JK amemvua madaraka na kumtimua kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Albert Mnali kutokana na kitendo chake cha kuamrisha kuchapwa bakora hadharani waalimu wa shule za msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene juzi kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kuwajibika na kufanya shule hizo zidorore katika masomo.
Taarifa kutoka O fisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa sasa hivi nasema kwamba serikali imepokea kwa kwa masikitiko makubwa na kitendo hicho na kukitaja kuwa hakikubaliki na ni cha kudhalilisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. Nampongeza rais kwa uamuzi wa haraka ila kuvuliwa madaraka nadhani haitoshi, anatakiwa pia apelekwe shule hiyo hiyo akachapwe viboko mbele ya walimu na wanafunzi. Hii inaonyesha ni kiasi gani walimu wanavyodharauliwa!!!

    ReplyDelete
  2. duh!hii ni ajabu na kweli tumezowea kusikia wanafunzi kupigwa bakora lakini hili tukio ni la aina yake inafaa liandikwe kwenye guiness book of record.

    ReplyDelete
  3. Hatari lakini salama

    ReplyDelete
  4. Nilijua tuu maana hii issue ilikuwa imekaa vibaya sana kwa jamaa!

    ReplyDelete
  5. Thats too funny! Huyo mkuu wa wilaya ana mambo kweli...bakora tena?

    ReplyDelete
  6. Watu wengi wanafikiri kwamba walimu walikubali kuchapwa kwa hiari.Walilazimishwa kwa kupigwa na polisi mateke na ngumi na kuchapwa bakora huku wakijitetea lakini haikusaidia lolote.Hongera Rais kwa kumtimua huyo mkuu wa wilaya na waalimu wawafikishe kwenye vyombo vya sheria polisi na huyu mkuu wa zamani wa wilaya.

    ReplyDelete
  7. Sasa inabidi afanye hivyo hivyo pia kwa MAFISADI ambao wako kwenye Baraza lake la Mawaziri, Kuna Mawaziri kibao ambao ni MAFISADI na wananchemsha kila siku lakini JK huwa anauchuna na wala hachukui hatua zozote mpaka wajiuzulu wenyewe.

    ReplyDelete
  8. ninamshukuru rais wetu kwa kumadhibu huyo mkuu wa wilaya kwa kitendo chake hicho cha kinyama. mimi nilishangaa sana kusoma kuwa DC ana amuru walimu wachapwe. hivi hawa ma DC wanajua kazi zao. nani amewapa ruksa kuchapa watu. huu mtindo uachwe haraka. si ma DC tu hata wakuu wa vijiji huwachapa wanavijiji kwa kosa hili au lile. haya wananchi muwashtaki hao walio madarakani ambao wamechukua sheria kuwachapa au kuwapa adhabu za aina nyingine. msikae kimya wakati watu wanawaonea.

    ReplyDelete
  9. JK, vipi baba wacha wacharazwe bakora hadharani. Hawafanyi kazi yeyote, watoto wanafeli. Huyu Jamaa Albert Mnali ndio anafaa kuwa Raisi wa Tanzania. Atembeze bakora kwa mafisadi wote hadi wanyooke. Baada ya hapo ndio tutazungumzia Rule of Laws.

    Nchi hii inahitaji kichaa kama Albert Mnali kuinyoosha. Ukienda mwendo wa JK hatutafika. Nadhani mnakumbuka enzi za Mrema watu walivyokuwa hawafanyi kazi enzi za Mwinyi. Mrema alianza kufunga mageti kama haupo basi umekosa kazi. Nidhamu ilianza kupata juu. Huyu Albert Mnali ni shujaa kwangu, tunahitaji watu kama hao 10tu hii nchi itanyooka kwenye mstari

    ReplyDelete
  10. BRAVO JK NA PINDA NYERERE ALISEMA MTU KAMA HUYO AKIUKOSEA UMMA AADHIBIWE HAPOHAPO!

