NAEEM ADAM GIRE
MFANYABIASHARA NAEEM ADAM GIRE AMEFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU JIJINI DAR LEO AKIKABILIWA NA MAKOSA YA KUGUSHI, KUTOA HATI ZA UWONGO NA KUTOA TAARIFA ZA UWONGO KUHUSU UWEZO WA KAMPUNI YA RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY KUWA NA UWEZO WA KUZALISHA 100MW ZA UMEME TANZANIA.

MBELE YA HAKIMU MKAZI MH. WARIARWANDWE LEMA, MSHTAKIWA AMEKANA MASHITAKA NA AMEPELEKWA RUMANDE HADI KESHO WAKATI OMBI LAKE LA DHAMANA LITASIKILIZWA.
HABARI KAMILI
BOFYA HAPA (KIINGLISHI)
AMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Braza Michu

    Naomba kuuliza. Nasikia sana kwenye bendi zetu mapredejee wakiimbwa.

    Hivi Maana ya Predejee ni nini?

    ReplyDelete
  2. Heheheeeee....
    ngoma inogile! Hatimaye RICH-MONDULI imeanza kuguswa, I'm sure KAGODA itasogelewa japo kwa karibu...

    ReplyDelete
  3. Habari nzuri kuwa sasa angalau kila pesa kubwa ya nchi ikihisiwa imetumika visivyo uchunguzi wa kipolisi unafanyika na watuhumiwa kufikishwa mahakamani.

    Hii itarudisha utawala bora na kuwafanya watu wafikirie mara mbili kabla ya kutumia vyeo/nafasi/ rushwa kujinufaisha.

    Ila na serikali iwe inazifikiria mahakama kupewa fedha za kutosha ili kuweka mazingira ya majengo yake masafi.

    Maana naona katika picha hii utando wa buibui wenye vumbi la miaka kibao.

    ReplyDelete
  4. Duh!! Kweli simba mimya ndiyo muwindaji!!!

    Ndiyo JK, tunaona cheche zako raisi wetu. Tupo nawe katika kuhakikisha rasilimali za umma ni kwa ajili ya umma na siyo kwa ajili ya wachache ambao wanazitumia kunenepesha matumbo yao na kuhudumia nyumba ndogo nyingiiiiiii

    ReplyDelete
  5. Anonymious hapo juu, nikuite jirani, mbona uko nje ya mada.
    Heko Jakaya wakate woooooooooooooote, wapambane na mkono wa sheria, halafu ukikangalia asilimia kubwa ya 'wadau wa ufisadi' ni WAHINDI

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaaa sio wa pale RICHMONDINTERNET CAFE,pale mnazi mmoja, Dar?, wadau mnao jua tuelezeni wajameni, mimi huenda enda saana pale kwa mambo ya mtandao.

    ReplyDelete
  7. MICHUZI NAOMBA KUTOA MAONI YANGU HAPA MIMI SIONI KAMA HUYU MZUNGU NI MWIZI ANA HELA NYINGI SANA ALIZO RITHI KUTOKA KWA FAMILIA YAKE VIZAZI VILIVYO PITA ANA HELA NYINGI SAAANA SASA HUTO TUHELA TWA RICHMOND WATAKUWA NI WABUNGE TU WAMEGAWANA SASA WANATAKA KUMWANGUSHA. NASHANGAA MAMBUMBUMBU MENGINE YATACHEKELEA ETIHUYU MZUNGU AMESHIKWA BILA KUJUA HII NI GELESHA DANGANYA TOTO TU ILI TANZANIA IENDELEE KUPATA MISAADA YA NGUVU KWA KUONESHA INASHIKA MAFISADI. HUYU JAMAA MZUNGU NIMEMFANYIA KAZI NYINGI HANA MAKUU NA NITAJILI MKUBWA SANA HAPA BONGO NA EAST AFRIKA. ALINILIPIA HATA ADA YA SHULE NILIPOKUWA UNIVERSITY OF MUZUMBE KULE MULOGOLO ALIFURAHISHWA SANA NA MAKSI ZANGU ZA JUU AKANIPA UMARKETING MANAGER, MPAKA LEO HII WANAKUJA KUMSHIKA KWA AJILI YA DANGANYA TOTO. ASANTE MICHUZI KWA KUNIPA NAFASI KUTOA MAONI YANGU YA BUSARA NA HEKIMA NASUBILI MAMBUMBUMBU YAKURUPUKE NA KUONGEA PUMBA KAMA KAWAIDA YAO.

