Michuzi,
Nilikuwa nasoma maoni ya wadau kuhusu kisa cha dada Stella. Ila kunahii tabia ya watu kusema wenzao eti ni Waswahili.

Kwani mswahili ni nani? Si ni wote tunaoongea Kiswahili ni Waswahili?Si ni wote tuliozaliwa Tanzania - kitovu cha Kiswahili - ni Waswahili?
Mimi ni Mswahili na ninajivunia kuitwa Mswahili?

Wewe unayetumia neno "Mswahili" kama kukandia je wewe ni nani?
Mzungu? Na kama huo si usenene ni nini???

Kama ni mapungufu ya kitabia (mfano kuamini ushirikina, kuwa kigeugeu,na kadhalika) yapo sehemu nyingi tu duniani na vitu inafaaturekebishane taratibu, sio eti kuponda Uswahili.

Tukumbuke kuwa Waswahili tumejiunga na utamaduni wa kutumia pesa zamakaratasi na uchumi wa kibepari miaka kama 50 hivi iliyopita na badohaya mambo hayaeleweki vema kwa wengi wetu.

Umuhimu wa kujali muda unakuja wenyewe mtu akishaelewa pesa inavyofanya kazi.
Tumekuwa katika uchumi ambapo serikali imekuwa ikitulea lea kwa muda mrefu ili tuweze kujimudu. Lakini sasa hivi serikali inapunguza kulea lea kwa hiyo taratibu watuwatajifunza kutafuta fedha na kujali muda.
Mimi ni Mswahili, je wewe ni nani?
Ni hayo tu.
Ni mimi mdau mwenzenu,Fred

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. Kuna msemo unaosema ukitaka kumuua mbwa kwanza muite majina mabaya. Hiyo propaganda potofu ilizuliwa na watu wasiokipenda Kiswahili eti kwasababu zao wenyewe, hasa ukiangalia asili ya Kiswahili chenyewe, kimetokea wapi na vitu kama hivyo. Kwa vile wanaasili ya chuki binafsi, wakaona njia bora ni `kukiita majina mabaya, ili hatimaye kionekane hakifai. Lakini kwa majaliwa yake Muumba akakipa nuru, na akawajalia watu kama akina Mwalimu Nyerere na wengine kukipa nafasi ili kiwe lugha ya Taifa.
    Kukitusi Kiswahili kwa maneno ya kejeli ni kujitusi wenyewe, kwani kwanza hii ni lugha ya Taifa, kama Mtazania unatakiwa ujivunie, na sio Tanzania tu sasa hivi lugha hii ni bomba hata Wazungu wanaitamani,labda kinachotukwamisha ni umasikini wetu, ndio maana sisi tusiojua umuhimu wake tunapenda kukikebahi.
    Kiswahili ni chetu, na tulikuwa na haki ya kujisifia na kuyaita mambo mema kuwa ni ya Kiswahili, kwasababu hatuwezi tukasema Kiingereza ni chetu, Kiingereza kina wenyewe, kama zilivyo lugha nyingine, ila wenzetu wametuwahi na kukitukuza na hatimaye kimekuwa cha kimataifa, na ndivyo na sisi tulitakiwa tufanye hivyo.
    Ila kasumba tuliyo nayo, kila kitu kizuri ni cha `kidhungu’ kikiwa kibaya `acha uswahili’, huu ni utumwa na ugonjwa wa kasumba.
    M3

    ReplyDelete
  2. mdau! namimi naunga mkono hoja yako kwa mikono miwili!

    Watanzania tunakabila moja tu na nikabila la waswahili, inabidi tufike mahala tujitambue sisi niakina nani! watu wote walio zaliwa miaka ya 70s na kuendelea naamini lugha yao yakwanza kujifunza ilikua kiswahili,na your first language ndo lugha yako mama! nohiyo lugha nyingine unayo jiita kwayo is always second language. kwahiyo tufike mahala tujitambue.

    Watanzania inabidi tujivunie uswahili wetu kasababu haupo sehemu nyingine yoyote duniani, waganda na wakenya wanatutamani sana kwasababu ya uswahili wetu,nenda Hata west Africa,Nigeria wana tusifu kwa uswahili wetu, nenda south Africa wanatusifu kwa uswahili wetu.kila kona ya Africa anbayo mimi nimeenda watu wanaisifu Tanzania kwa umoja wetu na uswahili wetu.

    Kunajamaa mmoja alikua anahojiwa na BBC kipindikile ambacho Bush alikuja tanzania, huyo jamaa ni mu ivory coast, alisema Tanzania tunabahati ya pekee ukilinganisha na mataifa mengine,nakumbua kipindi hicho ndokulikua na machafuko ya Kenya.

    TUNAKABILA MOJA TU WASWAHILI.

    Ebu niambie kama baba yako ni mkerewe mama mnyakyusa, wewe nikabila gani, wakati umezaliwa ukasikia nyumbani kwenu wanakuongelesha kiswahili? nalugha yako yakwanza kujifunza ni kiswahili?

    Kaenichini mfikirie kabla hamja pitwa na wakati.

    ReplyDelete
  3. SASA WEWE FRED, KAMA HUJUI WANACHOANDIKA KWANINI USIKAE TU KIMYA? KWENYE KAMUSI YOYOTE KUNA MAANA ZAIDI YA MOJA YA NENO. SASA WEWE UMEJIFANYA HUJUI KABISA HILO. KAMA HUJUI NGOJA NIKUPE HABARI.
    1) MSWAHILI NI MTU ANAYEZUNGUMZA KISWAHILI, HASA MTU WA PWANI, NA ZAIDI WALE WA MAENEO YA VISIWA NA MIJI YA PWANI TOKA MPAKANI NA MSUMBIJI HADI MOGADISHU KINAKOZUNGUMZWA KISWAHILI.

    2) MSWAHILI NI MTU MWONGO, MAANA YA PILI. KWANINI. SABABU WATU WALIFANANISHA USWAHILI NI KAMA KUZUNGUMZA MANENO MENGI SANA YA KISWAHILI KAMA 'USANII' AU SABABU UNAKIJUA ZAIDI. KUONGEA MANENO MENGI YA KISWAHILI KULIKO LUGHA YA KABILA LAKE MTU KULIWEKA KWENYE TABAKA LA KUWA MSWAHILI, SABABU ZAMANI WENGI HAWAKUKIJUA VEMA SANA.

    3) MSWAHILI, MAANA YAKE NYINGINE NI MTU WA KUTOKA AFRIKA YA MASHARIKI, MAENEO YANAYOZUNGUMZA KISWAHILI, UKIONDOA NJE YA MIPKA HIYO.

    HALAFU UNAANZA KULETA DHARAU NAWE TENA KWA KUWEKA MISEMO KAMA "USENENE". UNARUDIA YALEYALE UNAYOJIDAI KUWAKOSOA WENZIO? JAMANI, TUTAJUA LINI KUJIKOSOA SISI KWANZA?

    TUELEZE MAANA YA USENENE BASI, MAANA NAWE UNAONEKANA MSWAHILI UNAYEKIJUA HASWA!!!

    Mdau.

