MAJOR NYIRENDA AKIWEKA MWENGE WA UHURU KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO MKESHA WA SIKU YA UHURU WA TANZANIA BARA DESEMBE 9, 1961
MAJOR NYIRENDA AKIWA NA MWENGE WA UHURU ALIUOPANDISHA MLIMA KILIMANJARO
MWALIMU NYERERE NA MAJOR NYIRENDA WAKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA HAFLA YA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANZANIA BARA IKULU, DAR. PICHA HIZI ZIPO PIA http://www.bongocelebrity.com/ KATIKA MAHAKAL YA MAHOJIANO YA HIVI KARIBUNI


MAJOR ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA ALIYEPANDISHA MWENGE WA UHURU JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO SIKU YA MKESHA WA UHURU WA TANZANIA BARA, HATUNAYE TENA.

HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI TOKA KWA FAMILI YAKE ZINASEMA MAJOR NYIRENDA ALIFARIKI JANA SAA MOJA JIONI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA. ALIKUWA NA UMRI WA MIAKA 72.

ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI YA KANSA KWA MUDA MREFU NA AMESHAKWENDA MARA KADHAA NCHINI INDIA KWA MATIBABU.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO ZA KIFAMILIA, MAZISHI YATAFANYIKA DAR JUMATANO KATIKAMAKABURI YA KINONDONI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU MBEZI BEACH, FLETI ZA NATIONAL MILLING, KUCHEPUKA NJIA YA KWENDA AFRICANA, DAR.

GLOBU YA JAMII INATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU, JAMAA NA RAFIKI WA MAJOR NYIRENDA AMBAYE ATAKUMBUKWA DAIMA KWA HISTORIA ALIYOIWEKA SIKU YA MKESHA WA KUPATA UHURU DESEMBA 9, 1961.
SOMA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA BONGO CELEBRITY HIVI KARIBUNI KWA KUBOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. `Shehena ya Barrick ilikuwa na mabomu`

    2008-12-20 14:41:55
    Na Grace Chilongola, Mwanza


    Ukaguzi uliofanywa kwenye shehena ya kampuni ya dhahabu ya Barrick Tanzania, iliyozuiliwa kwa muda katika uwanja ndege wa Mwanza imebainika kuwa ni mabomu ya kurushwa kwa mkono na yale ya kutoa machozi pamoja na risasi.

    Ukaguzi huo ulifanywa kwa kushirikisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Usalama wa Taifa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

    Katika mahojiano na waandishi wa habari ofisini kwake, Meneja Forodha wa TRA Mwanza, Leopold Kihumo alisema wao kama TRA baada ya kupata taarifa ya shehena hiyo waliikabidhi polisi kwa ajili ya utaratibu wa ukaguzi.

    ``Shehena kama hizo zikiingia TRA (forodha) huwa hatujiridhishi peke yetu na badala yake tunashirikiana na taasisi nyingine kama za jeshi la Polisi, JWTZ na Usalama wa Taifa,`` alisema.

    Kwa mujibu wa Kihumo shehena hiyo iliyokuwa ifike Desemba 5, ilichelewa kuondoka kwa ajili ya kuvipa nafasi vyombo vingine kufanya ukaguzi na kwamba ilikuwa na uzito wa tani 1.4 ambapo ililipiwa kodi inayofikia Sh. Mil 144.

    Kihumo alisema shehena hiyo ilitumia taratibu zote za kuombewa kibali na ndio maana baada ya kujiridhisha na ukaguzi iliruhusiwa kuendelea na safari.

    ``Shehena kama hii huwezi kuiacha ikaingia mtaani bila kukaguliwa na ndio maana walishirikisha vyombo vingine na walipojiridhisha Kamanda wa Polisi aliruhusu viendelee na safari na kutoa polisi wanne kwa ajili ya kusindikiza,`` alisema.

    Hata hivyo, alisema baada ya ukaguzi walipendekeza shehena kama hizo ziwe zinaagizwa na wakala wa serikali wanaojihusisha na silaha na sio mwekezaji.

    Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Khamis Bhai alisema taarifa aliyopewa asubuhi na Afisa Upelelezi wa Mkoa, Agustine Olomi alimweleza shehena hiyo ilikuwa na baruti za kulipulia miamba.

    Gazeti hili liliripoti kuwepo kwa shehena inayosadikiwa kuwa na baruti za kupasulia miamba, risasi na mabomu ya kurusha kwa mikono na yale ya kutoa machozi mali ya kampuni ya Barrick imezuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Mwanza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kubaini vitu vilivyomo.

    Wakati huohuo, Simon Mhina anaripoti kuwa kampuni ya Barrick imesema mzigo wake uliodaiwa kukamatwa mjini Mwanza haukuwa na silaha.

    Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Teweli Teweli, alisema Barrick haina sababu zo zote za kusafirisha shehena kama hizo kwa vile hazitumii katika shughuli zake za uchimbaji madini.

    Akifafanua, alisema hivi sasa walinzi wake hawaruhusiwi kabisa kutumia risasi za moto, na ndio maana hata mgodi wake ulipovamiwa hivi karibuni na wakazi wa Tarime walilazimika kukimbia.

    ``Shehena yetu haikuwa na mabomu wala risasi, hatuna sababu yo yote ya kuagiza vitu hivyo,`` alisema.