    ReplyDelete
  11. Kwa kuwa nami ni mwalimu, udhalilishaji huu umeniuma sana!
    Huyu jamaa asiachwe hivi hivi, kumfukuza kazi peke yake si adhabu ya kutosha.
    Afikishwe tu mahakamani, na si hivyo tu, bali kwa mguu wake ashurutishwe kwenda tena Bukoba kuwaomba radhi walimu wale.
    Lakini pia tukio hili ni ishara ya unyanyasaji dhidi ya walimu katika Tanzania. Hakuna anaejali kuwalipa mishahara walimu, hakuna anaejali kuwapatia walimu huduma bora za kujengewa nyumba au kupatiwa usafiri. Kila kukicha mwalimu wa Tanzania ni watu dhalili wasio na mbele wala nyuma. Mpaka lini?
    Hapa Ukerewe kazi ya ualimu inathaminiwa kisawasawa, hata malipo ni ya kuridhisha tu. Mwalimu akikuandikia reference ni ujiko kabisa. Na matokeo yake, wenzetu elimu zao zinaboreka na zetu huko nyumbani zinakosa thamani. Utitiri wa mashule huutamani, lakini quality ya elimu ni utumbo mtupu.
    Huyu mkuu wa Wilaya msimwache walimu wenzangu, liwe ni somo na fundisho kwa woote wenye jeuri kama yake.

    ReplyDelete
  12. na ndugu Issa Muhidini wa Michuzi amehamishiwa wilaya hiyo ya Katerero na uteuzi huo unaanza mara moja.

    ReplyDelete
  13. Hiyo ni hatua thabiti, lakini suala la msingi inabidi wale walimu walipwe fidia kutokana na kudhalilishwa na mkuu huyo wa wilaya aliyefukuzwa.Maana kisaikolojia hadhi yao imeshuka mno, imewaumiza mno kwani wanafunzi wanawacheka, mtaani hawana la kusema, wakisema kitu, wanataniwa kuwa mlichapwa viboko nk.

    CWT iendeleze kesi yake mahakamani, si suala la kuishia hapo tu kwa kuwa amefukuzwa basi iwe zima moto.Lazima wafundishwe adabu hao viongozi wanaodhani huo umonta wa ukuu wa wilaya ndio unakua juu ya sheria.

    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  14. I wish Mheshimiwa Rais angekuwa ana Act namna hii kwa watumishi wote wa umma wa dizaini bila kujali size ya vyeo vyao wala ngazi zao. angejingea heshima kubwa kwa Watanzania.

    ReplyDelete
  15. Taarifa hii ya kupigwa walimu imezagaa duniani, kupitia vyombo vya habari, na kuliletea Taifa letu aibu kubwa. Naungana na Watanzania wenzangu kulaani kitendo hicho.

    Ni muhimu pia Watanzania tujiulize: iwapo watoto wanafeli masomo mashuleni, chanzo cha tatizo ni nini na dawa yake ni ipi? Ni suala pana, ambalo linahitaji uwajibikaji kwa upande wa watoto, walimu, wazazi, jamii, na serikali. Sio kuwalaumu walimu tu, kama alivyofanya huyu mkuu wa wilaya. Siku chache zilizopita, niligusia kipengele kimoja cha suala hili la uwajibikaji, kwenye makala hii hapa.

    ReplyDelete
  16. BARUA YA WA WAZI KWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUMTIMUA FISADI WA MAADILI
    ------------------------------------------------------------------------------------------------------------
    MIMI KAMA MKEREKETWA NA MPINGA UFISADI NA USENENE NAMBA WANI, NAPENDA SANA KUTOA PONGEZI ZANGU ZA DHATI, KWA KAZI NZURI ULIYOIFANYA DHIDI YA FISADI NA ADUI WA MAADILI ALIYEWACHAPA NA KUWADHALILISHA WALIMU WETU.

    HUYU MKUU WA WILAYA NAYE PIA TUNGEFURAHI KUONA ANAPEWA MBOKO. KADHALIKA APELKWE RUANGO KEKO AU SEGEREA, ILI AKUTANE NA WANAUME HALISI HUKO NDANI KABLA YA KUNIPA UTAWALA WA WILAYA YAKE

    INAKUWA AIBU KUBWA SANA KWETU SISI WATANZANIA KUONA KWAMBA HAWA VIONGOZI WETU WANAJICHUKULIA SHERIA MIKONONI MWAO. ILI HAKI IWEPO, TUNAOMBA HUYU FISADI NAYE APEWE MBOKO JINSI ALIVYO WADAHALILISHA WALIMU WETU

    MZEE WA PAMBA, HESHIMA KWAKO, 2010 TUNAKUPIGIA KURA TENA, ILA NASI PIA UTUUNGE MKONO 2015, TUNAOMBWA UWABARIKI WANAO. MIMI NITAGOMBEA UKUU WA HIYO WILAYA AMBAYO IMECHAFULIWA JINA CHINI YA UONGOZI WA

    Mh. Mashaka, January, Dr. Shayo na Ridhwani. Kwa hiyo naomba mnipigie Kura 2015 kuchukua wilaya Mbili, iliyochafuliwa jina na Ile ya Yombo Vituka.