    ReplyDelete
  4. ME NI MDAU AMBAE NINGEPENDA KUWAELIMISHA WATANZANIA WENZANGU WASIEJUA NINI MAANA YA MSWAHILI EITHER KWA NAMNA MOJA AMA NYENGINE HAWAJUI MAANA KUNA AINA MBILI ZA MAKOSA KWENYE LUGHA WATU HUWA WANAZIFANYA EITHER NI MAKOSA YA KILESKIKA HAYA NI MAKOSA YA KIMAANA YANI KIMANTIKI MAKOSA HAYA HUSABABISHWA SANA NA MAZOEA YANI MTU ANAKUA ANAKUA NA MAZOE YA KUTUMIA NENO FLANI KUMANISHA KITU BILA KUJUA KAMA SIYO MAANA YAKE HALISI MFANO UTAMSIKIA MTU KAFANYWA KITU ANAKWAMBIA NO SWEET BWANA!KWAHIYO MTU HUFANYA MAKOSA BILA KUJUA.

    PILI NI MAKOSA YA KISARUFI AMBAYO MTU HUWA ANAYAFANYA KUTOKANA NA KUATHIRIKA NA AKSENTI EITHER INAWEZA KUSABABISHWA NA GEOGRAFIK POSITION ANAYOTOKEA AMA MOTHER TONGUE.

    TURUDI KTK MADA PIA KUNA WENGINE WANAKUA WANAJUA NINI MAANA YA KITU MFANO MSWAHILI ILA WANAKUA NA PROPAGANDA ZAO AMBAZO WANAKUA NA NIA YAKUTAKA KUZIPANDIKIZA KATIKA JAMII,HIVI UKILETA PICHA MBAYA JUU YA MSWAHILI UNAMKOMOA NANI?MAANA WEWE SIO FRANCOPHONE AU ANGLOPHONE PIA UPO KATIKA KUNDI HILOHILO LA WASWAHILI,NI SAWA NA KONDOO MWEUSI ANAEBAGUA KONDOO WAUSI WENZIE BILA KUJUA KUA NAYE NI MWEUSI KESHO ITARUDI KWAKE

    KWAHIYO NINGEPENDA KUWAELIMISHA WATANZANIA WENZANGU KUWA TUSIJIDHALILISHE KWA KULETA PICHA MBAYA AU KUTAKA KULIGEUZA KWA ITIKADI ZETU BINAFSI NENO MSWAHILI KWANI UKIWA NDANI YA TZ. UTAONA NI SAWA BUT UKITOKA NJE YA NJE AMA KUISHI NA JAMII NYENGINE UNAJIDHALILISHA HATA WEWE MWENYEWE KWA KUKOSA KUJUA NINI MAANA YA MSWAHILI NA KUTOKUJUA NAWE NI MSWAHILI PIA,

    KWA KIFUPI MAANA YA MSWAHILI NI MTU ALIYESTAARABIKA MWENYEKUJUA NINI MAANA YA USTAARABU,MWENYEKUJUA NINI MAANA YA STARA ANAEJUA UTU NI NINI
    PIA MSWAHILI NIYULE ANAEZUNGUMZA KISWAHILI NA ALIYEPWANI MWENYEKUKONTACT NA WATU WENGINE NA KUJUMUIKA NAO KATIKA SHUGHULI NYENGINE KAMA VILE ZA KIBIASHARA N.K
    NA NDIO MAANA HISTORIA YA TANZANIA INAONESHA MSWAHILI ALIWEZA KUFANYA BIASHARA NA WATU WOTE HATA WASIO WATANZANIA KAMA WARENO WAARABU N.K ILITUMIKA KUTUNGANISHA NAO NA NDIOMAANA MPAKA LEO WATANZANIA TUNASIFIKA KUWA WAKALIMU NA UPENDO,MSWAHILI YEYOTE HAWEZI KUWA FISADI UKIMPA MADARAKA AMA UKIMWACHIA BIASHARA ATAIFANYA KWA UAMINIFU HII KUTOKANA NA KUA NA HISTORIA NZURI.

    NI WASWAHILI AMBAO WANAJUA USTAARABU NA NDIOMAANA BABA WA TAIFA ALITUMIA KISWAHILI KUTUUNGANISHA ALIKUA ANAJUA WAZI KUA LUGHA HII YA WAUNGWANA WANAOJUA UTU ITAWAUNGANISHA WATANZANIA WOTE NA KULETA AMANI MIONGONI MWAO KWANI WAMEKULIA NA INAMAHADHI YA UTU NA NDIOMAANA TANZANIA TUMEKUA KITU KIMOJA HAKUNA UKABILA WALA UDINI UKILINGANISHA NA NCHI NYENGINE.

    WATANZANIA WENZANGU TUACHE KULALA NA INFERIORITY COMPLEX NA BADALA YAKE TUJIVUNIE KUWA WASWAHILI YANI WAUNGWANA TULIOSTAARABIKA NA TUNAZUNGUMZA KISWAHILI,MATOKEO YAKE NCHI KAMA KENYA KILA SIKU INATUACHA NYUMA KUTOKANA NA INFERIORITE COMPLEX ZETU,KENYA SASA HIVI INAJIVUNIA KUJIITA NCHI YA WASWAHILI WANAJIITA MOTHER LAND YA SWAHILI LANGUAGE KUJITANGAZA BUT UKWELI KWAMBA KISWAHILI KIMEZALIWA KWETU NA SISI NDIO TUNAOKITUMIA SANA NA VIZURI KULINGANISHA WAO.

    IMAGINE KWENYE UMOJA WA NCHI ZA KIAFRIKA RAISI ALIEOMBA KISWAHILI KIWE LUGHA YA MAWASILIANO KTK UMOJA HUO ALIKUA NI RAISI WA MSUMBIJI,SISI TUMELALA
    TUSIPOTOSHE MAANA NZURI YA MSWAHILI,KAMA TUNAMAANISHA NEGATIVE ME NADHANI HAO WAZUNGU NA JAMII NYENGINE KAMA AMERICA ULAYA N.K NDIO WANGEFAA TUWAITE HIVYO HII KWA MTU ALIEKAA AMERICA AU ULAYA ANAJUA JINSI WATU HAO WASIVYOKUA NA UBINADAMU AMA USTARAABU AMA TABIA ZA AJABU
    WATANZANIA TUJIVUNIE KUA WASWAHILI TUELIMISHANE TUELIMIKE ILITUE WASWAHILI NA WAZALENDO.