    ReplyDelete
  2. nyie wabara nanyi mna hashuo na kujitoa fahamu. hivi wakati mnapata huo uhuru wenu mlikuwa na jina hilo la Tanzania Bara? kwanini hamlitaki jina lenu la Tanganyika? Mungu atawasaidia, sie twaendelea kudai haki na nchi yetu pendwa, Zanzibar.

    Mzanzibari

    ReplyDelete
  3. We'll always remember that special smile, that caring heart, that warm embrace,

    Rest in peace.

    UK

    ReplyDelete
  4. Rest in Peace our National Hero!

    ReplyDelete
  5. R.I.P Nyirenda,utakumbukwa kama shujaa wa nchi yetu siku zote.
    Mdau Ugiriki

    ReplyDelete
  6. RIP ! Alex Gwebe Nyirenda! We loved you alot but God loved you most that's why he had to prove to us that he only takes the best! Chiuta wamovwirani, mfike makola!

    ReplyDelete
  7. Mungu amlaze mahali pema peponi na poleni wafiwa.

    Hawa watu ndio wanatakiwa kuwekwa kwenye vitabu vya historia. Wala nilikua sijui jina lake ila nakumbuka kuwa kuna mtu alipandisha mwenge wa uhuru hapo Kilimanjaro.

    Tunatakiwa tuwaenzi watu wetu hawa.

    ReplyDelete
  8. maisha haya jamani ni mafupi kuliko tunavyofikiria, juzi tu alikuwa anaojiwa na bongo celebriry leo kafa. Familia Mungu awatie nguvu. je marehemu alikuwa na watoto wangapi na wake wangapi?

    ReplyDelete
  9. Marehemu ameacha mke na watoto wanne (4) pamoja na wajukuu saba (7).

    ReplyDelete
  10. pole sana suzyo from your aunt.

    ReplyDelete
  11. Jamani neno kumuenzi mtu si lazima awe amekufa, kama mtu amefanya jambo la kizalendo la kujitoa mhanga au kipiganaji ni vema kiokosi/ tunzo/nishani whatever ziwapate kabla hawajafikwa na mauti au kuitwa marehemu au hayati, Jamani maua juu ya kaburi maana yake niniiiiii? ukifa ndo mashada yanamiminikaaa,Huyu mzee enzi za uhai wake alipokuwa mgonjwa, alisahaulika mpaka watoto wake wakaanza kupiga kelele kwenye vyombo vya khabari kuomba msaada wa kuokoa au kupigania maisha yake, kwani huyu mzee hakustahiliwa kihivyo mpaka watoto wanasimama kwenye TV na kulalamika kuwa mchango wake umesahaulika! narudia kuenzi wazee waliotoa michango yao mikubwa kuwafae wakati wako hai ili kuwaenzi wenyewe wakiona kisha tuendelee na historia na kumbukumbu.

    Poleni wafiwa, tuko nanyi kimawazo katika huzuni yenu,hii ni hatma ya kila bin-adam mungu amrehemu mzee wetu.

    ReplyDelete
  12. Marehemu kaacha mke. Marehemu alikuwa ana watoto watano. Mmoja (first born) alifariki mwaka 1990 ndani ya train ya TAZARA akitoka Dar kuelekea Lusaka. Huyo binti aliweka historia ya kuwa msichana wa kwanza mweusi kuongoza Student Association pale OXFORD University nchini Uingereza alipokuwa anasoma.

    RIP

    ReplyDelete
  13. Michuzi.....uhuru wa 'Tanzania Bara'? Hakuna kitu kama hicho! Ni uhuru wa Tanganyika.

    ReplyDelete
  14. NAWATAKIA POLE SANA WAFIWA HASAHASA WALE WANYASA WA MALAWI WAKINA SHABA, MTAWALI, GONDWE,MSOWOYA , KAMANGA, KWA MSIBAHUU MKUBWA ULIOWAKUTA . NAMFAHAMU MZEE HUYU SANA . HAWA NI WALE WATU WAMALAWI WA KWANZA WALIOL;ETA MAENDELEO NCHINI KWETU POLENI RONI MTAWALI NA WAKINA GRACE SHABA NA FOTI NA WENGINE .

    ReplyDelete
  15. kaela kamanga wa houston poleni kwa msiba huu

    ReplyDelete
  16. Profesa mmoja wa Havard University aliwahi kutoa theory kwamba sababu mojawapo ya kuyeyuka kwa barafu mlima Kilimanjaro ni huo mwenge. Waafrika na ujinga wetu siku zote hatukufikiria kwamba ukiwasha moto/joto karibu ba barafu, barafu itayeyuka!

    RIP Major Nyirenda. Ni kweli, it's crazy juzi tu kulikuwa na mahojiano naye (ambayo niliyasave kwa kumbukumbu), mara ametutoka.......mavumbini tutarudi.

    ReplyDelete
  17. Sasa wewe unayesema nanukuu "Waafrika na ujinga wetu siku zote hatukufikiria kwamba ukiwasha moto/joto karibu ba barafu, barafu itayeyuka!"
    Nikuulize swali moja tu?????!!!!
    ulitaka mwenge uwekwe wapi??????
    Nyumbani kwa Mwl. Nyerere?, Kwa Mjr. Nyirenda mwenyewe au ulitakaje????

    Angalieni maneno ya kuandika jamani, Pamoja na ujinga Uhuru tulipata, Uliwekwa kwa makusudi uweze kumulika dunia nzima ili wajue tupo HURUUUUUUUUUUU, SHABASH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...