained their first commissions free. From 1877 competitive examination led to the appointment to a cadetship rather than a commission; RMC became the normal route to a regular commission.

    The India Military Seminary at Addiscombe, near Croydon, trained the officers of the East India Company's army. The seminary closed in the 1870s when the company's forces were transferred to the Crown. This caused the building of the two tridents at the back of Old College to accommodate gentlemen cadets for the Indian Army.

    New College was completed in 1912, built as a result of the enlargement accompanying the general shake-up accompanying public outcry over the shape of the army after the Boer War.

    At the outbreak of World War II, RMA Woolwich and RMC were closed and RMC students were either commissioned or remained at Sandhurst where they joined either the cavalry or infantry OCTU.

    The Royal Military Academy Sandhurst (RMAS) opened its doors in 1947 in the former RMC at Sandhurst.

    Short Service officer cadets and university graduates were trained separately at Mons College. Aldershot, until 1972, as a follow-on from arrangements for National Service short service officers who would not attend the full course for regular officers at RMAS.

    Woman Officer Cadets were originally trained at the Women's Royal Army Corps College at Bagshot. Their training was moved to RMAS in 1984 and they were later integrated into the standard training courses of the Academy.

    In 1992 a new one-year Common Commissioning Course was introduced, becoming the single point of entry for commissioned service in the British Army for all except clerical and medical officers.


    The current Academy site

    The site the Academy occupies was originally enclosed after the English Civil War by a local farmer who fenced off the area of Windsor Forest between the Blackwater and the Wish Stream, named Sandhurst Park. The area is wooded - a hurst - and situated on light soil - sand. At the end of the 18th century a retired officer bought the land together with Frimley Park. The farmer was forced to sell the park in 1800 to his wife's uncle, Prime Minister William Pitt. He in turn sold it on to the government a few months later with the purpose of becoming the site of the newly-created Royal Military College. The area around the Academy is dotted with ancient monuments such as the Iron Age hill fort, Caesar's Camp, to the north of the Barossa training area, and the Roman road, the Devil's Highway, running from East to West. Three counties meet just outside the Academy grounds, probably under the Tesco's car park, where the Wishstream marks the border between Surrey, Hampshire and Berkshire.



    HAMNA HATA SEHEMU MOJA WANASEMA NI CHA KIFLME. KUNA VITU VINGI VINA JINA ROYAL KWA MFANO, ROYAL SOCIETY OF ARTS - NLONDON, ROYAL COLLEGE OF MUSIC - MANCHESTER, ROYAL SCHOOL OF DEAF - MANCHESTER, ROYAL BANK OF SCOTLAND - ALL OVER UK, ROYAL MILITARY ACADEMY - SCOTLAND, ROYAL MILITARY ACADEMY - CANADA

    ReplyDelete
  16. Mh.Balozi
    Historia kamilifu ya marehenu Brig Nyirenda toka gazeti RAIAMWEMA
    Mwalimu Julius Nyerere alisema, Meja Alex Nyirenda akatenda. Mpira ukarudi tena kwa Nyerere ambaye safari hii alifanya kweli kuhakikisha kwamba Afrika nzima inakuwa huru kabla ya kufariki kwake Oktoba 14, 1999.

    Lakini Mwalimu alisema nini? Alisema: “Sisi tunataka kuwasha Mwenge, na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau.”

    Desemba 9, 1961 wakati bendera ya kikoloni ya Mwingereza inateremshwa kwenye Uwanja wa zamani wa Taifa mjini Dar es Salaam, Alex Gwebe Nyirenda, mwanajeshi Mtanganyika alifanya kile Nyerere alichosema.

    Lakini, si tu aliwasha mwenge kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, bali alisimamisha pia bendera ya Tanganyika huru ipepee kwenye kilele hicho kirefu zaidi barani Afrika.

    Katika miaka iliyofuata, Mwalimu Nyerere aliongoza mapambano kwa kuwa mwenyekiti wa nchi zilizo msitari wa mbele kusaidiana na wapigania uhuru kukomboa nchi ambazo bado zilikuwa zinatawaliwa kimabavu.