    WAKATI SISI WENGINE MAKWETU HUKO TUNALALIA NYUMBA ZA MAVI YA NG'OMBE MSWAHILI ANALALA KWENYE NYUMBA ILIYOJENGWA KWA SARUJI KAMA MNABISHA NENDENI MAKUMBUSHO YA TAIFA.
    WAKATI SISI WENGINE TUNATUMIA BATER TRADE MSWAHILI ALISHAKUA NA PESA YAKE YAKUWEZA KUFANYIA BIASHARA MFANO ENZI HIZO MIJI MIKUBWA KAMA KILWA.
    WAKATI SISI WENGINE MAKWETU TULIKUA TUNAVAA NGUO ZA MAGOME YA MITI MSWAHILI ALIKUA TAYARI AMESHAANZA KUVAA NGUO.
    UAMINIFU WA MSWAHILI NDIO ULIMWEZESHA KUFANYA BIASHARA NAWAGENI BILA UGOMVI KAMA WACHINA WARENO WAARABU WAHINDI N.K
    UKIMPA MSWAHILI SERIKALI KINACHOFUATIA NIKUFUNGA MAFISADI WOTE,HAINGII MIKATABA FEKI NA HUYO NDIO MTANZANIA MZALENDO NANDIOMAANA NAJIVUNIA KUA MTANZANI MSWAHILI

    MDAU WA UTALII

    ReplyDelete
  5. hongera Fredi kwa kuguswa ma ishu ya "uswahili" kuhusiswa na mambo mabaya kama "uongo" "dharau" "ushirikina" na mengine.
    mimi nadhani ni matumizi tu ya lugha na inferiotirty complex pia. waswahili wengi wetu tumekuwa hatuthamini muda na ahadi tuwekazo (sisemi wote, ni wengi wetu) hii ilipelekea na inapelekea waswahili kubebeshwa lawama zote hizi.
    kuna haja jamii yetu kubadilika ki fikra lakini sisi waswahili pia tubadilike kitabia.
    mimi ni mswahili halisi, ila sipendi kujumuishwa katika baadhi ya sifa mbaya za baadhi yetu lakini jee nitafanyaje? waswahili sisi wenyewe tumesema SAMAKI AKIOZA MMOJA...........
    mswahili wa pwani.

    ReplyDelete
  6. mswahili ni mswahili haswa ndio wote twaongea kiswahili bali sio wote ni waswahili

    unaongea nini ukipelekwa kwa waswahili hata maneno ya kiswahili utayaelewa, na waswahili haswa wa uswahilini ni waswahili haswa

    hata sijui nikuelezee ipi

    ndio tupo proud kujiita watanzania.

    mie HUWA NA SEMA MIE MTANZANIA NA NAONGEA KISWAHILI...

    KAMWE SIWEZI SEMA MIE MTANZANIA NA MSWAHILI...

    NITASEMA MIE MTANZANIA NAONGEA KISWAHILI NA NI MKABILA HILI

    MIE SIJAKULIA USWAHILINI, SAMAHANI KAMA UNATAKA KUITWA MSWAHILI

    HIVYO UNATAKA SEMA NCHI ZINGINE ZINAZOONGEA KISWAHILI NAO WAITWE WASWAHILI

    ACHA KUONGEA PUMBA HUMU

    ULICHOONGEA AKILETI MAANA

    MIE NIMEKUA NAJUA WASWAHILI WANATABIA AMBAZO HUWA ZIPO ZA AJABU NA MUONGEO WAO KELELEEEE UTAJUA TU

    NA UJUE NCHI ZOTE DUNIANI ZINA WATU WAKE tofauti i mean class tofauti

    tafadhali

    kamwe usinisukume mie na wa kama mie tujiite waswahili.

    I am a tanzanian and not a swahilian

    kumbuka sio wote nchini tanzania wanaongea kiswahili... hivyo point yako pumba

    watu tuna language zetu za kikabila kuongea

    tembelea hapo around dar pwani ndio uone waswahili amboa lugha yao ni kiswahili hakuna ingene ya kuongea kusema ni lugha ya kabila

    OK

    ReplyDelete
  7. Nilishasema tangu zamani kuwa mswahili ni mtu anayezungumza kiswahili kama lgha yake ya kwanza. Mswahili anafikiri na anaota kwa kiswahili.
    Kuponda Uswahili ni tabia iliyojitokeza wakati watu wengine walipoanza kujifanya wazungu.

    Kwa mfano, kucheza ngoma na unyago ni gharama sana (ingawa ni mara moja tuu katika maisha ya mwanamke) Lakini kusherehekea birthdays (kila mwaka) si gharama.

    Kula kwa mkono ni uswahili kula kwa kijiko ni ustaarabu.

    Kuitwa Maganga Ufyole ni jina gumu lakini kuitwa Arthur Bryson ni jina jepesi.

    Kwa ufupi wanaouponda uswahili wote ni wale wenye tabia ya kujikataa.

    Amini usiamini, ukijikataa wewe mwenyewe hakuna atakayekukubali.

    ReplyDelete
  8. ME NINGEPENDA KUMUUNGA MKONO HUYO MDAU WA UTALII WA 12:50

    KWAELEWESHA VIZURI SANA!KUA KUNA MAKOSA YANAYOFANYIKA KTK LUGHA MOJAWAPO WATU KUTOKUJUA MAANA HALISI YA NENO!!AIDHA ATALITUMIA KUTOKANA NA MAZOE!UTAMSIKIA MTU ANAKWAMBIA MIMI NIMEZALIWA NIKAKUTA WATU WANALITUMIA!INAWEZEKANA HAO WALIOKUA WANALITUMIA HIVYO WALIKUA NA PROPAGANDA ZAO!!
    MAANA HATA UKIENDA UGANDA KUTOKANA NA NCHI YAO KUA WANAUPENDA UKABILA NA KUBAGUANA WANAKICHUKIA SANA KISWAHILI NA UTANZANIA WAKIJUA VIKA KISWAHILI KITAWAUNGANISHA NA KUWAFANYA WAWE WAUNGWA NAKUACHA TABIA ZAO CHAFU ZA KUBAGUANA NA UKABILA

    KWAHIYO WALE WENYE UKABILA UGANDA NA CHUKI WALIJITAHIDI KUKIPA KISWAHILI MAJINA MABAYA KWA WATOTO WAO WAKIKUA WAWE NA AIDIA NEGATIVE JUU YA MSWAHILI!KAMA LUGHA YA WEZI,MAASKARI,MAJAMBAZI N.K
    NAHII UKWELI WAKIJUA WAZI KUA KISWAHILI KITAWAFANYA WASTAARABIKE MFANO MZURI TIZAMA MIJI YOTE INAYOTUMIA KISWAHILI WATU WANAKAA KWA KUPENDANA BILA KUBAGUANA WEWE UMETOKA WAPI NA WANAFUNDISHIKA UUNGWANA KUJALIANA
    PIA UKIMPA UONGOZI MSWAHILI NI MWAMINIFU HATAKI UFISADI HEBU MTIZAMENI NYERERE BAADA YA KUA MSWAHILI,MWINYI MTIZAMENI JAKAYA NI MIFANO TOSHA YA KUIGWA

    ReplyDelete
  9. KWELI KABISA UKIJIKATAA MWENYEWE HAKUNA ATAKAE KUKUBALI
    YANI KWELI MSHAMBA NI MSHAMBA TU HATA AWEPO AMERICA ULAYA N.K
    NYANI NI NYANI TU HATA UKIMVALISHA SUTI.
    HIVI TUTAACHA LINI USHAMBA WETU WAKUA NA INFERIORITE COMPLEX?MAANA UNAKUTA MTU ANAKUAMBIA ANAJIVUNIA KUZUNGUMZA KISWAHILI HAJIVUNII KUA MSWAHILI HUU USHAMBA UTATUISHA LINI?
    NI SAWA NA MTU KUSEMA NAJIVUNIA UAFRICA BUT SIJIVUNII KUA MWEUSI

