HABARI ZA KUSIKITISHA ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI, FANUEL SEDEKIA, AMEFARIKI DUNIA JANA KATIKA HOSPITALI YA PORIYA TIBERIA, HUKO ISRAEL.
HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIKUWA AMELAZWA KWA WIKI TATU HOSPITALI HAPO AKISUMBULIWA NA KISUKARI PAMOJA NA NIMONIA. ALIKUWA HUKO KATIKA MSAFARA WA MAHUBIRI NA MCHUNGAJI MWAKASEGE.
MIPANGO YA KUULETA MWILI WAKE NYUMBANI KWA MAZISHI UNAFANYWA NA TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA HABARI ZINAPOTUJIA. KWA SASA KINACHOFAHAMIKA NI KWAMBA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE ARUSHA NA ATAKAPOZIKIWA BADO HAIJAJULIKANA KWANI YEYE KWAO NI KIGOMA.

MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMINA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Aaash its very sad dah! Sikukuu ya Noeli tulikuwa na Upendo nkone pale kanisani kwetu alitueleza yaliyomfika ndugu yetu huyu kule israel na alitusisitizia sana tumuweke kwenye maombi Fanuel, ila Upendo Nkene mwenyewe alishakata tamaa kabisa akasema inawezekana kabisa tunatiwa moyo tu kuwa atapona lakini hali ni mbaya sana na waimbaji wa muziki wa injili wanajitahidi kukemea roho ya mauti juu ya Fanuel lakini wengi wao wanakata tamaa dah, anyway tunapaswa kutambua kuwa hapa duniani sisi sote ni wapitaji tu ipo siku kila nafsi itarejea Mbinguni.
    Pole sana familia yake, watoto na mkewe ambaye mlikuwa mnaimba naye pamoja, poleni sana na ninaomba mfarijike na wimbo ambao aliuimba Fanuel unaosema JINA LA YESU NI NGOME YANGU: Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
    bwana alitoa na sasa ametwaa jina lake libarikiwe

    ReplyDelete
  2. Mungu ailaze roho ya Marehemu Fanuel Sedekia mahali pema peponi AMEN.
    Roho za marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa Amani. A.M.E.N

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli tumempoteza mwimbaji mzuri sana. Fanuel alikuwa anaimba kutoka rohoni.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  4. SEDY wetu!

    Yaniwia ngumu kuamini, nimepigwa butwaa. Duniani kuna shida, taabu na majonzi. Mbinguni tu ndipo tutapumzika milele daima. Natarajia kuonana nawe siku moja kwenye furaha ya milele. Nitazidi kukaza mwendo.

    Pole zangu za dhati kwa ayali yake, pamoja na wadau wote wenzangu duniani kote.

    Nitakukosa muda wangu wote uliosalia hapa chini ya jua :(

    SIMBA DUME AMELALA, SASA NI MUDA WETU SISI SOTE KUOKOTA SILAHA ZAKE TUKAPATE KUENDELEZA MAPAMBANO TUKIANZIA PALE ALIPOACHIA.

    John Adicka

    ReplyDelete
  5. It is with great shock kusikia kifo cha mpendwa wetu!!! Kweli sisi wanadamu hapa duniani ni kama maua ambayo huchanua na baadaye hunyauka na kuanguka chini na kuoza na kupotelea mavumbini. Huyu mpendwa wetu Fanuel Sedekia tulimpenda sana kwa sababu ya nyimbo zake za uinjilisti, nzuri, zenye mafundisho, za kuabudu na ambazo zilikuwa zimejaa upako. Hakika hata huwezi kuchoka kuzisikiliza. Mimi mdau hapa Oslo, Norway kweli nyimbo za Sedekia zilikuwa ndiyo kama Sara yangu ya kila siku. Ilikuwa haipiti siku bila kuzislikiza. Lakini basi Mungu alimpenda zaidi na ndiyo maana amemchukua akiwa anaendelea kutenda kazi yake. Amefariki katika kazi ya Bwana!! Katika kueneza injli kwa mataifa yote waweze kulikili jina lipitalo majina yote, Jina la Bwana wetu yetu Kristo. Bwana alitoa na Bwana ametoa. Jina la Bwana lihimidiwe.
    Amen!!

    NB: Brother Michuzi, ubarikiwe sana kwa kutapatia habari hasa sisi tulio mbali na Tanzania. Tunaiombea Blog hii idumu na hata milele katika kuhabarisha wadau. Ahsante sana Michuzi!!