    Hivyo hadi anafariki Oktoba 14, 1999, hakuna nchi ya Afrika iliyokuwa inateseka kutokana na ukoloni wa aina yoyote.

    Kutokana na tukio hilo la kupandisha bendera na mwenge kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, Alex Nyirenda amekuwa alama muhimu ya taifa katika kutimiza azma ya Mwalimu ya kuona Afrika nzima iko huru.

    Lakini Jumapili iliyopita ya Desemba 21, 2008 shujaa huyo wa mwenge alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na kansa ya koo.

    Alilazwa kwanza katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo Kinondoni (THI), Dar es Salaam na baadaye Muhimbili kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi Februari mwaka huu.

    Baada ya kupata nafuu huko India, alirudi nyumbani Mei mwaka huu na kwenda tena India kwa vipindi viwili vya uchunguzi wa afya yake ilivyokuwa ikiendelea. Mara ya mwisho alitoka huko Septemba mwaka huu.

    Alex Gwebe Nyirenda alikuwa ni mmoja wa maofisa wachache Watanganyika katika jeshi lililoachwa na wakoloni la Tanganyika Rifles.

    Katika mahojiano ambayo nilipata kufanya naye Machi mwaka 2001 mjini Dar es Salaam, Nyirenda alisema hata uteuzi wake wa kwenda kupandisha bendera na mwenge kwenye Mlima wa Kilimanjaro ulitokana pia na cheo alichokuwa nacho.

    Lakini aliingiaje jeshini? Kwa mujibu wa maelezo yake, ukakamavu wake na kipaji cha uongozi alichokuwa nacho ni vitu vilivyomfanya mmoja wa walimu wake, aliyemtaja kwa jina la Grabbe kumwambia kwamba kazi itakayomfaa baada ya kumaliza masomo itakuwa jeshini.

    “Mimi nilikuwa kiranja wa shule tangu shule za msingi. Popote niliposoma nilichaguliwa kuwa kiongozi. Kwenye shule ya Sekondari ya Malangali nilikuwa mkuu wa bweni na baadaye kiranja mkuu wa shule,” alisema.

    Alipokuwa Tabora School alikuwa kiranja mkuu msaidizi. Kiranja mkuu alikuwa Wilbroad Ntuyabaliwe ambaye ni mzazi wa Miss Tanzania wa mwaka 2000, Jacqueline.

    Akiwa anafuata maneno aliyoambiwa na mwalimu wake, Nyirenda aliomba kuingia jeshini baada ya kumaliza masomo. Alipata majibu kwamba anatakiwa kufanyiwa usaili mjini Dar es Salaam.

    Miongoni mwa aliokutana nao katika usaili huo alikuwa Mirisho Sarakikya ambaye baadaye alikuja kuwa mkuu wa kwanza wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

    Nyirenda alisema kwamba Sarakikya wakati huo alikuwa akijulikana zaidi kwa majina ya Sam Hagai Sarakikya. Katika usaili huo kulikuwa pia na mwingine aliyekuwa na asili ya kiasia, S. M. A. Kashmir.

    Kwa mujibu wa Nyirenda usaili ulikwenda vizuri na wote walikubaliwa kuingia katika jeshi ambalo lilikuwa wakati huo likiongozwa na maofisa Waingereza.

    Nyirenda, Sarakikya na Kashmir walikuwa Watanganyika wa kwanza kuandaliwa kupelekwa Uingereza kwa masomo ya juu ya kijeshi yaliyokuwa yakitolewa katika chuo cha kijeshi cha Sandhurst.

    Walipofika Nairobi kwa ndege wakiwa njiani kwenda Uingereza walipata taarifa iliyowasikitisha. Kulikuwa kumeletwa simu ya maandishi ikimtaka mmoja wao, Sarakikya arudi nyumbani kwa madai kwamba alifeli mtihani wa Kiingereza hivyo hakuwa na sifa ya kuchukua masomo wanayoendea.

    Nyirenda alisema kwamba ilikuwa ni jambo la kushangaza kwa sababu Sarakikya alikuwa amefaulu vizuri masomo yote 12 ambayo yalikuwa kwa lugha ya Kiingereza hivyo alijiuliza ilikuwaje ashindwe somo la Kiingereza?