    JAMANI TUKUMBUKE KUA USWAHILUI WETU NDIO UMETUFANYA TUPENDANE TUSHIRIKIANE TUWE WAMINIFU NA WENYE UMOJA POPOTE PALE TUNAPOKUA DUNIANI NA KUTUFANYA TUESHIMIKE TUWE MFANO WA KUIGWA,MFANO MZURI SIKU HIZI TUNAONA MPAKA MUVI NA COMEDY ZA BLACK AMERICA WANAJIVUNIA KUA WASWAHILI.MAPROFESA NA WANAHARATI WAKUBWA WA AMERICA NAKWENGINE WANAJIVUNIA KUA WASWAHILI MFANO YULE PROFESA ALIEANZISHA SIKUKUU YA WATU WEUSI AMERIKA NA KUIITA KWANZA AMEIPA BASIC FUNDAMENTAL YA SHEREHE HII NI UMOJA TENA KWA KISWAHILI.

    NI USWAHILI WETU ULIOTUFANYA TUKAWA NA UMOJA NA MAPENZI MIONGONI MWETU NA KUACHA KASUMBA ZETU CHAFU ZA UKABILA NA CHUKI,VITA VYA KIKABILA NAKADHARIKA
    IMAGINE NCHI KAMA GHANA KILA KABILA NA LUGHA YAKE WENGINE HAWAJUI KINGEREZA RAISI AKITAKA KWENDA KUHUTUBIA SEHEMU ANAKWENDA NA MKALIMANI.
    KUNA BAADHI YA NCHI WALIKUA WAKIKICHUKIA KISWAHILI NA KUKIPA MAJINA MABAYA BUT LEO WAMESHINDWA NA TUNAONA WAMESHAKIINGIA KATKA CONSTUTION ZAO KUA LUGHA YAO YA TAIFA MFANO UGANDA;WAMEONA HAKUNA SOLUTION NYENGINE YA KUFUTA UNYAMA NA UKABILA ILA KUINGIZA USWAHILI KTK JAMII ZAO
    RWANDA NA BURUNDI WANAJIVUNIA MNO USWAHILI LEO UNAWAUNGANISHA NA KUWAFANYA WASAHAU UKABILA ULIOKUBUHU.
    NYAMBAFU NYINYI MNAOUPONDA USWAHILI BILA USWAHILI MNGEKUA MNAISHI KAMA WANYAMA.

    KENYA INAJIITA MOTHERLAND OF SWAHILI N SWAHILI LANGUAGE ANGALIA WENZETU WALIVYOWAJANJA!SISI MIJINGA TUNAJIPONDA WENZETU WANAFAIDIKA NAUKIZINGATIA KISWAHILI SISI NDIO WENYEWE.

    RAISI WA MSUMBIJI CHISANO AMEPELEKA HOJA HII AU NAKUJIVUNIA USWAHILI SSI WASHAMBA TUNAJIVUNIA UPUUZI TUU

    HIVI JAMANI KUKAA KWETU KOTE NJE HATUELUIMIKI TU NA KUWAONA WENZETU WALIVYOKUA HAWAJAASTAARABIKA?(CIVILISED)
    MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  10. Du Fredi na wewe nae acha Uswahili mbona Mswahiliiiiiiiiii manake waswahili kwa kumaindisha du !!tehetehetehehehehe

    On a Serious note , Fredi na nyie wadau wote mnaomuunga mkono Fredi hapo juu mimi nawaona tuu hamnazo kwa sababu kuitwa Mswahili kwangu mimi ni ujiko moja na mbili huo ni msemo tuu wa mtaani kumreflect mtu ambae hajaacha tabia au sifa za jamii yetu na kama tunavyojua jamii yetu ya kibongo ni Waswahili na mambo yetu ni ya Kiswahili (sijui kama mnanielewa hapa) yaani kwa ufupi tuna mila na desturi zetu na hulka zetu ambazo zinatufanya sisi ni Waswahili na hata siku moja hatutabadilika kuwa Wazungu au Wajamaica. Watu pekee ambao tunaweza kurelate nao na huo uswahili wetu labda ni baadhi ya mataifa ya Kiafrica ya Kusini na Magharibi(niko naishi ukerewe so I nimejichanganya na watu tofauti) kwa hiyo ukweli ni kwamba mtu anaekuita wewe Mswahili ana mawili either yey anajiona sio mswahili na anataka kukimbia asili yake kitu ambacho hakiwezekani so ni ana matatizo ya kuhitaji msaada, na pili ukiitwa mswahili tena hii ndio sana sisi tunaitumia kwa Mzaha ama ni msemo tuu wa mtaani and really mimi kuitwa mswahili na kukaa kwangu Ulaya huwa hainisumbi kabisa na wala hainishtui kwni ndio mimi mswahili so WHAT ?? WHO CARES ? I AM SO PROUD TO BE ONE !! Fred acha kumaindisha sana huo ni USWAHILI , wazungu hawana hizo na ungekuwa Mjamaica wangeshakupiga shaba ! Sie Wabongo wacha tuu tukuseme na USAHILI WAKO ! hehehehehe

    ReplyDelete
  11. mimi ni mgogo na usenene ni neno la kigogo maana yake upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  12. mr.Fred na wadau wengine wa blog yetu hii ya bitozi wa zamani michuzi MNAONA RAHA YA KUA WASWAHILI?

    kama mnavyoona tunataniana na kupenda kidogo!!kama mdau wa juu na mr.Fred

    michuzi wewe mswahili kwa kua umenunua gali,flana yako ulimpa binti yako ukajifanya imepotea!!ilimradi raha tupu

    ReplyDelete
  13. Hao wote waojifanya kuiponda lugha yao na kujitoa kwenye lugha yao! ni wamelala. Wanasema usimwamshe aliye lala,usije lala wewe.ndio maana wakenya washaona lugha imekua hii, waanza kujivunia ulimwenguni yakua yakwao, kwa vile wameona Tanzania ina lala, Lugha yasifika kila kona ya ulimwengu sasa. kiasi kwamba wageni wa kutoka mbali wanadhani Africa nzima yaongea hiyo lugha.maneno kibao yamechukuliwa kwenye misamiati ya lugha ya kingereza kutoka kwenye kiswahili, na yanatumika kila penmbe ya ulimwengu. Kama vile SAFARI. jamaani hamkeni tusilale, kila siku watanzania wanapenda kujirudisha njuma sijui wanamatatizo gani,Hizo lugha za makabila, Hata wenzetu walikua nazo karne hizo! lakini wakaendelea na lugha inayowaunganisha, ndio maana leo hii mnaona kingereza,

    ReplyDelete
  14. we annony wa january 30; 2009 saa 1:06 ndio pumbavu kuliko wote humu nani kakuambia watu wa pwani hawana lugha nyingine zaidi ya kiswahili? we ndio pumbavu kabisa kuliko wote waliotoa maoni yao hapa.