    ReplyDelete
  6. its very sad, poleni sana wafiwa, nyimbo za Fanuel zilitubariki sana na tulifarijika sana kupitia nyimbo zake, japo sisi duniani ni wapitaji lakini when a young life is picked it doubles the sadness
    Mungu awape nguvu familia yake na wafarijike kupitia nyimbo zake za injili, amekufa katika bwana, he has finished the battle and kept the faith, bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete
  7. R.I.P
    AMEN

    ReplyDelete
  8. He was such a gret singer. His songs has delivered hundreds. R.I.P. Amen.

    ReplyDelete
  9. kwakweli Ni jambo lakusikitisha, lakini ni furaha pia pale unapoona mtu anaondoka duniani akiwa shahidi wa kristo katika maisha yake kifo cha sedekia ni pigo lakini pia ni fundisho kwetu sote tunaoishi...JE TUKO TAYARI KUFA? hofu ya kufa inatokana na utata wa mahali unapoenda baada ya kifo, but if we are living in christ nothing will frighten our souls...

    roho ya marehemu sedekia ikae mahali pema peponi. AMEN

    ReplyDelete
  10. Nimeshtushwa sana na habari ya msiba wa mwimbaji mahiri Fanuel Sedekia. Nyimbo zake zilikuwa zinanibariki sana. Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi daima tutamkumbuka.

    ReplyDelete
  11. R.I.P Fanuel Sedekia

    Moja ya nyimbo zake nzuri ni hii hapa
    http://www.eastafricantube.com/media/10565/Fanuel_Sedekia_-_Nani_Kama_Wewe/

    ReplyDelete
  12. Sedekia alikuwa mwimbaji mzuri sana sana na inasikitisha sana kumpoteza mwimbaji mzuri inatia uchungu sana haswa pale unaposikia nyimbo zake akiimba kwa kweli Bwana amevuna kondoo wake inabidi kushukuru kwa hili lililotokea japo linauma sana lakini Mungu awape familia yake Mke wake na watoto, ndugu jamaa na marafiki wote awape faraja na amani haswa katika kipindi hiki kigumu. Mungu Akulaze Mahali Pema Peponi Mpendwa wetu Sedekia.

    ReplyDelete
  13. RIP SORRY FOR THE FAMILY
    TUMAKUKUMBUKA KILA TUNAPOSIKILIZA NYIMBO ZAKE ZENYE UJUMBE NA FARAJA.
    BWANA YESU NDIYE FARAJA YA KWELI.

    ReplyDelete
  14. Bwana amemchukua Fanuel wakati bado tunamwihitaji. Kazi ya Bwana Haina Makosa, Biblia inasema'Sifurahishwi na kifo cha mtu mwovu....maana yake ni kwamba, Mungu hufurahishwa na kifo cha mtu Mwema. Fanuel Sedekia alikuwa mtu mwema sana, mimi ninamfahamu toka mwaka 1993 wakati wa Youth Camps za New Life Band. Kule Monduli wakati anaunda ETM. Nyimbo zake zilikuwa zinabariki kuliko maelezo. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE.

    NYANGUSI NDUKAI LAISER

    ReplyDelete
  15. ni habari ya kusikitisha sana!! On sunday nilikuwa kwenye bus ya dar express nikitokea arusha kuja dar, katika cku ile walituwekea VCD za nyimbo ya Fanuel alizorekodia kanisani. Binafsi nilifarijika sana na zile nyimbo, ni kama alikuwa live mbele ya uso wangu. Nimeshtuka sana kuona habari hii ya kuondokewa na m2 aliyemtanguliza Mungu katika maisha yake na kutu inspire kupitia nyimbo zake nyingi.

    ''Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe''

    ReplyDelete
  16. Jamani, ni neno gumu kusikia Fanuel Sedekia ni marehemu. Kifo ni andiko lakini jamani hakizoeleki kwa nini jamani. Kweli nina imani kwamba yawezekana Mungu ameruhusu kwa namna fulani alale katika pumziko la muda kabla hajarudi hivi karibuni. Lakini jamani INAUMA SANA KUSIKIA FANUEL NI MAREHEMU. Amenibariki kwa nyimbo zake za SIFA na heshima na kicho mbele za Mungu, ila ametuachia "Assignment", kwamba sisi tumefanya kazi ya Mungu kwa namna gani?. Yeye amekuafa kama askari akiwa vitani?. Alikwenda kumuinua YESU huko ISRAEL. Lakini mauti ikamkuta huko huko alikokuwa YESU. Jamani nina imani kubwa kama nitajitahidi kutengeneza maisha yangu yawe safi mbele za Mungu na kufanya kazi yake kama yeye alivykwenda huko, basi nina imani tutaonana huko. Nampa pole sana Mkewe na watoto wao ambao wameachiwa majonzi makubwa sana ni ngumu sana kukubali hata kama tunaamini BWANA AMEMCHUKUWA.
    Mwakasege, nakupa pole sana na mama na msidhani mmekwenda bure huko la,.... huyo ni shetani ameona kazi ya Mungu akaona wivu lakini ameshindwa kwa jina la YESU.
    Fanueli amelala anasubiri ufufuo pindi YESU atakapokuja mara ya pili.
    Poleni wote huko Israel kwa msiba huu, tunawaombea mtafika salama na tutawapokea kwa USHUJAA maana tunajuwa ASKARI wa YESU amepiga vita vizuri na mwendo ameumaliza anasubiri TAJI mbimguni.
    Amina.
    Anna Abduel, Dar es salaam