    Sarakikya ilibidi azuiwe Nairobi arudi nyumbani kufanya safari hiyo ya Sandhurst sasa iwe na Watanganyika wawili tu, Nyirenda na Kashmir.

    Nyirenda alisema katika mahojiano nami kwamba anaamini kuwa kitendo cha kumzuia kwenda Uingereza kilimpa nguvu Sarakikya kupambana vizuri na vizuizi vya maisha.

    Alisema Sarakikya alijibidisha kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kurudia mtihani wa Kiingereza waliokuwa wanadai ameshindwa. Alifaulu vizuri na hatimaye nay eye kwenda Sandhurst katika msafara mwingine wa Watanganyika wa kwenda huko.

    Akizungumzia masomo ya Sandhurst, Nyirenda alisema walipokuwa huko, kwa muda mfupi waliokuwa pamoja, yeye, Kashmir na Sarakikya walikuwa na mshikamano mkubwa na ulikuwa ni mshikamano wa aina yake ulioambatana na nidhamu ya hali ya juu ya kijeshi.

    Nyirenda alisema ni mshikamano kama huo na nidhamu ya hali ya juu ya kijeshi ambavyo vilimsaidia sana maishani kiasi na kufanya ailee vyema familia yake.

    Nyirenda alisema kuwa ubaguzi wa rangi wakati huo ulikuwa wa waziwazi. Ingawa yeye na Kashmir walikwenda Sandhurst wakiwa na sifa zinazolingana, walipofika huko Kashmir kwa vile alikuwa na asili ya Kiasia alionekana bora zaidi yake.

    Wakati mwenzake alianza mara moja kozi iliyowapeleka huko, yeye alitakiwa kwanza afanye mafunzo ya maandalizi ya miezi sita kabla ya kuanza kozi iliyowapeleka huko.

    Katika hali hiyo, Kashmir alimaliza mafunzo miezi sita kabla yake na kwa heshima ya jeshi, muda huo ulitosha kumfanya awe mkubwa zaidi yake. Kwa maneno mengine kuwa afande wake.

    Uasi wa jeshi uliofanyika Januari 1964 ndiyo uliomtoa Nyirenda jeshini. Alisema hakuhusika kwa namna yoyote na uasi huo, lakini matukio yaliyofuata baada ya uasi huo hayakumpendeza na aliona njia pekee ya kufanya ni kuliacha jeshi.

    Nyirenda alikuwa ni miongoni mwa maofisa wachache wa Kiafrika waliokuwa kwenye Tanganyika Rifles (jeshi aliloacha mkoloni). Kwa cheo chake alikuwa amepewa nyumba nzuri katika kambi ya Calito (sasa Lugalo). Pia kutokana na cheo chake alikuwa bega kwa bega na maofisa wenzake wakiwamo Waingereza.

    Alisema katika mahojiano nami kwamba ingawa askari wa chini walikuwa wanaujua ukweli huo, walikuwa hawataki kuukubali hivyo kumwona kama mtu anayejidai na anayejifananisha na Wazungu.

    Hata kitabu ha ‘Tanganyika Rifles Mutiny’ January 1964’ kilichochapishwa baada ya kuidhinishwa na JWTZ mwaka 1993, kinathibitisha mtazamo huo hasi dhidi ya Nyirenda.

    Pamoja na mambo mengine, kitabu hicho kinasema kwamba uwezo mkubwa wa Nyirenda wa kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiingereza ulimfanya awe karibu zaidi na maofisa Waingereza waliokuwa jeshini.

    Kitabu hicho kinasema kwamba katika uasi huo, wanajeshi walioshiriki walikuwa wakibishana ni nani anayefaa kuwa kiongozi watakayempandisha cheo kuwa Brigedia kati ya Luteni William Chacha na Kapteni Nyirenda.

    Nyirenda aliyekuwa amesoma katika Shule za Sekondari za Malangali na Tabora Schoool na baadaye kupata mafunzo ya juu Sandhurst, Uingereza ndiye aliyeonekana kuwa na sifa kubwa zaidi. Lakini wengi walimkataa kwa vile walikuwa wanamwona kama Mzungu aliyekuwa amejivika ngozi nyeusi.