    ReplyDelete
  15. NYIE VIPI? SISI WOTE SIO WASWAHILI KWA VILE TUNAONGEA KISWAHILI.INAAMANA MTU UKIONGEA KIINGEREZA UNAKUA MUINGEREZA? AU UKIONGEA KIFARANSA UNAKUWA MFARANSA? AU UKIONGEA KICHAGA UNAKUWA MCHAGA?
    WASWAHILI NI WATU WA PWANI INABIDI MRUDI KWENYE HISTORIA YENU KIDOGO.
    SASA MTU ANAPOKUITA WEWE MSWAHILI NI KUTOKANA NA KITENDO CHAKO WAKATI HUO KIMEFANANA NA VITENDO VYA WASWAHILI.
    LUGHA PIA INAKUWA SASA NENO USWAHILI LINATUMIKA KILA KONA.MARA UNAKAA USWAHILINI WEWE NA MENGI ZAIDI.
    KWAHIO TUSIJIDANGANYE KWA KUSEMA SISI WOTE WASWAHILI.
    mdau "mswahili wa kuzaliwa"

    ReplyDelete
  16. Kiswahili sio kabila ni lugha ya Taifa ya TZ, wala sio mnafanya kila mtu anaetumia lugha hii kuwa Mswahili. Je ndugu was kenya na Uganda na majirani wetu wengine wanaotumia Kiswahili wao ni Waswahili? Chukua mfano wa Uingereza, nchi ni Britain, wao ni wa British ambao ni pamoja na Scotland and Wales, wanatumia English kwa lugha ya taifa, na wa Wales wana lugha yao ya Welsh, mbona hawaitwi wote Englishmen?
    Neno la kuitwa Waswahili ilitokea na watu wa sehemu za Pwani kama Tanga mjini ambao walikuwa hawana lugha ye yote nyumbani isopkuwa Kiswahili, ndio hawa wakaitwa Waswahili, halafu vile vile ndio wao walijulikana kuzungumza ile standard Kiswahili.
    Nchi imefika mbali leo, wanainchi wote siku hizi wanazungumza standard kiswahili na tofauti kidogo hapa na pale kwa utamshi wa maneno fulani. Hata huko Uingereza vile vile Kingereza cha Kaskazini ni tofauti na cha Kusini, lakini bado ni lugha moja.
    Tuache kutafuta mabishano ambayo hayana faida yo yote. Kiswahili is our National Language and that is the end of story, no one has an ownership to it.
    Sam --USA

    ReplyDelete
  17. Sababu kubwa ya kufanya mtu aitwe mswahili ni kwamba waswahili wengi tumepoteza maadili kwahio ni kawaida ukienda kinyume na maadili kuitwa mswahili sana,mara nyingi taswira ya kikundi cha watu inaonekana kwa viongozi wao ndio mtu anapopata uhalisia wa kikundi hicho.Na tuyageukie maadili ya viongozi wa hao wanaoitwa waswahili tuyachambue UFISADI,UONGO,UROHO WA MADARAKA,UJUAJI MWINGI,UBINAFSI NA KUTORIDHIKA BILA KUSAHAU UIZI.kuna kila sababu ya kuitwa mswahili ukiwa na mjawapo ya hizo tabia hapo juu ambazo wengi wetu waswahili ndio tunazo tumezirithi bila kujijua kutoka kwa hao viongozi wetu tuliowapa mamlaka ya kutuongoza,tabia ya kutopenda mwenzio apate hata kama anastahili ni USWAHILI tu,uongo uliokithiri kwa wapiga kura wako ni USWAHILI tu,kibaya zaidi kwavile wananchi hawana wapiga kura waliowapigia kura basi wanadanganyadanganya ovyo ovyo tu kwavile nao wanadanganywa sana na waliowapigia kura kwahio unakuwa nao ni USWAHILI tu.kutokujali iwe kwa makusudi au kwa kutokujua nao ni USWAHILI tu
    unajua wazi uchafu utasababisha kipindupindu na bado hutaki kuuepuka ndio USWAHILI huo,tazama ajali za barabarani hazitushtui sana japo zinatupunguza sana lkn hatujali kwavile sisi ni nani?WASWAHILI na sio sisi tu wanaotuongoza nao na madereva wote hawajali kwavile ni WASWAHILI TU.ushirikina nao ni uswahili tu.

    ReplyDelete
  18. SIKILIZENI NDUGU ZANGU HAYO YOTE MNAYOSEMA NI SAHIHI KUWA MSWAHILI NI YULE MZAWA WA KISWAHILI, LAKINI KILICHOINGIA HAPA NI KASUMBA YA UKIFANYA BAYA UNAITWA MSWAHILI,UKIWA NA CHUKI UNAITWA MSWAHILI UKICHELEWA UNAITWA MSWAHILI,LAKINI UKISFIWA UNAITWA MSTA-ARABU,NDU'ZANGU HIZO NI KASUMBA ZA ZAMANI ZILIZOFANYWA NA WATAWALA WA KIARABU KUWAEKA CHINI WASIO WAARABU.USWAHILI NI KUFANYA MAMBO YA KISWAHILI AMBAYO YOTE NI MABAYA,NA USTA-ARABU NI KUFANYA MAMBO YA KIARABU AMBAYO YOTE MAZURI.
    NI KASUMBA AMBAZO WAZEE WOTE WALIZIACHA ZITUMIKE NA ZIMETO MZIZI.SINA NIA MBAYA NA NDU'ZANGU WA KIARABU LA,SOTE TUKO HUKU NA KULE LAKINI HUO NDIO UKWELI

    ReplyDelete
  19. Nakumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere aliposema kwamba, watanzania wakimuona mtu anaongea kingereza wanamuona ni wamaana sana!!!!!

    mwisho wa kunukuu!
    Kwa maana hiyo, kwa kifupi kwa mtazamo wangu, maoni yaliotolewa na ndugu aliye tumia neno (SAFARI) nipeke yake aliyetoa maoni ya maana kiasi kwamba atakama mwalimu angekuwepo angempongeza pia. Maoni mengine yalikuwa katika kuwafurahisha watu na kutoiboresha lugha yetu ya kiswahili.

    Mdau kutoka canada!

    ReplyDelete
  20. AMA KWELI WASWAHILI NI WASWAHILI HASA.

    ReplyDelete
  21. History:The inhabitants of the coastal areas of Kenya, Tanzania, and Mozambique share history, language, and cultural traditions, which some Swahili scholars claim date to at least 100 A.D., when an anonymous Greek traveler and author of The Periplus of the Erytharaean Sea wrote about a place in east Africa, which Arabs frequented to trade with those living on the mainland. This history is closely tied to Indian Ocean trade routes linking India, the Arabian Peninsula, and Africa. Despite the shared history and language of the peoples of the Swahili Coast, it remains difficult to describe a discreet Swahili culture. This is not to suggest that a Swahili culture does not exist, but instead that its boundaries are amorphous, changing whenever necessary to meet the demands of everyday life.