    ReplyDelete
  17. nimeshituka mno kwa taarifa hizi.last week nilisikia kafariki but tukaambiwa baade sio kweli.miongoni mwa wanamuziki wachache wa gospel waliomaanisha kufanya huduma kwa kuiishi imani!mara ya mwisho mbeya(semina ya mwakasege)nilipata wivu kwajili yake kwani alikua in another dimension,upako,kiwango!!Mungu nisaidie niimalize safari salama,NISIWE MWENYE KUWAHUBIRIA WENGINE KISHA MIMI KUACHWA!R.I.P

    ReplyDelete
  18. anon 8:56 umeongea la maana.tupo tayari kwa mauti?

    R.I.P. FANUEL

    ReplyDelete
  19. Napenda kuwapa pole familia ya Sedekia mjane,watoto wake na mdogo wake Nsenge.Mungu awape uvumilivu wakati huu mgumu wa majonzi.Nyimbo Sedekia tulizipenda sana na yeye pia tulimpenda ila Mungu alimpenda zaidi yetu.
    Bwana ametwaa jina lake libarikiwe Ame.

    ReplyDelete
  20. Kwakweli ni huzuni sana hasa kwa upande wangu..jamani mwaka 2001 nilikua napita katika changamoto kali sana! Mungu alizitumia nyimbo za Mpendwa Sedekia kuniwezesha kusimama na kunitia nguvu sijawahi kuona....Mungu tunakushukuru kwa yote tunaamini kuwa tutaonana na mpendwa wetu kaka Fanuel Sedekia

    ReplyDelete
  21. Kwa ni wasafirishe maiti kuja kuzikwa Tanzania.Si wamzike huko huko nchi takatifu alikofia?

    Waweza mzika hata Gaza au waombolezaji wanaogopa makombora ya Israel ndio maana wanataka azikwe Tanzania?

    ReplyDelete
  22. Kuna kipindi nilikuwa katika mazingira magumu ya kimaisha... nilikuwa kila kuanzia asubuhi saa kumi na mbili hivi nachukuwa CD ya Fanuel "Katika Ibada" na kuisikiliza kila siku .... kwa kweli ilikuwa inanifariji sana ...nawapa pole wote

    Fanuel alikuwa ni mwimbaji wa aina yake na nafikiri alizaliwa hivyo

    ReplyDelete
  23. siamini,mtumishi Fanuel
    his songs are my inspirational always,so blessing etc sina lugha ya kuelezea hii taarifa,,its paining
    nilishilikiana nae sana ktk hafla moja vizuri sana km watumishi na it was so blessing,,my first time to see him face to face & I always wanted to meet him,,ill never forgate that day i felt,
    nilipata taarifa kwanza ya kulazwa ICU then ya msiba wake siku kidogo zimepita sikuamini nilijikuta tu nalia.
    truly God's calling to rest.ila sielewi why him??chibalonza nk
    pole mkewe na watoto Yesu awatie nguvu kuu.
    i wish to attend his funeral ntasafiri nije Arusha pliz keep us informed when exactly!!thax michu

    ReplyDelete
  24. Mwanadamu ni nani basi jamani hata umthamini!!! Mungu kweli ana makusudi naye, Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake na libarikiwe! ni wakati wetu wa kujiweka tayari maana hatujui muda wa kujiliwa kwetu.Lord have mercy on us all and cover his family with heavely peace! you shall be missed indeed brother
    Gloria DSM

    ReplyDelete
  25. Jamani,kweli kazi ya Mungu haina makosa!!!!yani jana tu nilikuwa nasikiliza nyimbo zake especially UPENDO...yani...Mungu ailaze roho yake peponi....

    ReplyDelete
  26. Ni baraka kubwa na heshima kufa katika Bwana,Umetutangulia,Vita umevipiga,Imani umeitunza,Umepokelewa kwa Shangwe na Jeshi la Mbinguni.Tunakupenda Sedekia with beloved ETM team.