    ReplyDelete
  8. Kha! Natumai peter atakuwa nalitolela feki maana hata kiswahili hajui au unataka watu woshe vinywa tu hapa, kwanza huyi si mzungu hata sijui napoteza muda wangu wa nini kukuelezea

    ReplyDelete
  9. anon hata mimi namshangaa huyo jirani yako jinsi alivyotoka nje ya mada.WATU WENGINE BWANA WANAKERA SANA SEMA HAWAJUI TU.wee nawe nani mzungu sasa hapo????eti mzungu

    ReplyDelete
  10. we anonymous wa 13jan 9.18pm acha kutuzingua!..na ukome kutupiga mikwara wachangia mada bora

    we kulipiwa ada isiwe sababu ya huyo mtu kutokuwa mwizi sisi hatuangalii ana pesa za urithi au vp tunachotaka hela za walalahoi kama sisi zirudishwe
    kama kaiba ni ameiba tu hakuna cha unamjua wala anakujua hayo mambo yenu wenyewe mtajiju kivyenu

    ReplyDelete
  11. hahahah! Camon Peter you must be kiddin right? University? Aisee wewe kwa jinsi ulivyo mchovu hata katika kuandika lugha yako(kiswahili) lazima umeishia darasa la tatu na kwa huyo mhindi ambaye wewe unadhani ni mzungu ulikuwa mlinzi au houseboy flani.Angalia sana Watanzania tuna hasira sana sasa hivi tusije tukakuunganisha nae huyo bosi wako kima we.
    Mdau

    ReplyDelete
  12. Ndugu yangu Peter Nalitolela wa ex-Muzumbe Chuo kikuu, naona kitanda chako pale hospitali ya vichaa Mirembe kinaandaliwa/kinakusubiri. Sijui maisha ya Bongo maskini yamekuchanganya akili? Ningeweza ningekusaidia kuja huku kupiga boksi.

    ReplyDelete
  13. Nimegundua kitu. ishu ikiwa inwahusu warangirangi basi sisi wazawa tunasheherekea. ukweli ni sisi tuliokua na matattizo. Tunaa budu njaa. Ivi niambieni juu ya mahela yote alikuanayo kigoda na ndugu zake walioko madarakani na bado hayaridhiki. Sasa kama si kuabudu njaa ni nini tena?
    Hata kahera kido tu hiyo midomo wazi hii njaa itaisha lini? Hata kesi ya kugonga mbwa Dar basi hiyo mijitu inataka rushwa.

    Kitu muhimu ni mahaka iwe fair hata ikibidi akina kigona na ndugu zake wawajibike

    ReplyDelete
  14. HUYU JAMAA AMETUMIA (ADDRESS/MAKAZI/AKAUNTI) YA UGENINI KUHUJUMU TANZANIA. RAHISI KUMPATA/NASA YEYE NA WASHIRIKA WAKE.

    ReplyDelete
  15. Problem ya nyie black people mtabaki na wivu wenu ivyo ivyo. Amtaendleya. Muna akili ndogo kama kuku. Mnabaki kulaumu wageni kumbe mnajiibia wenyewe kwa tamaha ya vitu kidogo.

    Wivu tu. Bado tutaendleya kupata faida juu ya vichwa venyu paka siku mpate akili.