    ReplyDelete
  22. Nakumbuka watu walikuwa wakimwambia mtu kuwa jamaa ni wa kutoka bara....walikuwa wkimaanisha kuwa ni mshamba, kiswahili matatizo, ujinga, hakuna ustaarabu na ukarimu sifuri. Ndiyo maana wageni wote waliofika east africa kituo cha kwanza pwani kwa waliostaarabika, mpaka leo hii watu wote bongo wanataka kuishi uswahilini....Dar es Salaam.

    Mimi nipo hapa USA miaka kibao, watu weusi wana utamaduni wao na watu weupe wana wao, kuanzia vyakula,lugha jinsi wanavyozungumza mpaka jinsi wanavyoabudu M/Mungu . Kwa sisi wabongo kukandia wabongo kuwa waswahili na shangaa wewe ni nani. Ni ujinga mtupu, wewe tazama mambo ya ovyo ovyo yanayoendelea bongo kama mauwaji ya albinos, na vikongwe na ushirikina mwingine mwingi wa uchawi upo sehemu ambazo ni mbali na pwani na wenyeji wake ni ukabila ukabila, kiswahili matatizo, ustaarabu mdogo.

    Mimi ni mtazania lugha yangu ya kwanza ni kiswahili, baba na mama wanatoka kabila mbili tofauti. Kwahiyo ni mswahili. I'M PROUD TO BE MSWAHILI, there is no tribe called Swahili but I'M PROUD TO BE ONE.

    Mdau...USA

    ReplyDelete
  23. Haya basi waone WASWAHILI walivyo na midomo na maneno ? ndio mana WASAHILI tuu nyie ....na hii blogu ni ya WASWAHILI tuu ...hehehehehahahahateetettete

    ReplyDelete
  24. JK ni bonge la Mswahili origino wa pwani , so mnamuona mambo yake ? habla ya upresidaa maswahiba wote walikuwa wanajua their future is bright kwamba atawasoti hamna noma eeh bwana sasa hivi ni anawatosa kwa kwenda mbele yaani ni MSWAHILI ile mbaya mana hana MUAMANA yule baba !

    ReplyDelete
  25. Wee usie na jina hapo juu inaonekana hata USWAHILI wenyewe huujui, ingawa nawe MSWAHILI vilevile usiejijua.

    Kwa sie waswahili hasa mwenye kwenda kinyume na maadili twamuita MSHENZI na si MSWAHILI kama unavyonadi, Pia usichanganye uswahili na siasa naona umebase sana katika siasa. Je WaSWAHILI wote ni MAFISADI, WAROHO WA MADARAKA? hujui unachoongea kama huna la kuchangia bora uangalie kwa macho tu Waswahili wanavyomwaga points za maana.
    Nyie ndio Wakataa kwenu Watumwa!

    MIMI NI MSWAHILI najivunia kwa hilo na ntaendelea kuuenzi bila kujali wapi nipo iwe Tanzania au nje ya Tanzania, Daima ntabaki kuwa MSWAHILI DAIMA mpaka naingia kaburini!!

    Uzungu kwangu ni extra hobby tu upo hapoooo?

    Honger sana kaka Fred kwa kuwapasha hawa Ant-SWAHILIs!!

    ReplyDelete
  26. Wanaoukandia uswahili bado wana damu ya utumwa na inaelekea bado ni watumwa mpaka sasa. Dunia ya leo kama hujithamini mwenyewe pamoja na vitu vyako basi itakuwa vigumu sana kuthaminiwa na wengine kwani kila mtu sasa hivi yupo katika kutangaza utamaduni wake. Ni mshangao mkubwa kuona waswahili bado ni vibaraka wa kutangaza tamaduni za wenzao na kuiua ya kwao kwa kutumia maneno yale yale yaliyotumiwa na wakoloni, HATUWEZI kujulikana duniani kama tutakuwa bado watu wa kuiga mpaka tamaduni za watu. Naungana na watu wanaoutetea ushwahili. Mafisadi wa pesa za umma na vibaraka wa watu weupe ndiyo wanaopenda kuuponda uswahili ili wapate nafasi nzuri ya kutuibia kwa kutusingizia waswahili kwamba ni wavivu wa kufikiri, wanafiki, wachawi n.k. Nitaendelea kuwa mswahili kwa kuwa hatuwezi kutandawisha (globalise) tamaduni zetu. Wazee wetu walipigana sana na hata kujitolea maisha yao kwa kupinga udhalilishaji huu. (Ombi: kaka michuzi hebu tuwekee mziki wa Mr Ebbo unaozungumzia watu kudharau tamaduni zao)

    ReplyDelete
  27. yaani mie huyu Fred kanishangaza sana., kama mdau mmoja hapo juu alivyosema kuwa NENO MOJA linaweza kuwa na difinisheni tofauti, tunapoita fulani ni MSWAHILI hatumainishi kabila, tunamaanisha tabia fulani fulani ambazo jamii yetu imezidifaini kama USWAHILI. Kwani mbona neno SHENZI ni TUSI na wakati huo huo neno SHENZI hutumika kama sifa ya kitu fulani? Maneno mengi sana hutumika kwa maana tofauti na kila mtu anajua hilo. Mf. mtu anapokuwa kawini kitu halafu akasema k....ma...make walah! sasa hilo ni tusi? au ni mtu anaonyesha furaha yake iliyopitiliza?

    ReplyDelete
  28. Neno mswahili huambiwa mtu akiwa amefanya kitu kinyume na matarajio ya jamii, wala halimaanishi kukandia kiswahili na limekuwa linatumika toka enzi na enzi pengine hata wengi wenu mliotoa comments hapa hamjazaliwa, even 1940s, 1950s watu walikuwa wanatumia neno mswahili kumuita mtu mjanjajanja ambaye anachanganya na kudanganya watu katika kukamilisha mambo yake, hata huyo NYERERE mnayemsema mara nyingi tu ametumia neno mswahili akimaanisha mtu mjanjajanja/tapeli mara nyingi tu kweye mikutano na hotuba zake, wala halina maana ya kukandia kiswahili, ni term aliyokubalika katika jamii ikimaanisha mtu anayekamilisha mahitaji yake kiulaghai na ujanjajanja, hiyo haina ubishi, waulize wazee wote wa zamani watakueleza ni hivyo, waulizeni maanake nini mtu anapomuita mtu mswahili akiwa amefanya kitu kinyume na matarajio ya jamii. ni sawa pia kwa baadhi ya watu wa pwani wanaozungumza kiswahili na hawana lugha ingine kuitwa waswahili, walikuwepo sana siku za nyuma watu wa aina hiyo, hasa maaeno ya pwani, Tanga, Mtwara, Lindi, Dar. Mombasa. Kilwa. Mafia, Pemba, Lamu na Zanzibar maeneo haya kuna watu wanajuwa kiswahili tu na si lugha ingine na wengi wao walikuwa kama chotara wa kiarabu ambao wali-influence watu wengine kusahau lugha zao. Pia si kweli kuwa tulianza kutumia pesa za makaratasi miaka 50 iliyopita, miaka 50 iliyopita ni 1958, by this time tayari tulikuwa tumeshatawaliwa na Wajerumani na Waingereza hawa wote ni mabepari na walikuwa na pesa zao, pia wahindi walikuwa pia wanatumia rupia/rupee zao toka zamani, please get your facts right usipotoshe watu hasa watoto.