    ReplyDelete
  27. RIP SEDEKIA!!!

    UA lililochanua nimefunga!!!

    Poleni wafiwa, mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    Frida.

    ReplyDelete
  28. Nchi na Vyote viijazavyo ni Mali ya Bwana hata Sedekia alikuwa mali yake yatufundisha nini sisi tuliobaki ni kwamba tuwe tayari wakati wowote maana hatujui Mauti itatukuta lini hakuna Mji udumuo hada Duniani Mungu awape faraja ya kweli Familia watumishi wenzake yani waimbaji wahubiri wa neno marafiki na Jamaa.

    ReplyDelete
  29. Msiba wa Fanuel umeniumiza sana sana. Nyimbo zake zilikuwa zinanibariki sana. Mara ya mwisho nilimwona alipoimba kwenye sherehe za miaka 50 ya kanisa la TAG Calvary Temple, Arusha hatukutamani amalize. RIP Fanuel na Mungu aitie nguvu familia yako maana kwa kweli wameondokewa na mtu muhimu mno maishani.

    ReplyDelete
  30. Kwa kweli inatia simanzi kwa kifo cha ghafla namna hii. Lakini yote hayo ni mapenzi yake Mungu hatuna pingamizi. Nasikia kuna mchango ili waweze kulipa gharama za hospital na kusafirisha mwili, kwa anayejua account number tafadhali atujulishe nasi tuweze kusaidia.

    ReplyDelete
  31. I am speechless and sad about what has happened lakini tukumbuke sisi sote tupo safarini, atujuhi siku wala saa,tumuombe roho mtakatifu atuongoze na kutufundisha kuwa kwenye utayari wakati wote. Sedekia ametusaidia kutuhubiria wengi thru his music I pray for his wife and his children Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana Yesu lisifiwe.

    ReplyDelete
  32. Ni jambo la kusikitisha na wakati huohuo ni jambo la kutukumbusha kuwa sisi wote ni wasafiri ambao wakati wowote unaweza ukaondoka.Tunafanyiana visa tunakosa kupendana wakati wote sisi ni marehemu watarajiwa.Hebu vifo na matokeo ya kushitusha hivyo yatupe muda wa kusoma nyakati,tudumishe kupendana na kusaidiana badala ya kuwa na ubinafsi ambao unapokurupushwa ukaondoka ghafla kama Fanuel unaacha ndugu wakigombania.hili litufundishe kuacha ubinafsi tamaa fitina roho mbaya wizi n.k kwani wakati usioujua utayayuka.
    kwa heri/buriani Fanuel.

    ReplyDelete
  33. Kapumzike salama Jemedari hodari wa Yesu. Umepigana pigano jema na Bwana amekuita jemedari wake nyumbani ukapumzike. Mbegu za wokovu ulizopanda bila shaka zitamea vyema na matunda yake utayaona siku moja.

    Ukitaka kusikiliza baadhi ya nyimbo za Jemedari Sedekia tembelea hapa
    http://nyimbozadini.blogspot.com

    ReplyDelete
  34. Ndugu uliyeomba account no. kuchangia gharama za msiba wa mtumishi Fanuel Sedekia ni Renatha Fanuel Sedekia CRDB Arusha Branch 01J20995671200. Mungu akubariki. Kama upo Dar es Salaam unaweza kupeleka mchango wako Praise Power Radio au Wapo Mission Radio

    Tina Kasusa

    ReplyDelete
  35. Bi. Tina Kasusa,

    Asante sana kwa kunipatia account number, kwangu ni rahisi zaidi kwenda CRDB niko nao jirani kuliko huko Praise power au Wako Radio. Mungu akubariki sana!

    ReplyDelete
  36. Bi. Tina Kasusa,naona No. za A/c zimezidi,hebu rekebisha halafu tutumie tena, asante kwa moyo wa kutoa.Mungu akubariki.

    Mwakalebela,GT

    ReplyDelete
  37. Yaani mimi sina hata la kusema nimesikitka sana kusikia habari hii kuwa mpemndwa wetu Sedekia kafariki dunia.Nakumbuka nilipokuwa mdogo sana alikuwa anakuja nyumbani kwetu na alikuwa napemdasana kuimba na nyimbo zake zikilikuwa faraja kwangu kila siku hasa wakati wa shida.Nawapa pole sana ndugu zake na familia hasa mke wake na mdogo wake Phares na babake na mamake na worship froup yake na Mungu aendelee kuwatia nguvu na uvumilivivu.Sisi sote tutapitia njia hiyo an tutamukuta ndugu yetu fanuel

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...