    ReplyDelete
  16. mdau wa kwanza pedejee ni muunganiko wa herufi tatu za kifaransa na zote zimeunganishwa kuleta maana flan.waunganishaji ni vijana wa kiuni wa kongo ya
    kabila.
    pe for president

    de for director

    ge for general

    unapata pedege inasomeka kwa matamshi ya kiswahili isvyo rasmi kama pedejee
    by Ismail dsm

    ReplyDelete
  17. Mr. Michuzi, ahsante na pole kwa kazi, usinibanie tafadhali haka kamaoni kangu.

    Watz naomba tujiulize na kutafakari kwa kina. Watu weengi wameshakamatwa na kufikishwa mahakani kwa tuhuma za kifisadi. Je ni wangapi wameshahukumiwa kwa makosa hayo? Mwanzo tuliambiwa uchunguzi unafanyika kabla hawa jamaa kufikisha kizimbani. wameanza kufikishwa mahakani, zaidi ya kufikishwa kwa makeke, wanaishia nje kwa dhamana, na inakua jii kidogo kidogo.

    Mbona kesi za kina Mzee Sea na wanawe zilisikilizwa haraka na hukumu kutolewa mara moja? TID nae nae hakuchukua muda kuhukumiwa, au sivyo? Walala hoi ambao wanaondoka Bongo kwa kutafuta maisha bora, wakirudishwa nyumbani hawachukui muda kuhukumiwa. Wakiambiwa wameondoka kichume cha sheria, walala hoi hawa hata familia zao haziwezi kumudu dhamana. Sheria kwa walala hoi tu?

    Watz, tusirubuniwe kwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Hawa jamaa na walikua madarakani lao moja. Tunataka kuona hukumu zao zinafanyika haraka kutoka kwa Mahakimu. Kama walivyokua wapo haraka kuwahukumu Mzee Sea, TID, Wezi wa kuku, storaway na walala hoi wengine.

    ReplyDelete
  18. Anony wa kwanza, nakusaidia:
    Pe-de-jee unayosikia ni matamshi ya herufi tatu kwa Kifaransa PDG ambayo humaanisha Président Directeur Général, au CEO kwa mfumo wa Wamarekani au Managing Director kwa mfumo wa Watanzania. Huko Kongo na kwingineko watu hutumia maneno haya kumaanisha kuwa jamaa mambo yake ni ulimswano hata kama hana kazi ila ana kitambi na mavazi ya kiajabu.

    Mwisho napendekeza na wewe tukuite Pe-de-Jeeeeeee.

    ReplyDelete
  19. Michuzi kaka asante sana kwa kazi unayoifanya.
    Kwanza na muunga mkono jamaa anesema sheria ni kwa walala hoi tu. Ni kweli mkulu. Jamaa wenye visenti kesi zao uishia kiholela ama huchukua muda kaka mpaka unakufa kesi haija fika mwisho. Kuna kesi nyingi tu huko Kigamboni za walala Hoi kudhulumiwa Ardhi zao na jamaa wenye mahela, cha kushangaza wazawa wenzangu tunatumiwa sisi kuchinjana na mabupa yanaa kaa pembeni yanakula kuku kwa mrija

    Mahakimu wote wanaohusika na kesi hizo washalishwa. Mlala hoi kama mimi na wewe na hati zake bado kesi zinaburutwa mwaka wa nne sasa JE wakulaumiwa ni GABACHOLI aliwalisha wakubwa ama mzawa kumuumiza mzawa mwenzie kwa kukubali vijisenti??? Ndio yale tulioyasoma kwenye historia ya wazee wetu kuwauza wazee wenziwao halafu tunawalalamikia wakoloni. Kumbe babu yake nanihii ka muuza babu yake nanihii. Ndio hii kesi ya Richmond wakubwa wa serikali wangeeka munda jamani HELA zetu walala hoi zingeibiwa???

    Halafu watu hawalishani ndio wanapelekana mahakamani. Uchaguzi mwakani wasipo wahukumu tusiwapigie kura hata kama wataiba lakini watajua makosa yao yako wapi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...