    Aidha, tabia yake ya kucheza ‘michezo ya Kizungu’ kama skwashi na tenisi ilikuwa inawakera baadhi ya watu kwa kumwona kuwa anajidai.

    Kitabu hicho kilichoidhinishwa na JWTZ mwaka 1993 kimedai kwamba wakati wote wa uasi Nyirenda alichukua jukumu la kuhakikisha kwamba wake wa maofisa wa Kizungu pamoja na mbwa na paka wao wanakuwa salama.

    Baada ya kubishana sana kuhusu nani wamfanye mkuu wao wa jeshi, wakaamua kumfanya kuwa Brigedia, ofisa mdogo katika jeshi, Luteni Usu Elisha Kavana.

    Hata Kavana mwenyewe alishitushwa mno na uteuzi huo na kupanda huko kwa cheo kusikokuwa kwa kawaida na kufanywa mkuu wa jeshi.

    Kavana alikuwa miongoni mwa maofisa waliokamatwa na alipoambiwa kwamba amefanywa kuwa Brigedia hakuamini masikio yake. Kitabu hicho kinasema alipoonyesha wasiwasi alitishwa kwamba asipokubali atauawa hivyo hakuwa na la kufanya ila kukubali tu.

    Kavana ananukuliwa na kitabu hicho akisema: “Mmoja wa askari aliingia katika chumba ambacho tulikuwa tumefungiwa na kutaja jina langu. Luteni Marwa akaniombea heri na kusema ananisikitikia.”

    Aliendelea kusema: “Nilikuwa siwezi kuliongoza jeshi lakini nilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa familia za maofisa zinaendelea kuwa salama.

    “Ningewezaje kuliongoza jeshi. Ilikuwa ni ndoto. Ninaamisha kuwa suala zima lilikuwa halileti maana. Nilikuwa naachiwa kutoka kuzuizini na kufanywa Brigedia! Lilikuwa ni jambo lisilokuwa la kawaida kabisa.”

    Kavana ameelezwa katika kitabu hicho kwamba alikuwa anashangaa ni kwa vipi askari wa kawaida wakawa na uwezo wa kumfanya kuwa Brigedia . “Hivyo niliposita kupokea kofia nyekundu (ya ubrigedia) askari wakatishia kunipiga risasi papo hapo.”

    Je, ni kweli kwamba wakati maofisa walipokuwa wakikamatwa, Nyirenda alikuwa katika harakati za kulinda wake, mbwa na paka wa Wazungu?

    Katika mahojiano hayo Nyirenda alikataa kata kata kwamba alifanya jambo hilo. “Ningefanya vipi hivyo wakati na mimi nilikuwa nimekamatwa?” aliuliza.

    Alsiema kuwa yeye, kama walivyokuwa maofisa wote katika kambi ya Calito, alikamatwa hivyo alikuwa hajui ni kitu gani kinachoendelea.

    Alikiri kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano mzuri na maofisa wa Kizungu jeshini lakini uhusiano huo ulikuwa wa kikazi kulingana na vyeo vyao na si zaidi ya hapo.

    Lakini alisema ya kuwa pamoja na kuelewana mno na maofisa wa Kizungu, na yeye alikuwa anapata shida kama ‘weusi’ wenzake kutokana na rangi yake.

    Alisema kuwa mara kadhaa alijikuta anazuiwa kuingia katika sehemu wanazoingia Wazungu tu na hiyo wakati mwingine ilikuwa inawakera hata maofisa wenzake wa Kizungu aliokuwa akiambatana nao na kumpigania aruhusiwe kuingia.

    Anaitaja Dar es Salaam Club ambayo baadaye ikafanywa kuwa Hoteli ya Forodhani (sasa Mahakama ya Rufaa) kuwa ni sehemu mojawapo aliyokuwa akiingia kwa shida kutokana na rangi yake.