    ReplyDelete
  29. Swali hapa ni je tuendelee kutumia neno uswahili ambalo lilitumiwa na wakoloni weupe pamoja na wanaojifanya wakoloni weusi (vibaraka) kwa watu wanaofanya mambo ambayo hayakidhi mataratjio ya mtu? Kumbukeni kila jamii au taifa lina ustaarabu wake hivyo si vizuri kudharau tamadunizetu na kutukuza za wenzetu. Mf. kwa wafaransa unapoalikwa nyumbani kwa mtu unatakiwa uchelewe kidogo zaidi ya muda mliopanga ili kutoa nafasi kwa aliyekualika kujiandaa, hili likifanyika kwa watanzania wanaita uswahili!!!! kwa nini? Lazima tufundishe tamaduni zetu hata kwa wageni ili wazijue vinginevyo tutaendelea kuwa nyuma kwa kuiga za watu na kuua za kwetu.. TUACHE mawazo ya kitumwa kwani nina imani kizazi hiki kipo mbali na kile cha utumwa

    ReplyDelete
  30. Mimi sikubaliani nawe anony hapo juu maana usitulazimishe wote kuitwa waswahili.Kwasababu ukweli ni kwamba tabia ya mswahili ni tofauti na mtu mwingine hapo tz. kwamfano mimi ningependa kuitwa iwe kuliko kuitwa mswahili after all mimi nimekulia kwenye ndizi na sio minazi na mikorosho.Pale nikisha panda pipa na kushuka hapa kwa OBAMA, I don't care ukiniita mswahili lakini huko tz, tafadhali koma kuniita mswahili. maana naogopa nitajulikana kama mtu mwongo, mtu ambaye anaogopa vitabu.Niliambiwa kwamba kutokana na vibaka wengi kuwa waswahili, hela niwe nafisha kwenye vitabu na hasa vya math,phisics,na chemistry maana vibaka wanaangalia kwenye mito wanaogopa vitabu.
    Wenu IWE

    ReplyDelete
  31. hao wote wanaosema watanzania wote ni waswahili hawajui kitu. tanzania ina makabila mengi na yanaongea lugha tofauti only that a lot of them wanaongea kiswahili as a second language. mimi ninakumbuka toka nikiwa mdogo watu kutoka kwetu walikua wanadharau sana waswahili na hawakupenda kushirikiana nao. sisi kwenye kabila letu tulikua tunajua waswahili ni watu kutoka pwani. nyie waswahili ni watu wavivu sana na mnapenda maneno mengi. kwa maneno hakuna wakuwashinda. pia msisahau mna matabia ya kutemwa. PUU MBAKA. msitegemee watu wengine wanataka kuchanganishwa na nyie. jiiteni waswahili peke yenu. kabila langu halijaitwa waswahili hata siku moja na hatutaki kuitwa waswahili.

    ReplyDelete
  32. Huku Marekani wale watu wa mambo ambayo sisi tunaconsider 'uswahili' huku wanatumia sana neno 'ghetto'...ukisikia ure so ghetto yo...jst know that ungekua tz wangesema 'mswahili'....ni neno tu na halimaanishi ukilitumia wewe si mtanzania...bali unatenganisha makundi mawili ya watu in a community....

    ReplyDelete
  33. NYIE WAKUJA WALA MSITAKE KUTUPAKA MATOPE WASWAHILI NDIO WAJANJA WAKILA KITU;WAAMINIFU,WAKARIMU
    NYIE WAKUJA TULIKUA TUNAWAITA WASHAMBA MKIINGIA MJINI MKAONA MTUPANDIKIZIE PROPAGANDA ZENU ILI MTUCHAFULIE JINA.

    KAMA HIZO SIFA MNAZOMPA MSWAHILI TUANZE NA WIZI KUTOKUA WAAMINIFU NA KUTIMIZA AHADI HII SIFA NI YA MCHAGA NAWENGINE,HAKUNA ASIEJUA MCHAGA MWIZI MKUBWA ANGALIA IDADI YA MAFISADI NA DHULUMATI WAKUBWA WAABUDIA PESA KAMA UTAMPATA MSWAHILI.
    KUHUSU UCHAWI WAUA MAALBINO UMESHASKIA MAMBO HAYO PWANI!LAHASHA KILA SIKU HUKO KWENU

    MMEKUJA MJINI KWA WATU WALIOSTAARABIKA HATA KUVAA SURUALI HAMJUI TUMEWAFUNDISHA KUVAA THEN MNAANZA NYODO
    ENZI HIZO TULIKUA TUNAWAITA WASHENZI MMETOKA USHENZINI MKAONA MGEUZE ILI MPATE PROPAGANDA ZENU

    KILA ALIE MSTAARABU MWENYE KUJUA HUTU HUYO NI MTANZANIA MSWAHILI

    ReplyDelete
  34. UMEONA SASA KWA HAWA WATU WANAOJIITA SIO WASWAHILI!!NDUGU WADAU TIZAMA ITIKADI ZAO NI ZA KIKABILA KABILA TIZAMA MAONI YAO NDIO UJUE BILA YA USWAHILI TANZANIA TUNGEKUA KTK HALI MBAYA YA CHUKI NA UTENGANO MAANA HAWAJAWA CIVILISED.
    TUNGEKUA ZAIDI YA HATA WAGANDA,WANYARWANDA AMA WAKENYA KWA KUBAGUANA.
    HUYO MDAU ANAESEMA MSWAHILI MVIVU ANAMANENO MENGI SI KWELI!!ONA YEYE ALIVYO BINGWA WA KUSEMA KULIKO VITENDO.
    MKISHAFIKA MJINI NA VICHUPI VYENU MNASAHAU MLIKOTOKA KUA MASKINI WAKUTUPWA MLIOZOEA KULALIA VIJUMBA VYA MAVI YA NGOMBE MKIJA MJINI MNASAHAU AIBU ZENU NA MLIPOTOKA
    TIZAMA HATA WALE WANAOJIIUZA TOWN AMA UWANJA WA FISI WOTE NI WAKUJA TU.HAKUNA MSWAHILI HATA MOJA
    TUMEWAPOKEA MJINI NDIO MJUE KAMA MSWAHILI YUPO CIVILISED NYIO MAKWENU UKABILA MTUPU YANI SIFA MBAYA ZOTE KWENU
    MAUAJI YA ALBINO
    MAUAJI YA VIKONGWE UCHAWI WOTE UPOKWENU LAKINI HAMLIONI HILO NA KUTAKA KUWAPA WATU SIO SIFA ZAO HIZO NI PROPAGANDA TU MSWAHILI MTU SAFI WALA HUTOSIKIA KAWA FISADI KAUA AMA KUBAGUA MTU ILI MRADI MJINI RAHA TU YEYE NA STAREHE ZAKE TU
    KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA WAKUJA UTABAKI KUA WAKUJA TU NA NDIOMAANA UNAINFERIORITY COMPLEX UNAJIKATAA KUWA WWE SIO MSWAHILI
    MIMI NAJIVUNIA KUA MSWAHILI