    RAIA WA KAWAIDA NDO AMEKUWA AKIUMIA, MAFISADI YANAPETA TU MUJINI NA MAGARI YENYE UBARIDI NDANI YAKE.

    HAO WAHESHIMIWA HAPO JUU WAKICHUKUA MDARAKA, TUTAWAWEKA HAO MAFISADI HADHARANI ILI NAO WAPIGWE MBOKO……..WOTE HAKUNA ATAKAYEPONA

    ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
    ZIDUMU

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    KIDUMU

    KIDUMU FIRKA ZA LAIS MTARAJIWA 2015
    ZIDUMU

    ZIDUMU FIKRA ZA MAKAMU 2015
    ZIDUMU


    MAFISADI YOTE NAYO YACHAPWE MBOKO
    YACHAPWE

    MKEREKETWA, YOMBO VITUKA !!!!
    ---------------------------------------
    Dakika 30 za Internet Café Zimekwisha

    ReplyDelete
  17. BARUA YA WA WAZI KWA ALBERT MNALI, MKUU WA WILAYA YA ZAMANI
    -----------------------------------------------------------------------------------
    WEWE MKUU WA WILAYA YA ZAMANI, MIMI NINAKUHAKIKISHIA, KWAMBA HIKI KITENDO ULICHOKIFANYA LAZIMA TUKILIPIZIE KISASI 2015. TUTAKUFUTA HATA KAMA NI KWAKO NAWE UCHPWE MBOKO
    KWA SASA MIMI NDO MKUU WA HIYO WILAYA PAMOJA NA ILE YA YOMBO VITUKA.
    RAIA WA KAWAIDA NDO AMEKUWA AKIUMIA, MAFISADI YANAPETA TU MUJINI NA MAGARI YENYE UBARIDI NDANI YAKE. HAO WAHESHIMIWA HAPO JUU WAKICHUKUA MDARAKA, TUTAWAWEKA HAO MAFISADI HADHARANI ILI NAO WAPIGWE MBOKO……..WOTE HAKUNA ATAKAYEPONA

    ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
    ZIDUMU

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    KIDUMU

    KIDUMU FIRKA ZA LAIS MTARAJIWA 2015
    ZIDUMU

    ZIDUMU FIKRA ZA MAKAMU 2015
    ZIDUMU

    KIDUMU FIKRA ZA MKUU WA WILAYA 2015 (MIMI)
    KIDUMU
    MAFISADI WOTE WALAANIWE,
    WALAANIWE.

    MASENENE WOTE WAKAFIE HUKO U.S.A NA U.K. WABEBE BOXI HADI WAFE KWENYE SHIFTI NA UROHO MBAYA

    MKEREKETWA, YOMBO VITUKA !!!!
    -----------------------------------------
    Dakika 30 za Internet Café Zimekwisha

    ReplyDelete
  18. Albert Mnali nenda ukale jeuri yako mtaani sasa. Ulipopewa ukuu wa wilaya umejiona kama 'nusu mungu', je ungekuwa hakimu mkazi ingekuwaje limbukeni wewe.
    Poleni wanafamilia ya Mnali kwa ujinga wa baba yenu.

    ReplyDelete
  19. Bwana misupu mfikishie salamu JK kuwa tuanfurahia utendaji wake kazi ila ombi langu lingine mtafute yule mwanajeshi aliye mloweka dereva wa daladala kwenye dimbwi ili na yeye afutwe kazi kwa kuchukua sheria mkononi.

    ReplyDelete
  20. makini kabisa.watu wengine wanakuwa kama wamechangnyikiwa vile.kwanza nae anatakiwa apate adhabu ya viboko "...akamwonyeshe mkewe...."kama alivyokuwa anasema Mwl.Nyerere..

    ReplyDelete
  21. Tunashukuru JK kuchukua hatua za haraka dhiki ya watu wanaolewa madaraka. Lakini tunamuomba hatua hizo zisiishie kwa mkuu wa wilaya tu, hilo lungu liwadondokee akina Masha pia. Anakotupeleka Masha ni kubaya zaidi ya hayo makosa ya DC. Masha inabidi achapwe viboko kwanza na baadae aondolewe madarakani

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  22. JAMANI, NAMSHUKU5U RAIS KWA KULIONA HILO. LAKINI HATA HIVO, MKUU WA WILAYA HIYO ANATAKIWA AWEKWE RUMANDE AKISUBIRI KESI YAKE. AMETUDHALILISHA SANA WALIMU WOTE NCHINI. HATA HIYO ADHABU YA KUFUKUZWA HAITOSHI.