    Sehemu nyingine ambayo alisema anaikumbuka kuwa alinyanyasika kwa sababu ya rangi yake ni Itigi ambako walikuwa ziarani na maofisa wenzake wa Kizungu kuwashawishi vijana wa Tanganyika kujiunga na jeshi.

    Je, nini ulikuwa mtazamo wake juu ya uasi uliofanyika jeshini ambao ulitikisa taifa na kumfanya Mwalimu na msaidizi wake wa karibu, Rashidi Mfaume Kawawa waikimbie Ikulu?

    Nyirenda alisema kuwa askari wa chini waliokuwa na madai lukuki kwa serikali walikuwa na haraka mno. Mambo waliyokuwa wakiyataka si ya kufanywa kienyeji kama walivyokuwa wanafikiria.

    Alisema ya kuwa serikali ilikwisha kutoa ahadi kuwa suala la ‘africanization’ (kutoa vyeo kwa Watanganyika) litafanyika lakini wao hawakutaka kuwa na subira.

    Alisema ya kuwa wao kwa kuwa Waafrika walitaka kupewa upendeleo usiokuwa wa kawaida jambo ambalo lilikuwa haliwezekani kwani walikuwa katika chombo nyeti cha taifa.

    Nyirenda alisema kuwa vyeo vya jeshi ni nyeti kama madaraja ya madaktari hospitalini. Alisema ya kuwa watu wanapanda kwa hatua kulingana na sifa wanazokuwa nazo na si hivi hivi.

    “Ni kama hospitalini, mfunga vidonda hata kama ni mchapakazi namna gani, hawezi, akapanda ghafla bali kwa mlolongo wa kazi yake. Hawezi ghafla akapanda kuwa daktari,” alisema.

    Alisema kuwa askari wa chini wakati huo walitaka kuvunja mwiko huo kwa kutaka vyeo vitolewe kama pipi.

    Nyirenda aliamua kutoka jeshini kufanya shughuli nyingine za kuendeshea maisha yake miezi michache baada ya uasi huo kuzimwa na majeshi ya Uingereza na Tanganyika Rifles kuundwa upya kuzaliwa kwa JWTZ.

    Ni kwa nini Nyirenda aliamua kufanya hivyo wakati alikuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa jeshi hilo?

    Katika mahojiano hayo, Nyirenda alisema alifanya uamuzi wa kuachana na jeshi baada ya kufadhaishwa na kebehi za mara kwa mara alizokuwa akizisikia kuwa si Mtanganyika halisi.

    Alisema ya kuwa kebehi hizo zilianza kuota mbawa wakati wa uasi wa jeshi. Baada ya maofisa wote kukamatwa akiwamo yeye, kukawa na mjadala wawafanye nini baada ya kuwakamata.

    Alisema walifikia uamuzi wa kuwarudisha Uingereza maofisa wote Waingereza. Walipofika kwa Kashmir kwa kuwa yeye alikuwa na asili ya kiasia wakasema anarudishwa kwao Bombay.

    Walipofika kwake Nyirenda wakasema watamwingiza katika kundi la Waingereza kumrudisha Uingereza kwa kuwa ati na yeye ni Mzungu.

    Wakaleta lori maalum ambalo waliwapakia maofisa wote wa Kizungu pamoja na yeye kwa safari ya kwenda Uwanja wa Ndege ili warudishwe Uingereza.

    Lakini haikuwa hivyo, kwani lori hilo lilikwenda kuwabwaga sehemu nyingine na siyo Uwanja wa Ndege kama ilivyokuwa imetangazwa na hao askari wa kawaida kwenye kambi ya Calito.

    Nyirenda alisema kwamba hata baada ya uasi kuzimwa, kebehi za hapa na pale ziliendelea kusikika dhidi yake.

    “Safari hii walikuwa hawasemi tena kwamba mimi ni Mzungu, bali walikuwa wanasema kwamba ni Mnyasa,” alisema.

    Nyirenda alisema kuwa madai hayo yalimshangaza kweli kwa sababu Nyasaland, nchi ambayo sasa inaitwa Malawi hakuwa anaikubali kuwa ni nchi yake.