    ReplyDelete
  35. me pia najivunia kua mswahili ingawa sitokei pwani
    niukweli usioficha kua waswahili ndio watu wastaarabu!!tizama tunavyojihanganya nao bila anzisha ubaguzi.
    angaleni southafrica wanavyoagua watu wasio wasouth huo ni mfano tu
    enzi hizo wazee wetu walikua wanajaribu kuwapa majina mabaya waswahili ilikupandikiza propaganda MAANA HATA KUOA TULIKUA HATUENDI KOA MAKWETU.
    wazee kuona hivyo ilimira na desturi zetu zisipote wakaona njia nikuanzisha kitu kitakachopunguza nguvu za mila za kiswahili zisienee kwa kasi
    maana mswahili katufundisha kula,kuvaa,na hata kuthaminiana na kutokua wabaguzi.
    niukweli usiofichika kila uchafu upo huko kwetu ila tunaficha tu hebu angalieni
    KUCHUNA NGOZI
    MAUAJI YA VIKONGWE
    MAUAJI YA ALBINO
    KUMTUIA TU RADI
    UFISADI
    KUDHULUMU
    UJAMBAZ
    UMALAYA(KUJIUZA NI KULE KWA KINA NANII)
    WAKATI HUKU KWA WASWAHILI WANATUFUNDISHA KUHESHIMU NA KUTHAMINI UTU NA WAZEE
    KUTOLEANA SALAMU N.K
    SASA JAMANI KWANINI TUSIANZE KUITANA MWIZI AMA FISADI TUMWITE MCHAGA!!KILA MWIZI MWONGO TAPEL FISADI JAMBAZI AKITOKEA TUWE TUNAMWITA JAMAA MCHAGA HUYU
    KILA MALAYA TUWE TUNAMWITA JAMAA NANIHINO HUYU
    KILA MCHUNA NGOZI MAUAJI YA ALBINO VIKONGWE KUABUDU USHIRIKINA JAMAA NANIHINO HUYU!!
    MAANA KIVITENDO TUNAONA HAKUNA HATA SIFA MOJA MBAYA INAYOMHUSU MSWAHILI
    NAWEWE ULIECHANGIA KUHUSU SIUI MFARANSA MARA MWINGEREZA UNACHOONGELEA WWE NI UTAIFA NA UKINGDOM NASIO MAHADHI
    SISI TUNAONGELEA MAHADHI WATANZANI TULIO WASTAARABU NI WASWAHILI NAUNGANA KILA ALIE MSTAARABU NI MSWAHILI
    NYIE WAKINA NANIHI WENYE FIKRA ZA KITWANA ENDELEENI NA UTWANA WENU MAANA TUNAONA KUNA BAADHI YA FAMILIA INAJIVUNIA MWANANGU ANASOMA INTERNATIONAL ANAONGEA KINGEREZA UPUZI MTUPU

    ReplyDelete
  36. NIKWELI KABISA WAZEE WETU WALIONA MILA ZETU ZINAMEZWA NA DESTURI ZA KISWAHILI NDIOMAANA WAKAONA BORA WAPANDIKIZE PROPAGANDA
    MAANA ILIFIKA KIPINDI HATA KWENDA KUOA KWETU TULIKUA HATUTAKI WOTE TULIKUA TUNAISHIA KWENYE VIJITOTO VINAVYOJUA MAPENZI WANAOJUA NINI THAMANI YAKUA MKE WA MTU NA NINI THAMANI YAKUA MUME
    VITOTO VINAVYOJUA MAHABA!!WANAJUA KUJIPODOA NA KUTUMIA MARASHI
    MAANA WANAWAKE WA KWETU WENGI WAKITOKA KULIMA HATA HAJAJISWAFI VIZURI ANAKWEDA LALA.
    WAZEE WAKATUMIA AJENDA YA KUMPA MBWA JINA BAYA ILIUWEZE KUMUHUKUMU MAANA TUNESAHAU KWETU
    UKWELI WATANZANIA USWAHILI WETU METUSAIDIA SANA

    ReplyDelete
  37. khaaaaaaaaa watu mnaandika magazeti umu ndani adi hatuwezi kusoma?
    michu yan awa wote ni waswahili aswaa jinsi tu wanavochonga umu
    hahahahaaaa
    aku babu mtuache na uswazi wetu nyie yawahusu nini?watoto wa pwani sie acheni tujifalague na yetu lugha,mshanfahamu apo?

    ReplyDelete
  38. duh basi jamani msitoea aibu zetu sana!!
    niukweli usiopingika watu wanaojifanya sio waswahili wanamapungufu makubwa sana na ndio maana hawajiamini kazi yao kijisifia wasivyo navyo!!tizama anajiita iwe anaesema akiwa bongo hataki kuitwa mswahili hivi kunakabila linalosifika kwa machafu kama hao wanaojiita wakina iwe?
    kwanza hupenda sana majivuno hii kutokana kwao hawajamaa kama umeshawahi kufika kagera ni maskini wakutupwa na ukiwa kule wao wenyewe wanapenda kubaguana yani wanasifa za kiganda mimi MTANI WAO NAWAJUA VIZURI SANA
    majivuno tu ndio waliyonayo

    ReplyDelete
  39. huyo mswahili anayesema wengine wanatoka kwenye nyumba za mavi ya ng'ombe amesahau kua nyumba zao ni za udongo na makuti. walivyokua wavivu hawawezi hata kuzikarabati nyumba zao kwasababu wako too busy wakiota jua na kuongea umbea. wenzao wakiwa shambani wanalima wao wanacheza bao au kupiga domo. hilo ndio wanalijua. for your information dar imejengwa na WAKUJA. tafadhali usiwalazimishe watu wengine uswahili.

    ReplyDelete
  40. Je niwaulizeni nyie mnao dai wakenya sio waswahili, wanaoishi visiwani lamu, pate, na sehemu kama malindi ni akina nani? Kamwe mkome kuropokwa na maneno msioyamenya. Fahamuni ya kwamba lugha hii ya kiswahili ilizaliwa pwani ya kenya na waliokuwa wakiizungumza ni wangozi amabo kwa sasa wamepakacha na kabila zile za kimijikenda. Hao pia waswahili halisi kuliko nyinyi!

    ReplyDelete
  41. Je niwaulizeni nyie mnao dai wakenya sio waswahili, wanaoishi visiwani lamu, pate, na sehemu kama malindi ni akina nani? Kamwe mkome kuropokwa na maneno msioyamenya. Fahamuni ya kwamba lugha hii ya kiswahili ilizaliwa pwani ya kenya na waliokuwa wakiizungumza ni wangozi ambao kwa sasa wamepakacha na kabila zile za kimijikenda. Hao pia waswahili halisi kuliko nyinyi! Jiulizeni sababu gani kisiwa cha lamu kagunduliwa kile kizee zaidi katika pwani ya afrika mashariki na watafiti. Kukana hayo si ni kukataa historia yenu waafrika wenzangu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...