    LAKINI, NDUGU ZANGU WATANZANIA, TUNATAKIWA KUJIFIKIRIA JUU YA UTEUZI WA WAWAKILISHI WA RAIS, KAMA WAKUU WA MIKOA, WILAYA NK. RAIS ANATAKIWA KUWA MAKINI SANA. MTU KAMA HUYU MKUU WA WILAYA, HATA SIKU MOJA HUWEZI KUNIAMBIA KAFANYA KOSA HILO KWA BAHATI MBAYA. NDIO SHIDA YA KUTEUANA SABABU YA KUFAHAMIANA NA MTU.

    NINA MACHUNGU SANA.

    ReplyDelete
  23. JAMANI, NAMSHUKU5U RAIS KWA KULIONA HILO. LAKINI HATA HIVO, MKUU WA WILAYA HIYO ANATAKIWA AWEKWE RUMANDE AKISUBIRI KESI YAKE. AMETUDHALILISHA SANA WALIMU WOTE NCHINI. HATA HIYO ADHABU YA KUFUKUZWA HAITOSHI.

    LAKINI, NDUGU ZANGU WATANZANIA, TUNATAKIWA KUJIFIKIRIA JUU YA UTEUZI WA WAWAKILISHI WA RAIS, KAMA WAKUU WA MIKOA, WILAYA NK. RAIS ANATAKIWA KUWA MAKINI SANA. MTU KAMA HUYU MKUU WA WILAYA, HATA SIKU MOJA HUWEZI KUNIAMBIA KAFANYA KOSA HILO KWA BAHATI MBAYA. NDIO SHIDA YA KUTEUANA SABABU YA KUFAHAMIANA NA MTU.

    NINA MACHUNGU SANA.

    ReplyDelete
  24. Ndugu Michu, Hongera kwa kazi nzuri sana ya kutuhabarisha, kuelimisha na mengine kibao ikiwemo vunja mbavu moja mbili za kusisimua kabisa!
    Nilishtushwa na kufedheheshwa sana na taarifa juu ya tukio la huyo mkuu wa Wilaya! Nilijiuliza hivi inawezekanaje nchi ikawa na viongozi wendawazimu kiasi hiki?
    Rai yangu ni kwqamba huyu jamaa lazima asimamishwe kizimbani kwani katenda kosa la jinai! Hebu fikiria athari za kisaikolojia watakazopata WAALIMU hawa achilia mbali walizokuwa nazo kutokana na ugumu wa mazingira ya kazi zao na kipato kisichokidhi!
    LAKINI JAMANI, Hebu na tujiulize ilikuwaje waalimu wetu hawa wakakubali KUCHAPWA?? Tabia hii ya kuendekeza unyongwa na HEWALA BWANA hata katika mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu kuyakataa itatupeleka pabaya! Walidhani watafukuzwa kazi wakimgomea huyo mwendawazimu??
    Hapa tunalo la kujifunza juu ya mfumo wetu wa ELIMU uzalishao watu WAOGA na wasiojua HAKI zao! Uko wapi UJASIRI tuliofundishwa na Mwalimu NYERERE wa kukataa DHULUMA na KUONEWA?? Nchi yetu inahitaji kujenga upya mfumo mzima wa ELIMU kwani wa sasa haufai utatupeleka GIZANI.

    NB: SIO UTANI, NILIVYOONA HIYO HABARI KWAMABA JK amtimua..... Duuuu Nikajua MASHA KIBARUA KIMEOTA MBAWA!!! Tehehehehtehehtehe
    JK anayo KAZI ya kutimua wengi tu!!

    LIPITISHWE AZIMIO LA KUHAKIKISHA huyo mchapa watu huyo anafikishwa MAHAKAMANI haraka iwezekanavyo.