    Hata hivyo, alikiri kwamba ni kweli kwamba wazazi wake wana mizizi ya huko, lakini maisha yao yote yalikuwa Tanganyika.

    Alisema kuwa yeye alizaliwa Karonga, Nyasaland Februari 2, 1936 kwa bahati mbaya tu kwani wazazi wake walikwenda huko kwa likizo kutembelea ndugu mama yake akiwa na mimba yake.

    “Mimi leo (mwaka 2003) ukinipeleka Malawi ni kama unanionea. Inawezekana kweli nina ndugu ambao wanatoka katika koo za wazazi wangu lakini mimi mwenyewe sijawahi kuishi huko na sikujui,” alisema.

    Alex Gwebe Nyirenda alipata elimu yake ya msingi katika shule za Mchikichini mjini Dar es Salaam na Mlandege, Iringa kabla ya kwenda Shule ya Sekondari ya Malangali, Iringa na baadaye Tabora School.

    Alikuwa akiwakumbuka wengi aliosoma nao. Miongoni mwao ni Brigedia mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa naye darasa moja na Bakari Mwapachu aliyekuwa nyuma yake.

    Mwingine ni aliyekuwa jaji Mkuu, Francis Nyalali ambaye alikuwa mbele yake katika Shule ya Sekondari ya Malangali. Pia mwanasheria Peter Bakilana aliyekuwa naye darasa moja Tabora School.

    Wengine ni Hatibu Lweno aliyekuwa mbele yake na Jaji Lameck Mfalila aliyekuwa nyuma yake. Pia alisoma na Godwin Kaduma katika Shule ya Malangali.

    Kiongozi wa siku nyingi wa mpira wa miguu nchini ambaye pia ni mwanasheria, Said Hamad El Maamry na Bob Makani walikuwa mbele yake Tabora School.

    Aliyekuwa balozi wwa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Daud Mwakawago alisoma naye Shule ya Msingi ya Mlandege, Iringa.

    Baada ya kutoka jeshini alifanya kazi katika kampuni binafsi ya BP Shell ambayo kwanza ilimpeleka kufanya kazi Nairobi, Kenya kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kurejea tena Dar es Salaam.

    Baadaye aliiacha kampuni hiyo na kuingia kazi katika kampuni nyingine binafsi ya AMI. Kampuni hiyo ilimpeleka Zambia kufanya kazi kwenye tawi lake la nchi hiyo.

    Alikuwa Zambia kwa miaka 18 na kurejea Dar es Salaam kuendelea na kazi katika tawi la kampuni hiyo.

    Wakati Tanzania inapigana vita yake na nduli Idi Amin wa Uganda mwaka 1978/79, Nyirenda alikuwa nchini Zambia.

    Nyirenda amefariki akiwa na watoto wanne baada ya mtoto wake wa kwanza wa kike kuzaliwa kufariki dunia.

    Je, anajuta kwa nini aliliacha jeshi? Katika mahojiano hayo Nyirenda alisema hajutii hata kidogo uamuzi huo akisema maisha ni popote na mtu hawezi kulazimisha mambo ambayo hupangwa na Mungu.

    “Ninachoweza kusema tu ni kwamba nilipokuwa jeshini nilitimiza wajibu wangu kama Mtanganyika ninayeipenda nchi yangu,” alisema.

    Hadi katika miaka ya mwisho ya uhai wake, Nyirenda aliendelea kuwa mtu anayendelea kucheza skwashi na tenisi katika Klabu ya Gymkhana, Dar es Salaam ambako alikuwa mdau mzuri.

    Source:www.raiamwema.co.tz 24/12/08

    ReplyDelete
  17. Just kuongezea, huyu aliyetupa mgongo ni Brigadier-General mstaafu Burton Lupembe, mmoja ya wanajeshi wakongwe Tanzania na aliyehitimu Sandhurst pia.

    ReplyDelete
  18. NI KWELI HUYO ALIYETUPA MGONGO NI BRG.GEN.LUPEMBE MMOJA WA MAKAMANDA WAKONGWE WA JWTZ NA ALIKUWA MSAIDIZI WA KAMANDA MAYUNGA KWENYE VITA YA KAGERA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...