    Mdau toka Oslo, Norway

    ReplyDelete
  25. mkuu wa wilaya ya nanii hapa umeteleza kidogo, Mh.Rais hajamfukuza kazi huyo mkuun wa wilaya isipokuwa amemsimamisha kazi. Kisheria huwezi kumfukuza mtu kazi kabla hujampa muda wa kujitetea. Hata kama vyombo vya habari vimeripoti kuhusu huyo jamaa kuwatandika viboko walimu lakini haijathibitishwa rasmi kwamba ni kweli au si kweli.RAis alichofanya ni kumsimamisha kazi huyo jamaaa
    Sijui kitu

    ReplyDelete
  26. Angalau kwa uamuzi huu tunaweza kusema ya kwamba serikali ipo macho na wavunja sheria ila tunaimba itupie macho kwa watendaji wengine, hasa polisi kwani wao ndiyo wavunja sheria wa kwanza na ni mara chache sasa kusikia maamuzi mazito yanatolewa na mkuu wa jeshi la polisi dhidi ya polisi wahalifu. Napongeza uamuzi huu, kwani hivyo viboko walipaswa kuchapwa wao na wakurugenzi wa halmashauri kwa wizi wa pesa za umma na kuzorotesha maendeleo ya umma

    ReplyDelete
  27. Safiii JK kwa uamuzi mzuri, nikitendo cha udhalilishwaji kabisa wale ni watu wazima halafu unawachapa hadharani maana yake nini ? tena adhabu hiyo ya mkuuwa wilaya iambatane na adhabu kali kwa mujibu wa sheria

    ReplyDelete
  28. JK your so unfair kwakweli kwa huyo DC, sio kwamba ameshindwa kufanya kazi ila ni kwamba alikuwa anawakumbusha walimu wajibu wao na sio kuwa watoro. Huyo DC mimi kwangu ni shujaa maana Tanzania bila viboko sasa haiwezi kuendelea maana huyo aliona hamna jinsi ya kuwakumbusha watu wajibu wao zaidi ya kuwachapa viboko. VIboko tuu mnapiga kelele mbona watu wananyongwa sembuse Viboko mimi ningekuwa JK nimgempa cheo huyo DC kwa kitemdo cha kishujaa alichofanya Tanzani ni wavivu sana. Na huyo anafaa sana kuwa Rais wetu maana mafisadi hawataiba sababu wanajua wakiiba Viboko vinawasubiri tena hadharani. Hongera sana DC hata kama huna Kazi ila Naimani wale walimu waliochapwa viboko hawatakusahau na hawatakuwa wavivu kabisa katika kazi zao maana watakukumbuka sana na baadaye wataona kuwa ilikuwa ni haki yao kuchapwa viboko. Na nyie mafisadi Mjiandae sio mnasemasema tuu tutawachapa Viboko ngojeni mimi niwe Rais.

    ReplyDelete
  29. THANK YOU jakaya! mtu wa wa2! wakumbushe hawa viongozi haya madaraka yanakuja na kuondoka! mi niomeona aibu kwani nimona news leo ktk bbc huku U.S. wat embarssment was!!

    ReplyDelete
  30. Huyo mkuu wa wilaya aliyetimuliwa, Albert Mnali ndo mtu pekee anayefaa kuwa rais wa nchi yetu. Kwa upumbavu uliomo miongoni mwa watanzania, kwa hakika adhabu za viboko zinatakiwa ziwepo mpaka kazini.

    ReplyDelete
  31. Asante sana Mkuu wa Nchi, lakini bado hiyo adhabu haitoshi...

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    TUNATAAAAKA... ALBERT MNALI... APIGWE VIBOKO.... HADHARANI!

    ....

    ReplyDelete
  32. Na afikishwe mahakamni

    ReplyDelete
  33. WADAU HAPA NDIO SISI WENGINE TUNACHANGANYIKIWA , IKIWA WENGI WETU TUNAPINGA KITENDO CHA KINYAMA CHA HUYU LIMBUKENI KWA KUZINGATIA KIPENGELE CHA KUWADHALILISHA WAHESHIMIWA WALIMU WETU, MBONA MNASHAURI SERIKALI AU MWENYE MADARAKA WARUDIE UNYAMA HUO KWA HUYU MKUU WA NANIHII, WAKATI TUNA VYOMBO VYA SHERIA VYENYE UWEZO WA KUMHUKUMU?

    MDAU KANADA

    ReplyDelete
  34. tatizo la kuchangua wakuu wa ngazi za juu kwa sababu ni kada wa chama kilichopo madarakani bila kuelewa kama jamaa ana sifa ya kuongoza wananchi....mtu yeyote, tena mkuu wa wilaya anayejua sheria za nchi fika. kuburuza walimu na kucharaza ni kudhalilisha chama kilichomuweka madarakani...wait a minute. hiki ndio chama ambacho kimekubwa na kashifa zote za kuibomoa nchi bila haya....hii ni ccm.ndugu wananchi mnakumbuka lile soo la mwinyi na mrema enzi zileee za kambarage...mwinyi kichwa juu kaenda zake kusurubisha wachawi shinyanga...baadaye akawa rais....knuckle head akaongoza nchi.
    maadamu rais ameona hii ni hatia kwa mkuu wa wilaya kutumia uendawazimu wake. ndugu walimu muda wa kuachana na kazi ya ualimu umefika....fidia yenu ni kubwa zaidi ya fedha ya epa iliibiwa. just imagine mwalimu uliyecharazwa unatoa nasaha kwa watoto wa shule...nani atayekusiliza. je? watoto wako, na mke wako au mume wako atakuonaje, looser!!! siku nyigine unaambiwa na partner wako leo leo hupati kitu looser.hii ni serious issue!hawa watu wanahitaji therapy.kosa la kushindwa kufaulu sio la shule ile ni mfumo mzima wa wizara ya elimu ilivyoundwa, uwajibikaji kuanzia ngazi za juu. kama mkuu wa wilaya haja-set mfumo mzima wa taaruma ya wilaya yake, na mwisho wa mwaka anataka wanafunzi wafaulu basi akili yake sio sawa, kama siyo yeye basi aliyemweka hapo akili zao zinafanana.

    ReplyDelete
  35. JK UMEMWONEA, HUYU MKUU WA WILAYA NDIYE ANAYEFAA KABISA KABISA TENA YAELEKEA ANAUCHUNGU WA NCHI YAKE KWA NINI ASINGEPEWA UWAZIRI MKUU,???? HATA WAGANDA WANASEMA IDD AMINI SIFA MOJA ATAKUMBUKWA ALIKUWA NA UCHUNGU NA NCHI YAKE ,NASHANGAA WENGI WANAMPINGA TANZANIA INAFAA KABISA KUWA NA WATU KAMA HAWA,MUNGU MBALIKI MNALI NAKUPA KILA LA KHERI

    BY ISMA KABENGO,KAMPALA,UG

    ReplyDelete
  36. JK UMEMWONEA, HUYU MKUU WA WILAYA NDIYE ANAYEFAA KABISA KABISA TENA YAELEKEA ANAUCHUNGU WA NCHI YAKE KWA NINI ASINGEPEWA UWAZIRI MKUU,???? HATA WAGANDA WANASEMA IDD AMINI SIFA MOJA ATAKUMBUKWA ALIKUWA NA UCHUNGU NA NCHI YAKE ,NASHANGAA WENGI WANAMPINGA TANZANIA INAFAA KABISA KUWA NA WATU KAMA HAWA,MUNGU MBALIKI MNALI NAKUPA KILA LA KHERI

    BY ISMA KABENGO,KAMPALA,UG

    ReplyDelete
  37. JK UMEMWONEA, HUYU MKUU WA WILAYA NDIYE ANAYEFAA KABISA KABISA TENA YAELEKEA ANAUCHUNGU WA NCHI YAKE KWA NINI ASINGEPEWA UWAZIRI MKUU,???? HATA WAGANDA WANASEMA IDD AMINI SIFA MOJA ATAKUMBUKWA ALIKUWA NA UCHUNGU NA NCHI YAKE ,NASHANGAA WENGI WANAMPINGA TANZANIA INAFAA KABISA KUWA NA WATU KAMA HAWA,MUNGU MBALIKI MNALI NAKUPA KILA LA KHERI

    BY ISMA KABENGO,KAMPALA,UG

    ReplyDelete
  38. Hiyo habari ilikuwa hata kwenye BBC

    ReplyDelete
  39. MSEMA KWELI NAKUUNGA MKONO KABISA HAWA WALIMU WAMELALA SANA HUYU MR MNALI ANAUCHUNGU SANA NA MAENDELEO YA NCHI YAKE KAMA NINGEKUWA RAISI NINGEMPANDISHA CHEO HE IS MY HERO KISHERIA ANASTAHILI KUPANDISHWA CHEO MIAKA YA 80 UNCLE WANGU ALIKUWA MWALIMU MKUU ALISHA MCHAPA MWL MMOJA SABABU YA UZEMBE KAZINI NA TOKEA SIKU ILE KILA MWALIMU HAJAZEMBEA TENA KUOGOPA KICHAPO HAWA WALIMU WAZEMBE SANA NCHI HII BILA KICHAPO HATUTAENDELEA KABISA SIKUBALIANI NA SWALA LA KUMSIMAMISHA KAZI NA KIKWETE ANAJUA HILO ANAZUGA TU MACHONI KWA WENGI PUNDA HAENDI BILA BAKORA

    ReplyDelete
  40. akachekiwe akili kwanza jamani
    sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  41. Pamoja na kumpongeza rais kuchukua hatua kwa ajili ya kuwazuia wanaotaka kutumia vibaya madaraka waliyopewa au kwa kuonea wengine, nina hoja....

    Kitendo cha waalimu kuchapwa ni cha kudhalilisha...LAKINI kwamba waalimu wenyewe wamekubali kuchapwa mbele ya wanafunzi wao kwa sababu eti ni amri ya Mkuu wa Wilaya ni kitendo cha kudhalilisha zaidi. Kwamba waalimu wetu hawajui haki zao na wanafanya kazi kwa woga usio na msingi. Pengine ndiyo maana hata wanafunzi wao wanafeli kwa kuwa hawazingatii maadili yakufundisha kama walivyoelekezwa bali wanasikiliza viongozi wanasema nini...

    Poleni sana kwa hizo mboko!

    ReplyDelete
  42. MBONA WALIMU WAO WANAWACHAPA WANAFUNZI NA HAWAFUKUZWI KAZI???AU TANZANIA MWANAFUNZI ANAKUWA NI MTU NUSU MWALIMU NDIO MTU KAMILI??KWELI WAZUNGU WANAPOSEMA WAAFRIKA HAWATUTHAMINI WATOTO NA WANAWAKE HAWAKOSEI.IWEJE AKICHAPWA MWALIMU IWE NI KUMDHALILISHA AKICHAPWA MWANAFUNZI IWE NI KUMFUNDISHA???JAMANI WATANZANIA NA NYIE WATU WA HAKI ZA BINADAMU HUKO TANZANIA MNAPASWA KUJUA WATU WOTE NI SAWA HAMNA MTU BORA KAMA MWANAFUNZI AKICHAPWA MNAONA NI SAWA BASI NA IWE SAWA PIA KWA MWALIMU.HUYO MKUU WA WILAYA ANA TOFAUTI GANI NA WAZIRI MKUU BWANA PINDA ALIEAMRISHA WAUAJI NAO WAULIWE KWANINI JK ASIMCHUKULIE NAE HATUA ZA KUMSIMAMISHA???AU NDIO MKUKI KWA NGURUWE???JE LIPI KOSA KUBWA KUWACHAPA VIBOKO WALIMU WANAOWACHAPAGA VIBOKO WANAFUNZI NA KUZEMBEA KAZINI AU WIZI UNAOFANYWA NA MAFISADI AMBAO UNAIKOSESHA JAMII HAKI ZA MSINGI???JK KACHEMSHA HAPO TUNATAKA RAIS KAMA HUYU MNALI SIO RAIS MUONEVU KAMA JK.

    ReplyDelete
  43. Mie namuunga mkono mkuu wa wilaya aliyefukuzwa. Nchi hii inataka watu kama wao.
    Kesho JK naye awatandike viboko mawaziri wake kwa kushindwa kufanya kazi vema. Akianzia na yule waziri wa vitambulisho.
    Mambo ya haki za binadamu na viumbe vinavyofanana no vitasubiri kwanza.
    Poleni waimu mliochapwa. Hii iwe ni fundisho kwenu. Mfanye kazi sasa

    ReplyDelete
  44. tatizo la wenzetu wahaya ndilo hilo. Mkipewa madaraka mnayatumia vibaya kwa kukomoa haya sasa mkuu wa wilaya kazi unayo??? unankumbusha kina Marehemu Kilivata wa Lushoto ambaye naye alikuwa na tabia hii. Good to know change yaani mabadiliko yameitembelea Tanzania. Rais wetu anaitikia wito wa kuheshimu haki za binadamu na watoto kwa kutoendekeza corporal punishment kokote-swafi sana. siku hizi mambo ni kusemezana siyo kushurutishana na kukomoana.

    ReplyDelete
  45. Duu! Mkuu wa wilaya aliyepiga Katerero amepoteza kazi? Ukisikia chapuchapu ndio kama hivyo.

    ReplyDelete
  46. MNALI POPOTE ULIPO WEWE NI HERO UNAFAA SANA ...MNALI FOR PRESIDENT!!!
    KWA WASIOJUA UTEGAJI WA WAALIM VIJIJINI WATAMLAUMU SANA MNALI ILA KUNA HOJA YA MSINGI HAPO WATOTO WANFELI HUKU AKILI WANAZO,WAALIM WANALIPWA MISHAHARA SHULENI WANATOROKA

    ReplyDelete
  47. Yote tisa, KUMI NI JE, HAO WALIMU WALISHIKIWA BASTOLA? KWELI LEO HII UTAKUBALI KUINAMISHWA NA MWANAUME (or say mtu mzima) MWENZAKO?

    Nakumbuka usemi mmoja kwamba "ni rahisi kumtoa binadamu msituni ila ni vigumu kumtoa msitu kichwani/akilini kwake." Huyu inabidi mkewe na wanawe wahojiwe kujua anawachapa viboka mara ngapi kwa muda fulani.

    ReplyDelete
  48. Amekosea sana kumfukuza kazi kwani alikuwa anatimiza wajibu wake waalimu hawasikii wanaingia shule saa sita na kuendelea halafu wanatuma watoto kuwabebea kuni, maji na maharage na mahindi ya chakula cha watoto shuleni wanagawana. Naomba wachapwe tena na Rais please usiwafukuze kazi wanao timiza wajibu kama huyo Mhe. DC kweli I love him sana

    ReplyDelete
  49. Huyu ISMA KABENGO wa Kampala anawakilisha aina mpya ya ubinadamu, ule wa kujichukulia sheria mkononi.
    Wapenda amani hebu someni maoni yake.
    Na kwa bahati mbaya huo umekuwa mtindo wa maisha wa baadhi ya waafrika wengine, yaani mtu mmoja kwa sababu ya ukubwa wa madaraka yake awe na haki ya kujichukulia sheria mkononi.
    Watanzania wengi tunalipinga hilo KWA NGUVU ZOOTE!
    Amani inayoonekana Tanzania leo haikuja kimchezo mchezo, tumeileta kwa busara na uvumilivu mkubwa. Ni simanzi na sikitiko kwamba karibu jirani zetu wote hawakubarikiwa AMANI tunayoendelea kujivunia. Jamii yetu haifurahi hata kidogo madaraka yakatumika kuwa ni SHERIA MKONONI. Tumechukua reference kutoka wapi?
    Huo ni unyama, na samahani, kama ndugu yetu ISMA huo ndio utaratibu wa maisha yako, SAMAHANI, wabongo umetuchefua mno, hatuukubali kwani tunaamini KILA MTU ANASTAHILI HESHIMA.
    Hebu imagine kwamba wewe ISMA ni mume, na memsapu wako ni mwalimu kule Katerero, kisha zinakufikia habari mkuu wa wilaya kamramba bakora!! Think that way, na kama hupati hisia zozote, think kwamba mmoja wa walimu wale ni mjombako kaka waq mamako mzazi.
    Then andika tena!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  50. YANI ILIBIDI WACHAPWE ADI BASI
    kasimasmishwa kazi tuuuu jamen

    ReplyDelete
  51. SIVURUGI MADA ILA MSAADA JAMANI

    HIVI ISMA KABENGO WA KAMPALA - UGANDA

    SAMAHANI SANA, NAOMBA KUULIZA KUNA MWALIMU MMOJA ALIKUWA ANAITWA JANE KABENGO, ALIKUWA ANAFUNDISHA TABATA KIMANGA PRIMARY SCHOOL. HUYU MWALIMU ALIFARIKI, SASA KATIKA MADAI HAYA YA WALIMU JINA LAKE PIA LIMO, MIMI NI RAFIKI NA JIRANI NILIYEKUWA NAISHI NAYE HAPA TABATA, NAKUMBUKA KULIKUWA NA MDOGO WAKE MMOJA ANAITWA OLIVA KABENGO KAMA SIKOSEI ALIKUWA HOSPITALI YA BUNGANDO SIJUI KAMA YUPO WAPI KWA SASA NA WALA SINA MAWASILIANO NAYE; KAMA KUNA MTU ANAMFAHAMU AU KAMA WEWE NI MMOJA WA NDUGU ZAKE TAFADHALI NAOMBA UFUATILIE MALIPO YA NDUGU YENU MAREHEMU JANE KABENGO.

    MUNGU AMUWEKE MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

    SAMAHANI WAPENDWA SI NIA YANGU KUVURUGA MADA HIYO.


    HATA MIMI NASHAURI KUWA ASHITAKIWE KWA KUWADHALILISHA WALIMU.

    FRIDA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...